Wimbo wa Injili | Ni Lazima Mfuatilie Ukweli Ili Kusalia (Music Video) | Sauti za Sifa 2026
14/01/2026
1
Utendaji rahisi zaidi wa kufuatilia ukweli ni kwamba ni lazima ukubali mambo yote kutoka kwa Mungu na utii katika mambo yote. Hiki ni kipengele kimoja. Kipengele kingine ni kwamba linapohusu wajibu wako na majukumu yako, na, kusema kwa njia ya upana zaidi, agizo ulilopewa na Mungu na kazi fulani muhimu uliyopewa na Mungu, unapaswa kulipa gharama kila wakati. Haijalishi jinsi inavyoweza kuwa ngumu—haijalishi kama inakulazimu kufanya kazi kwa bidii bila kupumzika, haijalishi kama mateso yatakupata, au hata kama itayaweka maisha yako hatarini—hupaswi kujutia gharama, lakini utoe uaminifu wako na utii hadi kifo. Huu ni udhihirisho halisi, kujitumia halisi, na utendaji wa kweli wa kufuatilia ukweli. Ikiwa watu wana moyo wa hamu, azimio, na imani kuhusu kufuatilia ukweli—ikiwa wana nguvu hii mioyoni mwao—kwa hivyo hakuna kitu kinachowapata kilicho kigumu. Jambo la kutia wasiwasi ni kwamba baadhi ya watu hukosa imani.
2
Hatimaye, katika hatua hii ya kazi katika hatua ya mwisho, Mungu anawaambia watu waziwazi kila kipengele cha kweli ambazo wanapaswa kuzitenda. Kuwafanya watu wafuatilie ukweli katika kipindi hiki cha sasa cha kupitia kazi ya Mungu si kuwafanyia mambo kuwa magumu; badala yake ni kitu ambacho wana uwezo wa kukifanikisha. Kwa upande mmoja, takwa hili la Mungu linafaa kikamilifu; kwa upande mwingine, watu wana masharti ya kutosha na msingi wa kutosha wa kufuatilia ukweli. Mtu bado akishindwa kuupata ukweli mwishowe, ni kwa sababu matatizo yake ni makali mno. Mtu wa namna hiyo anastahili adhabu yoyote anayopitia, matokeo yoyote anayopata, kifo chochote anachokutana nacho. Hastahili huruma. Kwa Mungu, hakuna hali kama huruma au kuonea huruma kama kwa wanadamu. Yeye huhukumu matokeo ambayo mtu anapaswa kuwa nayo, na huamua jinsi maisha haya na dunia ijayo yalivyo kwa mtu, kulingana na tabia Yake, na vile vile sheria na kanuni Alizoweka, matakwa Yake kwa watu, na ni udhihirisho gani ambao mtu huyo anao. Ni rahisi hivyo.
3
Mungu hajali ni watu wangapi watakaosalia, au ni wangapi wataangamizwa na kuadhibiwa mwishowe. Hili linawaonyesha nini? Linawaonyesha kwamba Mungu hajaamua kimbele idadi iliyopangwa ya watu na kwamba unaweza kujitahidi kuipata. Mungu hunena na hufanya kazi jinsi Afanyavyo sasa; Yeye humtendea kila mtu kwa haki na humpa kila mtu fursa ya kutosha. Yeye hukupa wewe fursa ya kutosha, na neema ya kutosha, na kiasi cha kutosha cha maneno Yake, na kazi Yake, na rehema Yake na uvumilivu Wake. Yeye ni mwenye haki kwa kila mtu. Ikiwa wewe unafuatilia ukweli, na umeanza kuitembea njia ya kumfuata Mungu, na ikiwa, bila kujali mateso unayovumilia ni makubwa kiasi gani au ni matatizo mangapi unayokumbana nayo, wewe unaweza kukubali ukweli na tabia zako potovu zinatakaswa, basi utaokolewa. Ikiwa wewe unaweza kumshuhudia Mungu na kuwa kiumbe aliyeumbwa ambaye anafikia kiwango kinachostahili, bwana wa vitu vyote ambaye anafikia kiwango kinachostahili, wewe utasalia.
kutoka katika Neno, Vol. 6. Kuhusu Ufuatiliaji wa Ukweli. Kwa Nini Mwanadamu Lazima Afuatilie Ukweli
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video