Kumfuata Mungu ni nini?
Maneno Husika ya Mungu:
Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno ya Mungu leo. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno ya Mungu leo, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu hutaka ni watu ambao huzifuata nyayo Zake. Haijalishi vile ulichoelewa awali ni cha ajabu na safi, Mungu hakitaki, na kama huwezi kuweka kando vitu hivyo, basi vitakuwa kizuizi kikubwa mno kwa kuingia kwako katika siku za baadaye. Wale wote ambao wanaweza kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Watu wa enzi zilizopita pia walifuata nyayo za Mungu, ilhali hawangeweza kufuata mpaka leo; hii ndiyo baraka ya watu wa siku za mwisho.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake
Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii moyoni mwake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni zozote, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika. Badala yake, kazi Anayofanya daima ni mpya zaidi na daima ni juu zaidi. Kazi Yake inazidi kuwa ya utendaji kwa kila hatua, sambamba zaidi na matendo halisi ya mwanadamu. Baada tu ya mwanadamu kuwa na uzoefu wa aina hii ya kazi ndipo anaweza kufikia mabadiliko ya mwisho ya tabia yake. … Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa katika awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu ambaye ni mtiifu kwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima katika utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haikubaliki na Mungu. Kama huwezi kwenda sambamba na kazi mpya Ninayoshiriki na uendelee kuyashikilia maneno ya zamani, basi kutakuaje na ukuaji katika maisha yako? Kazi ya Mungu ni kukuruzuku kupitia neno Lake. Unapotii na kulikubali neno Lake, basi Roho Mtakatifu hakika atafanya kazi ndani yako. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa njia Ninayozungumza kabisa. Fanya Nilivyosema, na Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako mara moja.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu
Je, unajua kumfuata Mungu ni nini? Bila maono, ni njia gani ungeitembea? Katika kazi ya leo, kama huna maono hutaweza kufanywa mkamilifu kamwe. Unaamini katika nani? Kwa nini unamwamini Yeye? Mbona unamfuata Yeye? Je, unaamini kama aina ya mchezo? Je, unashughulikia maisha yako kama aina ya mtu anayechezewa? Mungu wa leo ndiye maono makubwa zaidi. Je, ni kiasi gani Chake unachokijua? Je, ni kiasi gani Chake ambacho umekiona? Je, baada ya kumwona Mungu wa leo, msingi wa imani yako katika Mungu u salama? Je, unafikiri kwamba mradi unafuata katika njia hii iliyovurugika, utapata wokovu? Unafikiri unaweza kuvua samaki katika maji yenye tope? Je, ni rahisi hivyo? Je, ni maoni mangapi yako kuhusu kile ambacho Mungu wa leo anasema umeweka chini? Je, una maono ya Mungu wa leo? Ufahamu wako wa Mungu wa leo umesimamia wapi? Daima wewe huamini kuwa unaweza kumpata Yeye[a] kwa kumfuata tu, kwamba kwa kumuona Yeye, na kwamba hakuna yeyote anayeweza kukukwepa. Usifikiri kwamba kumfuata Mungu ni rahisi sana. Cha muhimu ni kwamba ni lazima umjue Yeye, lazima uijue kazi Yake, na lazima uwe na nia ya kuvumilia shida kwa ajili Yake, uwe na nia ya kutoa maisha yako kwa ajili Yake, na uwe na nia ya kukamilishwa na Yeye. Haya ndiyo maono ambayo unapaswa kuwa nayo. Haitafaidi kama wewe daima unafikiria kufurahia neema. Usifikiri kwamba Mungu yupo tu kwa ajili ya starehe za watu, na kukirimu neema kwa watu. Wewe ulifikiri vibaya! Kama mtu hawezi kuhatarisha maisha yake ili kufuata, ama mtu hawezi kuacha kila mali ya dunia ili kufuata, basi kwa uhalisi hataweza kufuata hadi mwisho.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Lazima Muielewe Kazi—Msifuate kwa Rabsha!
Petro alimfuata Yesu kwa miaka kadhaa na aliona mambo mengi ndani ya Yesu ambayo watu hawana. Baada ya kumfuata Yeye kwa mwaka mmoja, aliteuliwa na Yesu kama mkuu wa wanafunzi kumi na wawili. (Bila shaka hili lilikuwa jambo la moyo wa Yesu, na watu hawakuweza kabisa kuliona.) Kila kitendo cha Yesu kilikuwa mfano kwake katika maisha yake, na mahubiri ya Yesu yaliwekwa hasa katika kumbukumbu ndani ya moyo wake. Alikuwa mwenye busara sana na wa kujitolea kwa Yesu, na kamwe hakuwa na malalamiko kumhusu Yesu. Hii ndiyo maana alikuwa mwandani mwaminifu wa Yesu popote Alipoenda. Petro alichunguza mafunzo ya Yesu, maneno Yake yasiyo makali, na kile Alichokula, Alichovaa, maisha Yake ya kila siku, na safari Zake. Alifuata mfano wa Yesu katika kila njia. Hakuwa wa kujidai, lakini alitupa vitu vyake yote vya awali vilivyopitwa na wakati akafuata mfano wa Yesu katika maneno na matendo. Ni wakati huo ndipo alihisi kwamba mbingu na dunia na vitu vyote vilikuwa ndani ya mikono ya Mwenyezi, na kwa sababu hii hakuwa na chaguo lake mwenyewe, lakini alichukua kila kitu ambacho Yesu alikuwa ili kiwe mfano wake. Angeweza kuona kutoka kwa maisha yake kwamba Yesu hakuwa wa kujivuna katika kile Alichofanya, wala Hakujigamba kuhusu Mwenyewe, lakini badala yake, Aliwavuta watu na upendo. Katika hali mbalimbali Petro angeweza kuona kile ambacho Yesu alikuwa. Hiyo ndiyo maana kila kitu ndani ya Yesu kilikuwa chombo ambacho Petro alikifuata kama mfano.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Kuhusu Maisha ya Petro
Chochote katika maisha ya Petro ambacho hakikukimu mapenzi ya Mungu kilimfanya kuhisi wasiwasi. Kama hakikukidhi mapenzi ya Mungu, basi angehisi kujuta, na angetafuta njia mwafaka ambayo angejitahidi kuridhisha moyo wa Mungu. Hata katika masuala madogo kabisa maishani mwake yasiyokuwa na maana, bado alijishurutisha mwenyewe kukidhi mapenzi ya Mungu. Alikuwa pia mkali ilipofikia tabia yake ya asili na alikuwa daima mkali katika masharti yake mwenyewe ili kuelekea ndani zaidi kwa ukweli. … Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na kuwa bila kitu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake kwa Mungu. Je, huu haukuwa upendo mkamilifu kwa Mungu? Je, huku hakukuwa ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? Kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo kwa Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Kumfuata Mungu kimsingi kunamaanisha kufuata kazi ya sasa ya Mungu, kutii na kuyatenda maneno ya sasa ya Mungu, kuwa na uwezo wa kuzifuata amri za Mungu, kutafuta mapenzi ya Mungu katika masuala yote, kutenda kulingana na neno la Mungu, na kutii kabisa kazi na mwongozo wa Roho Mtakatifu. Hatimaye, kunamaanisha kuwa mtu anayetenda ukweli na kuyafuata mapenzi ya Mungu. Ni mtu wa aina hii pekee ndiye mfuasi wa Mungu, mtu anayepata wokovu wa Mungu. Kama katika imani yetu tunaitegemea na kuitukuza Biblia kwa nje, huku kwa kweli utendaji na kupitia kwetu ni kulingana na maneno na mafundisho ya binadamu katika Biblia badala ya kutii na kutenda neno la Mungu kutoka katika Biblia, na ikiwa hatuzielewi nia za Mungu na badala yake kushikilia tu taratibu na amri za dini, huku ni kumfuata mwanadamu. Tukifuata na kutenda maneno ya watu kutoka katika Biblia kana kwamba hayo yalikuwa maneno ya Mungu, lakini bado tumchukulie Bwana Yesu kuwa mkubwa wa jina tu, tukipuuza maneno Yake na kutofanya chochote kufuata amri Zake, basi hakika tutasukumwa mbali na kulaaniwa na Bwana Yesu, kama tu walivyofanyiwa Mafarisayo wanafiki. Kuna watu wengi walio na imani katika Bwana, lakini bado wanawaabudu bila kufikiria watu maarufu wa roho au wachungaji na wazee—wanawacha Mafarisayo wanafiki. Chochote kinachowakumba wanakimbia kwa wachungaji na wazee kutafuta mwongozo na kufanya vivyo hivyo inapofikia kuchunguza njia ya kweli. Kama matokeo, wanadanganywa na kupotoshwa na Mafarisayo wanafiki na viongozi wa dini na wanaingia katika njia ya kumpinga Mungu—haya ndiyo matokeo na miisho ya kumfuata mwanadamu badala ya Mungu. Njia ya pekee ya kumfuata Mungu kweli ni kuweka imani yetu kwa msingi wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu pekee, kuyafuata maneno ya sasa ya Mungu, kuzifuata nyayo za kazi ya Roho Mtakatifu, na kufanya liwezekanalo kukamilisha wajibu wetu. Hasa wakati Mungu anafanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, dunia ya dini imepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na imekuwa yenye ukiwa. Wakati tunalazimishwa kuitafuta njia ya kweli, tunapaswa kuwa makini hata zaidi katika kuyatafuta maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa; lazima tuyatafute maneno na matamshi ya Mungu na kazi ya Roho Mtakatifu. Tusipotafuta maneno na kazi ya Roho Mtakatifu, tusipoweza kuisikia sauti ya Mungu, tusipoweza kupata lishe ya maneno ya sasa ya Mungu, basi badala yake tutaondolewa, kutupwa kando wakati wa kazi ya Mungu katika siku za mwisho, tukibiringika katika giza, tukilia na kusaga meno yetu. Watu wanaomfuata na kumtii Mungu kwa kweli hawatawahi kuachwa na Yeye kamwe. Wale wanaowaabudu wachungaji na wazee wa dini wanamtii mwanadamu na ni wafuasi wa mwanadamu. Watu hawa hatimaye watawekwa wazi na na kazi ya Mungu—wataondolewa na kutupwa kando.
Hata ingawa kutoka kwa vinywa vyetu tunapaza sauti kwamba tunamwamini Mungu na kwamba tunapaswa kumfuata Mungu tu na kumtii Yeye, hata hivyo, nini kinafanyika katika uhalisi si sawa. Tunaweza kuona hili dhahiri kutoka kwa njia ambayo wale wa imani ya Kiyahudi katika Enzi ya Neema walivyomtendea Bwana Yesu kinyume na jinsi Petro na Yohana na wengine walivyofanya. Bwana Yesu alitekeleza kazi Yake mpya, akatoa ukweli, na kuleta njia ya toba, lakini watu wengi wa Kiyahudi wakati huo waliyasikiza mafundisho ya makuhani wakuu na Mafarisayo tu. Hawakukubali kazi na maneno ya Bwana Yesu, na kwa kama matokeo waliupoteza wokovu wa Bwana Yesu. Kwa jina tu, walimwamini Mungu, lakini kwa kweli waliwaamini makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo. Hata hivyo, Petro, Yohana, Mathayo, Filipo na wale wengine waliona kwamba maneno na kazi ya Bwana Yesu yalikuwa na mamlaka na nguvu, na kwamba yalikuwa ukweli. Waliona kwamba maneno na kazi ya Bwana Yesu yalitoka kwa Mungu na hivyo walimfuata kwa karibu. Hawakupitia hata kidogo udhibiti wa Mafarisayo na walikuwa ndio wale waliomfuata na kumtii Mungu kweli. Katika siku za mwisho, njia ya pekee ya kumfuata na kumtii Mungu kweli ni kukubali na kutii kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu, na huku kunakamilisha unabii unaopatikana katika Kitabu cha Ufunuo: “Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo” (Ufunuo 14:4).
Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme
Inamaanisha nini kumfuata Mungu? Na unawezaje kutia hilo katika vitendo? Kumfuata Mungu hakuhusishi tu kumwomba Mungu na kumsifu Mungu; kilicho muhimu zaidi ni kula na kunywa maneno ya Mungu na kuishi kulingana na maneno ya Mungu, kutenda kulingana na ukweli, kutafuta njia ya kupata uzoefu wa maisha katikati ya maneno ya Mungu, kukubali agizo la Mungu, kutekeleza kila moja ya wajibu wako vizuri, na kuitembea njia iliyo mbele yako kama unavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Hasa, katika nyakati muhimu, wakati matatizo makuu yanapokufika, kuna hata haja kubwa zaidi ya kutafuta maana ya Mungu, kuwa na hadhari ya kudanganywa na mafundisho ya mwanadamu, na kutokuwa chini ya udhibiti wa mtu yeyote. “Kile kitokacho kwa Mungu mimi hukitii na kukifuata, lakini ikiwa kinatoka kwa mapenzi ya mwanadamu mimi hukikataa kwa uthabiti; wakati kile kinachohubiriwa na viongozi au wafanyakazi kina mgongano na mipango ya Mungu, basi mimi bila shaka humfuata Mungu na kuwakataa watu. Kama kina makubaliano kamili na mipango na mapenzi ya Mungu, basi naweza kukisikiliza.” Watu ambao hutenda kwa njia hii ni wale ambao humfuata Mungu.
Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu
Tanbihi:
a. Maandishi ya awali hayana neno “Yeye.”
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?