Baraka za Mungu

10/09/2019

Mwa 17:4-6 Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwako.

Mwa 18:18-19 Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye. Kwani namjua, kuwa atawatawala watoto wake na nyumba yake kufuata yeye, na wataishika njia ya Yehova, kufanya haki na hukumu; ili Yehova aweze kumletea Ibrahimu yale ambayo amemwambia.

Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kujipitia, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.

Ayu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.

Njia na Sifa za Kipekee za Matamshi ya Muumba Ni Ishara ya Utambulisho na Mamlaka ya Kipekee ya Muumba

Baraka za Mungu

Wengi hupenda kutafuta, na kufaidi, baraka za Mungu, lakini si kila mmoja anayeweza kufaidi baraka hizi, kwani Mungu anazo kanuni Zake binafsi, na Yeye hubariki binadamu kulingana na njia Zake binafsi. Ahadi ambazo Mungu hutoa kwa binadamu, na kiwango cha neema ambacho Yeye humpa binadamu, vyote vinatolewa kulingana na fikira na vitendo vya binadamu. Hivyo, ni nini huonyeshwa kupitia kwa baraka za Mungu? Watu wanaweza kuona nini ndani yake? Wakati huu, hebu tuweke kando mazungumzo kuhusu ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki, na kanuni anazofuata Mungu katika kubariki binadamu. Badala yake, hebu tuangalie baraka za Mungu kwa binadamu kwa kusudio la kujua mamlaka ya Mungu, kutoka kwenye mtazamo wa kujua mamlaka ya Mungu.

Mafungu manne ya maandiko yaliyotajwa hapo juu yote ni rekodi kuhusu baraka za Mungu kwa binadamu. Yanatupa ufafanuzi wenye maelezo kuhusu wapokeaji wa baraka za Mungu, kama vile Ibrahimu na Ayubu, vilevile yanatupa sababu zinazoelezea kwa nini Mungu alitoa baraka Zake, na ni nini kilichokuwa kwenye baraka hizi. Ile sauti na njia ya matamshi ya Mungu, mtazamo na mahali ambapo Alitamka, huturuhusu kushukuru kwamba Yule anayetoa baraka na mpokeaji wa baraka kama hizo ni wenye utambulisho, hadhi, na hali halisi tofauti kabisa. Sauti na njia ambayo matamshi haya yanatolewa, na mahali ambapo yalitamkwa, vinaonyesha upekee wao kwa Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba. Anayo mamlaka na uwezo, pamoja na heshima ya Muumba, na adhama isiyovumilia shaka kutoka kwa binadamu yeyote.

Kwanza hebu tuangalie Mwa 17:4-6: “Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwa wewe.” Matamshi haya ndiyo yaliyokuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, pamoja na baraka za Mungu kwa Ibrahimu: Mungu angemfanya Ibrahimu baba wa mataifa, Angemfanya kuwa na uzao mwingi, na Angemfanya kuwa na mataifa mengi, nao wafalme wangetoka kwake. Je, unayaona mamlaka ya Mungu katika maneno haya? Na unayaonaje mamlaka kama hayo? Ni dhana gani ya hali halisi ya mamlaka ya Mungu unayoona? Kutoka kwa usomaji wa makini wa maneno haya, si vigumu kutambua kwamba mamlaka na utambulisho wa Mungu vyote vimefichuliwa waziwazi na maneno ya matamshi ya Mungu. Kwa mfano, Mungu anaposema “agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa … kuwa nimekufanya … Mimi nitafanya uwe…,” kauli kama vile “wewe utakuwa” na “nitayaunda,” ambazo maneno yake yanasheheni thibitisho la utambulisho na mamlaka ya Mungu, kwa upande mmoja ni onyesho la uaminifu wa Muumba; kwa upande mwingine, ni maneno maalum yaliyotumiwa na Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba—pamoja na kuwa sehemu ya msamiati uliozoeleka. Kama mtu atasema anatumai kuwa mtu mwingine atazidisha uzao, kwamba mataifa yatatokana na wao, na kuwa wafalme watatoka miongoni mwao, basi hiyo bila shaka ni aina ya tamanio, na si ahadi wala baraka. Na hivyo, hawathubutu kusema “Mimi nitakufanya kuwa hivi na hivi, kutafanya hivi na hivi…,” kwani wanajua kwamba hawamiliki nguvu kama hizo; si juu yao, na hata kama watasema maneno kama hayo, maneno yao yatakuwa matupu, na ya kipuzi, yanayoendeshwa na matamanio na maono yao. Je, yupo yeyote anayethubutu kuongea kwa sauti kuu kama hiyo ilhali wanahisi kwamba hawawezi kutimiza matamanio yao? Kila mtu hutamani mema yafikie kizazi chake, na kutumai kwamba kitafanikiwa na kufurahia ufanisi mkubwa. “Ni utajiri upi mkubwa utakaokuwepo kama mmoja wao angekuwa mfalme mkuu! Kama mmoja angekuwa gavana ingekuwa vizuri, pia—mradi tu wawe ni watu muhimu!” Haya yote ni matamanio ya watu wote, lakini watu wanaweza kutamani tu baraka juu ya kizazi chao, na hawawezi kutimiza au kufanya ahadi zao zozote kuwa kweli. Katika mioyo yao, kila mtu anajua waziwazi kwamba wao hawamiliki nguvu za kutimiza mambo kama hayo, kwani kila kitu chao ni zaidi ya udhibiti wao, na hivyo basi watawezaje kuamuru hatima ya wengine? Sababu inayomfanya Mungu kusema mambo kama haya ni kwa vile Mungu anamiliki mamlaka kama hayo, na Anaweza kutekeleza na kutambua ahadi zote Anazotoa kwa ajili ya binadamu, na kufanya baraka zote Anazomwombea binadamu kuwa kweli. Binadamu aliumbwa na Mungu, na ili Mungu aweze kumuumba mtu atakayezidi kwa uzao ni jambo ambalo litakuwa rahisi sana; kufanya kizazi cha mtu kufanikiwa kutahitaji neno moja tu kutoka Kwake. Hatawahi kufanya kazi Mwenyewe na kutoa jasho kwa ajili ya kitu kama hicho, au kushughulisha akili Yake, au kujifunga mafunda mbalimbali; hii ndiyo nguvu halisi ya Mungu, mamlaka halisi ya Mungu.

Baada ya kusoma “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye” kwenye Mwanzo 18:18, je, unaweza kuhisi mamlaka ya Mungu hapo? Unaweza kuhisi hali isiyokuwa ya kawaida ya Muumba? Unaweza kuhisi hali ya mamlaka ya juu ya Muumba? Maneno ya Mungu yana uhakika. Mungu hasemi maneno kama hayo kwa sababu ya, au kwa kuwakilisha, ujasiri Wake katika ufanisi; hayo ni, badala yake, ithibati ya mamlaka ya matamshi, na ni amri inayotimiza maneno ya Mungu. Kunazo semi mbili ambazo unafaa kutilia maanani hapa. Wakati Mungu anaposema “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye,” kunayo dalili ya kutoeleweka kwenye maneno haya? Kunayo dalili yoyote ya wasiwasi? Kunayo dalili yoyote ya woga? Kwa sababu ya matamshi “ataweza kwa hakika” na “atakuwa” kwenye matamshi ya Mungu, dalili hizi, ambazo zinapatikana tu kwa binadamu na mara nyingi zinajionyesha ndani yake, hazijawahi kupata uhusiano wowote na Muumba. Hakuna mtu angethubutu kutumia maneno kama haya wakati akiwatakia wengine mema, hakuna yule angethubutu kubariki mwingine apate taifa kubwa na lenye nguvu kwa uhakika kama huo, au kutoa ahadi kwamba mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia kwake. Maneno ya Mungu yanapokuwa na uhakika zaidi, ndipo yanathibitisha kitu fulani—na kitu hicho ni nini? Yanathibitisha kuwa Mungu anayo mamlaka kama hayo, kuwa mamlaka Yake yanaweza kutimiza mambo haya, na kwamba ufanisi wake ni lazima. Mungu alikuwa na uhakika katika moyo Wake, bila kusita kokote, kwa kila kitu Alichombariki Ibrahimu. Aidha, uzima wa haya utakamilishwa kulingana na maneno Yake, na hakuna nguvu ingeweza kubadilisha, kuzuia, kuharibu, au kutatiza kukamilika kwake. Licha ya kilichotendeka, hakuna kitu ambacho kingebatilisha au kuathiri kutimia na kukamilika kwa matamshi ya Mungu. Huu ndio uzito wenyewe wa maneno yaliyotamkwa kutoka kinywa cha Muumba, na mamlaka ya Muumba ambayo hayavumilii kanusho la binadamu! Baada ya kuyasoma maneno haya, ungali unahisi shaka? Maneno haya yalitamkwa kutoka kinywa cha Mungu, na kunazo nguvu, adhama na mamlaka katika maneno ya Mungu. Uwezo na mamlaka kama haya, na kutozuilika kwa kukamilika kwa hoja, haviwezi kufikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa na haviwezi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa. Muumba pekee ndiye anaweza kuongea na binadamu kwa sauti na mkazo kama huo, na hoja zimethibitisha kuwa ahadi Zake si maneno matupu, au majigambo ya kupitisha wakati, lakini ni maonyesho ya mamlaka ya kipekee yasiyoweza kupitwa na mtu, kitu, au kifaa chochote.

Ni nini tofauti kati ya maneno yanayotamkwa na Mungu na yale yanayotamkwa na binadamu? Unaposoma maneno haya yaliyotamkwa na Mungu, unahisi nguvu za maneno ya Mungu, na mamlaka ya Mungu. Je, unahisi vipi unaposikia watu wakitamka maneno kama hayo? Je, unafikiria kuwa wao wana kiburi kupindukia, na ni wenye kujigamba na kujionyesha? Kwani hawana nguvu hizi, hawamiliki mamlaka kama haya, na hivyo basi hawawezi kabisa kutimiza mambo kama hayo. Kwamba wao wana hakika kabisa kuhusu ahadi zao, yaonyesha tu kutojali kwa matamshi yao. Kama mtu anasema maneno kama hayo, basi bila shaka watakuwa wenye kiburi, na waliozidisha ujasiri wao, huku wakijifichua kama mfano wa pekee wa tabia ya malaika mkuu. Maneno haya yalitoka kinywani mwa Mungu; je, unahisi dalili yoyote ya kiburi hapa? Je, unahisi ya kwamba matamshi ya Mungu ni mzaha tu? Matamshi ya Mungu ni mamlaka, Maneno ya Mungu ni hoja za kweli, na kabla hajatamka maneno kutoka kinywani Mwake, hivi ni kusema, wakati Anapofanya uamuzi wa kufanya kitu, tayari kitu hicho kimefanyika. Yaweza kusemwa kwamba kila kitu alichosema Mungu kwa Ibrahimu kilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, na ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu. Ahadi hii ilikuwa hoja iliyoanzishwa, pamoja na hoja iliyokamilika, na hoja hizi zilitimizwa kwa utaratibu kwa fikira za Mungu kulingana na mpango wa Mungu. Kwa hivyo, Mungu kusema maneno kama hayo haimaanishi kuwa Ana tabia ya kiburi, kwani Mungu anaweza kutimiza mambo kama hayo. Anazo nguvu na mamlaka, na ana uwezo wa kutimiza hoja hizi, na mafanikio yake kwa jumla yanapatikana ndani ya uwezo Wake. Wakati maneno kama haya yanapotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, yanakuwa ufunuo na maonyesho ya tabia ya kweli ya Mungu, ufunuo na maonyesho timilifu ya hali halisi na mamlaka ya Mungu, na hakuna kitu ambacho kinafaa zaidi na kizuri kama ithibati ya utambulisho wa Mungu. Namna, sauti, na mpangilio wa maneno ya matamshi kama hayo ndiyo alama haswa ya utambulisho wa Muumba, na vyote hivi vinalingana kwa njia timilifu na maonyesho na utambulisho wa Mungu, na ndani yao hakuna kusingizia, au kasoro; vyote hivi ni, onyesho timilifu na lililo kamili kabisa, la hali halisi na mamlaka ya Muumba. Lakini Kuhusu viumbe, havimiliki mamlaka haya, wala hali hii halisi, vilevile havimiliki nguvu inayotolewa na Mungu. Kama binadamu atasaliti tabia kama hiyo, basi hali hiyo itakuwa bila shaka mlipuko wa tabia yake iliyopotoka, na itaishia kwa athari ya kujihusisha visivyofaa na kiburi cha binadamu na maono yasiyo na mipaka, na kufichuliwa kwa nia haribifu za yuleyule ibilisi, Shetani, anayependa kudanganya watu na kuwashawishi kuweza kusaliti Mungu. Naye Mungu anachukuliaje kile ambacho kimefichuliwa kwa lugha kama hii? Mungu angesema kwamba ungependa kunyakua nafasi Yake na kwamba unapenda kumwiga Yeye na kumbadili Yeye. Wakati unaiga sauti ya matamshi ya Mungu, nia yako ni ya kubadilisha mahali pa Mungu katika mioyo ya watu, kujitwalia mwanadamu ambaye anamilikiwa kwa haki na Mungu. Huyu ni Shetani, wazi na bila kukuficha; haya ni matendo ya vizazi vya malaika mkuu visivyovumilika Mbinguni! Miongoni mwenu, kunao wowote waliowahi kuiga Mungu kwa njia fulani kwa kuongea maneno machache, kwa nia ya kupotosha na kudanganya watu na kuwafanya watu kuhisi kuwa maneno na matendo ya mtu huyu yana mamlaka na nguvu za Mungu, kama kwamba hali halisi na utambulisho wa mtu huyo ni vya upekee, na hata ni kana kwamba sauti ya mtu huyu ni sawa na ile ya Mungu? Umewahi kufanya jambo kama hili? Umewahi kuiga sauti ya Mungu kwenye matamshi yako, kwa miondoko iliyodai kuwakilisha tabia za Mungu, ikiwa pamoja na uwezo na mamlaka ya kudhaniwa? Je, wengi wenu huwa mara nyingi mnatenda, au kupanga kutenda kwa njia kama hiyo? Sasa, unapoona kwa kweli, kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, na kutazama kile ulichokuwa ukikifanya, na ulichokuwa ukifichua kujihusu, je, unahisi vibaya? Je, unatambua hali yako ya kutoheshimu na kuwa na utovu wa haya? Baada ya kuchambua tabia na hali halisi ya watu kama hawa, je, inaweza kusemekana kuwa wao ndio walaaniwa wa jahanamu? Yaweza kusemekana kuwa kila mtu anayefanya mambo kama haya anajiletea udhalilishaji? Je, unatambua uzito wa asili yake? Na uzito wake ni wa kiasi kipi? Nia ya watu wanaotenda mambo kwa njia hii ni kuiga Mungu. Wanataka kuwa Mungu, na kuwafanya watu kuwaabudu kama Mungu. Wanataka kuondoa nafasi ya Mungu katika mioyo ya watu, na kutupilia mbali yule Mungu anayefanya kazi miongoni mwa binadamu, ili kutimiza nia ya kuwadhibiti watu, na kuwateketeza watu, na kuwamiliki watu hao. Kila mmoja anayo matamanio na maono kama hayo yaliyofichika akilini, na kila mmoja anaishi katika hali halisi potovu na ya kishetani kama hiyo na anaishi katika asili ya kishetani ambapo yumo katika uadui na Mungu, na anamsaliti Mungu, na anapenda kuwa Mungu. Kufuatia Ushirika Wangu katika mada hii ya Mungu, bado ungependa au ungetamani kujifanya wewe ni Mungu, au kuiga Mungu? Na bado unatamani kuwa Mungu? Ungali unapenda kuwa Mungu? Mamlaka ya Mungu hayawezi kuigwa na binadamu, na utambulisho na hadhi ya Mungu haiwezi kuigizwa na binadamu. Ingawa unaweza kuiga sauti ambayo Mungu huongea nayo, huwezi kuiga hali halisi ya Mungu. Ingawa unaweza kusimama mahali pa Mungu na kujifanya kuwa Mungu, hutawahi kuweza kufanya kile ambacho Mungu ananuia kukifanya, na hutawahi kutawala na kuamuru viumbe vyote. Katika macho ya Mungu, utabakia kuwa kiumbe kidogo, na haijalishi ni vipi ambavyo mbinu na uwezo wako ulivyo mkubwa, haijalishi ni vipaji vingapi unavyo, uzima wako wewe umetawaliwa na Muumba. Ingawa unaweza kusema maneno fulani ya kijeuri, hilo haliwezi kuonyesha kuwa unayo hali halisi ya Muumba, wala kuwakilisha ya kwamba unamiliki mamlaka ya Muumba. Mamlaka na nguvu za Mungu ni hali halisi ya Mungu Mwenyewe. Hayakufunzwa wala kusomwa, au kuongezewa kutoka nje, lakini ni hali ya asili ya Mungu Mwenyewe. Na kwa hivyo uhusiano kati ya Muumba na viumbe hauwezi katu kubadilishwa. Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkubwa au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndiyo shabaha pekee ambayo watu wote wanafaa kufuatilia.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp