Mungu Pekee, Ambaye Anao Utambulisho wa Muumba, Anamiliki Mamlaka ya Kipekee

10/09/2019

Ule utambulisho wa pekee wa Shetani umesababisha watu wengi kuonyesha shauku thabiti kwenye maonyesho yake ya dhana mbalimbali. Kunao hata watu wengi wajinga wanaosadiki kwamba, kama vile Mungu, Shetani anamiliki mamlaka, kwani Shetani anaweza kuonyesha miujiza, na anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kufanya. Kwa hivyo, mbali na kumwabudu Mungu, mwanadamu pia anahifadhi nafasi kwenye moyo wake, na hata humwabudu Shetani kama Mungu. Watu hawa wote ni wa kusikitikiwa na kuchukiwa. Ni wa kusikitikiwa kwa sababu ya kutojua kwao, na wa kuchukiwa kwa sababu ya hali yao ya uasi wa kidini na hali halisi ya maovu ya ndani kwa ndani. Wakati huu Nahisi kwamba ni muhimu niwafahamishe kuhusu maana ya mamlaka, yanaashiria nini, na yanawakilisha nini. Kwa mazungumzo ya jumla, Mungu Mwenyewe ni mamlaka, mamlaka Yake yanaashiria mamlaka ya juu na hali halisi ya Mungu, na mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanawakilisha hadhi na utambulisho wa Mungu. Kwa hiyo, je, Shetani huthubutu kusema kwamba yeye ni Mungu? Je, Shetani huthubutu kusema kwamba aliumba viumbe vyote, na anashikilia ukuu juu ya viumbe vyote? Bila shaka la! Kwani hawezi kuumba viumbe vyote; mpaka leo, hajawahi kuumba chochote kilichoumbwa na Mungu, na hajawahi kuumba chochote kilicho na maisha. Kwa sababu hana mamlaka ya Mungu, hatawahi endapo itawezekana kumiliki hadhi na utambulisho wa Mungu, na hili linaamuliwa na hali yake halisi. Je, anazo nguvu sawa na Mungu? Bila shaka hana! Tunaita nini vitendo vya Shetani, na miujiza inayoonyeshwa na Shetani? Je, ni nguvu? Vitendo hivi vinaweza kuitwa mamlaka? Bila shaka la! Shetani huelekeza wimbi la maovu, na misukosuko, uharibifu, na kuchachawiza kila dhana ya kazi ya Mungu. Kwa miaka elfu kadhaa iliyopita, mbali na kupotosha na kunyanyasa mwanadamu, na kumjaribu na kumdanganya binadamu hadi kufikia kiwango cha uovu, na ukataaji wa Mungu, ili binadamu aweze kutembea kwenye bonde la kivuli cha mauti, je, Shetani amefanya chochote ambacho kinastahili hata kumbukumbu ndogo zaidi, pongezi au sherehe ndogo zaidi kutoka kwa binadamu? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, binadamu angepotoshwa naye? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angepata madhara kutokana nayo? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angemwacha Mungu na kugeukia mauti? Kwa sababu Shetani hana mamlaka au nguvu, ni nini ambacho tunafaa kuhitimisha kuhusu hali halisi ya kila kitu anachofanya? Kunao wale wanaofafanua kila kitu ambacho Shetani hufanya kama ujanja mtupu, ilhali Nasadiki kwamba ufafanuzi kama huo haufai sana. Je, Matendo maovu ya kupotosha mwanadamu ni ujanja mtupu tu? Nguvu za maovu ambazo Shetani alimnyanyasia Ayubu, na tamanio lake kali la kumnyanyasa na kumpotosha, lisingewezekana kutimizwa kupitia kwa ujanja mtupu tu. Tukiangalia nyuma, tunaona kwamba, mara moja, kondoo na ng’ombe wa Ayubu walitawanyishwa kila pahali kotekote kwenye milima na vilima, walikuwa hawapo tena; kwa muda mfupi tu, utajiri mwingi wa Ayubu ukatoweka. Je, yawezekana kwamba haya yote yalitimizwa kupitia kwa ujanja mtupu tu? Asili ya yale yote ambayo Shetani hufanya yanalingana na kuingiliana na istilahi mbaya kama vile kudhoofisha, kukatiza, kuharibu, kudhuru, maovu, hali ya kuwa na kijicho, na giza, na kwa hivyo matukio haya yote ambayo si ya haki na ni maovu yanahusiana na kuunganika kwenye vitendo vya Shetani, na hayawezi kutenganishwa na ile hali halisi ya uovu wa Shetani. Haijalishi ni vipi ambavyo Shetani “alivyo na nguvu”, haijalishi ni vipi Shetani alivyo mwenye kuthubutu na haijalishi ni vipi uwezo wake ulivyo mwingi katika kusababisha madhara, haijalishi ni vipi anavyotumia mbinu zenye mseto mpana ambazo zinapotosha na kudanganya binadamu, haijalishi ni vipi alivyo mwerevu kupitia kwenye ujanja na njama zake ambazo anadhalilisha binadamu, haijalishi ni vipi anavyoweza kujibadilisha katika mfumo ule aliomo, hajawahi kuweza kuumba kiumbe chochote kimoja, hajawahi kuweza kuweka wazi sheria au kanuni za uwepo wa viumbe vyote, na hajawahi kutawala na kudhibiti kifaa chochote, kiwe ni chenye uhai au kisichokuwa na uhai. Ndani ya ulimwengu na mbingu, hakuna hata mtu au kifaa kimoja kilichotokana na Shetani, au kilichopo kwa sababu ya Shetani; hakuna hata mtu au kifaa kimoja ambacho kimetawaliwa na Shetani, au kudhibitiwa na Shetani. Kinyume cha mambo ni kwamba, hana budi kuishi katika utawala wa Mungu lakini, vilevile, lazima atii shurutisho na amri zote za Mungu. Bila ruhusa ya Mungu, ni vigumu sana kwa Shetani kugusa hata tone la maji au chembechembe ya mchanga kwenye ardhi; bila ruhusa ya Mungu, Shetani hana hata hiari ya kusongea mchwa wanaojiendea zao kwenye ardhi, sikwambii hata mwanadamu, aliyeumbwa na Mungu. Kwenye macho ya Mungu, Shetani ni duni zaidi ya yungiyungi kwenye mlima, hadi kwenye ndege wanaopaa hewani, hadi kwenye samaki walio baharini, hadi kwenye funza kwenye juu ya nchi. Wajibu wake miongoni mwa viumbe vyote ni kuhudumia viumbe vyote, na kufanyia kazi mwanadamu, na kuhudumia kazi ya Mungu na mpango Wake wa usimamizi. Licha ya vile anavyoonea wenzake kijicho katika asili yake, na vile ambavyo hali yake halisi ya maovu ilivyo, kitu ambacho Shetani anaweza kufanya tu ni kuweza kukubaliana kwa wajibu kuhusiana na kazi yake: kuwa mwenye huduma kwa Mungu, na kuwa mjalizo kwa Mungu. Hiki ndicho kiini na nafasi ya Shetani. Hali yake halisi haijaungana na maisha, haijaungana na nguvu, haijaungana na mamlaka; ni kitu cha kuchezea tu kwenye mikono ya Mungu, mtambo tu kwenye huduma ya Mungu!

Mungu Pekee, Ambaye Anao Utambulisho wa Muumba, Anamiliki Mamlaka ya Kipekee

Baada ya kuelewa uso wa kweli wa Shetani, watu wengi bado wangali hawajaelewa ni nini maana ya mamlaka, hivyo basi wacha Mimi nikuelezee! Mamlaka yenyewe yanaweza kufafanuliwa kama nguvu za Mungu. Kwanza, inaweza kusemekana kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni vizuri. Havina uunganisho wowote na kitu chochote kibaya, na havina uhusiano wowote na viumbe vyovyote vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Nguvu za Mungu zinaweza kuumba viumbe vya mfumo wowote ulio na uzima na nguvu, na haya yote yanaamuliwa na uzima wa Mungu. Mungu ni uzima, kwa hivyo Yeye ndiye chanzo cha viumbe hai vyote. Vilevile, mamlaka ya Mungu yanaweza kufanya viumbe vyote kutii kila neno la Mungu, yaani kuumbika kulingana na matamshi yanayotoka kwenye kinywa cha Mungu, na kuishi na kuzaana kwa amri ya Mungu, ambapo baadaye Mungu anatawala na kuamuru viumbe vyote hai, na hakutakuwa na kupotoka kokote, daima dawamu. Hakuna mtu au kifaa kilicho na mambo haya; Muumba tu ndiye anayemiliki na aliye na nguvu kama hizo, na hivyo basi yanaitwa mamlaka. Huu ndio upekee wa Muumba. Kwa hivyo, haijalishi kama ni neno lenyewe “mamlaka” au hali halisi ya mamlaka haya, kila mojawapo linaweza tu kuhusishwa na Muumba kwa sababu ni ishara ya utambulisho na hali halisi ya kipekee ya Muumba; na inawakilisha utambulisho na hadhi ya Muumba, mbali na Muumba, hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuhusishwa na neno “mamlaka” Huu ni ufasiri wa mamlaka ya kipekee ya Muumba.

Ingawa Shetani alimwangalia Ayubu kwa macho ya kutamani mali yake, bila ya ruhusa ya Mungu hakuthubutu kugusa hata unywele mmoja wa mwili wa Ayubu. Ingawa ni mwenye uovu na unyama wa ndani, baada ya Mungu kutoa shurutisho Lake kwake, Shetani hakuwa na chaguo lakini kutii shurutisho la Mungu. Na kwa hivyo, hata Ingawa Shetani alionekana kana kwamba ameshikwa na kichaa sawa na mbwa-mwitu miongoni mwa kondoo alipomjia Ayubu, hakuthubutu kusahau mipaka aliyowekewa wazi na Mungu, hakuthubutu kukiuka shurutisho za Mungu, na kwa hayo yote, Shetani hakuthubutu kutoka kwenye kanuni ya maneno ya Mungu—je, hii si kweli? Kutokana na mtazamo huu wa maisha, tunaona kwamba Shetani hathubutu kuvunja matamshi yoyote yale ya Yehova Mungu. Kwake Shetani, kila neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu ni shurutisho, na sheria ya mbinguni, na maonyesho ya mamlaka ya Mungu—kwani nyuma ya kila neno la Mungu kunadokezwa adhabu ya Mungu kwa wale wanaokiuka maagizo ya Mungu, na wale wasiotii na wanaopinga sheria za mbinguni. Shetani anajua wazi kwamba kama atakiuka shurutisho za Mungu, basi lazima akubali athari za kukiuka mamlaka ya Mungu na kupinga sheria za mbinguni. Na sasa athari hizi ni zipi? Sina haja ya kusema kwamba, athari hizi bila shaka, ni adhabu kutoka kwa Mungu. Vitendo vya Shetani kwake Ayubu vilikuwa tu mfano mdogo wa yeye kumpotosha binadamu, na wakati ambapo Shetani alipokuwa akitekeleza vitendo hivi, ile mipaka ambayo Mungu Aliweka na amri Alizotoa kwake Shetani vilikuwa tu mfano mdogo wa kanuni zinazotokana na kila kitu anachofanya. Aidha, wajibu na nafasi ya Shetani katika suala hili ulikuwa tu mfano mdogo wa wajibu na nafasi yake katika kazi ya usimamizi wa Mungu, na utiifu kamili wa Shetani kwa Mungu wakati alipomjaribu Ayubu, ulikuwa tu mfano mdogo wa namna ambavyo Shetani hakuthubutu kuweka hata upinzani mdogo kwa Mungu katika kazi ya usimamizi wa Mungu. Ni onyo gani ambalo mifano hii midogo inakupa? Miongoni mwa mambo yote, akiwemo Shetani, hakuna mtu au kitu kinachoweza kukiuka sheria na kanuni za mbinguni zilizowekwa wazi na Muumba, na hakuna mtu au kitu kinachothubutu kukiuka sheria na kanuni hizi za mbinguni, kwani hakuna mtu au kifaa kinaweza kubadilisha au kuepuka adhabu ambayo Mungu anawawekea wale wanaokosa kumtii. Ni Muumba tu anayeweza kuanzisha sheria na kanuni za mbinguni, ni Muumba tu aliye na nguvu za kuanza kuzitekeleza na nguvu za Muumba ndizo haziwezi kukiukwa na mtu au kitu chochote. Haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba, mamlaka haya yako juu zaidi miongoni mwa mambo yote, na kwa hivyo haiwezekani kusema kwamba “Mungu ndiye mkubwa zaidi naye Shetani ni nambari mbili.” Isipokuwa Muumba anayemiliki mamlaka ya kipekee, hakuna Mungu mwingine.

Je, sasa unayo maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu? Kwanza, kunayo tofauti kati ya mamlaka ya Mungu yaliyotajwa hivi punde na nguvu za binadamu? Na tofauti ni nini? Baadhi ya wanadamu husema kwamba hakuna ulinganifu wowote kati ya haya mawili. Hayo ni kweli! Ingawa watu husema kwamba hakuna ulinganisho kati ya haya mawili, kwenye fikira na mawazo ya binadamu, nguvu za binadamu mara nyingi zinadhaniwa kuwa mamlaka, na haya mawili hulinganishwa mara nyingi sako kwa bako. Ni nini kinachoendelea hapa? Je, si watu wanafanya kosa la kubadilisha bila ya kuwa waangalifu kitu kimoja na kingine? Vitu hivi viwili havina uhusiano wowote na hakuna ulinganisho wowote kati yavyo, ilhali watu bado hawawezi kuelewa. Je, haya yatatuliwe vipi? Kama ungependa kwa kweli kupata suluhu, njia ya pekee ni kuelewa na kujua mamlaka ya kipekee ya Mungu. Baada ya kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, hutataja kwa mkupuo mmoja nguvu za binadamu na mamlaka ya Mungu.

Nguvu za binadamu zinarejelea nini? Kwa ufupi, ni uwezo au mbinu inayowezesha tabia potovu, matamanio na malengo ya binadamu kuweza kupanuliwa au kutimizwa hadi kiwango cha juu zaidi. Je, haya yatumike kumaanisha mamlaka? Haijalishi ni vipi ambavyo malengo na matamanio ya binadamu yalivyo makubwa au yenye faida, mtu huyu hawezi kusemekana amemiliki mamlaka; kama amezidi sana, haya majivuno na ufanisi ni maonyesho tu ya upumbavu wa Shetani miongoni mwa binadamu; kama imezidi sana, ni upuzi ambao Shetani anaendeleza kama babu yake mwenyewe ili kutimiza maono yake ya kuwa Mungu.

Unatazama vipi haswa mamlaka ya Mungu sasa? Kwa vile sasa maneno haya yamezungumziwa kwenye ushirika, unafaa kuwa na maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu. Na kwa hivyo Nakuuliza: Mamlaka ya Mungu yanaashiria nini? Je, yanaashiria ule utambulisho wa Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria nguvu za Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria hadhi ya kipekee ya Mungu Mwenyewe? Miongoni mwa mambo yote, ni katika kitu gani umeona mamlaka ya Mungu? Uliyaona vipi? Kwa mujibu wa ile misimu minne inayopitiwa na binadamu, je, mtu yeyote anaweza kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya machipuko, kiangazi, mapukutiko na kipupwe? Wakati wa machipuko, miti huweza kuchomoza na kuchanua; katika kiangazi, inafunikwa na majani; katika mapukutiko inazaa matunda na katika kipupwe majani yanaanguka. Je, yupo anayeweza kubadilisha sheria hii? Je, hii inaonyesha dhana moja ya mamlaka ya Mungu? Mungu alisema “Iwe Nuru,” na ikawa nuru. Je, nuru hii ingali ipo? Nuru hii inakuwepo kwa ajili ya nini? Inakuwepo kwa sababu ya maneno ya Mungu, bila shaka, na kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Je, hewa iliyoumbwa na Mungu bado ipo? Je, hewa ambayo binadamu anapumua inatoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kuchukua vitu vinavyotoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kubadilisha hali yao halisi na kazi? Kuna yeyote anayeweza kutibua mpangilio wa usiku na mchana kama ulivyopangwa na Mungu, na sheria ya usiku na mchana kama ilivyoamrishwa na Mungu? Je, Shetani anaweza kufanya kitu kama hicho? Hata kama hulali wakati wa usiku, na unachukulia usiku kuwa wakati wa mchana, basi bado ni wakati wa usiku; unaweza kubadilisha mazoea yako ya kila siku, lakini huwezi kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya usiku na mchana—ukweli huu hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote, au sio? Kuna yeyote anayeweza kumfanya simba kulima ardhi kama afanyavyo ng’ombe? Je, yupo yeyote anayeweza kubadilisha ndovu kuwa punda? Je, yupo anayeweza kubadilisha kuku akapaa hewani kama tai? Je, yupo anayeweza kumfanya mbwa-mwitu kula nyasi kama kondoo? (La) Je, yupo anayeweza kumfanya samaki aliye majini kuishi kwenye ardhi kavu? Hilo haliwezi kufanywa na wanadamu. Na kwa nini haliwezi? Kwa sababu Mungu aliwaamuru samaki kuishi ndani ya maji, na kwa hivyo wanaishi ndani ya maji. Kwenye ardhi kavu hawataweza kuishi kwani watakufa; hawawezi kukiuka vipimo vya amri ya Mungu. Vitu vyote vina sheria na kipimo cha kuwepo kwao, na kila mojawapo kina silika zake binafsi. Haya yameamriwa na Muumba, na hayawezi kubadilishwa na kupitishwa na binadamu yeyote. Kwa mfano, simba siku zote ataishi jangwani, umbali fulani kutoka kwenye jumuia ya binadamu, na hatawahi kuwa mtulivu na mwaminifu kama vile ng’ombe alivyo na anavyoishi na kumfanyia binadamu kazi. Ingawa ndovu na punda ni wanyama, na wote wana miguu minne, na ni viumbe vinavyopumua hewa, ni aina tofauti, kwani waligawanywa kwenye aina tofauti na Mungu, kila mmoja wao anazo silika zake binafsi, na hivyo hawatawahi kubadilishana. Ingawa kuku ana miguu miwili, na mbawa kama vile alivyo tai, hatawahi kuweza kupaa hewani; kama amejaribu sana anaweza tu kupaa hadi kwenye mti—na hili linaamuliwa na silika yake. Sina haja kusema, haya yote ni kwa sababu ya amri za mamlaka ya Mungu.

Katika maendeleo ya mwanadamu leo, sayansi ya mwanadamu inaweza kusemekana kwamba inanawiri, na mafanikio ya uchunguzi wa kisayansi wa binadamu unaweza kufafanuliwa kama wa kuvutia. Uwezo wa kibinadamu, lazima isemwe, unazidi kukua mkubwa zaidi, lakini kunao ushindi mmoja wa kisayansi ambao mwanadamu hajaweza kufanya: Mwanadamu ameunda ndege, vibebaji vya ndege, na hata bomu la atomiki, mwanadamu ameenda angani, ametembea mwezini, amevumbua Intaneti, na ameishi maisha ya kiwango cha juu ya teknolojia, ilhali mwanadamu hawezi kuumba kiumbe hai kinachopumua. Silika za kila kiumbe kilicho hai na sheria ambazo zinatawala kuishi kwake na mzunguko wa maisha na kifo wa kila kiumbe kilicho hai—vyote hivi haviwezekani na havidhibitiki na sayansi ya mwanadamu. Wakati huu, lazima isemekane kwamba haijalishi ni viwango gani vya juu zaidi vitakavyofikiwa na sayansi ya binadamu, haviwezi kulinganishwa na fikira zozote za Muumba na haiwezekani kutambua miujiza ya uumbaji wa Muumba na uwezo wa mamlaka Yake. Kunazo bahari nyingi sana juu ya nchi, ilhali hazijawahi kukiuka mipaka yao na kuja kwenye ardhi kwa nguvu, na hiyo ni kwa sababu Mungu aliwekea mipaka kila mojawapo ya bahari hizo; zilikaa popote pale Aliziamuru kukaa; na bila ya ruhusa ya Mungu haziwezi kusongasonga ovyo. Bila ya ruhusa ya Mungu, haziwezi kuingiliana, na zinaweza kusonga tu pale ambapo Mungu anasema hivyo, na pale ambapo zinaenda na kubakia ni suala na uamuzi wa mamlaka ya Mungu.

Ili kuweka wazi zaidi, “mamlaka ya Mungu” yanamaanisha kwamba ni wajibu wa Mungu. Mungu anayo haki ya kuamua namna ya kufanya kitu na kinafanywa kwa vyovyote vile Anavyopenda. Sheria ya vitu vyote ni wajibu wa Mungu, na wala si wajibu wa binadamu; na wala haiwezi kubadilishwa na binadamu. Haiwezi kusongeshwa kwa mapenzi ya binadamu, lakini inaweza badala yake kubadilishwa kwa fikira za Mungu, na hekima ya Mungu, na amri za Mungu, na hii ni kweli ambayo haiwezi kukataliwa na binadamu yeyote. Mbingu na nchi na viumbe vyote, ulimwengu, mbingu yenye nyota, misimu minne ya mwaka, ile inayoonekana na isiyoonekana kwa binadamu—yote haya yapo, yanafanya kazi, na kubadilika bila ya kosa hata dogo, chini ya mamlaka ya Mungu, kulingana na shurutisho za Mungu, kulingana na amri za Mungu, na kulingana na sheria za mwanzo wa uumbaji. Si hata mtu mmoja au kifaa kimoja kinaweza kubadilisha sheria zao, au kubadilisha mkondo wa asili ambao sheria hizi zinafanya kazi; zilianza kutumika kwa sababu ya mamlaka ya Mungu, na zitaangamia kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ya Mungu. Sasa kwa sababu haya yote yamesemwa, je, unahisi kwamba mamlaka ya Mungu ni ishara ya utambulisho na ishara ya Mungu? Je, mamlaka ya Mungu yanaweza kumilikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au ambacho hakijaumbwa? Yanaweza kuigwa, kufananishwa, au kubadilishwa na mtu yeyote, na kitu chochote, au kifaa chochote?

Utambulisho wa Muumba ni wa Kipekee, na Hufai Kufuata lile Wazo la Imani ya Kuabudu Miungu Wengi

Ingawa mbinu na uwezo wa Shetani ni kubwa zaidi kuliko zile za binadamu, Ingawa anaweza kufanya mambo ambayo hayawezi kufanywa na binadamu, bila kujali kama waonea wivu au unatamani kile ambacho Shetani anafanya, bila kujali kama unachukia au unachukizwa na kile anachofanya, bila kujali kama unaweza au huwezi kuona hicho, bila kujali ni kiwango kipi ambacho Shetani anaweza kutimiza au ni watu wangapi anaweza kudanganya ili wakamwabudu na kumtolea kafara, na bila kujali ni vipi unavyomfafanua, haiwezekani wewe kusema kwamba Shetani anayo mamlaka na nguvu za Mungu. Unafaa kujua kwamba Mungu ni Mungu, tunaye Mungu mmoja tu, na zaidi ya yote unafaa kujua kwamba ni Mungu tu aliye na mamlaka, na kwamba Anazo nguvu za kudhibiti na kutawala viumbe vyote. Eti kwa sababu Shetani anao uwezo wa kudanganya watu, na anaweza kujifanya kuwa Mungu, na anaweza kuiga ishara na miujiza inayofanywa na Mungu, amefanya mambo sawa na yale ya Mungu, wewe unasadiki kimakosa kwamba Mungu si wa kipekee, kwamba tunayo miungu mingi, kwamba tofauti yao ni kule kuwa tu na mbinu nyingi au chache zaidi, na kwamba kunazo tofauti katika upana na nguvu zinazoonyeshwa. Unapima ukubwa wao katika mpangilio wa kuwasili kwao, na kulingana na umri wao, na unasadiki kwa njia isiyofaa kwamba kunayo miungu mingine mbali na Mungu, na unafikiri kwamba nguvu na mamlaka ya Mungu si ya kipekee. Kama unazo fikira kama hizo, kama hutambui upekee wa Mungu, husadiki ni Mungu pekee anayemiliki mamlaka na kama unatiiutatii tu imani ya kuabudu miungu wengi, basi Nasema kwamba wewe ni duni kabisa kuliko viumbe vyote, wewe ni mfano halisi na wa kweli wa Shetani, na wewe ni mtu kamili wa maovu! Je, unaelewa kile Ninachojaribu kufunza kwa kusema maneno haya? Haijalishi ni muda gani, mahali au maelezo ya ziada kuhusu wewe, haifai kuchanganya Mungu na mtu yeyote mwingine, kitu au kifaa. Haijalishi unavyohisi kwamba mamlaka ya Mungu na hali halisi ya Mungu Mwenyewe havijulikani wala kuweza kufikiwa, haijalishi ni kiwango kipi cha matendo na maneno ya Shetani yanavyokubaliana na mawazo na fikira zako, haijalishi ni vipi ambavyo mambo haya yanakutosheleza wewe, usiwe mjinga, usichanganye dhana hizi, usikatae uwepo wa Mungu, usikatae utambulisho na hadhi ya Mungu, usimsukume Mungu nje ya mlango na kumleta Shetani kuchukua nafasi ya “Mungu” aliye ndani ya moyo wako na kuwa Mungu wako. Sina shaka kwamba una uwezo wa kufikiria athari za kufanya hivyo!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Iliyotangulia: Amri ya Mungu kwa Shetani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Amri ya Mungu kwa Shetani

Ayubu 2:6 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake. Shetani Hajawahi Kuthubutu...

Baraka za Mungu

Mwa 17:4-6 Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena,...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp