Kumfuata mtu ni nini?

12/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa wanaitwa wanaotafuta mamlaka. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.

Unachopendezwa nacho sio unyenyekevu wa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Hupendi maarifa au kupendeza kwa Kristo, bali unapenda wale watukutu wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea wao, sifa zao, hadhi zao, na ushawishi wao. Ilhali unazidi kuchukua mtazamo ambapo unaona kazi ya Kristo kuwa ngumu sana kukubali na huko tayari kuikubali. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa hukuwa na chaguo jingine. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Kunao baadhi ya watu ambao mara nyingi wanadanganywa na wale ambao kwa nje wanaonekana wa kiroho, wanaonekana wa kilodi, wanaonekana kuwa na taswira za ukuu. Kuhusiana na watu hao wanaoweza kuzungumzia barua na falsafa, na ambao hotuba na vitendo vyao vinaonekana kuwa vyenye kustahili uvutiwaji, wale wanaodanganywa nawao hawajawahi kuangalia kiini halisi cha vitendo vyao, kanuni zinazoendesha vitendo vyao, au shabaha zao ni nini. Na hawajawahi kuangalia kama watu hawa wanatii Mungu kwa kweli, na kama wao ni watu wanaomcha Mungu kwa kweli na kujiepusha na uovu au la. Hawajawahi kutambua kile kiini halisi cha ubinadamu cha watu hawa. Badala yake, kutoka kwenye hatua ya kwanza ya kujua na kuzoeana nao, hatua kwa hatua wanaanza kuwapenda watu hawa, kuwatukuza watu hawa, na hatimaye watu hawa wanakuwa sanamu zao. Aidha, katika akili za baadhi ya watu, sanamu hizi wanazoziabudu, wanaosadiki wanaweza kuacha familia na kazi zao, na kulipa ile bei kwa juujuu—sanamu hizi ndizo ambazo kwa kweli zinatosheleza Mungu, ndizo zile zinazoweza kupokea kwa kweli matokeo mazuri na hatima nzuri. Katika akili zao, sanamu hizi ndizo wale watu ambao Mungu husifu. Ni nini husababisha watu kuwa na aina hii ya kusadiki? …

… Kunayo sababu moja tu ya chanzo cha haya ambayo huwafanya watu kuwa na vitendo wasivyovijua, mitazamo wasiyoijua, au mitazamo na vitendo vya upande mmoja, na leo Nitawaelezea kuhusu haya. Sababu ni kwamba ingawa watu wengi wanaweza kumfuata Mungu, kumwomba Yeye kila siku, na kusoma neno la Mungu kila siku, hawaelewi kwa hakika nia za Mungu. Hiki ndicho chanzo cha tatizo. Kama mtu huelewa moyo wa Mungu, huelewa kile anachopenda Mungu, kile humchukiza Mungu, kile anachotaka Mungu, kile anachokataa Mungu, ni mtu wa aina gani ambaye Mungu humpenda, ni mtu wa aina gani ambaye Mungu hampendi, ni kiwango kipi ambacho Mungu hutumia katika kutoa mahitaji Yake kwa binadamu, ni mtazamo gani ambao Anauchukua katika kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, je, mtu huyu anaweza bado kuwa na mawazo yake ya kibinafsi? Wanaweza tu kuenda na kumwabudu mtu mwingine? Mtu wa kawaida anaweza kuwa sanamu yao? Kama mtu anaelewa nia za Mungu, mtazamo wake ni wenye kirazini zaidi kuliko hapo. Hawatamwabudu kama Mungu kiongozi aliyepotoka kiholela, wala hawataweza, huku wakitembea njia ya kutia ukweli katika matendo, kusadiki kwamba kutii kiholela katika sheria au kanuni chache rahisi ni sawa na kutia ukweli katika matendo.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

Ingekuwa vyema kwa wale watu wanaosema kuwa wanamfuata Mungu kufungua macho yao watazame vizuri waone ni nani wanayemwamini hasa: Je, ni Mungu unayemwamini hakika, ama Shetani? Ikiwa unajua kuwa unayemwamini si Mungu ila sanamu zako mwenyewe, basi ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Ikiwa hakika hujui unayemwamini ni nani, basi, pia, ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Kusema hivi kutakuwa kukufuru! Hakuna anayekushurutisha umwamini Mungu. Msiseme kuwa mnaniamini Mimi, kwa kuwa Niliyasikia maneno hayo hapo kale wala Sitamani kuyasikia tena, kwa kuwa mnachoamini ni sanamu zilizo katika mioyo yenu na nyoka waovu wa ndani walio miongoni mwenu. Wale wanaotikisa vichwa vyao wanaposikia ukweli, wanaotabasamu sana wanaposikia mazungumzo ya kifo ni watoto wa Shetani, na wote ni vyombo vya kuondolewa. Kuna watu wengi kanisani ambao hawana ufahamu, na jambo la uongo linapotendeka wanasimama tu upande wa Shetani. Wanapoitwa vibaraka wa Shetani wanahisi kuwa wamekosewa sana. Wanasemekana kuwa hawana ufahamu, lakini daima wanasimama upande usiokuwa na ukweli. Hakujakuwa na wakati muhimu ambapo wamesimama upande wa ukweli, hakuna wakati mmoja ambapo hawasimami na kutetea mjadala juu ya ukweli. Je, kweli hawana ufahamu? Kwa nini daima wao husimama upande wa Shetani isipotarajiwa? Kwa nini hawasemi neno lolote la haki ama lenye mantiki kwa ukweli? Je, hali hii kweli imetokana na kuchanganyikiwa kwao kwa ghafla? Kadri mtu anapokuwa na ufahamu mdogo, ndivyo anavyozidi kushindwa kusimama upande wa ukweli. Je, hili linaonyesha nini? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu wanapenda uovu? Je, halionyeshi kuwa wale wasio na ufahamu ni watoto waaminifu wa Shetani? Je, ni kwa nini daima wanaweza kusimama upande wa Shetani na kuzungumza lugha moja naye? Kila neno na tendo lao, na maonyesho yao yanathibitisha vya kutosha kuwa wao sio wapenzi wa ukweli kwa namna yoyote, lakini badala yake wao ni watu wanaochukia ukweli. Kwamba wanaweza kusimama upande wa Shetani kunadhihirisha kuwa hakika Shetani anawapenda ibilisi hawa wadogo wanaopigana kwa ajili ya Shetani katika maisha yao yote. Je, taarifa hizi za kweli si wazi sana?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Inamaanisha nini kuwafuata watu? Kuwafuata watu inamaanisha mtu huwafuata wafanyakazi au viongozi anaowaabudu. Mungu hana nafasi kubwa katika mioyo yaomoyo wake; yeye hutundika kidokezo akisema anamwamini Mungu, na katika kila kitu anachofanya yeye ni kujifananisha na watu au kuwaiga. Hasa wakati ni jambo kuu, anawaacha watu kuamua, anawaacha watu waongoze jaala yao, yeye mwenyewe hatafuti maana ya Mungu, na anashindwa kutambua maneno yanayosemwa na watu. Mradi anachokisikia kinaonekana kuwa cha maana, basi bila kujali kama kinapatana na ukweli bado yeye hukikubali na kukisikiliza. Haya ni maonyesho ya kuwafuata watu. Imani ya watu kama hao katika Mungu haina kanuni, hakuna ukweli katika matendo yao, wao husikiliza mtu yeyote anayesema jambo la maana, na hata vijimungu vyao vikichukua njia mbaya, wao huvifuata mpaka mwisho. Mungu Akivilaani vijimungu vyao, basi watakuwa na dhana juu ya Mungu, na kushikilia kikiki vijimungu vyao. Sababu zao ni kwamba “tunapaswa kumsikiliza yeyote aliye na madaraka juu yetu; nguvu ya karibu ni bora kuliko nguvu ya juu.” Hii ni mantiki duni, upumbavu mtupu, lakini huo ndio upumbavu wa hao ambao huwafuata watu. Wale wanaowafuata watu hawana ukweli. Ni wale tu ambao humfuata Mungu wanaoamini kweli katika Mungu; Wale wanaowafuata watu huabudu sanamu, wamekuwa wakidanganywa na watu, na katika mioyo yao hakuna Mungu wala ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Mtu yeyote unayemwabudu moyoni mwako ni sanamu yako. Yeyote aabuduye viongozi ni mwabudu sanamu. Unapomwabudu mtu, utakuwa na hadhi yake moyoni mwako, na hakika utamilikiwa na yeye na utakuwa karagosi lake. Katika kazi yetu ya kueneza injili, tumegundua kwamba watu wote wa madhehebu mbalimbali huabudu sanamu, na wote hudhibitiwa na viongozi wao. Hawathubutu hata kuukubali ukweli, na wanaonyesha sura ya unyonge wa kusikitisha. Watu wanaoabudu viongozi wao ni waabudu sanamu, na hakika hakuna ukweli ndani ya mioyo yao. Hawamjui Mungu hata kidogo, hivyo Mungu hana hadhi katika mioyo yao. Wao ni watu ambao wanachukiwa na kulaaniwa na Mungu. Mungu ni Mungu mwenye haki, na Mungu ni Mungu mwenye wivu. Mungu huchukia zaidi ibada ya sanamu ya watu. Ni kufuru kubwa kwa Mungu mtu akimlinganisha kiongozi wake kwa kumweka sawa na Mungu. Kwa kweli, watu wanaorudi mbele ya Mungu wanapaswa kuwa na Mungu pekee katika mioyo yao; hawapaswi kuwa na nafasi ya mtu yeyote katika mioyo yao. Hata kama wana hili katika fikira na mawazo yao, ni chafu na potovu, na humfanya Mungu aidharau na kuichukia. Watu wengi huchanganyikiwa juu ya suala hili, na kwa kadiri mioyo yao ina sehemu fulani ya mtu wanayeabudu. Kwa mujibu wa tabia ya Mungu, ikiwa mtu ana hadhi ya mwanadamu hata kidogo katika moyo wake, haikubaliki. Ikiwa tangu mwanzo hadi mwisho moyo wake hauwezi kutakaswa, matokeo yake ni kwamba yeye atahukumiwa.

Kuna maonyesho maalum ndani ya wote wanaowaabudu viongozi wao katika mioyo yao. Wanaweza kutambuliwa kama ifuatavyo: Ikiwa utii wako kwa kiongozi wako ni mkubwa kuliko utii wako kwa Mungu, basi wewe huziabudu sanamu; ikiwa unawatamani sana na kuwataka sana watu unaowaabudu kuliko unavyomtamani sana na kumtaka sana Mungu, basi unaziabudu sanamu; Ikiwa wewe ni mwenye ari zaidi kwa kiongozi wako kuliko Mungu, basi unaziabudu sanamu; ikiwa, katika moyo wako, wewe u karibu na wale unaowaabudu na mbali na Mungu, basi unaziabudu sanamu; kama, katika moyo wako, wale unaowaabudu wana cheo sawa na Mungu, basi hili ni thibitisho hata kubwa mno kuwa unawachukulia watu unaowaabudu kuwa kama Mungu; na kama, bila kujali kinachokutokea, wewe hukubali kusikiliza kiongozi wako, na hukubali kuja mbele ya Mungu kutafuta ukweli, basi hili linatosha kuthibitisha kwamba humwamini Mungu, bali watu. Watu wengine, labda, watajaribu kujitetea, wakisema: “Kwa kweli namstahi fulani, kwa kweli ana mahali katika moyo wangu. Pasipo kulitambua, nimekuwa mbali kidogo na Mungu katika uhusiano wangu na Yeye.” Maneno haya yanaonyesha ukweli wa jambo hilo; mara tu mtu fulani anapopata mahali katika moyo wa mtu, mtu huyo huwa mbali na Mungu. Hili ni hatari, lakini baadhi ya watu hulichukulia kwa wepesi, hawana shughuli hata kidogo, jambo ambalo linaonyesha kwamba hawajui tabia ya Mungu. … kuwaabudu watu ni ujinga sana na upofu, ni upotovu sana na uovu. Kuwaabudu watu ni kumwabudu Shetani na pepo, ni kuwaabudu wapinga Kristo, na wale wanaowaabudu watu hawana ukweli hata kidogo. Watu kama hawa hakika hawana ujuzi wa Mungu hata kidogo; wao ni wapotovu ambao wamelaaniwa na Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kumfuata Mungu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu: Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo:...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp