Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Siri Kuhusu Biblia | Dondoo 272

02/10/2020

Leo, watu wanaamini kwamba Biblia ni Mungu, na kwamba Mungu ni Biblia. Na hivyo pia, wanaamini kwamba maneno yote ya Biblia ni maneno pekee ambayo Mungu alizungumza, na kwamba yote yalizungumzwa na Mungu. Wale wanaomwamini Mungu hata wanafikia hatua ya kufikiri kwamba ingawa vitabu vyote sitini na sita vya Agano la Kale na Agano Jipya viliandikwa na watu, vyote viliandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na ni rekodi ya matamshi ya Roho Mtakatifu. Hii ni tafsiri ya watu yenye makosa, na haiafikiani kabisa na kweli. Kimsingi, mbali na vitabu vya unabii, sehemu kubwa ya Agano la Kale ni rekodi ya kihistoria. Baadhi ya nyaraka za Agano Jipya zinatokana na uzoefu wa watu, na baadhi zinatokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu; nyaraka za Paulo, kwa mfano, zilitokana na kazi ya mwanadamu, zote zilitokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na ziliandikwa kwa ajili ya makanisa, yalikuwa ni maneno ya kushawishi na kutia moyo kwa kaka na dada wa makanisa. Hayakuwa maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu—Paulo asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu, na wala hakuwa nabii, achilia mbali kuona maono. Nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya makanisa ya Efeso, Filadefia, Galatia, na makanisa mengineyo. Na hivyo, nyaraka za Paulo za Agano Jipya ni nyaraka ambazo Paulo aliandika kwa ajili ya makanisa, na sio uvuvio wa Roho Mtakatifu, wala sio matamshi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu. Ni maneno tu ya kushawishi, faraja, na kutia moyo ambayo aliyaandika kwa ajili ya makanisa wakati wa kazi yake. Na hivyo pia, ni rekodi zaidi ya kazi na muda ya Paulo. Ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada wote katika Bwana, na zilikuwa ni kwa ajili ya kuwafanya kaka na dada wa makani yote ya wakati huo kufuata ushauri wake na kudumu siku zote katika njia zote za Bwana Yesu. Kwa namna yoyote ile Paulo hakusema kuwa, iwe ni kwa makanisa ya wakati huo au makanisa ya wakati ujao, yote yanapaswa kula na kunywa vitu vyake, wala hakusema kwamba maneno yake yote yalitoka kwa Mungu. Kulingana na mazingira ya kanisa wakati huo, aliwasiliana tu na kaka na dada, na aliwashawishi, na akawaimarisha imani kwao; na aliwahubiria na kuwakumbusha watu na kuwashawishi. Maneno yake yalijikita katika mzigo wake mwenyewe, na aliwasaidia watu kupitia maneno haya. Alifanya kazi ya mitume wa kanisa wa wakati huo, alikuwa mfanyakazi ambaye alitumiwa na Bwana Yesu, na hivyo alipewa jukumu la makanisa, alipewa jukumu la kufanya kazi ya makanisa, alipaswa kujifunza kuhusu hali za ndugu—na kwa sababu hii, aliandika nyaraka kwa kaka na dada wote katika Bwana. Yote aliyoyasema yale yaliyokuwa ni ya kuadilisha na mazuri kwa watu yalikuwa sahihi, lakini hayakuwa yanawakilisha matamshi ya Roho Mtakatifu, na hakuwa anamwakilisha Mungu. Ni uelewa mbaya kupita kiasi, na makufuru makubwa sana kwa watu kuchukulia rekodi za uzoefu wa mwanadamu na nyaraka za mwanadamu kama maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu kwa makanisa! Hiyo ni kweli kabisa tunapokuja katika nyaraka ambazo Paulo aliziandika kwa ajili ya makanisa, maana nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada kulingana na mazingira na hali ya kila kanisa kwa wakati huo, na yalikuwa ni kwa ajili ya kuwashawishi kaka na dada katika Bwana, ili waweze kupokea neema ya Bwana Yesu. Nyaraka zake zilikuwa ni kwa ajili ya kuwaamsha kaka na dada wa wakati huo. Inaweza kusemwa kuwa huu ulikuwa ni mzigo wake mwenyewe, na pia ulikuwa ni mzigo aliopewa na Roho Mtakatifu; hata hivyo, alikuwa ni mtume aliyeyaongoza makanisa ya wakati huo, ambaye aliandika nyaraka kwa ajili ya makanisa na kuwashawishi, huo ulikuwa wajibu wake. Utambulisho wake ulikuwa tu ni mtume anayefanya kazi, na alikuwa ni mtume tu aliyetumwa na Mungu; hakuwa mtabiri, wala mtoa unabii. Kwa hivyo kwake, kazi yake mwenyewe na maisha ya kaka na dada yalikuwa na umuhimu mkubwa sana. Hivyo, asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu. Maneno yake hayakuwa maneno ya Roho Mtakatifu, wala yasingesemwa kuwa ni maneno ya Mungu, maana Paulo hakuwa chochote zaidi ya kiumbe wa Mungu, na hakika hakuwa Mungu aliyepata mwili. Utambulisho wake haukuwa sawa na ule wa Yesu. Maneno ya Yesu yalikuwa ni maneno ya Roho Mtakatifu, yalikuwa ni maneno ya Mungu, maana utambulisho wake ulikuwa ule wa Kristo—Mwana wa Mungu. Inawezekanaje Awe sawa na Paulo? Ikiwa watu wanaona nyaraka au maneno kama ya Paulo kama matamshi ya Roho Mtakatifu, na kuwaabudu kama Mungu, basi inaweza kusemwa tu kuwa ni watu wasiochagua kwa busara. Tukisema kwa ukali zaidi, haya sio makufuru? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na inawezekanaje watu wapigie magoti rekodi za nyaraka zake na maneno aliyoyazungumza kana kwamba yalikuwa ni kitabu kitakatifu, au kitabu cha mbinguni? Je, inawezekana maneno ya Mungu kutamkwa kwa kawaida na mwanadamu? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na hivyo, unasemaje—kwamba nyaraka alizoandika kwa ajili ya makanisa haziwezi kutiwa doa na mawazo yake mwenyewe? Inawezekanaje zisitiwe doa na mawazo ya kibinadamu? Aliandika nyaraka kwa ajili ya makanisa kulingana na uzoefu wake binafsi, na kiwango cha maisha yake binafsi. Kwa mfano, Paulo aliandika waraka kwa kanisa la Wagalatia ambao ulikuwa na maoni fulani, na Petro aliandika waraka mwingine, ambao ulikuwa na mtazamo mwingine. Ni upi kati ya hizo ulitoka kwa Roho Mtakatifu? Hakuna anayeweza kutoa jibu, hakika. Hivyo inaweza kusemwa tu kwamba wote wanawiwa na mzigo kwa makanisa, lakini barua zao zinawakilisha kimo chao, zinawakilisha vile wanavyowapatia na kuwasaidia kaka na dada, na vile wanavyowiwa na makanisa, na zinawakilisha tu kazi ya binadamu; hayakuwa ya Roho Mtakatifu kabisa. Ikiwa unasema kwamba nyaraka zake ni maneno ya Roho Mtakatifu, basi wewe ni mpumbavu, na unafanya makufuru! Nyaraka za Paulo na nyaraka nyingine za Agano Jipya ni sawa na kumbukumbu za viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi karibuni. Zipo sawa na vitabu vya Watchman Nee au uzoefu wa Lawrence, na kadhalika. Ni vile tu vitabu vya viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi karibuni havijajumuishwa katika Agano Jipya, lakini hulka ya watu hawa ni sawa: Kulikuwa na watu ambao walitumiwa na Roho Mtakatifu wakati fulani, na hawakuweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (3)

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp