Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Siri Kuhusu Biblia | Dondoo 270

Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, mnajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika Agano la Kale linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao. Bila Shaka, uthibitisho wa haya makubaliano ulikuwa damu ya mwanakondoo iliyopakwa kwenye linta kupitia kwayo Mungu Alianzisha agano na mwanadamu, moja ambalo ilisemwa kuwa wale wote waliokuwa na damu ya mwanakondoo juu na pembeni mwa viunzi vya mlango walikuwa Waisraeli, walikuwa wateuliwa wa Mungu, na wote wangeokolewa na Yehova (kwa kuwa Yehova wakati ule Alikuwa karibu kuwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri wote na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe). Agano hili lina viwango viwili vya maana. Hakuna mmoja wa watu au wanyama wa Misri angeokolewa na Yehova; Angewaua wazaliwa wa kwanza wa kiume na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe wao wote. Kwa hivyo, katika vitabu vingi vya unabii kulitabiriwa kwamba Wamisri wangeadibiwa vikali kutokana na agano la Yehova. Hiki ndicho kiwango cha kwanza cha maana. Yehova Aliwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri na wazaliwa wa kwanza wa mifugo wao wote, na kuwaacha Waisraeli wote, jambo lililomaanisha kuwa wale wote waliokuwa wa nchi ya Israeli walipendwa na Yehova na wote wangeokolewa; Alidhamiria kufanya kazi ya muda mrefu ndani yao, na Alianzisha agano nao kwa kutumia damu ya mwanakondoo. Tangu wakati ule kuendelea, Yehova Asingewaua Waisraeli na Alisema kuwa daima wangekuwa wateuliwa Wake. Angeianza kazi Yake ya Enzi Nzima ya Sheria Miongoni mwa makabila kumi na mawili ya Israeli, Angeziweka wazi sheria Zake zote kwa Waisraeli, na kuchagua manabii na waamuzi kutoka kati yao, na wangekuwa katikati ya kazi Yake. Alifanya Agano nao: Angefanya kazi tu miongoni mwa wateuliwa isipokuwa enzi ibadilike. Agano la Yehova lilikuwa lisilobadilika kwani lilitengenezwa kwa damu, na lilianzishwa na wateuliwa Wake. La muhimu zaidi, Alikuwa Ameteua mawanda na malengo yafaayo ya kazi Yake katika enzi nzima, na kwa hivyo watu waliliona agano kuwa la umuhimu sana. Hiki ndicho kiwango cha pili cha maana ya agano. Isipokuwa kitabu cha Mwanzo, ambacho kilikuwepo kabla ya kuanzishwa kwa agano, vitabu vingine vyote vya Agano la Kale vinaeleza kuhusu kazi miongoni mwa Waisraeli baada ya kuanzishwa kwa agano hili. Bila shaka, yapo maelezo ya hapa na pale ya Watu wa Mataifa, ila kwa ujumla, Agano la Kale linaeleza kuhusu kazi ya Mungu nchini Israeli. Kwa sababu ya Agano kati ya Yehova na Waisraeli, vitabu vilivyoandikwa katika Enzi ya Sheria vinaitwa “Agano la Kale.” Vimepatiwa jina hili kutokana na agano la Yehova na Waisraeli.

Agano Jipya lilipatiwa jina hilo kutokana na damu iliyomwagwa na Yesu msalabani na agano Lake na wale wote waliomwamini. Agano la Yesu lilikuwa hili: Watu hawakuwa na budi kumwamini ili dhambi zao zisamehewe kwa kumwagika kwa damu Yake, na kwa njia hiyo wangeokolewa na kuzaliwa upya kupitia Kwake, na kamwe wasingeendelea kuwa wenye dhambi; watu walipaswa kumwamini ili wapokee neema Yake, na hawangeteseka jehanamu baada ya kufa. Vitabu vyote vilivyoandikwa wakati wa Enzi ya Neema vilizuka baada ya hili agano, na vyote vinaeleza kuhusu kazi na matamshi yaliyomo. Havielezi zaidi ya wokovu wa kusulubishwa kwa Bwana Yesu au hili agano; vyote ni vitabu vilivyoandikwa na wapendwa katika Bwana waliokuwa na tajriba. Kwa hivyo hivi vitabu vilevile vimepatiwa jina kutokana na agano: Vinaitwa Agano Jipya. Haya Maagano mawili yanajumuisha tu Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria na hayana uhusiano na enzi ya mwisho. Hivyo basi, Biblia haina msaada mkubwa kwa watu wa leo wa siku za mwisho. Zaidi, hutumika kama marejeleo ya muda mfupi, ila kimsingi haina matumizi ya thamani kubwa.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp