Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kazi na Kuonekana kwa Mungu | Dondoo 65

Siku hiyo ambayo vitu vyote vilifufuliwa, Nilikuja miongoni mwa wanadamu, na Nimeshinda naye kwa siku zilizokuwa za ajabu usiku na mchana. Ni katika hatua hii tu ndipo mwanadamu anaona wepesi Wangu wa kufikiwa, na vile uhusiano wake na Mimi unavyozidi kuwa mwingi, anaona baadhi ya kile Ninacho na Nilicho—na kwa sababu hii, anapata ufahamu kunihusu. Miongoni mwa watu wote, Ninainua kichwa Changu na kutazama, na wote wananiona. Hata hivyo, wakati maafa yanaikumba dunia, wanakuwa na wasiwasi mara moja, na sura Yangu inatoweka kutoka katika nyoyo zao; wakishikwa na hofu kutokana na kufika kwa maafa, hawasikii kusihi Kwangu. Nimepita kati ya wanadamu kwa miaka mingi, lakini hajawahi kufahamu hili, na hajawahi kunijua. Leo Namwambia kwa kinywa Changu mwenyewe, na kufanya watu wote waje mbele Yangu kupata kitu kutoka Kwangu, lakini bado wanaendelea kukaa mbali Nami, na hivyo basi hawanijui. Wakati nyayo Zangu zitaukanyaga ulimwengu mzima, mwanadamu ataanza kutafakari juu yake mwenyewe, na watu wote watakuja Kwangu na kusujudu mbele Zangu na kuniabudu. Hii itakuwa siku ya utukufu Wangu, siku ya kurudi Kwangu, na pia siku ya kuondoka Kwangu. Sasa, Nimeanza Kazi Yangu miongoni mwa watu wote, Nimeanza kirasmi, katika ulimwengu wote, ukamilishaji wa mpango Wangu wa usimamizi. Kuanzia sasa na kuendelea, wowote ambao si waangalifu wanastahili kutumbukizwa katikati ya kuadibu kusiko na huruma wakati wowote. Hii si kwa sababu Mimi sina utu, lakini ni hatua ya mpango Wangu wa usimamizi; zote lazima ziendelee kulingana na hatua za Mpango Wangu, na hakuna mwanadamu anayeweza kubadili hali hii. Ninapoanza kirasmi Kazi Yangu, watu wote wanatembea kama Mimi hatua kwa hatua, kiasi kwamba watu katika ulimwengu wote wanakuwa katika hatua na Mimi, kuna “shangwe” ulimwengu mzima, na mwanadamu anaendelezwa mbele na Mimi. Kwa sababu hii, joka kubwa jekundu mwenyewe anachapwa na Mimi mpaka anakuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na wazimu, na anahudumia Kazi Yangu, na, licha ya kutokuwa na nia, anashindwa kufuata tamaa zake mwenyewe, na kukosa njia nyingine ila kujiwasilisha kwa udhibiti Wangu. Katika mipango Yangu yote, joka kubwa jekundu ni foili Yangu, adui Wangu, na pia mtumishi Wangu; kwa hivyo, Sijawahi kushusha “mahitaji” Yangu kwake. Kwa hivyo, hatua ya mwisho ya kazi Yangu katika mwili inakamilika katika nyumba ya joka huyu. Kwa njia hii, joka kubwa jekundu anapata uwezo zaidi wa kunitumikia Mimi vizuri, kwa njia ambayo Mimi Nitamshinda na kukamilisha Mpango Wangu. Ninapofanya kazi, malaika wote wanaanzisha vita vya maamuzi na Mimi na kuamua kutimiza matakwa Yangu katika hatua ya mwisho, ili watu walio duniani wajitoe Kwangu kama malaika, na wasiwe na haja ya kunipinga Mimi, na wasifanye chochote ambacho kinaniasi. Hii ndio elimumwendo ya kazi Yangu kotekote katika ulimwengu.

Madhumuni na umuhimu wa kuwasili Kwangu miongoni mwa mwanadamu ni kuwaokoa wanadamu wote, kuwaleta watu wote katika nyumba Yangu, kuunganisha mbingu pamoja na ardhi, na kufanya mwanadamu kufikisha “ishara” kati ya mbingu na dunia, kwa maana hiyo ndiyo kazi asili ya mwanadamu. Wakati Nilimuumba mwanadamu, Nilifanya mambo yote yawe tayari kwa ajili ya mwanadamu, na baadaye, Mimi Nikamruhusu mwanadamu kupokea utajiri Niliompa kulingana na masharti Yangu. Ndio maana Nasema ni kwa uongozi Wangu ndio maana wanadamu wote wamefikia siku hii. Na haya yote ni Mpango Wangu. Miongoni mwa watu wote, idadi kubwa ya watu ipo chini ya ulinzi wa Upendo Wangu, na idadi kubwa inaishi chini ya kuadibu kwa chuki Yangu. Ingawa watu wote wanaomba Kwangu, bado hawana uwezo wa kubadili hali yao ya sasa; mara tu wamepoteza matumaini, wanaweza tu kuwacha hali asili ichukue mkondo wake na kusitisha uasi Kwangu, kwa maana haya ndiyo yote yanayoweza kukamilishwa na mwanadamu. Inapokuja kwa hali ya maisha ya mwanadamu, mwanadamu bado hajapata maisha halisi, yeye bado hajaona kupita katika udhalimu, ukiwa, na hali duni ya dunia—na hivyo, kama haingekuwa ujio wa maafa, watu wengi bado wangekumbatia hali halisi ya dunia, na bado wangejishughulisha katika ladha ya “uzima.” Je, hii si hali halisi ya dunia? Je, hii si sauti ya wokovu Ninayonena kwa mwanadamu? Kwa nini, miongoni mwa wanadamu, hakuna kamwe aliyenipenda kwa kweli? Ni kwa nini mwanadamu ananipenda tu katikati ya kuadibu na majaribu, lakini hakuna mwanadamu Anayenipenda chini ya ulinzi Wangu? Mimi Nimetoa kuadibu Kwangu mara nyingi juu ya mwanadamu. Wao wanaiangalia, kisha wanaipuuza, na hawawezi kujifunza na kutafakari juu yake kwa wakati huu, na hivyo yote yanayokuja juu ya mwanadamu ni hukumu isiyo na huruma. Hii ni mojawapo tu ya mbinu Zangu za kazi, lakini bado ni kwa ajili ya kumbadili mwanadamu na kumfanya aweze kunipenda.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 29

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp