Matendo mema ni nini? Maonyesho ya matendo mema ni yapi?

13/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Ukimiliki ukweli, unaweza kumfuata Mungu. Kama unaishi kwa kudhihirisha, unaweza kuwa onyesho la neno la Mungu. Kama unao uzima, unaweza kufurahia baraka ya Mungu. Ni wale tu walio na ukweli wanaweza kufurahia baraka ya Mungu. Mungu huhakikisha kwamba anawafidia wale wote wanaompenda kwa moyo wao wote pamoja na pia wanaovumilia magumu na mateso, na wala si kwa wale wanaojipenda tu na wamejipata kwenye mtego wa uwongo wa Shetani. Kunawezaje kuwa na wema miongoni mwa wale wasiopenda ukweli? Kunawezaje kuwa na haki miongoni mwa wale wanaopenda mwili tu? Si kweli kwamba haki na wema vyote vinarejelea ukweli? Si kweli kwamba vyote hivi vimehifadhiwa wale wanaompenda Mungu kwa moyo wao wote?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Kabla Sijawaacha, lazima bado Ninawasihi mjiepushe kufanya yale ambayo hayaambatani na ukweli. Badala yake, mnafaa kufanya kile ambacho kinawapendeza wote, kile kilicho na manufaa kwa wote, na kile kinachofaidi hatima yenu wenyewe, la sivyo, yule anayeteseka katika maafa hatakuwa mwingine ila wewe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Wale ambao wanaweza kutia ukweli katika vitendo wanaweza kukubali uchunguzi makini wa Mungu katika matendo yao. Unapokubali uchunguzi makini wa Mungu, moyo wako unawekwa kuwa sawa. Ikiwa daima unafanya tu mambo kwa ajili ya wengine kuona na hukubali uchunguzi makini wa Mungu, je, una Mungu moyoni mwako? Watu kama hawa hawana moyo unaomcha Mungu. Usifanye mambo kwa ajili yako daima na usiyafikirie masilahi, hadhi na sifa yako mwenyewe kila wakati. Pia usiyafikirie masilahi ya mwanadamu. Lazima kwanza uyafikirie masilahi ya nyumba ya Mungu, na uyape kipaumbele. Unapaswa kuyafikiria mapenzi ya Mungu na uanze kwa kutafakari kama umekuwa mwenye najisi katika utimizaji wa wajibu wako au la, kama umefanya kila uwezalo kuwa mwaminifu, kama umefanya kila uwezalo kutimiza majukumu yako, na kufanya kadiri uwezavyo au la, na vile vile kama umefikiria wajibu wako na kazi ya nyumba ya Mungu kwa moyo wote au la. Lazima uyazingatie mambo haya. Yafikirie mara kwa mara, na itakuwa rahisi kwako kutekeleza wajibu wako. Iwapo wewe ni mwenye ubora duni wa tabia, uzoefu wako ni wa juu juu, au wewe hujabobeba katika kazi yako ya kitaalamu, basi kunaweza kuwa na makosa au upungufu katika kazi yako, na matokeo huenda yasiwe mazuri sana—lakini utakuwa umetiajuhudi zako zote. Wakati hufikirii tamaa zako za binafsi ama kufikiria maslahi yako mwenyewe katika mambo unayoyafanya, na badala yake unafikiria kila wakati kuhusu kazi ya nyumba ya Mungu, ukifikiria maslahi yake, na kutimiza wajibu wako vizuri, basi utakuwa ukikusanya matendo mema mbele za Mungu. Watu wanaotenda matendo haya mema ndio wale walio na uhalisi wa ukweli; hivyo, wamekuwa na ushuhuda.

Kimetoholewa kutoka katika “Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Ikiwa kweli unamilikiwa na dhamiri, basi lazima uwe na mzigo, na hisia ya kuwajibika. Lazima useme: “Iwe nitashindwa au kufanywa mkamilifu, lazima niwe na hatua hii ya ushuhuda kwa kufaa.” Kama kiumbe wa Mungu, mtu anaweza kushindwa kabisa na Mungu, na hatimaye, mtu anakuwa na uwezo wa kumridhisha Mungu, kulipa upendo wa Mungu kwa moyo wenye upendo kwa Mungu na kwa kujitolea mwenyewe kabisa kwa Mungu. Hili ni jukumu la mwanadamu, ni wajibu unaopaswa kutekelezwa na mwanadamu, na ni mzigo unaopaswa kubebwa na mwanadamu, na mwanadamu lazima atimize agizo hili. Ni wakati huo tu ndipo atakuwa anaamini katika Mungu kwa hakika.

Kimetoholewa kutoka katika “Utendaji (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kanisani, mtasimama imara katika ushuhuda wenu Kwangu, mshikilie ukweli—haki ni haki na mabaya ni mabaya—wala msichanganye nyeusi na nyeupe. Mtakuwa vitani na Shetani na lazima mumshinde kabisa ili asiinuke kamwe. Lazima mtoe kila kitu kulinda ushuhuda Wangu. Hili litakuwa lengo la matendo yenu, usisahau jambo hili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 41

Mnapaswa kufanya wajibu wenu wenyewe kwa kadri ya uwezo wenu kwa mioyo iliyo wazi na wima, na muwe tayari kufanya chochote kitakachohitajika. Kama mlivyosema, wakati siku itakuja, Mungu hatakosa kumjali mtu yeyote ambaye aliteseka au kulipa gharama kwa ajili Yake. Aina hii ya imani ni yenye thamani kuishikilia, na hampaswi kuisahau kamwe. Ni tu kwa njia hii Ninaweza kutuliza akili Yangu kuwahusu. Vinginevyo, Sitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu, na milele mtakuwa malengo ya chuki Yangu. Kama nyote mnaweza kufuata dhamiri zenu na kutoa yote kwa ajili Yangu, msiwache jitihada zozote kwa ajili ya kazi Yangu, na kutenga maisha ya jitihada za kazi ya injili Yangu, basi si moyo Wangu mara kwa mara utaruka kwa furaha kwa ajili yenu? Si Mimi Nitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Juu ya Hatima

Unaweza kuutoa moyo wako na mwili na upendo wako wote wa kweli kwa Mungu, uyaweke mbele Zake, kuwa mtiifu kabisa Kwake, na kufikiria kabisa mapenzi Yake. Si kwa ajili ya mwili, si kwa ajili ya familia, wala si kwa ajili ya matamanio yako mwenyewe, bali ni kwa ajili ya maslahi ya nyumba ya Mungu. Katika kila kitu unaweza kuchukua neno la Mungu kama kanuni, kama msingi. Hivyo, malengo yako na mtazamo wako yote yatakuwa mahali sahihi, na utakuwa mtu ambaye anapata sifa za Mungu mbele Zake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Matendo Ishirini Mema Ambayo Watu wa Mungu Wateule Lazima Waandae:

1. Shiriki mara kwa mara kuhusu ukweli ili kutatua shida za watu wateule wa Mungu katika maisha ya kanisa, daima fadhili wale ambao kwa kweli wanamwamini Mungu ili kuwasaidia kuelewa ukweli na kuingia katika uhalisi. Hili ni tendo jema, na huu tu ndio upendo wa kweli.

2. Ikiwa wewe si wa kuendesha biashara au anayetafuta thawabu katika kufanya wajibu wako, huna nia za aina nyingine, hufanyi vitu kwa namna isiyo ya dhati, na kuna matokeo ya kiutendaji, hili ni tendo jema. Ni wale tu wanaofanya wajibu wao kwa njia hii ambao kwa kweli wanajitumia kwa ajili ya Mungu.

3. Ikiwa wale ambao wametengwa au kuondolewa kanisani kimakosa wamepatikana kuwa watu wazuri, jitahidi kuwasaidia na kuwafadhili na wakubali warudi kanisani. Hili ni tendo jema. Kuwapokea ndugu kutoka mahali pengine ambao wanatafuta kanisa, na kuweza kula na kunywa maneno ya Mungu na kuishi maisha ya kanisa pamoja nao pia ni tendo jema.

4. Kufanya kazi kwa bidii sana, kusahau kula na kulala ili watu wateule wa Mungu ambao wanamwamini Mungu kwa kweli waweze kuelewa ukweli, kuingia katika uhalisi na kukua katika maisha—hili ni tendo jema. Huu ndio uhalisi ambao wale wanaomtumikia Mungu na kweli wanafikiria mapenzi ya Mungu wanapaswa kuwa nao.

5. Lenga uinjilisti, shuhudia kazi ya Mungu wakati wowote unapokumbana na mtu anayefaa. Kuhubiri injili kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo ili kuwapata watu zaidi ni tendo jema. Ikiwa unaweza kuleta mbele za Mungu watu wachache wazuri walio na imani ya kweli wanaoweza kufuatilia ukweli kwa hakika, hili ni tendo jema hata zaidi.

6. Ukigundua kwamba mtu mwovu anavuruga kanisa, tumia kila aina za hekima kumzuia na kumwekea mipaka ili asitende uovu. Tumia ukweli na hekima kushughulikia fujo na kuhakikisha kwamba maisha ya kanisa yanaweza kuendelea kama kawaida. Hili ni tendo jema.

7. Bila kujali shida zinazoibuka kanisani, kusimama kando na Mungu, kukinga kazi ya Mungu, na kulinda kuingia kwa maisha kwa watu wateule wa Mungu ni tendo jema. Ikiwa unaweza kutumia ukweli kutatua shida ili watu wateule wa Mungu waweze kuelewa ukweli na kutambua mazuri na maovu, hilo ni tendo jema hata zaidi.

8. Kuweza waziwazi kufichua na kuwakanusha waovu wanaothubutu kuhukumu, kushambulia, na kumpinga mwanadamu ambaye Roho Mtakatifu anamtumia na kutetea kazi ya Mungu kweli ni tendo jema. Mtu yeyote anayetumia ukweli kutatua vurugu za aina zote za watu waovu na wapinga Kristo na kuleta faida kwa watu wateule wa Mungu ni tendo jema hata zaidi.

9. Kutafuta ukweli baada ya kugundua uwongo na uzushi mbalimbali ndani ya kanisa, kuyakanusha na kuyakosoa kulingana na maneno ya Mungu, kuwalinda watu wateule wa Mungu dhidi ya madhara, na kuwasaidia kutimiza ujenzi wa maadili na kukua katika maisha—hili ni tendo jema.

10. Ikigunduliwa kwamba waumini wa kweli wa Mungu ambao wako tayari kufuatilia ukweli wamedanganywa au kudhibitiwa, ni tendo jema kufanya kila kiwezekanacho kuwaokoa, kushiriki kuhusu ukweli kwa subira ili waweze kuhepa mikono ya waovu, kumrudia Mungu kwa kweli, na kukiacha giza kwa ajili ya nuru.

11. Ikipatikana kwamba kweli kuna kiongozi wa uongo au mpinga Kristo anayewaongoza wengine kimwinyi na kujaribu kuanzisha ufalme ulio, ni tendo jema kuripoti hili mara moja na kuwasiliana na watu wanaouelewa ukweli ili kuwaokoa watu wateule wa Mungu kutoka kwa madhara ya Shetani, ibilisi.

12. Mazingira mabaya yanapotokea, kufanya kila juhudi ili kulinda watu wa Mungu wateule, kufanya mipango inayofaa kwa ajili ya fedha na mali za nyumba ya Mungu, na kulinda sadaka za Mungu dhidi ya kuanguka mikononi mwa Shetani na joka kubwa jekundu ni tendo jema. Yule afanyaye hili ni mtu anayekinga kazi ya Mungu na kweli ni mwaminifu kwa Mungu.

13. Ni tendo jema kuwakinga waumini wa kweli ili kuzuia kukamatwa kwao na kutumia kila uhusiano kuwaokoa wale ndugu ambao wamekamatwa. Ni tendo jema hata zaidi kutumia hekima kukinga maisha ya kanisa na kulinda watu wateule wa Mungu wakati wa mazingira mabaya.

14. Unapoona kwamba wale ndugu wanaojitumia kweli kwa ajili ya Mungu na kufuatilia ukweli wanakabiliwa na taabu na ugumu, ni tendo jema kufanya kila kitu kuwafanya wayashinde matatizo haya. Pia ni tendo jema kuweza kuwasaidia viongozi na wafanyakazi wanaojitumia kwa ajili ya Mungu muda wote na ambao familia zao ziko katika ugumu.

15. Ni tendo jema kama unaweza kujaribu kila mbinu iwezekanayo kupokea na kuwasaidia ndugu ambao wanafuatiliwa na wanatafutwa bila hofu ya hatari au gharama ambayo huenda ukalipa, na kama unaweza kuvumilia kila aina za ukosoaji wa mambo madogomadogo, balaa na shida kutoka kwa wengine katika harakati ya kutimiza wajibu wako ili uweze kumridhisha Mungu.

16. Ni tendo jema kuwapanga ndugu ambao ni waumini wa kweli na hufuatilia ukweli kula na kunywa maneno ya Mungu, kuwa na ushirika kuhusu ukweli, na kuishi maisha ya kanisa katika majaribu. Ni tendo jema hata zaidi kuwasaidia ndugu wanyonge kuelewa ukweli na kushuhudia wakati wa majaribu na maafa.

17. Kufichua na kuripoti watu waovu wanaoiba sadaka na kubadhiri mali ya nyumba ya Mungu ni tendo jema. Hili linazuia hasara ya sadaka kwa Mungu na mali ya nyumba ya Mungu. Kulinda sadaka za Mungu dhidi ya kuanguka mikononi mwa waovu na kubadhiriwa na watu walio na nia iliyofichika pia ni tendo jema.

18. Ni tendo jema kutumia kila juhudi kuratibu katika utekelezaji wa mipango ya kazi kutoka kwa mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu na vile vile kutatua aina zote za shida za kiutendaji za watu wateule wa Mungu kanisani, na kufanya kiasi kikubwa cha kazi ya kiutendaji ili kulinda kazi ya Mungu na kuwaleta watu wateule wa Mungu kwenye njia sahihi ya imani.

19. Kushirikiana kwa vitendo katika kuongoza na kuchunga mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu, kuanzisha vita vya kufa na kupona na viongozi wa uongo na wapinga Kristo kwa ajili ya kuwaleta watu wateule wa Mungu kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu, kulipa gharama kulinda kazi ya Mungu na kutimiza matokeo—haya yote yameainishwa kama matendo mema.

20. Kuweza kutambua na kuamua viongozi wa uongo na wapinga Kristo kulingana na mipango ya kazi, kuwafichua kulingana na ukweli, na kuwashawishi wajiuzulu ili kuepuka madhara makubwa zaidi kwa watu wateule wa Mungu ni tendo jema. Kuwasaidia na kuwalinda wale viongozi ambao wana dhambi, lakini wanaweza kutubu kwa kweli na wana ubinadamu mzuri ili waweze kuendelea kufanya wajibu wao pia ni tendo jema.

Kimetoholewa kutoka katika Mipango ya Kazi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp