Wimbo wa Injili | Moyo Mwaminifu kwa Ajili ya Mungu (Music Video) | Sauti za Sifa 2026

14/01/2026

1

Ee Mungu! Ingawa maisha yangu hayana thamani nyingi Kwako, ningependa kuyatoa Kwako. Ingawa binadamu hawastahili kukupenda, na upendo wao na mioyo yao havina thamani, naamini kwamba unajua nia za binadamu. Na hata ingawa mwili wa binadamu haufikii kibali Chako, ningependa Uukubali moyo wangu. Niko tayari kuutoa moyo wangu wote kwa Mungu. Ingawa siwezi kumfanyia Mungu chochote, niko tayari kumtosheleza Mungu kwa uaminifu na kuwa mwenye moyo na mawazo sawa na Yeye. Ninaamini Mungu lazima Auchunguze moyo wangu.

2

Eee Mungu! Siombi chochote maishani mwangu ila kwamba fikira zangu za upendo kwa Mungu na tamanio la moyo wangu ziweze kukubaliwa na Mungu. Nilikuwa na Mungu kwa muda mrefu, lakini sikuwahi kumpenda; hili ndilo deni langu kubwa zaidi. Ingawa niliishi na Yeye, sikumjua, na hata nilisema mambo fulani yasiyofaa nyuma Yake. Kufikiria kuhusu mambo haya kunanifanya nihisi mdeni wa Mungu hata zaidi. Mimi ni duni kuliko vumbi. Siwezi kufanya chochote ila kuutoa moyo huu mwaminifu kwa Mungu.

kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp