Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mungu Anuia kuangamiza Ulimwengu kwa Gharika, Amwagiza Nuhu Kuijenga Safina

111

Mwa 6:9-14 Hivi ni vizazi vyake Nuhu: Nuhu alikuwa mtu mwenye haki na mtimilifu katika vizazi vyake, naye Nuhu alitembea na Mungu. Naye Nuhu akapata watoto watatu wa kiume, Shemu, Hamu, na Yafethi. Dunia pia ilikuwa potovu mbele za Mungu, nayo dunia ilijaa vurugu. Naye Mungu akaiangalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani. Naye Mungu akasema kwake Nuhu, Mwisho wa wote walio na mwili umefika mbele zangu; kwa kuwa dunia imejawa na vurugu kupitia kwao; na, tazama, nitawaangamiza pamoja na dunia. Ujitengenezee safina ya mbao wa mvinje; utatengeneza vyumba ndani ya safina, na uipake lami ndani na nje.

Mwa 6:18-22 Lakini na wewe nitaliimarisha agano langu; na utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako, na mke wako, na wake zao wana wako pamoja na wewe. Na kwa kila kilicho na uhai chenye mwili, utawaleta wawili wa kila aina katika safina, kuwaweka hai pamoja nawe; watakuwa wa kiume na wa kike. Kila ndege arukaye kwa aina yake, na mifugo kwa aina yake, kila kinachotambaa duniani kwa aina yake, wawili wa aina yote watakuja kwa wewe, ili uwaweke hai. Na ujichukulie chakula cha kila aina kinacholika, nawe ukikusanye kwako; na kitakuwa kwa ajili ya chakula cha ninyi, na cha wao. Nuhu alifanya hivyo; kulingana na vyote ambavyo Mungu alimwamrisha, alifanya hivyo.

……

Katika enzi hiyo, Mungu alinuia kumuita Nuhu ili kufanya kitu muhimu sana. Kwa nini ilikuwa lazima Afanye hivyo? Kwa sababu Mungu alikuwa na mpango kwa moyo Wake wakati huo. Mpango Wake ulikuwa kuangamiza ulimwengu kwa gharika. Kwa nini auangamize ulimwengu? Maandiko yanasema hivi: “Dunia pia ilikuwa potovu mbele za Mungu, nayo dunia ilijaa vurugu.” Mnaona nini kutoka kwenye kauli “dunia ilijaa vurugu”? Ni ajabu duniani wakati ulimwengu na watu wake wanapotoka kwa kupindukia, na ni hivi: “dunia ilijaa vurugu.” Katika lugha ya leo, “ilijaa vurugu” inamaanisha kila kitu kimechanganyika. Kwa binadamu, inamaanisha kwamba katika nyanja zote za maisha hakuna mpangilio, na mambo yamejaa fujo kweli na ni magumu kudhibiti. Katika macho ya Mungu, inamaanisha watu wa ulimwengu wamepotoka sana. Wamepotoka hadi kiwango gani? Wamepotoka hadi kiwango ambacho Mungu hawezi tena kuvumilia kuangalia na hawezi tena kuwa na subira kuhusu hali hiyo. Wamepotoka hadi kiwango ambacho Mungu anaamua kuwaangamiza. Wakati Mungu alipoamua kuuangamiza ulimwengu, Alipanga kupata mtu wa kuijenga safina. Kisha Mungu akamchagua Nuhu kufanya kitu hicho, ambacho ni kumruhusu Nuhu kuijenga safina. Kwa nini Mungu alimchagua Nuhu? Katika macho ya Mungu, Nuhu ni mtu mwenye haki na haijalishi kile ambacho Mungu atamwagiza yeye kufanya, atafanya vivyohivyo. Hii inamaanisha atafanya chochote anachoambiwa kufanya na Mungu. Mungu alitaka kumtafuta mtu kama huyu ili afanye kazi na Yeye, kukamilisha kile alichokuwa amemwaminia kufanya, kuikamilisha kazi Yake hapa duniani. Hapo nyuma, kulikuwa na mtu mwingine kando na Nuhu ambaye angekamilisha kazi hiyo? Bila shaka la! Nuhu ndiye aliyekuwa mtu wa pekee ambaye angeweza kukamilisha kile ambacho Mungu alikuwa amemwaminia kufanya, na hivyo Mungu alimchagua yeye. Lakini je upana na viwango vya Mungu vya kuwaokoa watu hapo nyuma vilikuwa sawa na vile vya sasa? Jibu ni bila shaka kunayo tofauti! Kwa nini Nauliza hivi? Nuhu alikuwa ndiye mwanaume pekee mwenye haki katika macho ya Mungu wakati huo, kwa dokezo watoto wake wa kiume na mke na wakwe wake wote hawakukuwa watu wenye haki, lakini Mungu aliwalinda watu hawa kwa sababu ya Nuhu. Mungu hakuwataka wao kufanya kile anachowataka watu kufanya leo, na badala yake Aliwaweka hai wanachama wote wanane wa familia ya Nuhu. Walipata baraka za Mungu kwa sababu ya Nuhu kuwa mwenye haki. Kama Nuhu asingekuwepo, hakuna yeyote kati yao ambaye angekamilisha kile ambacho Mungu alikuwa amemwaminia kufanya. Hivyo basi Nuhu alikuwa ndiye mtu wa pekee ambaye alitakikana kubakia hai baada ya ulimwengu kuangamizwa wakati huo, na wale wengine walikuwa tu wafadhiliwa wa ziada. Hii inaonyesha kwamba, katika enzi kabla ya Mungu kuanza rasmi kazi Yake ya usimamizi, kanuni na viwango ambavyo Alishughulikia watu na kuwadai mahitaji vilikuwa vimelegezwa kidogo. Kwa watu wa leo, namna ambavyo Mungu alivyoshughulikia familia ya Nuhu ya watu wanane yaonekana kukosa haki. Lakini tukilinganisha na wingi wa kazi ambayo Yeye Anafanya kwa watu na kiwango cha neno Lake Analopitisha, namna Mungu alivyoshughulikia familia ya Nuhu ya watu wanane ilikuwa tu ni kanuni ya kazi Yake aliyoifanyia katika usuli wa kazi Yake wakati huu. Kwa kulinganisha, familia ya Nuhu ya watu wanane ndio ilipokea mengi zaidi kutoka kwa Mungu au ni watu wa Mungu ndio waliopokea?

Kwamba Nuhu aliitwa ni ukweli mdogo, lakini hoja kuu ya kile tunachozungumzia sasa—tabia ya Mungu, mapenzi Yake kiini Chake halisi katika rekodi hii—si rahisi. Ili kuelewa dhana hizi mbalimbali za Mungu lazima kwanza tuelewe ni mtu wa aina gani ambaye Mungu hutamani kuita, nakupitia hii, tuweze kuelewa tabia yake, mapenzi yake na kiini chake halisi. Kufanya hivi ni muhimu. Hivyo katika macho ya Mungu, mtu huyu ni wa aina gani ambaye yeye humwita? Huyu lazima awe ni mtu anayeweza kuyasikiza maneno Yake. Wakati huohuo, lazima mtu huyu awe yule wa kuwajibika, mtu atakayetekeleza neno la Mungu kwa kuliona kuwa jukumu na wajibu ambao anahitajika kukamilisha. Basi mtu huyu anahitajika kuwa mtu anayemjua Mungu? La. Hapo nyuma, Nuhu hakuwa ameyasikia sana mafundisho ya Mungu wala kupitia kazi yoyote ile ya Mungu. Hivyo basi, maarifa ya Nuhu kumhusu Mungu yalikuwa madogo mno. Ingawaje imerekodiwa hapa kwamba Nuhu alitembea na Mungu, aliwahi kuiona nafsi ya Mungu? Jibu ni bila shaka la! Kwa sababu katika siku hizo, wajumbe wa Mungu tu ndio waliowaendea watu. Ingawa waliweza kuwakilisha Mungu katika kusema na kufanya mambo, walikuwa wakipitisha tu mapenzi na nia Zake. Nafsi ya Mungu haikufichuliwa kwa binadamu uso kwa macho. Kwenye sehemu hii ya maandiko, chote tunachoona tu ni kile ambacho mtu huyu Nuhu alilazimika kufanya na maagizo ya Mungu kwake yalikuwa gani. Hivyo basi ni kiini kipi kilichoonyeshwa na Mungu hapa? Kila kitu anachofanya Mungu kimepangiliwa kwa uhakika. Anapoona jambo au hali ikitokea, kutakuwa na kiwango cha kulipima jambo hilo katika macho Yake, na kiwango hiki kitaamua kama Ataanza mpango wa kulishughulikia au namna ya kuchukulia jambo na hali hii. Yeye anajali na ana hisia kwa kila kitu. Kwa hakika ni kinyume kabisa cha mambo. Kunao mstari hapa ambao Mungu alimwambia Nuhu: “Mwisho wa wote walio na mwili umefika mbele zangu; kwa kuwa dunia imejawa na vurugu kupitia kwao; na, tazama, nitawaangamiza pamoja na dunia.” Katika maneno ya Mungu wakati huu, Alisema kwamba Angeangamiza binadamu tu? La! Mungu Alisema kwamba Angeangamiza viumbe wote hai wenye mwili. Kwa nini Mungu alitaka kuangamiza? Kunao ufunuo mwingine wa tabia ya Mungu hapa: Katika macho ya Mungu, kunayo mipaka ya subira yake kwa kupotoka kwa binadamu, kwa uchafu, vurugu, na kutotii kwa mwili wote. Mipaka Yake ni ipi? Ni kama vile alivyosema Mungu: “Mungu akaiangalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani.” Kauli hii “kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani” inamaanisha nini? Inamaanisha kiumbe yeyote hai, wakiwemo wale waliofuata Mungu, wale walioita jina la Mungu, wale waliowahi kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu, wale waliomtambua Mungu kwa vinywa vyao na hata kumsifia Mungu—pindi tabia yao ilipojaa upotovu na kufikia macho ya Mungu, basi ingemlazimu kuwaangamiza. Hiyo ndiyo ilikuwa mipaka ya Mungu. Hivyo basi ni hadi kiwango kipi Mungu alibakia kuwa mwenye subira kwa binadamu na upotovu wa mwili wote? Hadi katika kiwango ambacho watu wote, wawe wafuasi wa Mungu au wasioamini, walikuwa hawatembelei njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu alikuwa hajapotoshwa tu katika maadili na mwenye wingi wa maovu, lakini pia pale ambapo hakukuwa na mtu aliyesadiki uwepo wa Mungu, tupilia mbali yeyote aliyesadiki kuwa ulimwengu unatawaliwa na Mungu na kwamba Mungu anaweza kuwaletea watu nuru na njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu aliudharau uwepo wa Mungu, na hakumruhusu Mungu kuwepo. Pindi upotovu wa mwanadamu ulipofikia kiwango hiki, Mungu asingeweza tena kuwa na subira Ni nini kingechukua nafasi yake? Kuja kwa hasira ya Mungu na adhabu ya Mungu. Huu haukuwa ufunuo kiasi wa tabia ya Mungu? Katika enzi hii ya sasa, yupo bado binadamu mwenye haki katika macho ya Mungu? Yupo bado binadamu mtimilifu katika macho ya Mungu? Enzi hii ndiyo ile ambayo tabia ya miili yote duniani imepotoka mbele ya macho ya Mungu? Katika siku na enzi hii, mbali na wale Mungu anataka kuwafanya kuwa kamili, wale wanaoweza kumfuata Mungu na kuukubali wokovu Wake, huoni kwamba watu wote wa mwili wanapatia changamoto ile mipaka ya subira ya Mungu? Si kila kitu kinachofanyika kando yenu, kila mnachoona kwa macho yenu, na kusikia kwa masikio yenu, na kupitia ninyi binafsi kila siku katika ulimwengu huu kimejaa vurugu? Katika macho ya Mungu, si ulimwengu kama huu, enzi kama hii, inafaa kukomeshwa? Ingawaje usuli wa enzi ya sasa ni tofauti kabisa na usuli wa enzi ya Nuhu, hisia na hasira Alizo nazo Mungu kwa kupotoka kwa binadamu inabakia ileile sawa na ilivyokuwa wakati huo. Mungu anaweza kuwa mwenye subira kwa sababu ya kazi Yake, lakini kulingana na hali na masharti ya aina yote, ulimwengu huu unafaa kuwa uliangamizwa kitambo katika macho ya Mungu. Hali imepita na kupitiliza ile iliyokuwa hapo nyuma wakati ulimwengu uliangamizwa na gharika.

……

Katika hali hizi, Mungu anajali kuhusu nini zaidi? Si vile wale wasiomfuata Yeye kabisa au wale wanaompinga Yeye kwa vyovyote vile wanamshughulikia Yeye au kumpinga Yeye, au namna ambavyo mwanadamu anamdanganya Yeye. Anajali tu kuhusu kama wale wanaomfuata Yeye, walengwa wa wokovu Wake katika mpango Wake wa usimamizi, wamewekwa kamili na Yeye, na kama wametimiza utoshelezi Wake. Kuhusiana na watu wale wengine bali na wale wanaomfuata Yeye, Anawatolea tu adhabu kidogo mara kwa mara ili kuonyesha ghadhabu Yake. Kwa mfano tsunami, mitetemeko ya ardhi, kuibuka kwa volkano na kadhalika. Wakati huohuo, Anawalinda kwa dhati na kuwashughulikia wale wanaomfuata Yeye na karibu wanaokolewa na Yeye. Tabia ya Mungu ni hii: Kwa mkono mmoja, Anaweza kuwapatia watu Anaonuia kutekeleza subira na ustahimilivu kamili wa kupindukia na kuwasubiria wao kwa muda mrefu Anavyoweza; kwa mkono mwingine, Mungu anachukia na kuchukizwa kwa dhati na watu wa aina ya Shetani wasiomfuata Yeye na wanaompinga Yeye. Ingawaje Hajali kama hawa watu wa aina ya Shetani wanamfuata au wanamwabudu Yeye, bado Anawachukia wao huku akiwa na subira na wao katika moyo Wake, na Anapoamua mwisho wa hawa watu wa aina ya Shetani, Yeye pia anasubiria kufika kwa hatua za mpango Wake wa usimamizi.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Maudhui Yanayohusiana