Ni nini maana ya “acha kila kitu nyuma na kumfuata Mungu”?

12/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Unaweza kuutoa moyo wako na mwili na upendo wako wote wa kweli kwa Mungu, uyaweke mbele Zake, kuwa mtiifu kabisa Kwake, na kufikiria kabisa mapenzi Yake. Si kwa ajili ya mwili, si kwa ajili ya familia, wala si kwa ajili ya matamanio yako mwenyewe, bali ni kwa ajili ya maslahi ya nyumba ya Mungu. Katika kila kitu unaweza kuchukua neno la Mungu kama kanuni, kama msingi. Hivyo, malengo yako na mtazamo wako yote yatakuwa mahali sahihi, na utakuwa mtu ambaye anapata sifa za Mungu mbele Zake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa

Unamwamini Mungu na unafuata Mungu, na kwa hivyo moyoni mwako ni lazima umpende Mungu. Ni lazima uache tabia yako potovu, lazima utafute kutimiza mapenzi ya Mungu, na ni lazima utekeleze wajibu wako kama kiumbe wa Mungu. Kwa kuwa unamwamini na kumfuata Mungu, unapaswa kutoa kila kitu kwake, na hupaswi kufanya uamuzi au madai ya kibinafsi, na unapaswa kutimiza ukamilishaji wa mapenzi ya Mungu. Kwa kuwa uliumbwa, unapaswa kumtii Bwana aliyekuumba, kwa kuwa wewe huna mamlaka kiasili juu yako mwenyewe, na huna uwezo wa kudhibiti hatima yako. Kwa kuwa wewe ni mtu ambaye anamwamini Mungu, inapaswa utafute utakatifu na mabadiliko. Kwa kuwa wewe ni kiumbe wa Mungu, unapaswa kushika wajibu wako, na kuhifadhi nafasi yako, na ni lazima usivuke mpaka wa wajibu wako. Hii si kwa ajili ya kukuzuia, ama kukukandamiza kupitia mafundisho, bali ndiyo njia ambayo utaweza kutekelezea wajibu wako, na inaweza kufikiwa—na inapaswa kufikiwa—na wote wanaotenda haki.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

9. Mawazo yako yanapasa kuwa ya kazi ya kanisa. Unapaswa kuweka kando matarajio ya mwili wako, uwe na msimamo thabiti kuhusu mambo ya kifamilia, na ujitoe kwa moyo wako wote kwa kazi ya Mungu, na uiweke kazi ya Mungu kwanza kisha maisha yako katika nafasi ya pili. Huu ndio mwenendo mwema wa utakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu Katika Enzi ya Ufalme Wazitii

Lazima uvumilie mateso kwa ajili ya ukweli, lazima ujitoe kwa ajili ya ukweli, lazima uvumilie udhalilishaji kwa ajili ya ukweli, na kupata ukweli zaidi lazima upate mateso zaidi. Hili ndilo unalopaswa kufanya. Msitupilie mbali ukweli kwa ajili ya maisha ya amani ya familia, na lazima msiipoteze heshima na uadilifu wa maisha kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Unapaswa kufuata yote ambayo ni ya kupendeza na mema, na unapaswa kufuatilia njia katika maisha ambayo ni ya maana zaidi. Kama wewe unaishi maisha ya kishenzi, na wala hufuati malengo yoyote, je, si huko ni kupoteza maisha Yako? Ni nini unachoweza kupata kutoka kwa maisha ya aina hii? Unapaswa kuziacha starehe zote za mwili kwa ajili ya ukweli mmoja, na hupaswi kutupilia mbali ukweli wote kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Watu kama hawa hawana uadilifu au heshima; hakuna maana ya kuwepo kwao!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Mungu anahitaji hili kutoka kwa wale wanaomwamini: acha kila kitu umfuate Mungu. Kutoka Enzi ya Neema hadi Enzi ya Ufalme, kumekuwa na watu wengi sana walioacha kila kitu kumfuata Mungu. Ni watu hawa tu wanaostahili kuitwa watakatifu, ambao ni watu wa Mungu katika Enzi ya Ufalme. Inamaanisha nini kuacha kila kitu na kumfuata Mungu? Ni kutoa moyo wako mzima, nafsi yako yote kwa Mungu, na kujishughulisha kikamilifu na kazi ya Mungu na kujitumia kwa ajili Yake. Hii ndiyo maana ya kweli ya kuacha kila kitu kumfuata Mungu. Kuna watu wanaoamini kwamba ni wale tu ambao hawajaanzisha familia zao wenyewe na hawana chochote cha kuwa na wasiwasi nacho ndio wanaweza kuacha kila kitu, wakati wale ambao wana familia, ambao wana wazazi, mume au mke au watoto hawawezi kufanya hivyo. Mtazamo huu si sahihi. Kwanza, watu lazima wajue kwamba madai ya Mungu kwa watu ni ya haki na ya maana. Hadai kwamba watu wawaache wazazi, waume au wake, au watoto wao. Badala yake, Anaomba kwamba watu watoe mioyo yao na watekeleze wajibu wao kikamilifu bila kuzuiwa na mtu, tukio au kitu chochote. Hii ni sawa na kuacha kila kitu na kumfuata Mungu. Mungu hawalazimishi watu kufanya vitu ambavyo hawataki kufanya. Inatosha kwa mtu kutumia juhudi zake zote kumridhisha Mungu. Ni kawaida tu kwamba mtu lazima aweke kando vitu fulani ambavyo vinapaswa kuwekwa kando. Ikiwa kwa sasa mtu hawezi kuacha kitu, yote inayohitajika ni kutozuiwa na kitu hicho. Ikiwa moyo wake bado unazuiwa na hawezi kutekeleza wajibu wake kikamilifu, basi hili halihesabiki kama kuacha kila kitu. Suala la kujitolea kwa Mungu liko katika tendo la kuacha kila kitu. Ikiwa kweli wewe ni mtu ambaye amejitolea kwa Mungu, moyoni mwako utaweza kuepuka kuzuiwa na familia, mume au mke, au watoto. Ndugu wengi wana mahusiano ya jamii, lakini mioyo yao haizuiliwi na familia zao; wanatekeleza wajibu wao vizuri sana. Ingawa wanaondoka mara chache kutunza familia zao, hawaruhusu hili liingilie wajibu wao hata kidogo. Je, unaweza kusema kwamba hawajaacha kila kitu kumfuata Mungu? Kuwa na familia kweli ni ugumu—hakuna anayeweza kupinga hili. Hata hivyo, ikiwa mioyo yao inaweza kuwa miaminifu kwa Mungu, wataweza kuondoa mitego ya familia. Ingawa mwili unapitia taabu kiasi, kuna baraka kubwa kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kukua kwao maishani. Na watu hao wanaoshikilia raha za mwili hupata nini? Mwishowe hawapati chochote. Na mtu anapaswaje kushughulikia taabu za mwili? Inaweza kusemekana kwamba kiasi chochote cha taabu ya mwili ni jambo zuri. Alimradi Mungu ameridhishwa, basi roho ya mtu inaweza kufurahia. Uchungu mkubwa zaidi unaweza kuwa kumkosea Mungu kwa sababu ya kushikilia raha za mwili. Wale wote wanaoacha kila kitu kujitumia kwa ajili ya Mungu watafurahishwa kwa sababu wametekeleza wajibu wa binadamu vizuri na wamemridhisha Mungu. Aidha, watasifiwa na Mungu, kwa sababu Mungu huwapa wale wote ambao kweli wanajitumia kwa ajili Yake baraka kubwa. Wale wanaoshikilia raha za familia na mwili na hawawezi kuacha kila kitu kumfuata Mungu ni wale wote waliojitolea kwa Shetani ibilisi. Hakika hawawezi kuokolewa na Mungu, na hasa hawatakuwa na baraka ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp