Kuna tofauti ipi kati ya mtu kutekeleza wajibu wake na kutoa huduma?
Maneno Husika ya Mungu:
Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana. Acha Niwaambie hiki kitu kimoja: Ikiwa mwanadamu anaweza kufanya wajibu wake, inamaanisha kuwa anafanya anachopaswa kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufanya wajibu wake, inaonyesha uasi wake. Kila mara ni katika harakati ya kufanya wajibu wake ndipo mwanadamu polepole anabadilishwa, na ni katika harakati hii ndipo anapoonyesha utiifu wake. Kwa hivyo, kadiri uwezavyo kufanya wajibu wako, ndivyo ukweli utakaopokea unavyoongezeka, na vivyo hivyo mwonekano wako utakuwa halisi zaidi. Wale ambao hufanya tu mambo bila ari yoyote katika kufanya wajibu wao na hawautafuti ukweli mwishowe wataondolewa, kwani watu kama hao hawafanyi wajibu wao katika utendaji wa ukweli, na hawatendi ukweli katika kutekeleza wajibu wao. Watu kama hao ni wale wanaobaki bila kubadilika na watalaaniwa. Misemo yao haijajaa najisi tu, ila wakitamkacho si kingine bali ni uovu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu
Bila kujali vipaji, vipawa, au ujuzi ambavyo watu wanavyo, wakifanya tu mambo na kutumia nguvu zao katika kutimiza wajibu wao; ikiwa, bila kujali wanachofanya, wanategemea mawazo yao, dhana, au silika zao wenyewe; wakionyesha tu nguvu zao, na kutowahi kutafuta mapenzi ya Mungu, na hawana dhana au mahitaji mioyoni mwao yanayosema, “Lazima niweke ukweli katika vitendo. Natenda wajibu wangu”; na ikiwa mawazo yao yanaanza tu na kufanya kazi yao vizuri na kumaliza kazi yao, basi wao ni watu wanaoishi kwa kutegemea vipaji, talanta, uwezo, na ujuzi wao kabisa? Je, kuna watu wengi kama hawa? Katika imani, wanafikiria tu kujitahidi, kuuza kazi yao wenyewe, na kuuza ujuzi wao wenyewe. Ni hasa wakati nyumba ya Mungu inawapa kazi za kawaida kufanya ndipo watu wengi wanayachukulia mambo kwa mtazamo huu. Kila wanachofanya ni kujitahidi. Wakati mwingine hiyo inamaanisha kutumia mdomo wao, wakati mwingine ni kutumia mikono na nguvu za kimwili, na wakati mwingine inamaanisha kwenda huku na huko. Kwa nini inasemekana kuwa kuishi kulingana na mambo hayo ni kutumia nguvu za mtu, na si kuweka ukweli katika vitendo? Mtu anapewa kazi na nyumba ya Mungu, na anapoipata anafikiria tu jinsi ya kukamilisha kazi hii haraka iwezekanavyo ili aweze kutoa maelezo kwa viongozi wa kanisa na kupata sifa zao. Anaweza kubuni mpango wa hatua kwa hatua. Anaonekana kuwa mwenye bidii sana, lakini analenga tu kukamilisha kazi hiyo kwa ajili ya maonyesho, au anapokuwa akiifanya, anajiwekea kiwango chake mwenyewe: jinsi ya kuifanya ili ahisi furaha na mwenye kuridhika, kufikia kiwango cha ukamilifu anachohangaikia. Bila kujali kiwango ambacho anaweka, ikiwa hakuna uhusiano na ukweli, ikiwa hatafuti ukweli ama kutafuta kufahamu na kudhibitisha kile Mungu anachotaka kutoka kwake kabla ya kuchukua hatua, lakini kinyume chake atende bila kufikiri, kwa mshangao, huku ni kujitahidi mwenyewe tu. Anatenda kulingana na matakwa yake mwenyewe, kulingana na ubongo wake au vipaji, au kulingana na uwezo na ujuzi wake mwenyewe. Na matokeo ya kufanya kazi yake namna hii ni yapi? Kazi hiyo inaweza kuwa imekamilika, hakuna mtu anayeweza kuwa amepata makosa yoyote, na unaweza kuhisi furaha sana nayo. Lakini wakati wa kuifanya, kwanza: hukuelewa nia ya Mungu; na pili: hukuifanya kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote—hukuweka moyo wako wote kwayo. Kama ungetafuta kanuni za ukweli, kama ungetafuta mapenzi ya Mungu, basi ungekuwa umefikia asilimia 90% ya matokeo yanayotarajiwa katika kuikamilisha, ungekuwa pia umeweza kuingia katika uhalisi wa ukweli, na ungekuwa umeelewa kwa usahihi kwamba kile ulichokuwa ukifanya kilikuwa kinapatana na mapenzi ya Mungu. Lakini kama ulikuwa na uzembe na usiye mwangalifu, ingawa kazi hiyo ingekuwa imekamilika, moyoni mwako hungekuwa wazi juu ya jinsi ulivyoitekeleza vizuri. Hungekuwa na kigezo, hungejua ikiwa ilikuwa inalingana na mapenzi ya Mungu au la, au ikiwa ilikuwa inalingana na ukweli au la. Kwa hiyo, kila wakati ambapo wajibu unatimizwa katika hali ya aina hii, hili linaweza kutajwa kwa maneno mawili—kujitahidi mwenyewe.
Kila mtu anayemwamini Mungu anapaswa kuelewa mapenzi Yake. Ni wale tu wanaotimiza wajibu wao vizuri ndio wanaweza kumridhisha Mungu, na ni kwa kukamilisha tu kazi ambazo Yeye huwaaminia ndio wao kutimiza wajibu wao kutakuwa sawa kama kawaida. Kuna viwango vya ukamilishaji wa agizo la Mungu. Bwana Yesu alisema: “Wewe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima.” Kumpenda Mungu ni kipengele kimoja cha kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa watu. Kwa kweli, wakati Mungu anawapa watu agizo, wakati wanatimiza wajibu wao kutoka kwa imani yao, viwango ambavyo Anahitaji kwao ni hivi: kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima, na kwa nguvu zako zote. Ikiwa wewe upo lakini moyo wako haupo, ukifikiria juu ya kazi kwa kichwa chako na kuziweka kwenye kumbukumbu, lakini huweki moyo wako ndani yake, na ikiwa unatimiza mambo kwa kutumia uwezo wako, je, huko ni kukamilisha agizo la Mungu? Kwa hiyo ni aina gani ya kiwango ambacho lazima kitimizwe ili utimize wajibu wako vizuri na kukamilisha yale ambayo Mungu amekuaminia, na kutimiza wajibu wako kwa uaminifu? Hiyo ni kufanya kazi yako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima, kwa nguvu zako zote. Ikiwa huna moyo wa kumpenda Mungu, basi hutafaulu katika kujaribu kutekeleza wajibu wako vizuri. Ikiwa upendo wako kwa Mungu hukua thabiti zaidi na halisi zaidi, basi utaweza kutekeleza wajibu wako kwa urahisi kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu yako yote.
Kimetoholewa kutoka katika “Kile Ambacho Watu Wamekuwa Wakitegemea ili Kuishi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo
Kwa watu wengine, bila kujali suala wanalokumbana nalo wanapokuwa wakitimiza wajibu wao, hawatafuti ukweli na daima wanatenda kulingana na dhana, mawazo, fikira na tamaa zao wenyewe. Wao daima huridhisha tamaa zao za binafsi na tabia zao potovu huwa zinaongoza vitendo vyao kila mara. Ingawa wanaweza kukamilisha wajibu waliopewa, hawapati ukweli wowote. Kwa hiyo mtu huyu anategemea nini katika utimizaji wa wajibu wake? Hategemei ukweli na hamtegemei Mungu. Kiasi cha ukweli anachoelewa hakijachukua nafasi kuu moyoni mwake. Anategemea vipaji na uwezo wake, ujuzi ambao amepata na talanta zake, na pia utashi wao wenyewe au nia nzuri ya kuwezesha kazi hiyo kufanyika. Asili ni tofauti, siyo? Ingawa wakati mwingine unaweza kutegemea asili, mawazo, fikira, ujuzi na kujifunza kwako katika kutimiza wajibu wako, hakuna masuala ya kanuni hujitokeza katika mambo unayofanya. Kwa juu inaonekana kana kwamba hujachukua njia mbaya, lakini kuna jambo moja ambalo haliwezi kupuuzwa: Wakati wa mchakato wa kufanya wajibu wako, ikiwa mawazo, fikira na tamaa zako za kibinafsi hazibadiliki kamwe na hazibadilishwi kamwe na ukweli, ikiwa vitendo na matendo yako hayalingani kamwe na kanuni za kweli, basi matokeo ya mwisho yatakuwa nini? Utakuwa mtendaji huduma, na hili ndilo tu lililoandikwa katika Biblia: “Wengi watasema Kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina Lako? Na kutoa mapepo kupitia jina Lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina Lako? Na hapo ndipo Nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni Kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.” Je, kwa nini Mungu huwaita watu hawa ambao huchangia juhudi zao na ambao hutoa huduma “ninyi ambao hutenda udhalimu”? Kuna hoja moja ambayo tunaweza kuwa na uhakika nayo, na hiyo ni kwamba, haijalishi watu hawa wanafanya wajibu upi au ni kazi ipi wanayoifanya, motisha, chanzo, nia na mawazo ya watu hawa yanatokana kabisa na tamaa zao za ubinafsi, yametegemezwa kabisa kwa mawazo yao wenyewe na juu ya masilahi yao ya kibinafsi, na yamelenga kabisa maanani na mipango kama vile kujiheshimu, hadhi na majivuno, na matarajio ya siku za usoni. Hawana ukweli mioyoni mwao, na hawatendi kulingana na kanuni za ukweli. Kwa hivyo, cha muhimu wewe kufuatilia sasa ni nini? (Kutafuta ukweli, na kutenda wajibu wetu kulingana na mapenzi ya Mungu na mahitaji ya Mungu.) Unapaswa kufanya nini hasa, wakati ambapo unatekeleza wajibu wako kulingana na mahitaji ya Mungu? Kuhusiana na nia na mawazo uliyo nayo unapokuwa ukifanya kitu, lazima ujue jinsi ya kutambua kama yanakubaliana na ukweli au la, na kama hayo ni kwa ajili ya matamanio yako ya kibinafsi au kwa ajili ya masilahi ya familia ya Mungu. Ikiwa yanakubaliana na ukweli, basi unaweza kufuata mwelekeo wa mawazo yako kufanya wajibu wako. Ikiwa hayakubaliani na ukweli, basi lazima ugeuke upesi na uachane na njia hiyo. Njia hiyo si sahihi, na huwezi kutenda kwa namna hiyo; ukitenda kwa namna hiyo, basi utakuwa mtu anayeshiriki katika udhalimu.
Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kupitia Maneno ya Mungu katika Wajibu wa Mtu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo
Petro alifanywa mkamilifu kwa kupitia ushughulishaji na usafishaji. Alisema, “Mimi ni lazima nikidhi mapenzi ya Mungu wakati wote. Kwa yote nifanyayo mimi natafuta tu kukidhi mapenzi ya Mungu, na kama mimi ninaadibiwa, au kuhukumiwa, bado nina furaha kufanya hivyo.” Petro alimpa Mungu kila kitu chake, na kazi yake, maneno, na maisha yote yalikuwa yote kwa ajili ya kumpenda Mungu. Alikuwa mtu ambaye alitafuta utakatifu, na alipopitia zaidi, ndivyo upendo wake wa Mungu ndani ya moyo wake ulikuwa mkubwa zaidi. Paulo, wakati huo huo, alifanya tu kazi ya nje, na ingawa alitia bidii katika kazi yake, juhudi zake zilikuwa kwa ajili ya kufanya kazi yake vizuri na hivyo kupata tuzo. Angalijua kuwa hatapokea tuzo, yeye angalikata tamaa katika kazi yake. Kitu ambacho Petro alijali mno ni upendo wa kweli moyoni mwake, na ule ambao ulikuwa wa vitendo na ungeweza kutimizika. Yeye hakujali kuhusu iwapo angepokea tuzo, lakini kuhusu iwapo tabia yake ingebadilishwa. Paulo alijali kuhusu kufanya kazi kwa bidii hata zaidi, yeye alijali kuhusu kazi ya nje na kujitolea, na kuhusu mafundisho ambayo hayashuhudiwi na watu wa kawaida. Yeye hakujali chochote kuhusu mabadiliko ndani yake wala kwa ajili ya upendo wa kweli kwa Mungu. Uzoefu wa Petro ulikuwa kwa ajili ya kupata upendo wa kweli na maarifa ya kweli kuhusu Mungu. Uzoefu wake ulikuwa ili kupata uhusiano wa karibu na Mungu, na kwa kuishi kwa kudhihirisha kwa vitendo. Kazi ya Paulo ilifanywa kwa sababu ya kile alichoaminiwa na Yesu, na ili apate vitu ambavyo alitamani, lakini haya hayakuwa na uhusiano na elimu yake mwenyewe na ya Mungu. Kazi yake ilikuwa tu kwa ajili ya kuepuka kuadibu na hukumu. Kitu ambacho Petro alitafuta kilikuwa ni upendo safi, na Paulo alitafuta taji ya hali ya kuwa mwenye haki. Petro alishuhudia miaka mingi ya kazi ya Roho Mtakatifu, na alikuwa na elimu ya vitendo kuhusu Kristo, na vile vile elimu ya kina kujihusu yeye mwenyewe. Na hivyo, upendo wake wa Mungu ulikuwa safi. Miaka mingi ya usafishaji ilikuwa imeinua elimu yake kuhusu Yesu na maisha, na upendo wake ulikuwa upendo usio na masharti, ulikuwa upendo wa hiari, na hakuagiza chochote akitarajia malipo, na wala hakutumainia kuwa na faida yeyote. Paulo alifanya kazi kwa miaka mingi, ilhali hakumiliki elimu kubwa ya Yesu, na elimu yake ya kibinafsi ilikuwa ndogo mno. Yeye kwa kifupi hakuwa na upendo kwa Kristo, na kazi yake na mwendo ambao alikimbia ilikuwa ili apate heshima na taji la mwisho. Kitu ambacho alitafuta kilikuwa taji zuri kabisa, wala si upendo safi. Yeye hakutafuta kikamilifu, lakini kwa kutoonyesha hisia; hakuwa anatekeleza majukumu yake, lakini alilazimika katika harakati yake baada ya kukamatwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa hivyo, harakati yake haithibitishi kuwa yeye alikuwa kiumbe wa Mungu kilichokuwa na sifa zinazostahili; ilikuwa ni Petro ambaye alikuwa kiumbe wa Mungu aliyekuwa na sifa zilizostahili na ambaye alitekeleza wajibu wake.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea
Kazi ya Paulo inahusiana na utoaji makanisani, na msaada wa makanisa. Kile ambacho Petro alishuhudia ni mabadiliko ya tabia ya maisha yake; alishuhudia upendo kwa Mungu. Kwa kuwa sasa unajua tofauti katika kiini cha kila mmoja wao, unaweza kuona ni nani, hatimaye, kwa kweli alimwamini Mungu, na ni nani ambaye kwa kweli hakumwamini Mungu. Mmoja wao alimpenda Mungu kwa kweli, na mwingine hakumpenda Mungu kwa kweli; mmoja alipitia mabadiliko katika tabia yake, na mwingine hakupitia; mmoja alihudumu kwa unyenyekevu, na hakuonekana na watu kwa urahisi na mwingine aliabudiwa na watu, na alikuwa na picha nzuri; mmoja alitafuta utakatifu, na mwingine hakuutafuta, na ingawa hakuwa najisi, hakuwa amemilikiwa na upendo safi; mmoja alimilikiwa na ubinadamu wa kweli, na mwingine hakuwa nao; mmoja alikuwa na hisia ya kiumbe wa Mungu, na mwingine hakuwa na hisia hiyo. Tofauti kama hizi ndizo zilizo katika kiini cha Paulo sawa na Petro. Njia ambayo Petro alitembea ni njia ya mafanikio, ambayo pia ni njia ya kutimiza kupatwa tena kwa ubinadamu wa kawaida na wajibu wa kiumbe wa Mungu. Petro anawakilisha wote hao waliofaulu. Njia ambayo Paulo aliitembea ni njia ya kushindwa, na anawakilisha wale wote ambao wanajisalimisha na kujipa matarajio yao wenyewe ya kijuu juu, na hawampendi Mungu kwa dhati. Paulo anawakilisha wote ambao hawana ukweli.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Wale wote ambao hawajaingia njia sahihi ya imani katika Mungu, ambao tabia yao ya maisha haijapitia mabadiliko yoyote kamwe na wale wasioelewa ukweli kidogo, almuradi wanategemea shauku yao na motisha yao kupata baraka, na wako tayari kufanya jitihada kidogo, basi wanaweza kutoa huduma. Mara tu mtu anapoelewa ukweli kiasi, ana imani ya kweli kwa Mungu, hana shaka tena kuhusu Mungu hata kidogo, ana ufahamu wa kazi ya Mungu, anaona kwamba kusudi la kazi ya Mungu ni kuwaokoa na kukamilisha watu kabisa na anaweza kuona kwamba upendo wa Mungu kwa mwanadamu kwa hakika ni mkuu, na amekuza moyo unaompenda Mungu na moyo ambao hurudisha upendo ambao Mungu hutupa, basi wajibu ambao mtu wa aina hii hutimiza unaweza kusemwa kuwa matendo mazuri. Wajibu ambao mtu huyu hutimiza unaweza kuonekana rasmi kama wajibu unaotimizwa na mmoja wa viumbe wa Mungu na hautoi huduma. Kutimiza wajibu kunamaanisha kwamba uko tayari kutekeleza wajibu wako kama njia ya kulipiza upendo wa Mungu. Hii ndiyo tofauti kati ya kutimiza wajibu na kutoa huduma. Nia si moja. Tabia na hali ndani ya moyo si moja. Kutoa huduma ni kutekelezwa wajibu kiasi wakati mtu anatawaliwa na nia yake ya kupata baraka na shauku ya mtu. Mtu kutimiza wajibu wake kwa hakika hufanywa kwa msingi wa ufahamu wa ukweli. Kunategemea ufahamu kwamba walioumbwa kutimiza wajibu wao ndiyo sheria ya mbinguni, na ni kwa msingi wa kuujua upendo wa Mungu na hamu ya kuurudisha upendo huu kwa Mungu ambako hamu ya kutimiza wajibu wa mtu inaibuka. Hivi ndivyo inamaanisha kutimiza wajibu wa mtu kwa hakika na kikamilifu.
Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha
Watu wote wanaolenga uzima na kutafuta kuwa watu wa Mungu wanaweza kuchukua kutekeleza wajibu wao kama jukumu ambalo haliwezi kukwepwa; wanafanya hili ili kulipiza upendo wa Mungu. Hawabishani juu ya thawabu katika kutekeleza wajibu wao na hawana madai. Kila kitu wakifanyacho kinaweza kuitwa kutekeleza wajibu wao. Kikundi cha wale wanaoitwa watendaji huduma pale hali ikiwa bora zaidi huweka juhudi kidogo kumridhisha Mungu ili waweze kubarikiwa. Imani yao ina doa. Hawana dhamiri au mantiki, sembuse wao kufuatilia ukweli au uzima. Kwa sababu wanaweza kuona jinsi walivyo wabaya sana kwa asili na hivyo haiwezekani wao kuwa watu wa Mungu, wanaacha ufuatiliaji wao kuwa watu wa Mungu, daima wakiishi katika hali ya uhasi. Kwa hiyo, kila kitu wanachokifanya ni kutoa huduma kwa sababu wamefungwa na dhana zao wenyewe potovu za mapenzi ya Mungu. Njia ambayo mtu huchukua huamua iwapo kile anachokifanya ni kutekeleza wajibu wake au kutoa huduma. Akifuatilia ukweli na kulenga uzima, atekeleze wajibu wake vizuri ili kulipiza upendo wa Mungu na kumridhisha Mungu, na afanye kazi kwa bidii kwa lengo la kuwa mmoja wa watu wa Mungu, ikiwa maono ya aina hii ndiyo msaada wake, basi kile anachokifanya bila shaka ni kutekeleza wajibu wake. Wale wote wasio na ukweli, ambao wanavunjika moyo na kuishi katika hali ya uasi, wakiweka tu juhudi kidogo kumtuliza na kumhadaa Mungu ni aina za watu ambao wanatoa huduma tu. Ni dhahiri kwamba watendaji huduma wote kweli ni watu wasio na dhamiri au mantiki, na ni wale ambao hawafuatilii ukweli na hawana uzima. Kutokana na hili, ni dhahiri kwamba wale ambao hawana azimio, wasiofuatilia ukweli, na hawalengi uzima pengine hata hawastahili kuwa watendaji huduma. Wao ni wenye asili mbaya sana; hawako tayari kukubali ukweli na hawamwamini Mungu. Hata wanahodhi tashwishi kwa maneno ya Mungu. Hili hasa ni udanganyifu wao ukiwaua. Ikiwa mtu kweli ni mtendaji huduma, bado anahitaji kutekeleza huduma vizuri na asiwe mzembe na ovyoovyo. Hili tu ndilo linaloweza kumwezesha kuwa mtendaji huduma anayebaki; hilo litamfanya awe mwenye bahati sana. Kuwa mtendaji huduma kwa kweli si suala rahisi.
Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?