Wimbo wa Kusifu | Mwili na Roho ya Mungu ni Sawa Kiasili

23/09/2020

Mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu ni mwili wa Mungu mwenyewe.

Roho wa Mungu ni mwenye mamlaka;

Yeye ni mwenye uweza, mtakatifu, na mwenye haki.

Vivyo hivyo, mwili Wake pia ni wenye mamlaka,

wenye uweza, mtakatifu, na wenye haki.

Vivyo hivyo, mwili Wake pia ni wenye mamlaka,

wenye uweza, mtakatifu, na wenye haki.

Mwili kama huo unaweza kufanya tu kile

ambacho ni cha haki na chenye faida kwa wanadamu,

kile ambacho ni kitakatifu, kitukufu na chenye nguvu;

Yeye hawezi kutenda jambo lolote ambalo linakiuka ukweli,

ambalo linakiuka maadili na haki,

sembuse kufanya jambo lolote linaloweza kumsaliti Roho wa Mungu.

Roho wa Mungu ni mtakatifu,

na kwa hiyo mwili Wake hauwezi kupotoshwa na Shetani;

mwili Wake ni wenye kiini tofauti na mwili wa mwanadamu,

mwili Wake ni wenye kiini tofauti na mwili wa mwanadamu.

Kwa maana ni mwanadamu na si Mungu,

ambaye anapotoshwa na Shetani;

Shetani hawezi kamwe kuupotosha mwili wa Mungu.

Kwa hiyo, licha ya ukweli kwamba mwanadamu na Kristo wanaishi katika sehemu sawa,

ni mwanadamu tu ndiye anayemilikiwa,

anayetumiwa, na anayenaswa na Shetani.

Kinyume na hilo, Kristo hapenyeki kabisa na upotovu wa Shetani,

kwa sababu Shetani hatawahi kuweza kupanda hadi mahali pa juu zaidi,

na hatawahi kuweza kumkaribia Mungu,

na hatawahi kuweza kumkaribia Mungu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp