Wimbo wa Injili | Maneno Yote ya Mungu ni Ukweli (Music Video) | Sauti za Sifa 2026
18/01/2026
1
Mungu amekuja duniani kuishi na mwanadamu, akionyesha kweli nyingi.
Sitafuti tena katika hali zisizo dhahiri, ninayo maneno ya Mungu yaniongozayo.
Kila siku, ninakula na kunywa maneno ya Mungu na kuishi mbele za Mungu;
Roho Mtakatifu ananitia nuru na kuniangaza.
Ninaelewa ukweli kwa uwazi zaidi, na maisha yangu yanaendelea mbele kila siku.
Maneno ya Mungu hufichua kikamilifu ukweli wa upotovu wa mwanadamu,
na kumfanya kila mtu asadikishwe kabisa.
Kupitia hukumu ya maneno ya Mungu na majaribu mengi ya mateso,
tabia yangu potovu imetakaswa.
Nikifurahia utajiri wa maneno ya Mungu, kwa kweli nimepata mengi.
Nikiona haki na utakatifu wa tabia ya Mungu,
ninamcha Mungu na kumwabudu.
Maneno Yote ya Mungu ni Ukweli.
2
Nikisoma maneno ya Mungu, ninaelewa ukweli na kuvuka vifungo vya mwili.
Nikitafuta ukweli na kumtii Mungu ninapotekeleza wajibu wangu,
ninaishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu mwaminifu.
Ninaelewa ukweli na kutupilia mbali tabia yangu potovu;
ukweli wa maneno ya Mungu ni wa thamani sana.
Nikitenda maneno ya Mungu, ninapata ukweli na uzima,
na moyo wangu hautamani kingine chochote.
Nikiuona upendo wa Mungu ulivyo mkuu na halisi,
ninautoa moyo wangu wa kweli kwa Mungu kwa furaha.
Haijalishi jinsi njia iliyo mbele ilivyo yenye mashimoshimo na isiyo laini,
nitamfuata Mungu kwa imani kuu.
Ninafuatilia kumpenda Mungu, kumcha Mungu na kuepuka maovu;
njia iliyo mbele inazidi kuwa yenye kung'aa.
Nitamfuata Kristo hadi mwisho kabisa na kutimiza uaminifu wangu
ili kukaribisha kuonekana kwa uso wa Mungu wenye tabasamu.
Maneno Yote ya Mungu ni Ukweli.
kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video