Kujihusisha katika sherehe ya kidini ni nini?

12/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Maisha ya kawaida ya kiroho hayazuiliwi katika matendo kama kuomba, kuimba nyimbo za kidini, kushiriki katika maisha ya kanisa, na kula na kunywa maneno ya Mungu. Badala yake, yanahusisha kuishi maisha mapya na machangamfu ya kiroho. Kilicho muhimu si jinsi unavyotenda, lakini matunda yanayozalishwa na kutenda kwako. Watu wengi sana huamini kwamba maisha ya kawaida ya kiroho ni lazima yahusishe kuomba, kuimba nyimbo za kidini, kula na kunywa maneno ya Mungu ama kutafakari maneno Yake, bila kujali iwapo matendo kama haya kweli yana athari yoyote ama yanasababisha ufahamu wa kweli. Watu hawa hulenga kufuata taratibu za kijuujuu bila kufikiria matokeo yake, wao ni watu wanaoishi katika kaida za kidini, sio watu wanaoishi ndani ya kanisa, sembuse watu wa ufalme. Maombi yao, kuimba nyimbo za kidini, na kula na kunywa maneno ya Mungu ni kufuata kanuni tu, vitu vinavyofanywa kwa sababu ya kulazimishwa na kuwa sambamba na mitindo, sio kwa sababu ya kutaka wala kutoka moyoni. Bila kujali jinsi watu hawa wanavyoomba ama kuimba, juhudi zao hazitazaa matunda, kwa kuwa kile wanachotenda ni kanuni na kaida za kidini tu; kwa kweli hawatendi maneno ya Mungu. Wanalenga tu kulalamika kuhusu jinsi ya kutenda, na wanayachukulia maneno ya Mungu kama kanuni za kufuatwa. Watu kama hawa hawatii maneno ya Mungu katika vitendo; wanaridhisha tu mwili, na kutenda ili watu wengine wawaone. Kanuni na kaida hizi za kidini zote zina asili yake kwa binadamu; hazitoki kwa Mungu. Mungu hafuati sheria, wala Haathiriwi na sheria yoyote. Badala yake, Yeye hufanya mambo mapya kila siku, Akitimiza kazi ya vitendo. Kama watu katika Kanisa la Kanuni Tatu za Binafsi, wanaojiwekea mipaka kwa matendo kama vile kuhudhuria ibada za asubuhi kila siku, kutoa sala za jioni na sala za shukrani kabla ya milo, na kutoa shukrani katika vitu vyote—bila kujali kiasi wanachofanya ama wanakifanya kwa muda gani, hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanapoishi kati ya kanuni na kuzingatia mbinu za utendaji, Roho Mtakatifu hawezi kufanya kazi, kwa sababu mioyo yao imejazwa na kanuni na fikira za kibinadamu. Kwa hivyo, Mungu hawezi kuingilia kati na kuwafanyia kazi, na wanaweza tu kuendelea kuishi wakidhibitiwa na sheria. Watu kama hawa daima hawawezi kupokea sifa ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Ikiwa, katika imani yao, watu wanachukulia ukweli kuwa seti ya kanuni ya kufuatwa, basi si imani yao ina uwezekano wa kugeuka kuwa taratibu za dini? Na tofauti kati ya taratibu hizi za dini na Ukristo ni ipi? Wanaweza kuwa wa kina na wenye maendeleo zaidi katika jinsi wanavyosema mambo, lakini iwapo imani yao imegeuka tu kuwa seti ya kanuni na aina ya utaratibu, basi hilo halimaanishi kwamba imegeuka kuwa Ukristo? (Ndiyo, linamaanisha hivyo.) Kuna tofauti kati ya mafundisho ya kale na mapya, lakini ikiwa mafundisho hayo ni aina ya nadharia tu na yamekuwa tu aina ya utaratibu, aina ya mafundisho kwa watu—na, vilevile, ikiwa hawawezi kupata ukweli kutoka kwayo au kuingia katika uhalisi wa ukweli—basi si imani yao ni sawa na Ukristo? Kimsingi, je, si huu ni Ukristo? (Ndiyo, ni Ukristo.) Kwa hivyo katika tabia yenu na utendaji wa wajibu wenu, ni katika vitu vipi ambavyo mna maoni na hali ambazo ni sawa na ama zinazofanana na zile za waumini wa Ukristo? (Katika kufuata kanuni, na katika kujihami kwa maneno na mafundisho. ) (Katika kuzingatia sura ya kuwa watu wa dini na kuonyesha tabia nzuri, na kuwa wanaomcha Mungu na wanyenyekevu.) Mnatafuta kuwa na tabia nzuri kwa nje, kufanya kila mwezalo kujionyesha kuwa na sura ya dini, kuzungumza kanuni za dini, kusema mambo ambayo ni sahihi kidini, kufanya mambo yanayokubalika kiasi katika fikira na mawazo ya binadamu, na kujifanya kuwa waadilifu. Mnazungumza maneno na kanuni kwa kujigamba, mkiwafundisha watu kufanya mema, wawe watu waadilifu, na kuelewa ukweli; mnajidai kuwa watu wa dini, na mnaonyesha hali ya juujuu ya dini katika kila kitu msemacho na kufanya. Hata hivyo, kwa vitendo, hamjawahi kutafuta ukweli; punde tu mnapokabiliwa na tatizo, mnatenda kulingana na mapenzi ya binadamu, mkimtupa Mungu kando. Hamjawahi kutenda kulingana na kanuni za ukweli, hamjawahi kuelewa kinachozungumziwa katika ukweli, yale yaliyo mapenzi ya Mungu, viwango anavyohitaji kutoka kwa mwanadamu ni vipi—hamjawahi kuyachukulia mambo haya kwa uzito ama kujishughulisha nayo. Je, haya matendo ya nje na hali hizi za ndani za watu—yaani, imani kama hii—zinajumuisha kumcha Mungu na kuepuka uovu? Ikiwa hakuna uhusiano kati ya imani ya watu na ufuatiliaji wao wa ukweli, basi wanamwamini Mungu au la? Bila kujali idadi ya miaka ambayo watu wasio na uhusiano na kufuatilia ukweli wanaweza kumwamini, je, wanaweza kupata uchaji Mungu wa kweli na halisi na kuepuka uovu au la? (Hawawezi.) Kwa hivyo tabia ya nje ya watu kama hao ni ipi? Wanaweza kuitembea njia ya aina ipi? (Njia ya Mafarisayo) Je, wao hutumia siku zao wakijiandaa na nini? Je, si ni kwa maneno na nadharia? Je, wao hutumia siku zao wakijiandaa, wakivalia maneno na nadharia ili kujifanya kama Mafarisayo zaidi, wa dini zaidi, kama watu ambao hudhaniwa kwamba humtumikia Mungu zaidi? Asili ya mbinu hizi zote ni ipi hasa? Je, ni kumwabudu Mungu? Ni imani ya kweli Kwake? (La, siyo.) Kwa hivyo wanafanya nini? Wanamdanganya Mungu; wanapitia tu hatua za mchakato fulani, na kujihusisha katika taratibu za dini. Wanapeperusha bendera ya imani na kufanya kaida za dini, wakijaribu kumdanganya Mungu ili kufikia lengo lao la kubarikiwa. Hawamwabudu Mungu hata kidogo. Mwishoni, je, si kundi kama hilo la watu litaishia tu kama wale walio ndani ya kanisa ambao hudhaniwa kwamba wanamtumikia Mungu, na ambao hudhaniwa kwamba wanamwamini na kumfuata Mungu?

Kimetoholewa kutoka katika “Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Wanadamu wengine wana upendeleo wa kujivutia nadhari. Mbele ya ndugu zao, wanasema kweli ni wadeni wa Mungu, lakini akiwapa kisogo, hawatendi ukweli ila wanafanya tofauti kabisa. Je, hawa si ni Mafarisayo wa dini? Mtu ambaye anampenda Mungu kwa kweli na ana ukweli ni yule ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, lakini bila ya hafichui kwa nje. Yeye yuko tayari kutenda ukweli wakati mambo yanapotokea wala hasemi au kutenda kinyume cha dhamiri yake. Anaonyesha hekima wakati mambo yanapotokea na ni mwenye maadili katika matendo yake, bila kujali hali. Mtu kama huyu ni mtu ambaye anahudumu kwa kweli. Kuna watu wengine ambao mara nyingi shukrani zao kwa kuwa wadeni wa Mungu ni kwa mdomo tu. Siku zao huisha wakiwa na nyuso za wasiwasi, kuonekana wameathiriwa, na kuvalia nyuso za huzuni. Hali ya kuchukiza kweli! Na kama ungewauliza, “Ni kwa njia zipi wewe ni mdeni wa Mungu? Tafadhali niambie!” Hawangeweza kutamka lolote. Kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu, basi usizungumze kwa nje kuhusu hilo; badala yake, onyesha upendo wako kwa Mungu kwa njia ya matendo halisi, na kumwomba kwa moyo wa kweli. Wale wanaotumia maneno pekee kushughulika na Mungu ni wanafiki wote! Baadhi yao husema kuwa wao ni wadeni kwa Mungu katika kila sala, na kuanza kulia wakati wowote wanaposali, hata bila kuguswa na Roho Mtakatifu. Watu kama hawa wamepagawa na kaidi na fikira za kidini; wanaishi kulingana na hizo kaidi na fikra, daima wakiamini kwamba matendo kama hayo humpendeza Mungu, na kwamba kumcha Mungu kijuujuu au machozi ya huzuni ndivyo Mungu hupendelea. Ni kitu kipi kizuri kinachoweza kutoka kwa watu kama hao wa kushangaza? Ili kuonyesha unyenyekevu wao, baadhi yao huonyesha neema bandia wakati wanapozungumza mbele ya watu wengine. Baadhi yao kwa makusudi ni wanyonge mbele ya watu wengine, kama mwanakondoo asiye na nguvu yoyote. Je, hii ni tabia ya watu wa ufalme? Mtu wa ufalme sharti awe wa kusisimua na aliye huru, asiye na hatia na aliye na uwazi, mwaminifu na wa kupendeza; mtu aishiye katika hali ya uhuru. Ana uadilifu na heshima, na anaweza kushuhudia kokote aendako; yeye ni yule anayependwa na Mungu na wanadamu. Wale ambao ni wanafunzi katika imani huwa na matendo mengi ya nje; lazima kwanza wapitie kipindi cha ushughulikiaji na kuvunjwa. Wale ambao wana imani kwa Mungu katika nyoyo zao hawawezi kutofautishwa na wengine kwa nje, lakini vitendo na matendo yao ni ya kupongezwa kwa wengine. Watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza chukuliwa kuwa wanaishi kwa kudhihirisha neno la Mungu. Ukihubiri injili kila siku kwa mtu huyu na yule, ukiwaleta kwa wokovu, ilhali mwishowe, wewe bado unaishi katika sheria na mafundisho, basi wewe huwezi kuleta utukufu kwa Mungu. Watu wa aina hii ni watu wa dini, na wanafiki pia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Katika Imani, Mtu Lazima Alenge Ukweli—Kujihusisha na Kaida za Dini Sio Imani

Wakati wa kuingia kwa mwanadamu, maisha huwa ya kuchosha daima, yaliyojaa sifa za lazima zisizobadilika za maisha ya kiroho, kama vile kufanya maombi, kula na kunywa maneno ya Mungu kiasi, au kufanya mikusanyiko, ili watu wahisi daima kwamba kumwamini Mungu hakuleti raha kuu. Shughuli za kiroho kama hizo kila mara hutekelezwa kwa msingi wa tabia ya asili ya binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani. Ingawa wakati mwingine watu wanaweza kupokea nuru ya Roho Mtakatifu, kufikiri kwao kwa asili, tabia, mitindo ya maisha na mienendo bado imekita mizizi, na kwa hiyo asili yao husalia isiyobadilika. Shughuli za kishirikina ambazo watu wanashughulika nazo ndizo Mungu anazichukia sana, lakini watu wengi bado hawawezi kuachana nazo, wakifikiri kwamba shughuli hizi za kishirikina zimeamriwa na Mungu, na hata leo bado hawajaziacha kabisa. Mambo kama mipango ambayo vijana hufanya kwa ajili ya sherehe za arusi au mahari, zawadi za pesa, dhifa, na maneno mengine na virai vinavyohusiana na matukio ya sherehe; maneno ya zamani ambayo yamerithishwa; shughuli zote za kishirikina zisizokuwa na maana zinazofanywa kwa niaba ya wafu na taratibu za mazishi; yote haya yanachukiwa sana na Mungu. Hata siku ya ibada (ikiwemo Sabato, kama inavyoadhimishwa na ulimwengu wa dini) inachukiwa naye; mahusiano ya kijamii na mawasiliano ya kidunia kati ya mwanamme na mwanamme pia yanachukiwa na kukataliwa zaidi na Mungu. Hata Sikukuu ya Machipuko na Siku ya Krismasi, ambazo zinajulikana kwa kila mtu, haziamriwi na Mungu, sembuse wanasesere na mapambo ya sherehe za siku kuu hizi kama vile mashairi, mafataki, kandili, Komunyo, zawadi za Krismasi na sherehe za Krismasi—je, sio sanamu katika akili za wanadamu? Kumega mkate siku ya Sabato, mvinyo, na kitani nyembamba navyo ni sanamu zaidi. Siku zote za sherehe za kijadi ambazo ni maarufu sana nchini China, kama vile Siku ya kuinua Vichwa vya Joka, Sikukuu ya Mashua ya Joka, Sikukuu ya Majira ya Kati ya Kupukutika, Sikukuu ya Laba, na Siku ya Mwaka Mpya, na sikukuu zisizothibitika katika ulimwengu wa kidini, kama vile Pasaka, Siku ya Ubatizo, na Siku ya Krismasi, zote hizi zimepangwa na kurithishwa kwa watu wengi tangu zama za kale hadi leo. Ni uwezo mkubwa wa fikra za binadamu na dhana bunifu ambazo zimewaruhusu kurithishwa hadi leo. Zinaonekana kuwa hazina kasoro, lakini kwa kweli ni hila ambazo Shetani alifanya kwa binadamu. Kadri Shetani wanavyoishi katika eneo fulani, na kadri eneo hilo lilivyo nyuma kimaendeleo na kutofaa, ndivyo desturi zake za kikabaila zinakuwa nyingi zaidi. Vitu hivi vinawafunga watu kwa nguvu, bila kutoa nafasi kwa ajili ya maendeleo. Sikukuu nyingi katika ulimwengu wa kidini zinaonekana kuonyesha ubunifu mkubwa na zinaonekana kujenga daraja kwa kazi ya Mungu, lakini kweli ni vifungo visivyoshikika ambavyo Shetani hutumia kuwafunga watu ili wasije kumjua Mungu—hizi zote ni hila za ujanja za Shetani. Kwa kweli, hatua ya kazi ya Mungu inapomalizika, tayari Amekwishaharibu zana na mtindo wa wakati huo, bila kuacha alama yoyote. Hata hivyo, “waumini wasalihina” bado wanaabudu vitu hivyo vya kushikika; wakati huo huo wanaacha kile Alicho nacho Mungu, bila hata kukichunguza zaidi, wakionekana wamejawa na upendo wa Mungu lakini kwa uhalisi walimtoa ndani ya nyumba zamani sana na kumweka Shetani mezani kwa ajili ya kumwabudu. Sanamu ya Yesu, Msalaba, Maria, Ubatizo wa Yesu na Karamu ya Mwisho—watu wanavichukulia hivi kama Bwana wa Mbinguni, wanaviabudu wakati wote wakilia kwa sauti kwa kurudiarudia “Bwana, Baba wa Mbinguni.” Je, huu wote sio utani? …

Njia bora zaidi ya kubadilisha tabia ya mwanadamu ni kuondoa vitu hivi vyenye sumu kubwa katika mioyo ya wanadamu, kuwaruhusu watu kuanza kubadilisha fikira na maadili yao. Kwanza kabisa, watu wanatakiwa kuona waziwazi kwamba kaida zote hizi za kidini, shughuli za kidini, miaka na miezi, na sikukuu zote ni za kumchukiza Mungu. Wanatakiwa kuwa huru kutoka kwa vifungo hivi vya fikira za kishirikina na kuondoa kila alama ya kishirikina iliyozama kabisa ndani. Mambo haya yote ni sehemu ya kuingia kwa mwanadamu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Maisha ya kiroho yanayofaa yanajumuisha kusali, kula na kunywa neno la Mungu, kushiriki kuhusu ukweli, kufanya wajibu wa mtu, na kuimba nyimbo za kidini za sifa vizuri. Matendo haya ni ya manufaa sana kwa watu kuingia katika ukweli na mabadiliko ya tabia. Hata hivyo, kaida za dini, ni kufanya vitu kwa namna isiyo ya dhati tu, kutomaanisha kile anachosema mtu, na kuwa hafifu, mzembe, na mnafiki. Hizi zote ni mbinu za juu juu zinazomdanganya Mungu. Kutekeleza kaida za dini kumetengwa na uhalisi na hauna uhalisi hata kidogo—ni kusema maneno bila sauti tu ili kujionyesha, na ni jambi lisilo na matokeo kabisa. Maisha ya kufaa ya kiroho yanategemezwa kwa uhalisi kabisa; yanafanyika kutokana na kuunganishwa na uhalisi, na aidha, ni uaminifu utokao kwa moyo, na hivyo, ni ya kufaa na hukubaliwa na Mungu kwa furaha. Chukua, kwa mfano, maombi yanayofaa: Yanatoka kwa taabu za kweli za mtu na hutoka kwa mahitaji yake maishani. Yanawakilisha umuhimu wa kweli wa nafsi yake ya ndani, na kwa hiyo hupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hata hivyo, maombi katika muktadha wa kaida za dini hukiuka kanuni hii. Mtu anaweza kwa nasibu kusema mistari michache ya maombi bila sauti wakati wowote au mahali popote bila kuyamaanisha, wakati moyoni mwake anahisi kuchoshwa na kukosa msukumo. Anawezaje kupokea kazi ya Roho Mtakatifu? Ni dhahiri kwamba hataki kuomba lakini anajilazimisha kufanya hivyo—hili ni jambo linalokiuka kanuni. Katika hali za kawaida, haiwezekani kwa mtu kuomba bila kukoma; wakati haombi, mtu anaweza kula na kunywa neno la Mungu na anaweza kushiriki kuhusu ukweli. Hii ni kwa sababu maisha ya kiroho ni jambo ambalo haliwezi kudhibitiwa, lakini yanaamuliwa tu kulingana na hali ya mtu mwenyewe na mahitaji ya kweli. Hii ndiyo njia ya pekee ya kupata matokeo mazuri. Maisha ya kweli ya kiroho ni ya kufaa na yanafanyika wakati mambo yanatokea kwa kawaida. Hayajumuishi hata kidogo kutii kanuni au kufanya kaida. Kaida zote za dini ni kanuni na unafiki uliotengenezwa na watu; hazihusishi kutafuta kwa ari. Hii ndiyo maana Mungu anaziita za kinafiki. Maisha ya kufaa ya kiroho hutukia kwa kupitia kazi ya Mungu, na ni muungano wa kazi ya Roho Mtakatifu na tendo lililoanzishwa na binadamu. Ingawa hakuna kanuni au kaida katika aina hii ya maisha ya kiroho, kweli yanaleta matokeo thabiti ya manufaa. Unapohamia kutoka kwa kaida za dini hadi maisha ya kufaa ya kiroho, ni hapo tu ndipo umeingia kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp