Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 77
08/07/2020
Kufufuka kwa Lazaro Kwampa Mungu Utukufu
Yohana 11:43-44 Na baada ya yeye kuzungumza, akasema kwa sauti kuu, Lazaro, kuja nje. Na yeye ambaye alikuwa amefariki akatoka nje, akiwa amefungwa mkono na mguu na sanda: na uso wake ulikuwa umefungwa kwa kitambaa. Yesu akasema kwao, Mfungueni yeye, na mwache aondoke.
Mnayo picha gani baada ya kusoma dondoo hii? Umuhimu wa muujiza huu ambao Bwana Yesu alitenda ulikuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa awali kwa sababu hakuna muujiza ambao unajitokeza zaidi kuliko ule wa kufufua binadamu aliyekufa na kutoka katika kaburi. Bwana Yesu kufanya kitu kama hiki kulikuwa na umuhimu mkubwa mno katika enzi hiyo. Kwa sababu Mungu alikuwa mwili, watu waliweza kuona tu kuonekana Kwake kwa kimwili, upande Wake wa kimatendo, na upande Wake usio na umuhimu. Hata kama baadhi ya watu waliona na kuelewa hulka Yake fulani au nguvu Zake ambazo alionekana kuwa nazo, hakuna aliyejua pale ambapo Bwana Yesu alipotokea, ambaye kiini Chake cha kweli kilikuwa, na nini kingine zaidi ambacho Angeweza kufanya. Haya yote hayakujulikana kwa mwanadamu. Watu wengi mno walitaka ithibati ya kitu hiki, na kuujua ukweli. Je, Mungu angeweza kufanya kitu ili kuthibitisha utambulisho Wake Mwenyewe? Kwa Mungu, huu ulikuwa upepo mwanana—lilikuwa jambo rahisi sana. Angefanya kitu popote, wakati wowote ili kuthibitisha utambulisho na kiini Chake, lakini Mungu alifanya mambo kwa mpango, na kwa hatua. Hakufanya vitu bila mpangilio; Alitafuta muda unaofaa, na fursa inayofaa kufanya kitu chenye maana zaidi kwa wanadamu kuweza kuona. Hili lilithibitisha mamlaka Yake na utambulisho Wake. Hivyo basi, kufufuka kwa Lazaro kungeweza kuthibitisha utambulisho wa Bwana Yesu? Hebu tuangalie kifungu hiki cha maandiko: “Na baada ya yeye kuzungumza, akasema kwa sauti kuu, Lazaro, kuja nje. Na yeye ambaye alikuwa amefariki akatoka nje.” Wakati Bwana Yesu alipofanya haya, Alisema tu jambo moja: “Lazaro, kuja nje.” Kisha Lazaro akatoka nje ya kaburi—hii ilikamilika kwa sababu ya mstari mmoja uliotamkwa na Bwana. Katika wakati huu, Bwana Yesu hakuweza kuandaa madhabahu, na Hakutekeleza hatua zote nyingine. Alisema tu jambo moja. Hili linaweza kutaitwa muujiza au amri? Au lilikuwa aina fulani wa uchawi? Kwa juujuu, yaonekana ingeweza kuitwa muujiza, na ukiangalia hali hiyo kutoka mtazamo wa kisasa, bila shaka mnaweza bado kuliita muujiza. Hata hivyo, bila shaka hali hiyo isingeweza kuitwa apizo la kuiita nafsi kurudi kutoka kwa wafu, na bila shaka si uchawi. Ni sahihi kusema kwamba muujiza huu ulikuwa ni onyesho la kawaida zaidi, dogo ajabu la mamlaka ya Muumba. Haya ndiyo mamlaka, na uwezo wa Mungu. Mungu ana mamlaka ya kumwacha mtu afe, kuruhusu nafsi yake iondoke mwilini mwake na kurudi kuzimu au popote pale itakapoenda. Mtu anapokufa, na anakokwenda baada ya kifo—haya yanaamuliwa na Mungu. Yeye anaweza kufanya haya wakati wowote na mahali popote. Yeye hazuiliwi na binadamu, matukio, vifaa, nafasi au mahali. Akitaka kulifanya Anaweza kulifanya, kwa sababu vitu vyote na viumbe vyenye uhai vinatawaliwa na Yeye, na vitu vyote vinaishi na kufa kwa neno Lake, mamlaka Yake. Anaweza kumfufua binadamu aliyekufa—pia hiki ni kitu Anachoweza kufanya wakati wowote mahali popote. Haya ndiyo mamlaka ambayo Muumbaji pekee humiliki.
Bwana Yesu alipofanya kitu kama vile kumleta Lazaro kutoka kwa wafu, lengo Lake lilikuwa ni kutoa ithibati kwa wanadamu na Shetani aweze kuona, na kuacha wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu, maisha na kifo cha wanadamu vyote vinaamuliwa na Mungu, na kwamba ingawa Alikuwa amekuwa mwili ilivyo kama siku zote, Alibaki katika mamlaka juu ya ulimwengu wa kimwili unaoweza kuonekana pamoja na ulimwengu wa kiroho ambao wanadamu hawawezi kuuona. Huku kulikuwa kuwaruhusu wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu hakiko katika amri ya Shetani. Huu ulikuwa ni ufunuo na onyesho la mamlaka ya Mungu, na ilikuwa pia njia ya Mungu kuutuma ujumbe wake kwa viumbe vyote kwamba maisha na kifo cha wanadamu kimo mikononi mwa Mungu. Bwana Yesu kumfufua Lazaro—kutenda kwa aina hii ni mojawapo ya njia za Muumba za kumfunza na kumwelekeza wanadamu. Ilikuwa ni hatua thabiti ambapo Aliutumia uwezo Wake na mamlaka Yake kuwaelekeza wanadamu, na kuwatolea wanadamu. Ilikuwa njia bila matumizi ya maneno kwa Muumba ya kuwaruhusu wanadamu kuweza kuuona ukweli wa Yeye kuwa na mamlaka juu ya viumbe vyote. Ilikuwa njia Yake ya kuwaambia binadamu kupitia kwa hatua za kimatendo kwamba hamna wokovu mbali na kupitia Yeye. Mbinu za aina hii za kimya za Yeye kuwaelekeza wanadamu zinadumu milele—hazifutiki, na iliweza kuleta katika mioyo ya wanadamu mshtuko na kupatikana kwa nuru ambayo haiwezi kufifia. Kufufuliwa kwa Lazaro kulimtukuza Mungu—hali hii inayo athari ya kina katika kila mojawapo wa wafuasi wa Mungu. Inakita mizizi kwa kila mmoja anayeelewa kwa kina tukio hili, ufahamu, maono kwamba ni Mungu tu anayeweza kuamuru maisha na kifo cha wanadamu. Ingawa Mungu ana aina hii ya mamlaka, na ingawa Aliutuma ujumbe kuhusu uhuru Wake dhidi ya maisha na kifo cha wanadamu kupitia kwa kufufuka kwa Lazaro, hii haikuwa kazi Yake ya msingi. Mungu katu hafanyi kitu bila maana. Kila kitu Anachofanya kina thamani kuu; ni hazina ya mufti. Bila shaka Yeye hatamfanya mtu kutoka katika kaburi lake kuwa sababu ya kimsingi au lengo au sababu kuu katika kazi Yake. Mungu hafanyi chochote ambacho hakina maana. Kufufuka kumoja kwa Lazaro kunatosha kuonyesha mamlaka ya Mungu. Kunatosha kuthibitisha utambulisho wa Bwana Yesu. Hii ndiyo sababu Bwana Yesu hakurudia aina hii ya muujiza. Mungu hufanya mambo kulingana na kanuni Zake binafsi. Katika lugha ya binadamu, ingekuwa kwamba Mungu anajali kazi muhimu. Yaani, wakati Mungu anapofanya mambo Hapotoki kutoka kwenye kusudio Lake la kazi. Anajua ni kazi gani Anayotaka kutekeleza katika awamu hii, kile Anachotaka kukamilisha, na Atafanya kazi mahususi kulingana na mpango Wake. Kama mtu aliyepotoka angekuwa na aina hiyo ya uwezo, angekuwa akifikiria tu kuhusu njia za kufichua uwezo wake ili wengine wajue namna alivyokuwa thabiti, hivyo basi kumwinamia, ili aweze kuwadhibiti na kuwameza. Huu ndio uovu unaotoka kwa Shetani—huu unaitwa upotovu. Mungu hana tabia kama hiyo, na Hana kiini kama hicho. Kusudio Lake katika kufanya mambo si kujionyesha Mwenyewe, lakini kuwapa wanadamu ufunuo na mwongozo zaidi, ili watu waweze kuiona mifano michache katika Biblia kuhusu aina hii ya jambo. Hii haimaanishi kwamba uwezo wa Bwana Yesu ulikuwa finyu, au kwamba asingeweza kufanya jambo la aina hiyo. Ni kwamba Mungu hakutaka tu kulifanya jambo hilo, kwa sababu Bwana Yesu kumfufua Lazaro kulikuwa na umuhimu wa kimatendo kabisa, na pia kwa sababu kazi kuu ya Mungu kuwa mwili haikuwa ni kutenda miujiza, haikuwa ni kuwaleta watu kutoka katika kifo, lakini ilikuwa ni kazi ya ukombozi wa wanadamu. Hivyo basi, wingi wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha ilikuwa ni kuwafunza watu, kuwatoshelezea haja zao, na kuwasaidia, na mambo kama vile kumfufua Lazaro yalikuwa tu mambo madogo ya huduma ambayo Bwana Yesu alitekeleza. Hata zaidi, mnaweza kusema kwamba “kujionyesha” si sehemu ya kiini cha Mungu, hivyo basi kutoonyesha miujiza zaidi hakukuwa kujizuia kimakusudi, wala hakukuwa kwa sababu ya vizuizi vya kimazingira, na bila shaka hakukuwa kwa sababu ya ukosefu wa uwezo.
Bwana Yesu alipomleta Lazaro kutoka kwa wafu, Alitumia mstari mmoja: “Lazaro, kuja nje.” Hakusema kitu kingine mbali na hiki—maneno haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha hoja kwamba Mungu anaweza kukamilisha chochote kupitia maongezi, kukiwemo kumfufua mtu aliyekufa. Mungu alipoumba viumbe vyote, Alipouumba ulimwengu, Alifanya hivyo kwa maneno. Alitumia amri, maneno yaliyotamkwa kwa mamlaka, na hivyo tu viumbe vyote viliumbwa. Yalikamilishwa hivyo. Mstari huu mmoja uliozungumzwa na Bwana Yesu ulikuwa sawa na maneno yaliyotamkwa na Mungu alipoziumba mbingu na dunia na viumbe vyote; mstari huo pia uliweza kushikilia mamlaka ya Mungu, uwezo wa Muumba. Viumbe vyote viliumbwa na vikasimama kwa sababu ya matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu, na vivyo hivyo, Lazaro alitembea kutoka katika kaburi lake kwa sababu ya matamshi kutoka katika kinywa cha Bwana Yesu. Haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ya Mungu, yaliyoonyeshwa na kutambuliwa katika mwili Wake. Aina hii ya mamlaka na uwezo vilimilikiwa na Muumba, na kwa Mwana wa Adamu ambaye kwake Muumba alitambuliwa. Huu ndio ufahamu uliofunzwa kwa mwanadamu kwa Mungu kumleta Lazaro kutoka kwa wafu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video