Swahili Christian Testimony Video | Ukombozi wa Moyo

05/06/2020

Mhusika mkuu, kiongozi wa kanisa, anagundua kutoka katika kura iliyopigwa kanisani kwamba ndugu wengine wamemripoti Dada Li kuwa asiyejali katika wajibu wake; wanaripoti kwamba yeye hakubali ukweli, huwakaripia watu kwa kiburi, na anawakandamiza. Kiongozi wa kanisa anajua vyema kwamba, kulingana na kanuni za ukweli, Dada Li anapaswa kuachishwa kazi, lakini amepotoshwa na kushawishiwa na falsafa za kishetani kama “Damu ni nzito kuliko maji” na “Mwanadamu asiye na uhai anawezaje kukosa hisia?” Kwa kuzingatia kuwa wanatoka katika mji mmoja wa nyumbani na alikuwa karibu kila wakati, yeye anatenda kulingana na hisia zake, anamkinga na kumlinda Dada Li mara kwa mara. Baadaye, ni kwa sababu tu ya hukumu na ufunuo wa maneno ya Mungu, ndiyo anaweza kuona asili na matokeo ya kutegemea hisia katika vitendo vyake. Anakuja kuwa na utambuzi fulani wa falsafa hizi za kishetani na hategemei tena hisia zake anapokumbana na maswala, lakini badala yake anatenda kwa dhamiri kulingana na kanuni za ukweli.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp