Kuna tofauti ipi kati ya maneno ya Mungu yaliyowasilishwa na manabii katika Enzi ya Sheria na maneno yaliyoonyeshwa na Mungu mwenye mwili?
Maneno Husika ya Mungu:
Katika Enzi ya Neema, Yesu pia Alinena mengi na kufanya kazi nyingi. Alikuwaje tofauti na Isaya? Alikuwaje tofauti na Danieli? Je, Alikuwa nabii? Ni kwa nini inasemekana kwamba Yeye ni Kristo? Kuna tofauti gani baina yao? Wote walikuwa wanadamu walionena maneno, na maneno yao yalionekana sawa kwa wanadamu. Wote walinena na kufanya kazi. Manabii wa Agano la Kale walitoa unabii, na vivyo hivyo, pia na Yesu. Ni kwa nini iwe hivi? Tofauti hapa inapatikana katika aina ya kazi zao. Ili kutambua suala hili, huwezi kuangazia asili ya mwili na hufai kuangazia upurukushani wa maneno ya mtu. Daima ni sharti kwanza uangazie kazi yake na athari ambayo kazi yake inafanikisha ndani ya mwanadamu. Unabii uliotolewa na manabii wakati ule, haukuyaruzuku maisha ya mwanadamu, na ujumbe uliopokelewa na watu kama Isaya na Danieli ulikuwa tu unabii na si njia ya uzima. Ingekuwa si kuonekana moja kwa moja kwa Yehova, hakuna ambaye angefanya hiyo kazi, ambayo haiwezekani kwa wanadamu. Yesu pia Alisema mengi, lakini maneno yake yalikuwa njia ya uzima ambayo kwayo mwanadamu angepata njia ya kutenda. Hii ni kusema kuwa, kwanza, Angeukimu uzima wa mwanadamu, kwa kuwa Yesu ni uzima; pili, Angeweza kuugeuza upotovu wa mwanadamu; tatu, kazi Yake ingeweza kuifuata ile ya Yehova ili kuendeleza enzi; nne, Angeweza kutambua mahitaji ya mwanadamu kwa ndani na kufahamu anachokosa mwanadamu; tano, Angeweza kuanzisha enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Ndiyo maana Anaitwa Mungu na Kristo; Yeye si tofauti na Isaya tu; bali pia na manabii wengine wote. Chukua Isaya kama ulinganisho wa kazi za manabii. Kwanza, asingeweza kuukimu uzima wa mwanadamu; pili, asingeweza kuanzisha enzi mpya. Alikuwa akifanya kazi chini ya uongozi wa Yehova wala si kuanzisha enzi mpya. Tatu, alichokizungumza yeye mwenyewe kilikuwa nje ya ufahamu wake. Alikuwa akipata ufunuo moja kwa moja kutoka kwa Roho wa Mungu, na wengine wasingeelewa hata baada ya kuusikiliza ufunuo huo. Haya machache yanatosha kuthibitisha kuwa kazi yake haikuwa zaidi ya unabii, si zaidi ya kazi iliyofanywa kwa niaba ya Yehova. Hata hivyo, asingeweza kumwakilisha Yehova kikamilifu. Alikuwa mtumishi wa Yehova, chombo katika kazi ya Yehova. Aidha alikuwa anafanya kazi katika Enzi ya Sheria tu na katika mawanda ya kazi ya Yehova; hakufanya kazi nje ya Enzi ya Sheria. Kinyume na haya, kazi ya Yesu ilikuwa tofauti. Alivuka mipaka ya kazi ya Yehova; Alifanya kazi kama Mungu mwenye mwili na kupitia mateso ili amkomboe mwanadamu. Hiyo ni kusema kuwa Alifanya kazi mpya nje ya ile iliyofanywa na Yehova. Huku kulikuwa kukaribisha kwa enzi mpya. Jambo jingine ni kuwa Aliweza kuyazungumzia mambo ambayo mwanadamu asingeweza kupata. Kazi Yake ilikuwa kazi ndani ya usimamizi wa Mungu na ilijumuisha wanadamu wote. Hakufanya kazi miongoni mwa watu wachache tu, na wala kazi yake haikuwa kuwaongoza watu wachache tu. Kuhusu jinsi Mungu alivyopata mwili kuwa mwanadamu, jinsi Roho alivyotoa ufunuo wakati ule, na jinsi Roho alivyomshukia mwanadamu kufanya kazi, haya ni mambo ambayo mwanadamu hawezi kuona au kugusa. Haiwezekani kabisa ukweli huu kuwa thibitisho kuwa Yeye ni Mungu mwenye mwili. Kwa sababu hii, tofauti inaweza kupatikana tu kwenye maneno na kazi ya Mungu ambayo ni mambo dhahiri kwa mwanadamu. Hili tu ndilo halisi. Hii ni kwa sababu masuala ya Roho hayaonekani kwako na yanafahamika wazi na Mungu Mwenyewe peke Yake, wala hata mwili wa Mungu haufahamu yote; unaweza kuthibitisha tu kama Yeye ni Mungu[a] kutokana na kazi Aliyoifanya tu. Kutokana na kazi Yake, inaweza kuonekana kuwa, kwanza, Anaweza kufungua enzi mpya; pili, Yeye ana uwezo wa kuyaruzuku maisha ya mwanadamu na kumwonyesha mwanadamu njia ya kufuata. Hii inatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Angalau kazi Aifanyayo yaweza kumwakilisha kikamilifu Roho Mtakatifu wa Mungu na kutokana na kazi hiyo inaonekana kuwa Roho wa Mungu yupo ndani Yake. Kwa kuwa kazi iliyofanywa na Mungu mwenye mwili ilikuwa kuanzisha enzi mpya, kuongoza kazi mpya, na kuanzisha na kufungua mazingira mapya, haya mambo machache tu yanatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hili kwa hivyo linamtofautisha na Isaya, Danieli, na manabii wengine wakuu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu
Katika hatua hii ya mwisho ya kazi, matokeo yanapatikana kupitia kwa neno. Kupitia kwa neno, mwanadamu anaelewa mafumbo mengi na kazi ya Mungu katika vizazi vilivyopita; kupitia kwa neno, mwanadamu anapewa nuru na Roho Mtakatifu; kupitia kwa neno, mwanadamu anapata kuelewa mafumbo ambayo hayajawahi kuelezwa na vizazi vilivyopita, na pia kazi za manabii na, mitume wa enzi zilizopita, na kanuni ambazo walitumia kufanya kazi; kupitia kwa neno, mwanadamu anatambua tabia ya Mungu Mwenyewe, na pia uasi na pingamizi ya mwanadamu, na kujua dutu yao. Kupitia kwa hatua hizi za kazi na maneno yote yaliyonenwa, mwanadamu anatambua kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya mwili wa Mungu, na zaidi ya hayo, tabia Yake yote. Maarifa yako ya kazi ya usimamizi wa Mungu wa kupita miaka elfu sita ulitwaliwa kupitia kwa neno. Je, maarifa yako hayakuwa ya fikira zako za awali na mafanikio kwa kuyaweka kando pia yalipatikana kupitia neno? Katika hatua ya awali, Yesu Alifanya ishara na maajabu, lakini sio hivyo katika hatua hii. Je si kuelewa kwako kwa nini Hafanyi hivyo pia kulipatikana kupitia neno? Kwa hivyo, maneno yanenwayo katika hatua hii, yanashinda kazi iliyofanywa na mitume na manabii wa vizazi vilivyopita. Hata unabii uliotabiriwa na manabii haungeweza kupata matokeo haya. Manabii waliongelea unabii pekee, ya kile kitakachotendeka hapo baadaye, lakini sio kazi ambayo Mungu angefanya katika wakati huo. Hawakuongea kuongoza mwanadamu katika maisha yao, kuhifadhi ukweli juu ya mwanadamu ama kumfichulia mwanadamu mafumbo, ama hata kutawaza maisha. Kwa maneno yaliyonenwa katika hatua hii, kuna unabii na ukweli, lakini hasa yanafanya kazi ya kutawaza maisha juu ya mwanadamu. Maneno ya wakati huu sio kama unabii wa manabii. Hii ni hatua ya kazi isiyo ya unabii ila ya maisha ya mwanadamu, kubadili tabia ya maisha ya mwanadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)
Tanbihi:
a. Maandiko asili hayana kauli “kama Yeye ni Mungu.”
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?