Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

"Mji Utaangushwa" (1) - Ulimwengu wa Dini Umepotoka na kuwa Mji wa Babeli

Dondoo za Filamu   295  

Utambulisho

Viongozi wa ulimwengu wa dini wanapotea toka kwenye njia ya Bwana na kufuata mitindo ya kidunia, pia wao hushirikiana na uasi mkali wa mamlaka ya utawala na shutuma ya Umeme wa Mashariki, na tayari wameanza kutembea kwenye njia ya upinzani kwa Mungu. Ulimwengu wa dini umepotoka na kuwa mji wa Babeli. Biblia inasema, "Na Yesu akaingia katika hekalu la Mungu, na akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua katika hekalu, na akazipindua meza za wabadilishaji wa fedha, na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa, Na akawaambia, imeandikwa, nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; lakini mmeifanya pango la wezi" (Mathayo 21:12-13). "Babeli kuu imeanguka, imeanguka, na imekuwa makazi ya pepo, ngome ya kila pepo mwovu, na tundu la kila ndege mchafu na wa kuchukiza. Kwani mataifa yote yamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa ulimwengu wamefanya naye uasherati, na wafanya biashara wa ulimwengu wametajirika kupitia kwa utele wa uzuri wake" (Ufunuo 18:2-3).