Wimbo wa Kikristo | Utambulisho wa Mungu ni Mungu Mwenyewe (Music Video)

19/08/2020

Na kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili,

Yeye Anafanya kazi katika utambulisho wa mwili Wake;

kwa kuwa Yeye hukuja katika mwili,

kisha Yeye humaliza katika mwili kazi hiyo Anayoazimia kufanya.

Iwe ni Roho wa Mungu au ni Kristo, wote ni Mungu Mwenyewe,

na Anafanya kazi hiyo Anayoazimia kufanya

na hufanya huduma hiyo Anayopaswa kufanya.

Bila kujali jinsi Yeye hufanya kazi Yake,

wala Naye hangewahi kutenda kwa namna inayomuasi Mungu.

Haijalishi Analomuuliza mwanadamu,

hakuna mahitaji Yake yanayozidi uwezo wa mwanadamu kupata.

Yote Afanyayo ni kutenda mapenzi ya Mungu

na ni kwa ajili ya usimamizi Wake.

Uungu wa Kristo ni zaidi ya wanadamu wote,

kwa hivyo Yeye Anayo mamlaka ya juu ya viumbe vyote vilivyoumbwa.

Mamlaka haya ni uungu Wake,

yaani, nafsi na tabia ya Mungu Mwenyewe,

ambayo huamua utambulisho Wake.

Kwa hiyo, haijalishi jinsi ubinadamu Wake ni wa kawaida

ni wazi kuwa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe;

haijalishi upande Anaosimama Akiongea

na kwa vyovyote vile Yeye hutii mapenzi ya Mungu,

haiwezi kusemwa kwamba Yeye si Mungu Mwenyewe.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp