Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

New Swahili Christian Video "Kufufuka" | Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho Iliniokoa

Maisha ya Kanisa   1470  

Utambulisho

New Swahili Christian Video "Kufufuka" | Hukumu ya Mungu katika Siku za Mwisho Iliniokoa


Jina lake ni Zheng Lu, na tangu utotoni, alikuwa hasa ovyo. Kwa sababu ya ushawishi wa kijamii na elimu ya utamaduni wa kidesturi wa Kichina, alisoma bila kuchoka, akitumai kufikia chuo kikuu na kufanikisha ndoto yake ya kuwapiku marika wake na kuwa na mafanikio, lakini ajali isiyotarajiwa ilimharibia ndoto yake. Wakati tu alipohisi vibaya, mnyonge, na asiyeweza kuupata mwelekeo maishani, wokovu wa Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ulimpata. Baada ya kuanza kumsadiki Mungu, alifuatilia kwa shauku, akatenda wajibu wake kwa kujitolea, akapata idhini ya kaka na dada zake na miaka miwili baadaye alichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa. Lakini bila kujua, tamanio lake la ufanisi lilianza tena kukua ndani yake, na kiburi, majivuno na tamanio lake la umaarufu na heshima na fahari kuu ya asili yake ya kishetani vyote vilijifichua kila mara katika wajibu wake, na kutatiza pakubwa kazi ya kanisa. Kwa kupitia hukumu tena na tena, kuadibu, upogoaji, na kushughulikiwa na neno la Mungu, anatafakari kwa kina, na hatimaye kuona waziwazi kwamba amekuwa mpotovu sana na ametiwa sumu za kishetani kama vile "Kupata fanaka, kutaka kuwa bora zaidi kuliko wengine," "Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake," "Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo," vyote ambavyo vilimsababisha kuwa hasa mwenye kiburi na asili ya majivuno na kuabudu cheo na mamlaka, na kumsababisha yeye kuzingatia pakubwa kuufuatilia umaarufu na fahari kuu kutokana na miaka yake ya kuwa na imani katika Mungu badala ya kuufuatilia ukweli. Bila ya yeye kujijua, alikuwa ameitembelea njia ya mpingakristo. Wakati uo huo anapopata upenyezi wa kina katika kiini na hatari za ufuatiliaji wa umaarufu na cheo, anaanza kuuchukia sana umaarufu, cheo na asili yake binafsi ya kishetani, anabadilisha mtazamo wake wa kimakosa wa kimaisha na maadili na kwa taratibu anaanza kuitembelea njia bora na sahihi ya maisha, ile ya ufuatiliaji wa ukweli.


Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.


Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Pakua Programu Bila Malipo

Video za Ajabu Zakuongoza Kuielewa Kazi ya Mungu

Pakua Programu Bila Malipo

Video za Ajabu Zakuongoza Kuielewa Kazi ya Mungu