Ni nini tofauti muhimu kati ya kuokolewa na wokovu?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele” (Yohana 8:34-35).
“Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni” (Mathayo 7:21).
“Na waliimba kwani ilikuwa wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi, na mbele yao wao wanyama wanne, na wao wazee: na hakuna mwanadamu angeweza kujifunza wimbo huo ila wao elfu mia arobaini na nne, ambao walikuwa wamekombolewa kutoka duniani. Hao ndio wale hawakunajisiwa na wanawake; kwani wao ni bikira. Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo. Na vinywani mwao hakukuwa na hila: kwani hawana hatia mbele ya Kiti cha Mungu cha enzi” (Ufunuo 14:3-5).
Maneno Husika ya Mungu:
Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji
Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)
Baadhi ya watu siku zote hufikiria: “Je, si kumwamini Mungu ni suala la kuhudhuria tu mikutano, kuimba nyimbo, kulisikiliza neno la Mungu, kuomba, na kutekeleza wajibu fulani? Je, hayo si yote?” Haijalishi ni kwa muda gani mmemwamini Mungu, bado hamjapata ufahamu kamili wa umuhimu wa imani kwa Mungu. Kwa hakika, umuhimu wa imani kwa Mungu ni mkubwa kiasi kwamba watu hawawezi kuuelewa. Mwishowe, mambo yaliyo ndani ya watu ambayo ni ya Shetani na mambo ya asili yao lazima yabadilike na lazima yalingane na mahitaji ya ukweli; ni kwa njia hii tu ndiyo mtu anaweza kupata wokovu kwa kweli. Iwapo, kama ulivyofanya wakati ulikuwa ndani ya dini, unatoa tu baadhi ya maneno ya mafundisho au kupiga kelele ukitaja kaulimbiu, na kisha utende vitendo vichache vizuri, uonyeshe tabia nzuri zaidi na kuepuka kutenda dhambi kiasi, dhambi zozote za waziwazi, hii bado haimaanishi kwamba umeingia katika njia sahihi ya kumsadiki Mungu. Je, kuweza kuzitii sheria kunaonyesha kwamba unaitembelea njia sahihi? Je, kunamaanisha kuwa umechagua kwa usahihi? Kama mambo ndani ya asili yako hayajabadilika, na mwishowe ungali unampinga na kumkosea Mungu, basi hili ndilo tatizo lako kubwa zaidi. Iwapo, katika imani yako kwa Mungu, hulitatui tatizo hili, basi unaweza kuchukuliwa kuwa aliyeokolewa? Namaanisha nini kwa kusema hili? Nataka kuwafanya nyote muelewa ndani ya mioyo yenu kwamba imani kwa Mungu haiwezi kutenganishwa na maneno ya Mungu, na Mungu au na ukweli. Lazima uichague njia yako vyema, utie jitihada katika ukweli, na kutia jitihada ndani ya maneno ya Mungu. Usipate tu maarifa kiasi ya kijinga au kupata ufahamu kadiri, na kisha kufikiri kuwa umemaliza; ukijidanganya, utajidhuru tu mwenyewe. Watu hawafai kupotoka katika imani yao kwa Mungu; mwishowe, ikiwa hawana Mungu ndani ya mioyo yao, na wanashikilia tu kitabu na kukiangalia kwa muda mfupi tu, na wasiwache nafasi ya Mungu ndani ya mioyo yao, basi wameangamia. Ni nini maana ya maneno haya, “Imani ya binadamu kwa Mungu haiwezi kutenganishwa na maneno ya Mungu”? Unaelewa? Je, yanapinga maneno, “Imani katika Mungu haiwezi kutenganishwa na Mungu”? Unawezaje kuwa na Mungu ndani ya moyo wako kama maneno ya Mungu hayamo ndani ya moyo wako? Kama unamsadiki Mungu, lakini moyo wako hauna Mungu wala maneno Yake, wala uongozi Wake, basi umeangamia kabisa.
Umetoholewa kutoka katika “Wale Waliopoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Umuhimu wa kumwamini Mungu ni kuokolewa, kwa hiyo kuokolewa kunamaanisha nini? “Kuokolewa,” “kujitenga na ushawishi mwovu wa Shetani”—watu huzungumza juu ya mada hizi mara nyingi, lakini hawajui kuokolewa kunamaanisha nini. Je, kuokolewa kunamaanisha nini? Hii inahusiana na mapenzi ya Mungu. Ili kuokolewa, kuzungumza kwa lugha ya wenyeji, kunamaanisha unaweza kuendelea kuishi, na kwamba unafufuliwa. Kwa hiyo kabla ya hayo, je, umekufa? Unaweza kuzungumza, na unaweza kupumua, kwa hivyo unawezaje kusemekana kwamba umekufa? (Roho imekufa.) Kwa nini inasemekana kwamba watu wamekufa ikiwa roho yao imekufa? Msingi wa msemo huu ni upi? Kabla ya kuokolewa, wako wapi? (Wanamilikiwa na Shetani.) Watu wanaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Wanategemea nini ili kuishi? (Falsafa na sumu za Shetani.) Wanategemea asili yao ya kishetani na asili potovu ili kuishi. Mtu anapoishi kwa kufuata mambo haya, nafsi yake nzima—mwili wake, na vipengele vingine vyote kama vile roho na mawazo yao—wako hai au wamekufa? Kutoka katika mtazamo wa Mungu, wao ni wafu. Kwa juu juu, unaonekana kuwa unapumua na kufikiria, lakini kila kitu unachokifikiria daima ni kiovu; unafikiria kuhusu vitu ambavyo vinamwasi Mungu na vya ukaidi dhidi ya Mungu, vitu ambavyo Mungu huchukia, hukirihi, na kushutumu. Machoni pa Mungu, mambo haya yote si ya mwili tu, bali pia ni ya Shetani na ya pepo kikamilifu. Kwa hiyo watu ni nini machoni pa Mungu? Je, wao ni wanadamu? La, wao si wanadamu. Mungu huwaona kama pepo, kama wanyama, na kama Shetani, Shetani waishio! Watu wanaishi kulingana na vitu na asili ya Shetani, na machoni pa Mungu, wao ni Shetani waishio waliovalia miili ya binadamu. Mungu huwafafanua watu kama hao kama maiti zinazotembea; kama wafu. Mungu anafanya kazi Yake ya sasa ya wokovu kuwachukua watu kama hawa—maiti hizi zinazotembea zinazoishi kwa kufuata tabia zao za kishetani na kwa kufuata viini vyao vipotovu vya kishetani—Anawachukua hawa wanaodaiwa kuwa wafu na kuwageuza kuwa walio hai. Hii ndiyo maana ya kuokolewa.
Sababu ya kumwamini Mungu ni kupata wokovu. Kuokolewa kunamaanisha kuwa unageuka kutoka kuwa mtu aliyekufa hadi kuwa mtu aliye hai. Maana ya hili ni kwamba pumzi yako inafufuliwa, na wewe unakuwa hai; unaweza kumwona Mungu, unaweza kumtambua, na unaweza kusujudu ili umwabudu Yeye. Moyoni mwako huna upinzani zaidi dhidi ya Mungu; humkatai tena, humshambulii tena, au kumuasi tena. Watu kama hawa tu ndio walio hai kwa kweli machoni pa Mungu. Mtu akisema tu kwamba anamkubali Mungu na anaamini moyoni mwake kwamba kuna Mungu, basi ni mmoja wa walio hai au la? (La, sio.) Kwa hiyo watu walio hai ni wa aina gani? Je, walio hai wana uhalisi wa aina gani? Angalau, walio hai wanaweza kuzungumza lugha ya binadamu. Hiyo ni nini? Inamaanisha kwamba maneno wanayotamka yanahusu mawazo, fikira, na utambuzi. Watu walio hai hufikiri na kufanya nini mara nyingi? Wanaweza kujihusisha na shughuli za binadamu, na kutimiza wajibu wao. Asili ya kile wanachofanya na kusema ni ipi? Ni kwamba kila kitu wanachofichua, kila kitu wanachofikiria, na kila kitu wanachofanya kinafanywa na asili ya kumcha Mungu na kuepuka uovu. Ili kuliweka kwa usahihi zaidi, kila tendo na kila wazo lako hakihukumiwi na Mungu au kuchukiwa na kukataliwa na Mungu; badala yake, yanaidhinishwa na kusifiwa na Mungu. Hiki ndicho watu walio hai hufanya, na pia ndicho ambacho watu walio hai wanapaswa kufanya.
Umetoholewa kutoka katika “Kuwa Mtiifu Kwa Kweli Pekee Ndiyo Imani ya Kweli” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza, ni wale ambao wanaishi katikati ya kifo, ni wale ambao wametawaliwa na Shetani. Bila kuokolewa na Mungu, na kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu, watu wanakuwa hawana uwezo kukwepa athari ya kifo, hawawezi kuwa hai. Wafu hawa hawawezi kuwa ushuhuda kwa Mungu, wala hawawezi kutumiwa na Mungu, wala kuingia katika ufalme. Mungu anataka ushuhuda wa walio hai, na sio wafu, na Anaomba kwamba walio hai wafanye kazi kwa ajili Yake, na sio wafu. “Wafu” ni wale ambao wanampinga na kumwasi Mungu, ni wale ambao ni mbumbumbu katika roho na hawaelewi maneno ya Mungu, ni wale ambao hawaweki ukweli katika matendo na hawana utii hata kidogo kwa Mungu, na ni wale ambao wamemilikiwa na Shetani na kunyanyaswa na Shetani. Wafu wanajionyesha wenyewe kwa kuupinga ukweli, kwa kumwasi Mungu, na kwa kuwa duni, wa kudharaulika, kuwa waovu, katili, wadanganyifu, na kudhuru kwa siri. Ingawa watu wa namna hiyo wanakula na kunywa maneno ya Mungu, hawana uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu; wanaishi, lakini ni wafu wanaotembea, ni maiti zinazopumua. Wafu hawawezi kabisa kumridhisha Mungu, wala kumtii kikamilifu. Wanaweza tu kumdanganya, kusema maneno ya makufuru juu Yake, na kumsaliti, na yote wanayoyaishi kwa kudhihirisha hufichua asili ya Shetani. Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Ni hapo tu ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi. Mwanadamu wa asili aliyeumbwa na Mungu alikuwa hai, lakini kwa sababu ya uharibifu wa Shetani mwanadamu anaishi katikati ya kifo, na anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hivyo watu hawa wamekuwa wafu ambao hawana roho, wamekuwa ni maadui ambao wanampinga Mungu, wamekuwa nyenzo ya Shetani, na wamekuwa mateka wa Shetani. Watu wote walio hai ambao wameumbwa na Mungu wamekuwa wafu, na hivyo Mungu amepoteza ushuhuda wake, na Amempoteza mwanadamu, ambaye Alimuumba na ndiye kiumbe pekee aliye na pumzi Yake. Ikiwa Mungu ataamua kurejesha ushuhuda Wake, na kuwarejesha wale ambao waliumbwa kwa mkono wake lakini ambao wamechukuliwa mateka na Shetani, basi ni lazima awafufue ili waweze kuwa viumbe hai, na ni lazima awaongoe ili kwamba waweze kuishi katika nuru Yake. Wafu ni wale ambao hawana roho, wale ambao ni mbumbumbu kupita kiasi, na wale ambao wanampinga Mungu. Aidha, ni wale ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata ndogo ya kumtii Mungu, kazi yao ni kumpinga na kuasi dhidi Yake, na hawana hata chembe ya utii. Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe ni Mtu Ambaye Amepata Uzima?
Licha ya kile ambacho Mungu anafanya au mbinu ambazo Anatumia kufanya, licha ya gharama, au lengo Lake, kusudio la hatua Zake halibadiliki. Kusudio Lake ni kuweza kumshughulikia binadamu ili maneno ya Mungu yaingie ndani yake, mahitaji ya Mungu, na mapenzi ya Mungu kwa binadamu; kwa maneno mengine, ni kufanyia kazi huyu binadamu ili vyote ambavyo Mungu Anasadiki kuwa vizuri kulingana na hatua Zake, kumwezesha binadamu kuuelewa moyo wa Mungu na kufahamu kiini cha Mungu, na kumruhusu yeye kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, na hivyo basi kumruhusu binadamu kuweza kufikia kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—yote ambayo ni kipengele kimoja ya kusudio la Mungu katika kila kitu Anachofanya. Kipengele kingine ni kwamba, kwa sababu Shetani ndiye foili[a] na chombo cha huduma katika kazi ya Mungu, mara nyingi binadamu hukabidhiwa Shetani; hizi ndizo mbinu ambazo Mungu hutumia ili kuwaruhusu watu kuweza kuona maovu, ubaya, kudharaulika kwa Shetani katikati ya majaribio na mashambulizi ya Shetani na hivyo basi kuwasababisha watu kumchukia Shetani na kuweza kutambua kile ambacho ni kibaya. Mchakato huu unawaruhusu kwa utaratibu kuanza kuwa huru dhidi ya udhibiti wa Shetani, na dhidi ya mashtaka, uingiliaji kati, na mashambulizi ya Shetani—mpaka, kwa sababu ya maneno ya Mungu, maarifa yao na utiifu wao kwa Mungu, na imani yao kwa Mungu na kuweza kwao kumcha Mungu, wanashinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani na kushinda dhidi ya mashtaka ya Shetani; hapo tu ndipo watakapokuwa wamekombolewa kabisa dhidi ya utawala wa Shetani. Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si tena chakula kwenye kinywa cha Shetani—kwamba badala ya kuwameza wao, Shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemletea Shetani aibu, wamemfanya kuonekana mjinga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu. Kama wangependa kuokolewa, na wangependa Mungu awapate kabisa, basi wote wanaomfuata Mungu lazima wakabiliane na majaribio na mashambulizi yakiwa makubwa na hata madogo kutoka kwa Shetani. Wale wanaoibuka katika majaribio na mashambulizi haya na wanaweza kumshinda Shetani ni wale waliookolewa na Mungu. Hivi ni kusema kwamba wale waliookolewa na Mungu ni wale ambao wamepitia majaribio ya Mungu, na ambao wamejaribiwa na kushambuliwa na Shetani mara nyingi. Wale waliookolewa na Mungu wanayaelewa mapenzi na mahitaji ya Mungu, na wanaweza kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu na hawaachi njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katikati ya majaribio ya Shetani. Wale waliookolewa na Mungu wanamiliki uaminifu, wao ni wakarimu, na wanaweza kutofautisha upendo na chuki, wanayo hisia ya haki na urazini, na wanaweza kumtunza Mungu na kuthamini sana kila kitu ambacho ni cha Mungu. Watu kama hao hawatekwi bakunja, kufanyiwa upelelezi, kushtakiwa au kudhulumiwa na Shetani, wako huru kabisa, wamekombolewa na kuachiliwa kabisa.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?