Christian Testimony Video | Hili Jaribu Langu (Swahili Subtitles)

11/08/2020

Yeye ni Mkristo mcha Mungu ambaye amemwamini Mungu kwa miaka mingi na kujitumia kwa bidii, lakini miaka miwili kabla, alipatikana kuwa na saratani ya matiti. Huku akishindwa kukubali hilo, anaamini kwamba kwa sababu ameteseka na kulipa gharama ili kufanya wajibu wake, Mungu anapaswa kumtunza na kumlinda. Haelewi kabisa anawezaje kuwa na saratani. Moyo wake unajawa na suitafahamu na lawama, na anateseka sana. Kwa kusoma maneno ya Mungu, anakuja kuelewa kidogo baadhi ya mawazo mabaya aliyo nayo kuhusu kufuatilia baraka katika imani yake, na anakuwa tayari kutii sheria na mipango ya Mungu. Hali yake inaanza kuwa nzuri baada ya kupokea matibabu kwa muda, lakini anavunjika moyo anapoambiwa baada ya matibabu ya tibakemikali kwamba bado anahitaji upasuaji. Anazama tena katika jaribu lake. Je, hukumu, ufunuo, mwongozo na riziki itokanayo na maneno ya Mungu inamsaidiaje kushinda jaribu hili? Na anaelewa nini na kupata nini kama matokeo?

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp