Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri

07/09/2019

Kwa kuielewa mifano hii ya unenaji wa Mungu, fikira na vitendo vya Mungu, je, unaweza kuielewa tabia ya haki ya Mungu, tabia isiyoweza kukosewa? Mwishowe, hii ni dhana ya tabia ya kipekee kwa Mungu Mwenyewe, bila ya kujali ni kiwango kipi ambacho binadamu anaweza kuelewa. Mungu kutoweza kuvumilia kosa ndicho kiini Chake cha kipekee; hasira ya Mungu ndiyo tabia Yake ya kipekee; adhama ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya kipekee. Kanuni inayoelezea ghadhabu ya Mungu inaonyesha utambulisho na hadhi ambayo Yeye tu ndiye anayemiliki. Mtu hana haja kutaja kwamba ni ishara pia ya hali halisi ya Mungu Mwenyewe wa kipekee. Tabia ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya asili. Haibadiliki kamwe na kupita kwa muda, wala haibadiliki kila wakati mahali panapobadilika. Tabia Yake ya asili ndiyo kiini Chake halisi cha kweli. Haijalishi ni nani anayetekelezea kazi Yake, hali Yake halisi haibadiliki, na wala tabia ya haki Yake pia. Wakati mtu anapomghadhibisha Mungu, kile Anachomshushia ni tabia Yake ya asili; wakati huu kanuni inayoelezea ghadhabu Yake haibadiliki, wala utambulisho na hadhi Yake ya kipekee. Haghadhibishwi kwa sababu ya mabadiliko katika hali Yake halisi au kwa sababu ya tabia Yake kusababisha dalili tofauti, lakini kwa sababu upinzani wa binadamu dhidi Yake huikosea tabia Yake. Uchochezi waziwazi wa binadamu kwa Mungu ni changamoto kubwa katika utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu. Kwa mtazamo wa Mungu, wakati binadamu anapompinga Yeye, binadamu huyo anashindana na Yeye na anampima ghadhabu Yake. Wakati binadamu anapompinga Mungu, wakati binadamu anaposhindana na Mungu, wakati binadamu anapojaribu kila mara ghadhabu ya Mungu—na ndio maana pia dhambi huongezeka—hasira ya Mungu itaweza kufichuka kwa kawaida na kujitokeza yenyewe. Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitasita kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote katili zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu. Wakati heshima na utakatifu wa Mungu vinapopata changamoto, wakati nguvu za haki zinapata kuzuiliwa na hazionekani na binadamu, Mungu atashusha hasira Yake. Kwa sababu ya hali halisi ya Mungu, nguvu hizo zote ulimwenguni zinazoshindana na Mungu, zinazompinga Yeye na kushindana na Yeye ni za maovu, kupotoka na kutokuwa na dhalimu; zinatoka Kwake na zinamilikiwa na Shetani. Kwa sababu Mungu ni wa haki, wa nuru na mtakatifu bila dosari, vitu vyote viovu, vilivyopotoka na vinavyomilikiwa na Shetani vitatoweka baada ya kuachiliwa kwa hasira ya Mungu.

Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri

Ingawaje kumwagwa kwa hasira ya Mungu ni dhana ya maonyesho ya tabia ya haki Yake, hasira ya Mungu kwa vyovyote vile haibagui walengwa wake au haina kanuni. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu si mwepesi wa ghadhabu, wala Hakimbilii kufichua hasira Yake na adhama Yake. Aidha, hasira ya Mungu inadhibitiwa na kupimwa kwa kiwango fulani; hailinganishwi kamwe na namna ambavyo binadamu atakavyowaka kwa hasira kali au kutoa ghadhabu zake. Mazungumzo mengi kati ya binadamu na Mungu yamerekodiwa kwenye Biblia. Maneno ya baadhi ya watu hawa binafsi yalikuwa ya juujuu, yasiyo na ujuzi na yasiyofaa, lakini Mungu hakuwaangusha chini, wala Hakuwashutumu. Hususan, wakati wa majaribio ya Ayubu, je, Yehova Mungu aliwachukuliaje marafiki watatu wa Ayubu na wale wengine baada ya kusikia maneno waliyomzungumzia Ayubu? Je, Aliwashutumu? Je, Aligeuka na kushikwa na hasira kali kwao? Hakufanya kitu kama hicho! Badala yake Alimwambia Ayubu kuwasihi, kuwaombea; Mungu, kwa mkono mwingine, hakuchukua lawama zao na kutia moyoni. Matukio haya yote yanawakilisha mtazamo mkuu ambao Mungu anashughulikia binadamu waliopotoka, na wasiojua. Kwa hivyo, kushushwa kwa hasira ya Mungu si kwa vyovyote vile maonyesho au hali ya kutoa nje hali Yake ya moyo. Hasira ya Mungu si mlipuko mkubwa wa hasira kali kama vile binadamu anavyoielewa. Mungu hawachilii hasira Yake kwa sababu hawezi kuidhibiti hali ya moyo Wake binafsi au kwa sababu ghadhabu Yake imefikia kilele na lazima itolewe. Kinyume cha mambo ni kwamba, hasira Yake ni maonyesho ya tabia ya haki Yake na maonyesho halisi ya tabia ya haki Yake; ni ufunuo wa ishara ya hali Yake halisi takatifu. Mungu ni hasira, asiyevumilia kosa—hivi si kusema kwamba ghadhabu ya Mungu haitofautishi sababu za kufanya hivyo au haifuati kanuni; ni binadamu uliopotoka ambao unafuata mkondo wa kipekee wa kutokuwa na kanuni, mlipuko wa hasira kali bila mpango usiotofautisha hali hii miongoni mwa sababu mbalimbali. Mara tu binadamu anapokuwa na hadhi, mara nyingi atapata ugumu wa kudhibiti hali ya moyo wake, na kwa hivyo atafurahia kutumia nafasi mbalimbali kueleza kutotosheka kwake na kutoa nje hisia zake; mara nyingi atawaka kwa hasira kali bila sababu yoyote, ili kuonyesha uwezo wake na kuwafanya wengine kujua kwamba hadhi yake na utambulisho wake ni tofauti na ule wa watu wa kawaida. Bila shaka, watu waliopotoka wasiokuwa na hadhi yoyote mara kwa mara pia watapoteza udhibiti wao. Ghadhabu yao mara nyingi husababishwa na uharibifu wa manufaa yao ya kibinafsi. Ili kulinda hadhi yake binafsi na heshima, mwanadamu aliyepotoka mara kwa mara atatoa nje hisia zake na kufichua asili yake yenye kiburi. Binadamu atalipuka kwa ghadhabu na kutoa nje hisia zake ili kutetea na kushikilia uwepo wa dhambi, na matendo haya ndiyo njia ambayo kwayo binadamu anaonyesha kutotosheka kwake; yamejaa dosari, mifumo na mbinu mbalimbali, kupotoka na maovu ya binadamu, na zaidi ya chochote kingine, yanajaa kwa malengo na matamanio ya binadamu. Wakati haki inaposhindana na maovu, binadamu hataruka juu kwa ghadhabu ili kutetea uwepo wa haki; kinyume ni kwamba, wakati nguvu za haki zinatishwa, zinateswa na kushambuliwa, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutotilia maanani, kukwepa, au kushtuka. Hata hivyo, wakati anapokabiliwa na nguvu za maovu, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutunza, na kunyenyekea mno. Hivyo basi, kutoa nje ghadhabu kwa binadamu ni kimbilio la nguvu za maovu, maonyesho ya mwenendo wa maovu uliokithiri na usiositishwa wa binadamu wa kimwili. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, hata hivyo, nguvu zote za maovu zitasitishwa; dhambi zote za kudhuru binadamu zitasitishwa; nguvu zote katili zinazozuia kazi ya Mungu zitawekwa wazi, zitatenganishwa na kulaaniwa; washirika wote wa Shetani ambao wanampinga Mungu wataadhibiwa, na kuondolewa. Badala yake, kazi ya Mungu itaendelea huru bila vizuizi vyovyote; mpango wa usimamizi wa Mungu utaendelea kuimarika hatua kwa hatua kulingana na utaratibu uliopo; watu walioteuliwa na Mungu watakuwa huru dhidi ya kusumbuliwa na Shetani na kudanganywa; wale wanaomfuata Mungu watafurahia uongozi na ujazo wa Mungu miongoni mwa mazingira yenye utulivu na amani. Hasira ya Mungu ni usalama unaozuia nguvu zote za maovu dhidi ya kuzidishwa na kutapakaa kwa nguvu, na pia ni usalama unaolinda kuwepo na kuenea kwa mambo yote ya haki na mazuri na daima dawamu unayalinda mambo haya dhidi ya kukandamizwa na kuangamizwa.

Unaweza kuona hali halisi ya hasira ya Mungu katika kuangamiza Kwake kwa Sodoma? Je, kuna jambo lolote lililochanganyika kwenye hasira Yake kali? Je, hasira kali ya Mungu ni safi? Ili kutumia maneno ya binadamu, je, hasira kali ya Mungu imetiwa najisi? Je, kunayo hila yoyote katika hasira Yake? Je, kunayo njama yoyote? Je, zipo siri zozote zisizotamkika? Ninaweza kukwambia wazi na kwa makini: Hakuna sehemu ya hasira ya Mungu inayoweza kumwongoza mtu kwa shaka. Ghadhabu yake haina kasoro, ni hasira ambayo haijatiwa najisi na haijasheheni nia au shabaha zozote zingine. Sababu ya ghadhabu Yake ni safi, haina lawama na haipingiki. Ni ufunuo wa kawaida na onyesho la hali Yake halisi ya utakatifu; ni kitu ambacho hakuna kiumbe chochote kinamiliki. Hii ni sehemu ya tabia ya kipekee ya haki ya Mungu, na ni tofauti ya wazi kati ya hali halisi husika ya Muumba na uumbaji Wake.

Haijalishi kama mtu anakuwa na ghadhabu akiwa mbele ya wengine au wakiwa hawako naye, kila mtu anayo nia na kusudi tofauti. Pengine wanajenga heshima zao, au pengine wanatetea masilahi yao binafsi, na kuendeleza taswira yao au kulinda sura yao. Baadhi yao huendeleza hali ya kuzuia ghadhabu yao, huku nao wengine wanakimbilia na wanapandwa na hasira kali kila wanapopenda bila ya hata kiwango kidogo zaidi cha kujizuia. Kwa ufupi, ghadhabu ya binadamu inatokana na tabia yake iliyopotoka. Haijalishi kusudi lake, ni la mwili na ni la asili; halina uhusiano wowote na haki au ukiukaji wa haki kwa sababu hakuna kitu katika asili ya binadamu na hali halisi vinavyolingana na ukweli. Kwa hivyo, hasira ya binadamu wapotovu na hasira ya Mungu vyote havifai kutajwa kwa kiwango sawa. Bila ya kuacha, tabia ya binadamu iliyopotoshwa na Shetani inaanza kwa tamanio la kusalimisha kupotoka, na inatokana na kupotoka; hivyo basi, ghadhabu ya binadamu haiwezi kutajwa kwa kiwango sawa na hasira ya Mungu, haijalishi ni bora namna gani kinadharia. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake kali, nguvu za giza zinakaguliwa, mambo ya giza yanaangamizwa, huku mambo ya haki na mazuri yakifurahia utunzaji wa Mungu, ulinzi, na yote yanaruhusiwa kuendelea. Mungu hushusha hasira Yake kwa sababu ya mambo dhalimu, mabaya na ya giza, yanayozuia, yanayotatiza au kuangamiza shughuli na maendeleo ya kawaida ya mambo ya haki na mazuri. Shabaha ya ghadhabu ya Mungu si kusalimisha hadhi na utambulisho Wake binafsi, lakini kusalimisha uwepo wa mambo ya haki, mazuri, ya kupendeza na kuvutia, kusalimisha sheria na mpangilio wa kuwepo kwa kawaida kwa binadamu. Hiki ndicho chanzo asilia cha hasira ya Mungu. Hasira kali ya Mungu ni bora sana, ya kiasili na ufunuo wa kweli wa tabia Yake. Hakuna makusudi yoyote katika hasira Yake kali, wala hakuna udanganyifu au njama yoyote; au hata zaidi, hasira Yake kali haina tamanio lolote, ujanja, mambo ya kijicho, udhalimu, maovu, au kitu kingine ambacho binadamu wote waliopotoka huwa navyo. Kabla ya Mungu kushusha hasira Yake kali, huwa tayari Ametambua hali halisi ya kila suala kwa uwazi na ukamilifu zaidi, na huwa tayari Amepangilia ufafanuzi na hitimisho sahihi na zilizo wazi. Hivyo basi, lengo la Mungu katika kila suala Analofanya ni wazi kabisa, vile ulivyo mtazamo Wake. Yeye si mtu aliyechanganyikiwa; Yeye si kipofu; Yeye si mtu wa kuamua ghafla; Yeye si mzembe; na zaidi, Yeye si mtu asiyefuata kanuni. Hii ndiyo dhana ya kimatendo ya hasira ya Mungu, na ni kwa sababu ya dhana hii ya kimatendo ya hasira ya Mungu ambapo binadamu umefikia uwepo wake wa kawaida. Bila ya hasira ya Mungu, binadamu ungeishia kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida; viumbe vyote vyenye haki, virembo na vizuri vingeangamizwa na kusita kuwepo. Bila ya hasira ya Mungu, sheria na amri za kuwepo kwa viumbe vingekiukwa au hata kupinduliwa kabisa. Tangu uumbwaji wa binadamu, Mungu ametumia bila kusita, tabia Yake ya haki kusalimisha na kuendeleza uwepo wa kawaida wa binadamu. Kwa sababu tabia Yake ya haki inayo hasira na adhama, watu wote waovu, vitu, vifaa na vitu vyote vinavyotatiza na kuharibu uwepo wa kawaida wa binadamu vinaadhibiwa, vinadhibitiwa na kuangamizwa kwa sababu ya hasira Yake. Kwenye milenia mbalimbali zilizopita, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki kuangusha na kuangamiza kila aina za roho chafu na za giza ambazo zinampinga Mungu na kuchukua nafasi ya wasaidizi na watumishi wa Shetani katika kazi ya Mungu ya kusimamia binadamu. Hivyo basi, kazi ya Mungu ya wokovu wa binadamu siku zote imeimarika kulingana na mpango Wake. Hivi ni kusema kwamba kwa sababu ya uwepo wa hasira ya Mungu, sababu za haki zaidi za binadamu hazijawahi kuangamizwa.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mungu Lazima Aangamize Sodoma

Mwa 18:26 Na Yehova akasema, Nikipata katika Sodoma watu hamsini wenye haki ndani ya mji huo, basi nitaacha pahali pote kwa sababu yao. Mwa...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp