Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato (Sehemu 2)

01/03/2021

Kisha, hebu tuangalie sentensi ya mwisho katika dondoo hii ya maandiko: “Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.” Je, kunao upande wa utendaji kwa sentensi hii? Je, unaweza kuona upande wa utendaji kwa sentensi hii? Kila kitu anachosema Mungu kinatoka moyoni Mwake, kwa hivyo kwa nini Alisema hivi? Unaielewa vipi sentensi hii? Unaweza kuelewa maana ya sentensi hii sasa, lakini wakati huo si watu wengi walikuwa wanaielewa kwa sababu binadamu alikuwa tu ametoka katika Enzi ya Sheria. Kwao, kutoka katika Sabato lilikuwa jambo gumu sana kufanya, sembuse kuelewa Sabato ya kweli ilikuwa nini.

Sentensi “Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.” inawaambia watu kwamba kila kitu cha Mungu ni visivyo vya mwili, na ingawa Mungu anaweza kukupa mahitaji yako yote ya kimwili, punde tu mahitaji yako yote ya mwili yametimizwa, utoshelevu unaotokana na mambo haya unaweza kuchukua nafasi ya ufuatiliaji wako wa ukweli? Kwa kweli hiyo haiwezekani! Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho ambayo tumeweza kushiriki pamoja ni kweli. Haiwezi kupimwa kupitia kwa gharama ya juu ya vifaa vya kimwili wala thamani yake kupimwa kwa pesa, kwa sababu si kifaa cha anasa, na kinatoa mahitaji ya moyo wa kila mmoja. Kwa kila mmoja, thamani ya ukweli huu usioshikika inafaa kuwa kubwa zaidi kuliko thamani ya vitu vyovyote vya anasa unavyofikiria kuwa ni vizuri, sivyo? Kauli hii ni kitu mnachohitaji kukiwazia. Hoja kuu ya kile nilichosema ni kwamba kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho na kila kitu cha Mungu ndivyo vitu muhimu zaidi kwa kila mtu na haviwezi kubadilishwa na kifaa chochote cha anasa. Nitakupa mfano: Ukiwa na njaa, unahitaji chakula. Chakula hiki kinaweza kuwa kizuri kwa kiasi fulani au kinaweza kuwa kimekosa kitu fulani kwa kiasi fulani, lakini mradi tu umekula ukashiba, hisia ile mbaya ya kuwa na njaa haitakuwepo tena—itakuwa imeondoka. Unaweza kuketi pale kwa amani, na mwili wako utakuwa umepumzika. Njaa ya watu inaweza kutatuliwa kwa chakula, lakini ukiwa unamfuata Mungu na kuhisi kwamba huna ufahamu wowote Wake, unawezaje kutatua utupu huu katika moyo wako? Hali hii inaweza kusuluhishwa kwa chakula? Au unapomfuata Mungu na huelewi mapenzi Yake, ni nini unachoweza kutumia ili kufidia ile njaa katika moyo wako? Katika mchakato wa uzoefu wako wa wokovu kupitia kwa Mungu, wakati ukifuatilia mabadiliko katika tabia yako, kama huelewi mapenzi Yake au hujui ukweli ni nini, kama huelewi tabia ya Mungu, huhisi wasiwasi sana? Huhisi njaa na kiu kuu katika moyo wako? Je, hizi hisia hazikuzuii dhidi ya kuhisi pumziko katika moyo wako? Hivyo basi unaweza kufidia vipi njaa hiyo katika moyo wako—kunayo njia ya kutatua suala hilo? Baadhi ya watu huenda kufanya ununuzi, baadhi hupata rafiki wa kuwaambia yaliyo moyoni, baadhi hulala mpaka watosheke, wengine husoma zaidi maneno ya Mungu, au wakatia bidii zaidi na kutumia jitihada nyingi zaidi kukamilisha wajibu wao. Je, mambo haya yanaweza kutatua ugumu wako halisi? Nyinyi nyote mnaelewa kikamilifu aina hizi za mazoea. Unapohisi kuwa huna nguvu, unapohisi tamanio kubwa la kupata nuru kutoka kwa Mungu ili kukuruhusu kujua uhalisi wa ukweli na mapenzi Yake, ni nini unachohitaji kingi zaidi? Kile unachohitaji si mlo kamili, na wala si maneno machache mema. Zaidi ya hayo, si lile tulizo na kutosheka kwa muda kwa mwili—kile unachohitaji ni Mungu kuweza kukueleza moja kwa moja, kwa wazi kile unachofaa kufanya na namna unavyofaa kukifanya, kuweza kukuonyesha wazi ukweli ni nini. Baada ya kuelewa haya, hata kama ni sehemu ndogo tu, huhisi kuwa umetosheka zaidi katika moyo wako kuliko vile ambavyo ungekuwa umekula mlo mzuri? Wakati moyo wako umetosheka, huo moyo wako, nafsi yako nzima, havipati pumziko la kweli? Kutokana na mfano huu na uchambuzi, je, mnaelewa sasa ni kwa nini Nilitaka kusemezana na nyinyi kuhusu sentensi hii, “Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato”? Maana yake ni kwamba kile kinachotoka kwa Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na kila kitu Chake vyote ni vikuu zaidi kuliko kitu kingine chochote, kikiwemo kile kitu au yule mtu ambaye uliwahi kuamini kuwa unamthamini zaidi. Hivyo ni kusema, kama mtu hawezi kupata maneno kutoka katika kinywa cha Mungu au kama haelewi mapenzi Yake, hawezi kupata pumziko. Katika yale mtakayopitia katika siku zako za usoni, mtaelewa ni kwa nini Nilitaka nyinyi kuona dondoo hii leo—hii ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya ni ukweli na maisha. Ukweli kwa mwanadamu ni kitu ambacho hawawezi kukosa katika maisha yao, kitu ambacho hawawezi kuishi bila; unaweza pia kusema kwamba ndicho kitu kikuu zaidi. Ingawa huwezi kukiangalia au kukigusa, umuhimu wake kwako hauwezi kupuuzwa; ndicho kitu cha pekee kinachoweza kukuletea pumziko moyoni mwako.

Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato (Sehemu 2)

Je, ufahamu wenu wa ukweli umefungamana na hali yenu ya kibinafsi? Katika maisha halisi, lazima kwanza ufikirie ukweli upi unahusiana na watu, matukio, na vitu ambavyo umekumbana navyo; ni miongoni mwa ukweli huu ndimo unaweza kupata mapenzi ya Mungu na kuunganisha kile ulichokumbana nacho na mapenzi Yake. Iwapo hujui ni vipengele vipi vya ukweli vinavyohusiana na mambo ambayo umekumbana nayo lakini badala yake unaenda kwa njia ya moja kwa moja kutafuta mapenzi ya Mungu, huu ni mtazamo ambao hauna mwelekeo ambao hauwezi kufanikisha matokeo. Kama unataka kutafuta ukweli na kuelewa mapenzi ya Mungu, kwanza unahitaji kuangalia ni mambo ya aina gani ambayo yametendeka kwako, ni vipengele vipi vya ukweli ambavyo mambo hayo yana uhusiano navyo, na kisha uutafute ukweli maalum katika neno la Mungu ambalo linahusiana na kile ulichopitia. Kisha utafute njia ya matendo ambayo ni sahihi kwako katika ukweli huo; kutokana na njia hii unaweza kupata ufahamu usio wa moja kwa moja kuhusu mapenzi ya Mungu. Kutafuta na kutenda ukweli si kutumia kanuni au kufuata fomyula bila kufikiria. Ukweli si wa kifomyula, wala si sheria. Haujakufa—ni uzima wenyewe, ni kitu ambacho kina uhai, na ni kanuni ambayo lazima kilichoumbwa kifuate katika Maisha na kanuni ambayo lazima mwanadamu awe nayo katika maisha yake. Hiki ni kitu ambacho lazima, kwa vyoyote vile, uelewe kupitia uzoefu. Haijalishi ni katika awamu gani ambayo umeifikia katika uzoefu wako, huwezi kutenganishwa na neno la Mungu au ukweli, na kile unachoelewa kuhusu tabia ya Mungu na kile unachojua kuhusu kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho ni vitu ambavyo vimeonyeshwa vyote katika maneno ya Mungu; vimeungana kabisa na ule ukweli. Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho mwenyewe ni ukweli kwa njia yake; ukweli ni dhihirisho halisi la tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Unafanya kile Mungu Alicho nacho kuonyesha waziwazi kile Mungu alisema; unakuonyesha moja kwa moja kile ambacho Mungu hapendi, kile ambacho Hapendi, kile Anachokutaka ufanye na kile ambacho Hakuruhusu ufanye, watu ambao Anawachukia na watu ambao Anawafurahia. Katika ule ukweli ambao Mungu anaonyesha watu wanaweza kuona furaha, hasira, huzuni, na shangwe Yake, pamoja na kiini Chake—huu ndio ufichuzi wa tabia Yake. Mbali na kujua kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na kuelewa tabia Yake kutoka katika neno Lake, kile kilicho muhimu zaidi ni haja ya kufikia ufahamu huu kupitia kwa uzoefu wa kimatendo. Kama mtu atajiondoa katika maisha halisi ili kumjua Mungu, hataweza kutimiza hayo. Hata kama kuna watu wanaoweza kupata ufahamu fulani kutoka katika neno la Mungu, ufahamu wao umewekewa mipaka ya nadharia na maneno, na kunatokea tofauti na vile ambavyo Mungu alivyo mwenyewe kwa kweli.

Kile tunachozungumzia sasa kimo ndani ya ule upana wa hadithi zilizorekodiwa katika Biblia. Kupitia katika hadithi hizi, na kupitia uchambuzi wa mambo haya yaliyofanyika, watu wanaweza kuelewa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho ambayo Ameonyesha, na kuwaruhusu kujua kila kipengele cha Mungu kwa upana zaidi, kwa kina zaidi, kikamilifu, na kwa undani zaidi. Hivyo basi, njia pekee ya kujua kila kipengele cha Mungu ni kupitia hadithi hizi? La, siyo! Kwani kile Mungu anachosema na kazi Anayofanya katika Enzi ya Ufalme kinaweza kuwasaidia watu kwa njia bora zaidi kujua tabia Yake, na kuijua kikamilifu. Hata hivyo, Nafikiri ni rahisi zaidi kujua tabia ya Mungu na kuelewa kile Alicho nacho na kile Alicho kupitia baadhi ya mifano au hadithi zilizorekodiwa katika Biblia ambazo watu wamezoeana nazo. Nikichukua maneno ya hukumu na kuadibu na ukweli ambao Mungu anaonyesha leo ili kukufanya umjue Yeye neno kwa neno, utahisi kwamba haipendezi sana inachosha mno, na baadhi ya watu hata watahisi kwamba maneno ya Mungu yanaonekana kuwa yanafuata fomyula fulani. Lakini tukichukulia hadithi hizi za Biblia kama mifano ya kuwasaidia watu kujua tabia ya Mungu, basi haitaonekana kuwa ya kuchosha. Unaweza kusema kwamba katika mkondo wa kuonyesha mifano hii, maelezo ya kile kilichokuwa moyoni mwa Mungu wakati huo—hali Yake ya moyo au hisia Zake za moyoni, au fikira na mawazo Yake—vimesimuliwa kwa watu katika lugha za kibinadamu, na lengo la haya yote ni kuwaruhusu kushukuru, kuhisi kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho na kujua kwamba si fomula. Si hadithi ya kale, au kitu ambacho watu hawawezi kuona wala kugusa. Ni kitu ambacho kwa kweli kipo ambacho watu wanaweza kuhisi, na kufahamu. Hili ndilo lengo la msingi. Unaweza kusema kwamba watu wanaoishi katika enzi hii wamebarikiwa. Wanaweza kuzitumia hadithi za Biblia kupata ufahamu mpana zaidi wa kazi za awali za Mungu; wanaweza kuiona tabia Yake kupitia katika kazi ambayo Amefanya. Na wanaweza kuelewa mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu kupitia kwa tabia hizi ambazo Ameonyesha, kuelewa maonyesho yale thabiti ya utakatifu Wake na utunzaji Wake kwa binadamu ili kuweza kufikia maelezo zaidi na maarifa ya kina zaidi kuhusu tabia ya Mungu. Naamini kwamba nyinyi nyote mnaweza kuhisi haya yote!

Ndani ya upana wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha katika Enzi ya Neema, unaweza kuona kipengele kingine cha kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho. Kilionyeshwa kupitia kwa mwili Wake, na kikawezeshwa kwa watu kuiona na kufahamu zaidi kupitia kwa ubinadamu Wake. Ndani ya Mwana wa Adamu, watu waliweza kuona namna ambavyo Mungu katika mwili alivyoishi kwa kudhihirisha ubinadamu Wake, na wakaona uungu wa Mungu ulioonyeshwa kupitia kwa mwili. Aina hizi mbili za maonyesho ziliwaruhusu watu kuweza kumwona Mungu aliye halisi sana, na kuwaruhusu kuwa na dhana tofauti ya Mungu. Hata hivyo, katika kipindi cha muda kati ya uumbaji wa ulimwengu na mwisho wa Enzi ya Sheria, yaani, kabla ya Enzi ya Neema, kile kilichoonekana, kilichosikizwa, na kupitiwa na watu kilikuwa tu kipengele kitakatifu cha Mungu. Kilikuwa kile ambacho Mungu alifanya na kusema katika himaya ile isiyoshikika, na mambo ambayo Aliyaonyesha kutoka katika nafsi Yake halisi ambayo yasingeweza kuonekana au kuguswa. Mara nyingi, mambo haya yaliwafanya watu kuhisi kwamba Mungu alikuwa mkubwa sana, na kwamba wasingeweza kusonga karibu na Yeye. Picha ambayo Mungu kwa kawaida aliwapa watu ilikuwa kwamba Alionekana akipotea, na watu walihisi hata kwamba kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake yalikuwa yenye mafumbo mno na yasiyoeleweka mno kiasi kwamba hakukuwa na njia ya kuyafikia, isitoshe hata kujaribu kuelewa na kuyashukuru. Kwa watu, kila kitu kuhusu Mungu kilikuwa cha mbali—mbali mno kiasi kwamba watu wasingeweza kukiona, wasingeweza kukigusa. Ilionekana Alikuwa juu katika mbingu, na ilionekana kwamba Hakukuwepo kamwe. Hivyo basi kwa watu, kuelewa moyo na akili ya Mungu au kufikiria Kwake kokote kusingeweza kutimizika, na hata kufikika. Ingawa Mungu alitenda kazi fulani thabiti katika Enzi ya Sheria, na Akaweza kutoa pia maneno fulani na kuonyesha tabia fulani mahususi ili kuwaruhusu watu kushukuru na kuona maarifa halisi fulani kumhusu, bado hatimaye, hilo lilikuwa ni maonyesho ya Mungu kuhusu Alicho nacho na kile Alicho katika ulimwengu usioshikika, na kile watu walielewa, kile walichojua kilikuwa bado kile cha kipengele takatifu kuhusu kile Alicho nacho na kile Alicho. Mwanadamu asingeweza kupata dhana thabiti kutoka kwa kile Alicho nacho na kile Alicho, na ile picha waliyokuwa nayo kuhusu Mungu ilikuwa bado ndani ya mawanda ya “mwili wa kiroho” ulio mgumu kukaribia, unaoonekana na kupotea ndani na nje ya mtazamo.” Kwa sababu Mungu hakutumia kifaa mahususi au taswira katika ulimwengu wa kimwili kuonekana kwa watu, bado wasingeweza kumfafanua Yeye kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Katika mioyo na akili za watu, siku zote walitaka kutumia lugha yao binafsi ili kuanzisha kiwango kwa ajili ya Mungu, kumfanya Agusike na kumfanya Awe binadamu, kama vile Alikuwa mrefu kiasi gani, Alikuwa mkubwa kiasi gani, Alifanana vipi, Anapenda nini hasa na hulka Yake mahususi ni gani. Kwa kweli, moyoni Mwake Mungu alijua kwamba watu walifikiria hivyo. Alikuwa wazi sana kuhusu mahitaji ya watu, na bila shaka Alijua pia kile Alichofaa kufanya, hivyo basi Alitenda kazi Yake kwa njia tofauti na Enzi ya Neema. Njia hii ilikuwa takatifu na vilevile iliyostaarabishwa. Katika kipindi cha Muda ambacho Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi, watu wangeweza kuona kwamba Mungu alikuwa na maonyesho mengi ya kibinadamu. Kwa mfano, Aliweza kucheza, Aliweza kuhudhuria harusi, Aliweza kuwasiliana kwa karibu na watu, kuongea na wao, na kujadili mambo pamoja nao. Aidha, Bwana Yesu aliweza pia kukamilisha kazi nyingi zilizowakilisha uungu Wake, na bila shaka kazi Yake yote ilikuwa ni maonyesho na ufichuzi wa tabia ya Mungu. Katika kipindi hiki, wakati uungu wa Mungu ulitambuliwa kupitia kwa mwili wa kawaida ambao watu wangeweza kuona na kugusa, hawakuhisi tena kwamba Alikuwa akionekana na kutoweka, na kwamba wangeweza kumkaribia. Kinyume cha mambo ni kwamba, wangejaribu kuelewa mapenzi ya Mungu au kuuelewa uungu Wake kupitia kila hatua, maneno, na kazi ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Mungu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hili liliwapa watu fursa ya kukumbana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa binadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukubwa Wake katikati ya unyenyekevu, vilevile na kupata ufahamu wa mwanzo na ufafanuzi wa mwanzo wa uhalali na uhalisi wa Mungu. Hata ingawa kazi iliyokamilishwa na Bwana Yesu, njia Zake za kufanya kazi, na mitazamo ambayo kutoka kwayo Aliongea ilitofautiana na ile ya nafsi halisi ya Mungu katika ulimwengu wa kiroho, kila kitu kumhusu kilimwakilisha kwa kweli Mungu Mwenyewe ambaye binadamu walikuwa hawajawahi kumwona awali—hili haliwezi kukataliwa! Hivi ni kusema, haijalishi ni kwa umbo gani ambalo Mungu huonekana, haijalishi huongea kutoka katika mtazamo upi, au Yeye hukabiliana na binadamu kupitia kwa taswira gani, Mungu hawakilishi chochote isipokuwa Yeye Mwenyewe. Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote—Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote aliyepotoka. Mungu ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kukataliwa.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mfano wa Kondoo Aliyepotea

Mat 18:12-14 Mnafikiri vipi? Iwapo mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi hao tisini na tisa, na kuenda milimani, na...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp