Kazi ya Roho Mtakatifu ni nini? Kazi ya Roho Mtakatifu hudhihirishwaje?

12/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu. Wakati watu wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndani yao ni watakatifu hasa. Wale ambao wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu huishi kwa kudhihirisha upendo wa Mungu, upendo wa kaka na dada zao, na kufurahia vitu ambavyo Mungu hufurahia na kuchukia vitu ambavyo Mungu huchukia. Watu ambao wanaguswa na kazi ya Roho Mtakatifu wana ubinadamu wa kawaida, na wao daima hufuatilia ukweli na wanamiliki ubinadamu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani ya watu, hali zao huwa nzuri zaidi na zaidi, na ubinadamu wao unakuwa wa kawaida zaidi na zaidi, na ingawa ushirikiano wao mwingine unaweza kuwa mpumbavu, motisha zao ziko sahihi, kuingia kwao ni kwa hali nzuri, hawajaribu kukatiza, na hakuna nia mbaya ndani yao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida na ya kweli, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa mwanadamu kulingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na Yeye huwapa nuru na kuongoza watu kulingana na ufuatiliaji halisi wa watu wa kawaida. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa watu, Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, Anawakimu kwa msingi wa mahitaji yao, na Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kwa hali nzuri kwa msingi wa kile ambacho wanakosa, na kwa upungufu wao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwapa watu nuru na kuwaongoza katika maisha halisi; wakipitia maneno ya Mungu katika maisha yao tu ndipo wanaweza kuona kazi ya Roho Mtakatifu. Iwapo, katika maisha yao ya kila siku, watu wako katika hali nzuri na wana maisha ya kawaida ya kiroho, basi wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali kama hiyo, wakati wanakula na kunywa maneno ya Mungu wana imani, wakati wanaomba wanatiwa moyo, wakati kitu kinawafanyikia wao si baridi, na wakati kinawafanyikia wanaweza kuona masomo ambayo Mungu anawahitaji kujifunza, na hawako baridi, ama dhaifu, na ingawa wana ugumu wa kweli, wako tayari kukubali mipango yote ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani

Roho Mtakatifu anapofanya kazi ili kuwapa watu nuru, kwa ujumla Yeye huwapa ufahamu wa kazi ya Mungu, na ufahamu wa kuingia kwao kwa kweli na hali yao ya kweli. Yeye pia huwasababisha waelewe nia za dharura za Mungu na madai Yake kwa mwanadamu leo, ili wawe na azimio la kudhabihu kila kitu ili wamridhishe Mungu, wampende Mungu hata wakikumbana na mateso na dhiki, na kuwa shahidi kwa Mungu hata ikimaanisha kumwaga damu yao au kutoa maisha yao, na kufanya hivyo bila majuto. Ukiwa na azimio la aina hii, inamaanisha unayo misisimko na kazi ya Roho Mtakatifu—lakini jua kwamba huna misismko ya aina hii kila wakati. Wakati mwingine katika mikutano unapoomba na kula na kunywa maneno ya Mungu, unaweza kuhisi kuguswa na kupata msukumo mno. Linaonekana jambo la kuburudisha kabisa wakati watu wengine wanashiriki baadhi ya uzoefu na ufahamu wao wa maneno ya Mungu, na moyo wako uko wazi na mchangamfu kabisa. Hii yote ni kazi ya Roho Mtakatifu. Kama wewe ni kiongozi na Roho Mtakatifu anakupa nuru na mwangaza usio wa kawaida unapoenda kanisani kufanya kazi, Anakupa umaizi wa shida ambazo zipo katika kanisa, Anakuwezesha kujua jinsi ya kushiriki kuhusu ukweli ili kuzitatua, Anakufanya uwe mwenye bidii ya ajabu sana, mwenye kuwajibika na uliye makini katika kazi yako, hii yote ni kazi ya Roho Mtakatifu.

Kimetoholewa kutoka katika “Utendaji (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni ya kawaida, na Anapofanya kazi kwa watu bado wana shida, bado wanalia, bado wanateseka, bado ni dhaifu, na bado kuna mengi ambayo si dhahiri kwao, ilhali katika hali kama hiyo wanaweza kujisitisha kurudia mazoea mabaya, na wanaweza kumpenda Mungu, na ingawa wanalia na wana dhiki ndani, bado wanaweza kumsifu Mungu; kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni ya kawaida, na si ya mwujiza hata kidogo. Watu wengi sana huamini kwamba, punde tu Roho Mtakatifu huanza kufanya kazi, mabadiliko hutokea katika hali ya watu na mambo muhimu kuwahusu yanaondolewa. Imani kama hizo ni za uwongo. Roho Mtakatifu afanyapo kazi ndani ya mwanadamu, mambo baridi ya mwanadamu bado yako hapo na kimo chake kinabaki sawa na awali, lakini ana mwangaza na nuru ya Roho Mtakatifu, na hivyo hali yake ni ya kimatendo zaidi, hali ndani yake ni za kawaida, na anabadilika kwa haraka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani

Kazi yote ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida, na halisi. Usomapo maneno ya Mungu na kuomba, ndani unang’aa na kuwa imara, dunia ya nje haiwezi kuhitilafiana na wewe, ndani unakuwa radhi kumpenda Mungu, uko radhi kushughulika na mambo chanya, na unachukia dunia potovu; huku ni kuishi ndani ya Mungu. Si kama watu wasemavyo, kufurahia kupindukia—maneno kama hayo si halisi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kujua Uhalisi

Mara nyingine, wakati ambapo unafurahia maneno ya Mungu, roho yako huguswa, na wewe huhisi kwamba huna budi kumpenda Mungu, kwamba kuna nguvu nyingi ndani yako, na kwamba hakuna chochote usichoweza kuweka kando. Kama wewe unahisi hivi, basi umeguswa na Roho wa Mungu, na moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na utamwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Sisi kweli tumejaaliwa na kuteuliwa na Wewe. Utukufu Wako hunipa fahari, na inaonekana ya kuleta sifa kuu kwa mimi kuwa mmoja wa watu Wako. Nitatumia chochote na kutoa chochote ili kufanya mapenzi Yako, na nitayatoa maisha yangu yote, na juhudi za maisha yangu yote, Kwako.” Unapoomba hivi, kutakuwa na upendo usioisha na utiifu wa kweli kwa Mungu ndani ya moyo wako. Je, umewahi kuwa na tukio kama hili? Kama watu huguswa mara kwa mara na Roho wa Mungu, basi wako radhi hasa kujitolea wenyewe kwa Mungu katika maombi yao: “Ee Mungu! Ningependa kutazama siku Yako ya utukufu, na ningependa kuishi kwa ajili Yako—hakuna kilicho cha thamani au maana zaidi kuliko kuishi kwa ajili Yako, na sina hamu hata kidogo ya kuishi kwa ajili ya Shetani na mwili. Wewe huniinua kwa kuniwezesha mimi kuishi kwa ajili Yako leo.” Wakati ambapo umeomba kwa njia hii, utahisi kwamba huna budi ila kutoa moyo wako kwa Mungu, kwamba lazima umpate Mungu, na kwamba ungechukia kufa bila kumpata Mungu wakati ambapo uko hai. Baada ya kunena ombi hilo, kutakuwa na nguvu isiyoisha ndani yako, na hutajua hiyo hutoka wapi; ndani ya moyo wako kutakuwa na nguvu bila kikomo, na utakuwa na hisi kwamba Mungu ni wa kupendeza sana, na kwamba Anastahili kupendwa. Huu ndio wakati ambapo utakuwa umeguswa na Mungu. Wale wote ambao wamekuwa na tukio hilo wameguswa na Mungu. Kwa wale ambao mara kwa mara huguswa na Mungu, mabadiliko hutokea ndani ya maisha yao, wao huweza kufanya azimio lao na wako radhi kumpata Mungu kabisa, upendo kwa Mungu ndani yao ni thabiti zaidi, mioyo yao imeelekea kwa Mungu kabisa, wao huwa hawastahi familia, ulimwengu, matatizo, au siku zao za baadaye, na wao huwa radhi kutoa juhudi za maisha yote kwa Mungu. Wale wote ambao wameguswa na Roho wa Mungu ni watu wanaofuatilia ukweli, na ambao huwa na tumaini la kufanywa wakamilifu na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

Unaweza kuwa mpumbavu, na kunaweza kuwa hakuna utofautishaji wowote ndani yako, lakini Roho Mtakatifu anapaswa tu kufanya kazi ili kuwe na imani ndani yako, ili wewe daima uhisi kwamba huwezi kumpenda Mungu vya kutosha, ili uwe tayari kushiriki, uwe tayari kushiriki bila kujali ugumu mkuu ulio mbele. Mambo yatakufanyikia na haitakuwa wazi kwako iwapo yanatoka kwa Mungu ama kwa Shetani, lakini utaweza kungoja, na hutakuwa baridi wala mzembe. Hii ndiyo kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao, watu bado hukabiliwa na ugumu wa kweli, wakati mwingine wanalia, na wakati mwingine kuna mambo ambayo hawawezi kuyashinda, lakini hii yote ni hatua ya kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Ingawa hawashindi mambo hayo, na ingawa, wakati huo, wao ni dhaifu na hulalamika, baadaye bado wanaweza kumpenda Mungu na imani dhabiti. Ubaridi wao hauwezi kuwazuia kuwa na uzoefu wa kawaida, na bila kujali kile watu wengine husema, na jinsi wanavyowashambulia, bado wanaweza kumpenda Mungu. Wakati wa maombi, daima wanahisi kwamba walikuwa wadeni wa Mungu sana, na wanaamua kumridhisha Mungu na kuukataa mwili wakati wanakabiliwa na mambo kama hayo tena. Nguvu hii inaonyesha kuna kazi ya Roho Mtakatifu ndani yao, na hii ndiyo hali ya kawaida ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani

Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisi, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo inazidi akili ya mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya akili ya kawaida ya mwanadamu, na haizidi ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, na ubinadamu wako unakuwa wa kawaida kabisa. Watu wanapata maarifa mengi ya tabia yao potovu ya kishetani, na iliyopotoka, na asili ya mwanadamu, na pia wanapata shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Hiyo ni kusema, maisha ya mwanadamu yanakua zaidi na zaidi, na tabia upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maisha ya mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Roho Mtakatifu ana njia ya kutembea katika kila mtu, na humpa kila mtu fursa za kukamilishwa. Kupitia uhasi wako unajulishwa upotovu wako mwenyewe, na kisha kwa njia ya kuacha uhasi utapata njia ya kutenda, na huku ndiko kukamilishwa kwako. Aidha, kwa njia ya mwongozo na mwangaza wa siku zote wa mambo fulani chanya ndani yako, utatimiza shughuli yako kwa kuamili na kukua katika umaizi na kupata utambuzi. Wakati hali zako ni nzuri, uko tayari hasa kusoma neno la Mungu, na hasa tayari kumwomba Mungu, na unaweza kuyahusisha mahubiri unayoyasikia na hali zako mwenyewe. Kwa nyakati kama hizo Mungu hukupatia nuru na kukuangaza ndani, na kukufanya utambue mambo fulani ya kipengele chanya. Huku ni kukamilishwa kwako katika kipengele chanya. Katika hali hasi, wewe ni dhaifu na hasi, na huhisi kuwa huna Mungu moyoni mwako, lakini Mungu hukuangaza, akikusaidia kupata njia ya kutenda. Kutoka nje ya hili ni kupata ukamilisho katika hali chanya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa

Wakati mwingine Mungu hukupa aina fulani ya hisia, hisia inayokusababisha upoteze starehe yako ya ndani kabisa, na unapoteza uwepo wa Mungu, kiasi kwamba unatumbukia gizani. Hii ni aina ya usafishaji. Wakati wowote unapofanya kitu chochote, hicho huenda mrama, au kugonga ukuta. Hii ni nidhamu ya Mungu. Wakati mwingine, unapofanya kitu ambacho si cha utiifu na cha uasi kwa Mungu, huenda hakuna mtu mwingine anajua kukihusu—lakini Mungu anajua. Yeye hatakuachilia, na Atakufundisha nidhamu. Kazi ya Roho Mtakatifu ni yenye kina sana. Kwa makini sana Anatazama kila neno na tendo la watu, kila tendo na mwendo wao, na kila wazo lao na fikira ili watu waweze kupata ufahamu wa ndani wa vitu hivi. Unafanya kitu mara moja na kinaenda mrama, unakifanya kitu tena na bado kinaenda mrama, na hatua kwa hatua utapata kuelewa kazi ya Roho Mtakatifu. Kupitia kufundishwa nidhamu mara nyingi, utajua cha kufanya ili kuwa sambamba na mapenzi ya Mungu na kile kisichoambatana na mapenzi Yake. Mwishowe, utakuwa na majibu sahihi kwa uongozi wa Roho Mtakatifu ndani yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp