Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 94

Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayakadiriki

Hebu tutazame Mwanzo 22:17-18. Hili ni fungu jingine lililozungumziwa na Yehova Mungu, Alisema kwa Ibrahimu, “Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.” Yehova Mungu alimbariki Ibrahimu mara nyingi ili uzao wake uweze kuzidishwa—na kuzidishwa hadi kiwango gani? Hadi kiwango kilichozungumziwa katika Maandiko: “kama nyota za mbinguni na mchanga ulio pwani.” Hii ni kusema kwamba Mungu alipenda kumpa Ibrahimu uzao uliokuwa mwingi kama nyota za mbinguni, na tele kama mchanga wa pwani. Mungu aliongea akitumia taswira, na kutoka kwenye taswira hii si vigumu kuona kwamba Mungu asingempa tu Ibrahimu uzao elfu moja, mbili, au hata elfu nyingi, lakini idadi isiyohesabika, iliyotosha kuwa uzao wa mataifa mengi ya dunia, kwani Mungu alimwahidi Ibrahimu kuwa atakuwa baba wa mataifa mengi. Na je, idadi hiyo iliamuliwa na binadamu au iliamuliwa na Mungu? Je, binadamu anaweza kudhibiti uzao kiasi gani atakaokuwa nao? Je, inategemea yeye? Haitegemei binadamu kujua kama atakuwa na uzao mbalimbali au la, sikwambii uzao mwingi kama “nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani.” Ni nani asiyetamani uzao wake kuwa mwingi kama nyota? Kwa bahati mbaya mambo huwa hayaendi namna unavyotaka. Licha ya vile mwanadamu anaweza kuwa na mbinu au kuweza kufanya jambo fulani, haitegemei binadamu; hakuna anayeweza kusimama nje ya kile ambacho kimeamriwa na Mungu. Kiasi ambacho Atakuruhusu, hicho ndicho utakachokuwa nacho: Kama Mungu atakupa kidogo, basi hutawahi kuwa na kingi, na kama Mungu Atakupa kingi haina faida wewe kuchukia kingi hicho ulichonacho. Je, hayo si kweli? Haya yote yanategemea Mungu, si binadamu! Binadamu hutawaliwa na Mungu, na hakuna yule anayeachwa!

Wakati Mungu alisema “nitazidisha mithili,” hili lilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, sawa na agano la upinde wa mvua, lingeweza kutimizwa milele hadi milele, na pia ilikuwa ahadi iliyotolewa na Mungu kwa Ibrahimu. Mungu pekee ndiye anayefuzu na kuweza kufanya ahadi hii kutimia. Bila kujali kama binadamu anaisadiki au la, bila kujali kama binadamu aikubali au la, na bila kujali namna binadamu anavyoitazama, na namna anavyoichukulia, haya yote yataweza kutimizwa, hadi mwisho wa maelezo ya agano hili, kulingana na matamshi yaliyotamkwa na Mungu. Matamshi ya Mungu hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko katika mapenzi au dhana za binadamu, na hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko ndani ya mtu yeyote, kitu au kifaa. Viumbe vyote vitaweza kutoweka lakini matamshi ya Mungu yatabaki milele hadi milele. Kinyume cha mambo ni, siku ambapo viumbe vyote vitatoweka ndiyo siku ile ile ambayo matamshi ya Mungu yataweza kutimizwa kabisa, kwani Yeye ndiye Muumba, na Anamiliki mamlaka ya Muumba, na nguvu za Muumba, na Anadhibiti vitu na viumbe vyote na nguvu zote za maisha; na Anaweza kusababisha kitu kutoka kule kusikokuwa na kitu, au kitu kuwa kile kisichokuwepo, na Anadhibiti mabadiliko ya viumbe vyote vilivyo na uhai na vile vilivyokufa, na kwa hivyo kwake Mungu, hakuna kinachokuwa rahisi kuliko kuzidisha uzao wa mtu. Haya yote yanaonekana ya kufikiria tu akilini mwa binadamu, sawa na hadithi za uwongo, lakini kwa Mungu, kile Anachoamua kufanya, na kuahidi kufanya, si cha kufikiria tu akilini wala si hadithi za uwongo. Badala yake ni hoja ambayo Mungu tayari ameiona, na ambayo kwa kweli itaweza kutimizwa. Je, unashukuru kuyasikia haya? Je, hoja hizi zinathibitisha kwamba uzao wa Ibrahimu ulikuwa mwingi? Na ulikuwa mwingi kiasi kipi? Mwingi kiasi cha “nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani” kama ilivyosemwa na Mungu? Je, uliweza kuenea kotekote katika mataifa na maeneo, kwenye kila sehemu ya ulimwengu? Na ni nini kilichotimiza hoja hii? Iliweza kutimizwa kutokana na mamlaka ya matamshi ya Mungu? Kwa miaka kadhaa ifikayo mamia au elfu baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, matamshi ya Mungu yaliendelea kutimizwa, na bila kusita yakaendelea kuwa hoja; huu ndio uwezo wa matamshi ya Mungu, na ithibati ya mamlaka ya Mungu. Wakati Mungu alipoumba viumbe vyote hapo mwanzo, Mungu alisema na hebu kuwe na nuru, na kukawa na nuru. Tokeo hili lilifanyika haraka sana, lilitimizwa kwa muda mfupi sana, na hakukuwa na kuchelewa kokote kuhusu kukamilika na kutimizwa kwake; athari za matamshi ya Mungu zilitokea papo hapo. Vyote vilikuwa onyesho la mamlaka ya Mungu, lakini wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Aliruhusu binadamu kuuona upande mwingine wa mamlaka ya Mungu, na Akaruhusu binadamu kuona mamlaka ya Muumba yasiyokadirika, na zaidi, Akaruhusu binadamu kuona upande halisi, bora zaidi wa mamlaka ya Muumba.

Punde tu matamshi ya Mungu yanapotamkwa, mamlaka ya Mungu yanachukua usukani wa kazi hii, na hoja iliyoahidiwa kwa kinywa cha Mungu kwa utaratibu huanza kugeuka na kuwa uhalisi. Miongoni mwa viumbe vyote, mabadiliko huanza kufanyika katika kila kitu kutokana na hayo, sawa na vile, kwenye mwanzo wa msimu wa mchipuko, nyasi hugeuka kuwa kijani, maua huchanua, macho ya maua yanachanua kutoka mitini, ndege wanaanza kuimba, nao batabukini wanaanza kurejea, nayo mashamba yanaanza kujaa watu…. Wakati wa msimu wa machipuko unapowadia viumbe vyote hupata nguvu, na hiki ndicho kitendo cha miujiza cha Muumba. Wakati Mungu anapokamilisha ahadi zake, viumbe vyote mbinguni na ardhini vinapata nguvu mpya na kubadilika kulingana na fikira za Mungu—na hakuna kiumbe ambacho kinaachwa. Wakati kujitolea au kuahidi kunapotamkwa kutoka kwa Mungu, viumbe vyote vinatimiza wajibu wake, na vinashughulikiwa kwa minajili ya kutimizwa kwake, na viumbe vyote vinaundwa na kupangiliwa chini ya utawala wa Mungu, na vinaendeleza wajibu wao maalum, na kuhudumu kazi zao husika. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya Muumba. Unaona nini katika mambo haya? Unajuaje mamlaka ya Mungu? Kunao upana wa mamlaka ya Mungu? Kuna kipimo cha muda? Je, inaweza kusemekana kuwa na kimo fulani, au urefu fulani? Je, inaweza kusemekana kuwa na ukubwa au nguvu fulani? Je, inaweza kupimwa kwa vipimo vya binadamu? Mamlaka ya Mungu hayawakiwaki yakizima, hayaji yakienda, na hakuna mtu anayeweza kupima namna ambavyo mamlaka Yake yalivyo makubwa. Haijalishi ni muda gani utakaopita, wakati Mungu anabariki mtu, baraka hizi zitaendelea kuwepo, na kuendelea kwake kutadhihirisha agano la mamlaka ya Mungu yasiyokadirika, na kutaruhusu mwanadamu kutazama kule kujitokeza upya kwa nguvu za maisha zisizozimika za Muumba, mara kwa mara. Kila onyesho la mamlaka Yake ni onyesho timilifu la maneno kutoka kwenye kinywa Chake, na linaonyeshwa kwa vitu vyote, na kwa mwanadamu. Zaidi ya hayo, kila kitu kinachokamilishwa na mamlaka Yake ni bora zaidi ya kulinganishwa, na hakina dosari kamwe. Yaweza kusemekana kwamba fikira Zake, matamshi Yake, mamlaka Yake, na kazi zote Anazozikamilisha, zote ni picha nzuri isiyolinganishwa, na kwa viumbe, lugha ya binadamu haiwezi kuelezea umuhimu na thamani yake. Mungu anapotoa ahadi kwa mtu, haijalishi kama ni kuhusiana na pale wanakoishi, au kile wanachofanya, asili yao kabla na baada ya kupata ahadi, au hata ni vipi ambavyo mageuzi makubwa yamekuwa makubwa katika harakati zao za kuishi kwenye mazingira yao—haya yote yanajulikana kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Haijalishi ni muda upi umepita baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, kwake Yeye, ni kama vile ndio mwanzo yametamkwa. Hivi ni kusema kwamba Mungu anazo nguvu, na Anayo mamlaka kama hayo, kiasi cha kwamba Anaweza kufuatilia, kudhibiti, na kutambua kila ahadi Anayotoa kwa mwanadamu, haijalishi ahadi hiyo ni nini, haijalishi ni muda gani itachukua kutimizwa kikamilifu, na, zaidi, haijalishi upana wa sehemu ambazo kukamilika huko kunagusia—kwa mfano, muda, jiografia, kabila, na kadhalika—ahadi hii itakamilishwa, na kutambuliwa, na, zaidi, kukamilishwa kwake na kutambuliwa kwake hakutahitaji jitihada Zake hata kidogo. Na haya yanathibitisha nini? Kwamba upana wa mamlaka ya Mungu na nguvu vinatosha kudhibiti ulimwengu mzima, na wanadamu wote. Mungu aliumba nuru, lakini hiyo haimaanishi kuwa Mungu anasimamia tu nuru, kwamba Yeye anasimamia maji tu kwa sababu Aliyaumba maji, na kwamba kila kitu kingine hakina uhusiano na Mungu. Je, hii siyo suitafahamu? Ingawaje baraka za Mungu kwa Ibrahimu zilikuwa zimefifia polepole kutoka kwenye kumbukumbu ya binadamu baada ya miaka mia kadhaa, kwake Mungu, ahadi hii ilibaki vilevile. Ilikuwa kwenye mchakato wa kukamilishwa, na haikuwahi kusitishwa. Binadamu hakuwahi kujua au kusikia namna ambavyo Mungu alisisitiza mamlaka Yake, namna ambavyo vitu vyote vilivyoundwa na kupangiliwa, na ni hadithi ngapi za ajabu zilifanyika miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji wa Mungu kwenye kipindi hiki cha muda, lakini kila kipande kizuri cha onyesho la mamlaka ya Mungu na ufunuo wa matendo Yake vilipitishwa na kutukuzwa miongoni mwa viumbe vyote, viumbe vyote vilijitokeza na kuongea kuhusu vitendo vya kimiujiza vya Muumba, na kila mojawapo ya hadithi iliyosimuliwa sana kuhusu ukuu wa Muumba juu ya viumbe vyote itaweza kutangazwa na viumbe vyote daima dawamu. Mamlaka ambayo Mungu anatawala viumbe vyote, na nguvu za Mungu, vinaonyesha viumbe vyote kwamba Mungu anapatikana kila pahali wakati wote. Wakati unashuhudia upekee wa mamlaka na nguvu za Mungu, utaona kwamba Mungu anapatikana kila mahali na nyakati zote. Mamlaka na nguvu za Mungu haviwekewi mipaka ya muda, jiografia, nafasi, au mtu yeyote, jambo au kitu. Upana wa mamlaka na nguvu za Mungu unazidi mawazo ya binadamu; haufikiriki kwa binadamu, hauwaziki kwa binadamu, na hautawahi kujulikana na binadamu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp