Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake

07/09/2019

Yohana 20:26-29 Na kufuatia siku nane tena wanafunzi wake walikuwa ndani, naye Tomaso alikuwa nao: kisha Yesu akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati, na kusema, Amani iwe nanyi. Kisha akasema kwa Tomaso, nyoosha kidole chako hapa, na uitazame mikono yangu, nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani. Naye Tomaso akajibu na kumwambia, BWANA Wangu na Mungu wangu. Yesu akasema kwake, Tomaso, kwa sababu umeniona, umeamini, wamebarikiwa wale ambao hawajaona, lakini wameamini.

Yohana 21:16-17 Akasema kwake tena mara ya pili, Simioni, mwana wa Yohana, unanipenda mimi? Akasema kwake, Ndiyo, Bwana, unajua kwamba mimi nakupenda. Akasema kwake, Walishe kondoo wangu. Akasema kwake mara ya tatu, Simioni, mwana wa Yohana, Unanipenda Mimi? Petro alisikitika kwa sababu alimwambia mara ya tatu, Unanipenda Mimi? Na akamwambia, Bwana, wewe unajua vitu vyote, unajua kwamba mimi nakupenda. Yesu akamwambia, Walishe kondoo wangu.

Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake

Kile ambacho dondoo hizi zinasimulia ni baadhi ya mambo ambayo Bwana Yesu alifanya na kusema kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka Kwake. Kwanza, hebu tuangalie tofauti zozote kati ya Bwana Yesu kabla na baada ya kufufuka Kwake. Alikuwa bado ni yule yule Bwana Yesu wa siku za kale? Maandiko yanao mstari ufuatao unaomfafanua Bwana Yesu baada ya kufufuka kwake: “Kisha Yesu akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati, na kusema, Amani iwe nanyi.” Ni wazi sana kwamba Bwana Yesu wakati huo hakuwa tena mwili, lakini alikuwa katika umbo la kiroho. Hii ni kwa sababu Alikuwa amepita ile mipaka ya mwili, na wakati ambapo mlango ulifungwa Aliweza bado kuja katikati ya watu na kuwaruhusu wao kumwona Yeye. Hii ndiyo tofauti kubwa zaidi kati ya Bwana Yesu baada ya kufufuka na Bwana Yesu aliyeishi kwa mwili kabla ya kufufuka. Hata ingawa hakukuwa na tofauti yoyote kati ya kutokea kwa ule mwili wa kiroho wa wakati huo na dhihirisho la Bwana Yesu kutoka awali, Yesu katika muda huo alikuwa amekuwa Yesu aliyehisi na kujioa mgeni kwa watu, kwa sababu Alikuwa amekuwa mwili wa kiroho baada ya kufufuka kutoka kwa wafu, na Akilinganishwa na mwili Wake wa awali, mwili huu wa kiroho ulikuwa wa kushangaza na kuchanganya kwa watu zaidi. Hali hii iliunda nafasi kubwa zaidi kati ya Bwana Yesu na watu, nao watu wakahisi katika mioyo yao kwamba Bwana Yesu wa wakati huo alikuwa haeleweki kabisa. Ufahamu na hisia hizi kwa upande wa watu ghafla uliwarudisha katika enzi ya kuamini kwa Mungu ambaye hakuweza kuonekana wala kugusika. Hivyo basi, kitu cha kwanza ambacho Bwana Yesu alifanya baada ya kufufuka Kwake kilikuwa kuruhusu kila mmoja kuweza kumwona, kuthibitisha kuwa yupo, kuthibitisha hoja ya kufufuka Kwake. Kuongezea hayo, hali hiyo ilirejesha uhusiano Wake na watu hadi ule uhusiano Aliokuwa nao Alipokuwa akifanya kazi kupitia kwa mwili, na Alikuwa Kristo ambaye wangeweza kuona na kugusa. Kwa njia hii, mojawapo ya matokeo ni kwamba watu hawakuwa na shaka kwamba Bwana Yesu alikuwa amefufuka kutoka kwa kifo baada ya kusulubishwa msalabani, na hakukuwa na shaka katika kazi ya Bwana Yesu ya kuwakomboa wanadamu. Na matokeo mengine ni kwamba hoja ya Bwana Yesu kujitokeza kwa watu baada ya kufufuka Kwake na kuwaruhusu watu kuweza kumwona na kumgusa Yeye kwa udhabiti kuliweza kuwasalimisha wanadamu katika Enzi ya Neema. Kuanzia wakati huu, watu hawakuweza kurudi katika enzi ya awali, Enzi ya Sheria, kwa sababu ya “kutoweka” au “kuacha na kuondoka” kwa Bwana Yesu lakini wangeendelea mbele, kufuata mafundisho ya Bwana Yesu na kazi Aliyokuwa amefanya. Hivyo basi, awamu mpya katika kazi ya Enzi ya Neema iliweza kufunguliwa rasmi na watu waliokuwa katika sheria walikuja rasmi kutoka katika sheria kuanzia hapo kuenda mbele, na kuingia katika enzi mpya, katika mwanzo mpya. Hizi ndizo maana nyingi za kujitokeza kwa Bwana Yesu kwa wanadamu baada ya kufufuka Kwake.

Kwa sababu Alikuwa mwili wa kiroho, watu waliwezaje kumgusa Yeye na kumwona Yeye? Hii inahusu umuhimu wa kujitokeza kwa Bwana Yesu kwa wanadamu. Je, mlitambua chochote katika dondoo hizi za maandiko? Kwa ujumla miili ya kiroho haiwezi kuonekana wala kuguswa, na baada ya kufufuka, kazi ambayo Bwana Yesu alikuwa amechukua tayari ilikuwa imekamilika. Hivyo basi, kinadharia Hakuwa na haja kabisa ya kurudi katikati ya watu akiwa katika taswira Yake ya asili ili kukutana na wao, lakini kujitokeza kwa mwili wa kiroho wa Bwana Yesu kwa watu kama vile Tomaso kulifanya umuhimu wake kuwa thabiti zaidi, na hali hii iliweza kupenyeza zaidi kwa kina katika mioyo ya watu. Alipomjia Tomaso, alimwacha Tomaso aliyekuwa akishuku kumgusa mkono Wake na kumwambia maneno haya: “Nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani.” Maneno haya, vitendo hivi vyote havikuwa vitu ambavyo Bwana Yesu alitaka kusema na kufanya tu baada ya Yeye kufufuka, lakini yalikuwa mambo Aliyotaka kuyafanya kabla ya kusulubishwa msalabani. Ni wazi kwamba Bwana Yesu ambaye alikuwa hajasulubishwa katika msalaba tayari alikuwa na ufahamu wa watu kama Tomaso. Hivyo basi, tunaweza kuona nini kutokana na haya? Alikuwa angali Bwana Yesu yule yule hata baada ya kufufuka Kwake. Kiini chake kilikuwa hakijabadilika. Kushuku kwa Tomaso hakukuwa kumeanza tu lakini kulikuwa ndani yake muda wote aliokuwa akimfuata Bwana Yesu, lakini Alikuwa Bwana Yesu aliyekuwa amefufuka kutoka kwa kifo na alikuwa amerudi kutoka katika ulimwengu wa kiroho akiwa na taswira Yake asilia, na tabia Yake binafsi, na kwa ufahamu huu wa wanadamu kutoka kwa wakati Wake akiwa mwili, kwa hivyo basi Alienda kumfuta Tomaso kwanza, ili kumfanya Tomaso kugusa mbavu Zake, kumfanya kutoona tu mwili Wake wa kiroho baada ya kufufuka, lakini pia kumruhusu auguse na kuuhisi uwepo wa mwili Wake wa kiroho, na kutupilia mbali kabisa shaka zake. Kabla ya Bwana Yesu kusulubishwa msalabani, Tomaso siku zote alishuku kwamba Yeye ni Kristo, na hakuweza kuamini. Imani yake katika Mungu ilianzishwa tu kwa msingi wa kile ambacho angeweza kuona kwa macho yake, kile ambacho angeweza kugusa kwa mikono yake. Bwana Yesu alikuwa na ufahamu mzuri wa imani ya mtu wa aina hii. Waliamini tu katika Mungu wa mbinguni, na hawakuamini kamwe, na wasingekubali Yule Aliyetumwa na Mungu, au Kristo katika mwili. Ili kufanya yeye kuweza kutambuliwa na kuaminiwa katika uwepo wa Bwana Yesu na kwamba kweli Alikuwa Mungu mwenye mwili, Alimruhusu Tomaso kuunyosha mkono wake na kugusa ubavu Wake. Je, Tomaso alikuwa akishuku kwa njia tofauti kabla na baada ya kufufuka kwa Bwana Yesu? Alikuwa daima akishuku, na mbali na mwili wa kiroho wa Bwana Yesu kujitokeza binafsi kwake na kumruhusu Tomaso kugusa alama za misumari katika mwili Wake, hakuna aliyeweza kutatua shaka zake, na hakuna mtu ambaye angemfanya kuziachilia. Hivyo basi, kuanzia muda ambao Bwana Yesu alimruhusu kuugusa ubavu Wake na kumwacha akihisi uwepo wa alama za misumari, shaka ya Tomaso ikatoweka na akajua kwa kweli kwamba Bwana Yesu alikuwa amefufuka na akatambua na kuamini kwamba Bwana Yesu ndiye aliyekuwa Kristo wa kweli, na kuamini kwamba alikuwa Mungu mwenye mwili. Ingawa wakati huu Tomaso hakushuku tena, alikuwa amepoteza milele fursa ya kukutana na Kristo. Alikuwa amepoteza milele fursa ya kuwa pamoja na Yeye, kumfuata Yeye, na kumjua Yeye. Alikuwa amepoteza fursa ya Kristo kumfanya yeye kuwa mtimilifu. Kuonekana kwa Bwana Yesu na maneno Yake yalitoa hitimisho, na hukumu kuhusiana na imani ya wale ambao walijawa na kutoamini kwingi. Alitumia maneno na vitendo Vyake halisi kuwaambia wale waliokuwa wakishuku, kuwaambia wale ambao waliamini tu katika Mungu aliye juu mbinguni lakini amini hawakumwamini Kristo: Mungu hakuitukuza imani yao, wala Hakuupongeza ufuasi wao uliojawa na shaka. Ile siku waliamini kikamilifu Mungu naye Kristo angeweza tu kufanya hivyo siku ile ambayo Mungu alikuwa akamilishe kazi Yake kuu. Bila shaka, siku hiyo ndiyo iliyokuwa siku ambayo kushuku kwao kulipokea uamuzi. Mwelekeo wao katika Kristo uliamua majaliwa yao, na kushuku kwao katika usumbufu kulimaanisha imani yao haikuwapatia matokeo yoyote, na ugumu wao kulimaanisha matumaini yao yaliambukia patupu. Kwa sababu imani yao katika Mungu aliye mbinguni ilisababishwa na njozi, na kushuku kwao katika Kristo kulikuwa kwa kweli mwelekeo wao wa kweli kwa Mungu, hata ingawa walizigusa alama za msumari kwenye mwili wa Bwana Yesu, imani yao ilikuwa bado bure bilashi na matokeo yao yangeweza tu kufafanuliwa kama kuchota maji na kikapu cha mianzi—yote ni bure bilashi. Kile Bwana Yesu Alichomwambia Tomaso kilikuwa kikisema hivyo waziwazi kwa kila mtu: Yule Bwana Yesu aliyefufuka ndiye Bwana Yesu ambaye mwanzo alikuwa ametumia miaka thelathini na mitatu na nusu akifanya kazi miongoni mwa wanadamu. Ingawa alikuwa amesulubishwa msalabani na kupitia bonde la kivuli cha mauti, alikuwa amepitia kitendo cha kufufuka, kila dhana Yake haikuwa imepitia mabadiliko. Ingawa kwa sasa alikuwa na alama za misumari kwenye mwili Wake, na ingawa Alikuwa amefufuka na kutoka kaburini akitembea, tabia Yake, ufahamu Wake wa wanadamu na nia Zake kwa wanadamu bado zilikuwa hazijabadilika hata kidogo. Pia, Alikuwa akiwaambia watu kwamba Alikuwa ameshuka kutoka kwenye msalaba, ameshinda dhambi, amepata ushindi juu ya ugumu, na akupata ushindi dhidi ya kifo. Alama zile za misumari zilikuwa tu ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani, ithibati ya kuwa sadaka ya dhambi ili kuweza kuwakomboa kwa ufanisi wanadamu wote. Alikuwa akiwaambia watu kwamba tayari Alikuwa ameanza kushughulikia dhambi za wanadamu na Alikuwa amekamilisha kazi Yake ya ukombozi. Aliporudi ili kuwaona wanafunzi Wake, Aliwaambia kwa kuonekana Kwake: “Mimi niko hai, bado Nipo; leo kwa kweli nasimama mbele yenu ili mweze kuniona na kunigusa Mimi. Siku zote nitakuwa na wewe.” Bwana Yesu alitaka pia kutumia mfano huo wa Tomaso kama onyo kwa watu wa siku za usoni: Ingawa unaamini Bwana Yesu, huwezi kumwona wala kumgusa Yeye, na bado, unaweza kubarikiwa kutokana na imani yako ya kweli, na unaweza kumwona Bwana Yesu kupitia kwa imani yako ya kweli; mtu aina hii amebarikiwa.

Maneno haya yaliyorekodiwa katika Biblia ambayo Bwana Yesu aliongea Alipojitokeza kwa Tomaso ni msaada mkubwa kwa watu wote katika Enzi ya Neema. Kuonekana Kwake na maneno Yake kwa Tomaso yamekuwa na athari kubwa kwa vizazi vijavyo, na yatakuwa na umuhimu wa kudumu daima dawamu. Tomaso anawakilisha mtu wa aina ya kuamini Mungu ilhali anamshuku Mungu. Wao wanayo maumbile ya kushuku, wana mioyo isiyoeleweka, wao wenyewe ni wadanganyifu, na hawaamini mambo ambayo Mungu anaweza kukamilisha. Hawaamini katika kudura ya Mungu na utawala Wake, na hawaamini katika Mungu kuwa mwili. Hata hivyo, kufufuka kwa Bwana Yesu kulikuwa ni sawa na kuzabwa kofi katika nyuso zao, na pia kuliwapa fursa ya kugundua ni shaka yao wenyewe, kutambua kushuku kwao binafsi, na kuukubali udanganyifu wao binafsi na hivyo basi kuamini katika kuwepo na kufufuka kwa Bwana Yesu. Kile kilichomfanyikia Tomaso kilikuwa onyo na tahadhari kwa vizazi vijavyo ili watu wengi zaidi waweze kujitahadharisha na ili wasiwe wa kushuku kama Tomaso, na kama wangekuwa hivyo, wangezama katika giza. Ukimfuata Mungu, lakini kama Tomaso, siku zote unataka kuugusa ubavu wa Bwana na kuhisi alama Zake za msumari ili kuthibitisha, ili kuhakikisha, ili kuchambua kama Mungu yupo, basi Mungu atakuacha. Hivyo basi, Bwana Yesu anawahitaji watu wasiwe kama Tomaso, kuamini tu kile wanachoweza kuona kwa macho yao, lakini kuwa bila kasoro, mtu mwaminifu, kutouwa na shaka yoyote dhidi ya Mungu, lakini kumwamini tu na kumfuata Yeye. Mtu wa aina hii amebarikiwa. Hili ni hitaji dogo sana la Bwana Yesu kwa watu, na onyo kwa wafuasi Wake.

Huu ndio mwelekeo wa Bwana Yesu kwa wale waliojaa shaka. Hivyo basi ni nini ambacho Bwana Yesu alimwambia, na ni nini Alichofanya kwa wale ambao wanaweza kuamini kwa uaminifu na kumfuata Yeye? Maswali hayo ndiyo tutakayoyaangalia katika kipindi kifuatacho, kuhusiana na kitu ambacho Bwana Yesu alimwambia Petro.

Katika mazungumzo haya, Bwana Yesu alimwuliza Petro mara kadhaa kuhusu jambo moja: “Simoni, mwana wa Yohana, je, unanipenda?” Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi ambacho Bwana Yesu alihitaji kutoka kwa watu kama vile Petro baada ya kufufuka Kwake, wanaoamini Kristo kwa kweli na kulenga kumpenda Bwana. Swali hili lilikuwa aina fulani ya uchunguzi, na aina fulani ya kuhoji, lakini hata zaidi lilikuwa hitaji na tarajio la watu kama Petro. Aliitumia mbinu hii ya kuuliza maswali ili watu waweze kuwaza na kuwazua kujihusu na kuangalia katika maisha yao wenyewe: Mahitaji ya Bwana Yesu kwa watu ni yapi? Je, nampenda Bwana? Mimi ni mtu anayempenda Mungu? Nafaa vipi kumpenda Mungu? Hata ingawa Bwana Yesu aliuliza tu swali hili kwa Petro, ukweli ni kwamba katika moyo Wake, Alitaka kutumia fursa hii ya kumwuliza Petro ili kuuliza swali la aina hii kwa watu wengi zaidi wanaoutafuta kumpenda Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa Petro alibarikiwa kuwa mwakilishi wa mtu wa aina hii, ili kupokea swali hilo kutoka kwa kinywa cha Bwana Yesu mwenyewe.

Likilinganishwa na “nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani,” ambalo Bwana Yesu alimwambia Tomaso baada ya kufufuka Kwake, Yeye kumwuliza Petro swali mara tatu: “Simioni, mwana wa Yohana, unanipenda mimi?” waruhusu watu kuweza kuhisi kwa njia bora zaidi ule ukali wa mwelekeo wa Bwana Yesu na umuhimu Aliouhisi wakati huu wa kuuliza maswali hayo. Kuhusiana naye Tomaso wa kushuku pamoja na asili yake ya udanganyifu, Bwana Yesu alimruhusu yeye kufikisha mkono wake na kuzigusa zile alama Zake za msumari, jambo ambalo lilimfanya yeye kuamini kwamba Bwana Yesu ndiye aliyekuwa Mwana wa Adamu aliyefufuka na akatambua utambulisho wa Bwana Yesu kama Kristo. Na ingawa Bwana Yesu hakumkemea kwa ukali Tomaso, wala hakuonyesha kwa matamshi hukumu yoyote ilio wazi kwake, Alimjuza kwamba Alimwelewa kupitia kwa hatua za kimatendo, huku pia akionyesha mtazamo Wake na uamuzi wa aina hiyo ya mtu. Mahitaji na matarajio ya Bwana Yesu ya mtu wa aina hiyo hayawezi kuonekana kutokana na kile Alichosema. Kwa sababu watu kama Tomaso hawana katu imani ya ukweli. Mahitaji ya Bwana Yesu kwao yanapatikana tu katika, lakini mwelekeo Alioufichua kwa watu kama Petro ni tofauti kabisa. Hakuhitaji kwamba Petro aunyoshe mkono wake na kuzigusa hizo alama Zake za misumari, wala hakumwambia Petro: “usiwe bila imani, ila mwenye imani.” Badala yake, Alimwuliza Petro kwa kurudia swali lilo hilo. Hili lilikuwa swali la kuchokonoa fikira, na lenye maana ambalo halina budi kumfanya kila mfuasi wa Kristo kuhisi majuto, na woga, lakini pia kuhisi ile hali ya moyo wa wasiwasi, na huzuni ya Bwana Yesu. Na wakati wakiwa katika maumivu na mateso makali, wanaweza kuelewa zaidi wasiwasi wa Bwana Yesu Kristo na utunzaji Wake; wanatambua mafundisho Yake ya dhati na mahitaji makali kuhusu watu wasio na kasoro, waaminifu. Swali la Bwana Yesu linawaruhusu watu kuhisi kwamba matarajio ya Bwana kwa watu yaliofichuliwa kupitia kwa maneno haya mepesi si ya kuamini tu na kumfuata Yeye, lakini kutimiza yote kwa kuwa na upendo, kumpenda Bwana wako, kumpenda Mungu wako. Upendo wa aina hii ni wa utunzaji na utiifu. Ni wanadamu kuishi kwa ajili ya Mungu, kufa kwa ajili ya Mungu, kujitolea kila kitu chao kwa ajili ya Mungu, na kutumia na kutoa kila kitu chao kwa ajili ya Mungu. Upendo wa aina hii pia ni kumpa Mungu tulizo, kumruhusu Yeye kufurahia ushuhuda, na kumruhusu Yeye kupumzika. Ni fidia ya wanadamu kwa Mungu, uwajibikaji wao, na wajibu wao, na ni njia ambayo wanadamu lazima wafuate kwa maisha yao yote. Haya maswali matatu yalikuwa mahitaji na ushawishi ambao Bwana Yesu alitoa kwa Petro na watu wote ambao wangefanywa kuwa watimilifu. Ni maswali haya matatu ndiyo yaliyomwongoza na kumpa motisha Petro kukamilisha njia yake ya maisha, na yalikuwa maswali haya wakati ule wa Bwana Yesu kuondoka ambayo yalimfanya Petro kuanza njia yake ya kufanywa mtimilifu, na yaliyomwongoza, kwa sababu ya upendo wake kwa Bwana, kuutunza moyo wa Bwana, kumtii Bwana, kumpa tulizo Bwana, na kuyatoa maisha yake yote na kila kitu chake chote kwa sababu ya upendo wake.

Katika Enzi ya Neema, kazi ya Mungu ilikuwa kimsingi ya aina mbili ya watu. Wa kwanza alikuwa aina ya aliyeamini Kwake na kumfuata, ambaye angetii amri Zake, ambaye angeweza kuuvumilia msalaba na kuushikilia hadi katika njia ya Enzi ya Neema. Mtu wa aina hii angepata baraka za Mungu na kufurahia neema ya Mungu. Aina ya pili ya mtu alikuwa kama Petro, mtu ambaye angeweza kufanywa kuwa mtimilifu. Hivyo basi, baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alifanya kwanza mambo haya mawili yenye umuhimu sana. Kwanza lilikuwa ni kwa Tomaso, na jingine lilikuwa kwa Petro. Mambo haya mawili yanawakilisha nini? Yanawakilisha nia za kweli za Mungu katika kuwaokoa binadamu? Yanawakilisha uaminifu wa Mungu kwa binadamu? Kazi Aliyoifanya na Tomaso ilikuwa ni kuwapa onyo watu wasiwe wanashuku, lakini kuamini tu. Kazi Aliyofanya na Petro ilikuwa ni kuipatia nguvu imani ya watu kama vile Petro, na kuweka wazi mahitaji ya aina hii ya watu, ili kuonyesha ni shabaha zipi wanafaa kuwa wakifuatilia.

Baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alijitokeza kwa watu aliofikiria walifaa, Akaongea na wao, na kuwapa wao mahitaji, huku akiacha nyuma nia Zake, na matarajio Yake kwa watu. Hivi ni kusema, kama Mungu mwenye mwili, haijalishi kama ulikuwa katika wakati Wake akiwa mwili, au katika mwili wa kiroho baada ya kusulubishwa msalabani na kufufuliwa—haja Yake kwa wanadamu na mahitaji kwa wanadamu hayakubadilika. Alijali kuwahusu wanafunzi hawa kabla ya kufika msalabani; ndani ya moyo Wake, Alikuwa wazi katika hali ya kila mmoja, Alielewa upungufu wa kila mmoja, na bila shaka ufahamu Wake wa kila mtu ulikuwa namna ile ile baada ya Yeye kuaga dunia, kufufuka, na kuwa mwili wa kiroho kama hali ilivyokuwa Alipokuwa katika mwili. Alijua kwamba watu hawakuwa kwa kikamilifu na uhakika kuuhusu utambulisho Wake kama Kristo, lakini katika kipindi Chake akiwa mwili Hakuwa anatoa amri kali kuhusu watu. Lakini baada ya kufufuliwa Alijitokeza kwao, na Akawafanya wawe na hakika kabisa kwamba Bwana Yesu alikuwa amekuja kutoka kwa Mungu, kwamba Alikuwa Mungu mwenye mwili, na Alitumia hoja hiyo ya uwepo Wake na kufufuka Kwake kama maono na motisha kubwa zaidi kwa muda mrefu katika ufuatiliaji wa wanadamu. Kufufuka kwake kutoka kifo hakukuwapa nguvu tu wale wote Waliomfuata, lakini pia kuliweka katika taathira kazi Yake ya Enzi ya Neema miongoni mwa wanadamu, na hivyo basi wokovu wa injili ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema kwa utaratibu ukaenea katika kila pembe ya binadamu. Unaweza kusema kwamba kutokea kwa Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake kulikuwa na umuhimu wowote? Kama ungekuwa Tomaso au Petro wakati huo, na ukumbane na kitu hiki kimoja katika maisha yako ambacho kilikuwa na maana sana, ni athari ya aina gani ambayo kitu hicho kingekuwa nayo kwako? Je, ungeona huu kama msukumo wako katika kumfuata Mungu? Ungeona hali hii kama nguvu endeshi zako wewe kumfuata Mungu, kujaribu kumridhisha Yeye, na kufuatilia upendo wa Mungu katika maisha yako? Ungeweza kutumia jitihada za maisha yako yote ili kueneza maono haya makubwa zaidi? Ungefanya kueneza wokovu wa Bwana Yesu kuwa kazi unayokubali kutoka kwa Mungu? Hata ingawa hamjapitia haya, zile hali mbili za Tomaso na Petro tayari zinatosha kwa watu wa kisasa kuwa na ufahamu wazi kuhusu mapenzi ya Mungu na kumhusu Mungu. Inaweza kusemekana kwamba baada ya Mungu kuwa mwili, baada ya Yeye binafsi kupitia maisha miongoni mwa wanadamu na kuwa na maisha ya binadamu, na baada ya Yeye kuona uharibifu wa tabia wa wanadamu na hali ya maisha ya binadamu, Mungu katika mwili alihisi kwa kina zaidi jinsi mwanadamu alikuwa asiyejiweza, mwenye masikitiko na wa kuonewa huruma. Mungu alipata huruma zaidi kwa hali ya binadamu kwa sababu ya ubinadamu Wake wakati akiishi katika mwili, kwa sababu ya silika Zake katika mwili. Hili lilimsababisha kuwa na wasiwasi mkubwa zaidi juu ya wafuasi Wake. Haya pengine ni mambo ambayo huwezi kuelewa, lakini Naweza kufafanua wasiwasi na utunzaji wa Mungu katika damu kwa kila mmojawapo wa wafuasi Wake kwa kauli hii: kujali kwingi. Hata ingawa kauli hii inatokana na lugha ya binadamu, na hata ingawa ni kauli yenye ubinadamu sana, inaonyesha kwa kweli na kufafanua hisia za Mungu kwa wafuasi Wake. Na kwa kujali kwingi kwa Mungu kwa ajili ya binadamu, kwa mkondo wa yale yote ambayo wewe umeyapitia utaanza kuhisi kwa utaratibu yote haya na kuyaonja. Hata hivyo, hali hii inaweza kutimizwa tu kwa kuelewa kwa utaratibu tabia ya Mungu kwa msingi wa kufuatilia mabadiliko katika tabia yako wewe binafsi. Kuonekana kwa Bwana Yesu kulifanikisha kujali Kwake kwingi kwa minajili ya wafuasi Wake katika ubinadamu na akakupokeza kwa mwili Wake wa kiroho, au unaweza kusema uungu Wake. Kuonekana Kwake kuliwaruhusu watu kuwa na hali nyingine waliyopitia na hisia walizopitia zinazohusu kujali na utunzaji wa Mungu huku kukithibitisha kwa uthabiti kwamba Mungu Ndiye anayefungua enzi, anayeiendeleza enzi, na Yeye ndiye anayetamatisha enzi. Kupitia kwa Kuonekana Kwake Aliipatia nguvu imani ya watu wote, na kupitia kwa Kuonekana Kwake alithibitishia ulimwengu hoja kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hali hii iliwapa wafuasi Wake uthibitisho wa milele, na kupitia kwa Kuonekana Kwake pia Aliweza kufungua awamu ya kazi Yake katika enzi mpya.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp