Umeme wa Mashariki Unatoka Wapi?

17/01/2021

Sasa tuko katika siku za mwisho, unabii wa kurudi kwa Bwana umetimizwa kimsingi, na waumini wengi sana wanaomcha Mungu wanatumai kurudi kwa Bwana Yesu kwa ari. Hata hivyo, wakati uo huo, Umeme wa Mashariki unatangaza ushuhuda wao kwamba Bwana Yesu tayari amerudi katika kupata mwili Kwake kwa siku za mwisho—Mwenyezi Mungu—na kwamba tayari Amefanya kazi Yake ya hukumu akianzia na familia ya Mungu. Kutokea kwa Umeme wa Mashariki kumetikisa ulimwengu wote wa dini na vile vile wale wote ambao wanamwamini Mungu kwa kweli na wanaotamani ukweli. Kupitia kutafuta na kuchunguza maneno na kazi ya Mwenyezi Mungu, watu wengi wanathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, na mmoja baada ya mwingine wanakuja mbele ya Mwenyezi Mungu. Hili limewahangaisha wachungaji na wazee wa dunia ya dini na serikali ya CCP na, ili kukandamiza na kuharamisha Umeme wa Mashariki, wachungaji na wazee wa dunia ya dini na serikali ya CCP wanashirikiana pamoja, wakibuni uvumi mwingi na kushutumu na kusingizia vikali Umeme wa Mashariki kama uzushi, na kufanya yote wawezayo kuzuia na kusumbua waumini wa kweli wanaotaka kutafuta na kuchunguza kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Katika siku zile za mwanzo, dunia ya dini ya Kiyahudi ilijiungan na serikali ya Kirumi na tanzia ya kihistoria ya ukandamizaji katili wa Bwana Yesu inafanyika tena. Maelezo yanatofautiana na maoni ni ya namna nyingi kuhusu iwapo Umeme wa Mashariki ni kurudi kwa Bwana Yesu au la, na iwapo ni kazi ya Mungu au la; watu wengine wanafuata nyayo za wachungaji na wazee wa dunia ya dini katika kukana na kushutumu kwao, lakini kuna wengine wanaoamini Umeme wa Mashariki unahusiana na unabii wa Bwana Yesu katika Biblia unaosema, “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27), na kwamba unahusiana na kuja kwa Mwana wa Adamu katika siku za mwisho. Kwa hivyo Umeme wa Mashariki unatoka wapi hasa, je, ni kazi ya Mungu, na una siri zipi?

Wote wanaoielewa kazi ya Mungu wanajua kwamba kazi Yake daima ni mpya na kwamba haikomi katika kusonga kwake mbele. Kama tu katika Enzi ya Sheria wakati Mungu alifanya kazi kupitia Roho na kutoa sheria ambazo zingeongoza maisha ya mwanadamu duniani. Kisha, katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili na kuonekana kama Mwana wa Adamu kufanya kazi Yake, kuwaponya wagonjwa na kuwafukuza pepo, kutekeleza matendo mengi ya muujiza na kuonyesha njia ya, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu(Mathayo 4:17), kabla ya kutundikwa msalabani na kukamilisha kazi Yake ili kuwakomboa wanadamu wote. Lakini kwa sababu watu hawajui kazi ya Mungu, na pia kuwa na tabia za majivuno na za kujigamba za kishetani, na wote wakiwa wa kujidai, wagumu na wakaidi sana, na wanashikilia dhana na mawazo, hadi kiwango ambapo hata wanachoshwa sana na ukweli na kuuchukia ukweli, kila wakati Mungu hutenda kazi mpya, lazima Apitie kufuru, mateso na shutuma ya shauku ya dunia ya dini na mamlaka tawala. Wale wanaoeneza na kushuhudia kazi mpya ya Mungu wanaweza pia kupachikwa na kila aina ya mashtaka na maneno ya kushusha hadhi, na pia kukandamiza kikatili. Ukweli huu umerekodiwa katika Agano Jipya: Ili kuwaokoa wanadamu kutokana na hatari ya kuadhibiwa kwa sababu ya kuvunja sheria ambazo hawangeweza kufuata, Mungu alipata mwili kama mfano wa Bwana Yesu na kuanza kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema. Wakati Bwana Yesu alikuwa akitenda kazi Yake huko Yudea, Alitenda matendo mengi ya muujiza, akawaponya wagonjwa na kufukuza pepo, kumpa mwanadamu neema tele na kuonyesha ukweli mwingi. Hili linatosha kudhibitisha kwamba Bwana Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe na kwamba Alikuwa Masiya ambaye Waisraeli walikuwa wamemtamani sana. Hata hivyo, makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo walishikilia dhana za kidini kwa ukaidi na kukataa kabisa kuamini kwamba Bwana Yesu alikuwa Masiya waliokuwa wamemtamani kwa muda mrefu sana. Kinyume chake, walitafuta kila mahali katika Biblia kitu ambacho wangeweza kutumia dhidi ya Yesu, walikashifu, kuhukumu na kushutumu kazi ya Bwana Yesu kama uzushi (tazama Matendo 24:14) na Yesu Mwenyewe kama “kiongozi wa waasi wa kikundi cha Nazareti” (tazama Matendo 24:5). Waliwadanganya na kuwachochea Wayahudi kumhukumu Bwana Yesu, na kuungana na serikali ya Kirumi kumtundika msalabani. Kwa hivyo, taifa lote la Kiyahudi lilikosea tabia ya Mungu, na lilipata maangamizi yasiyo na kifani. Inaweza kuonekana basi, kwamba kitu ambacho kinashutumiwa na kupingwa na dunia ya dini na wale walio mamlakani si lazima kiwe kitu kisicho sahihi, kwamba inawezekana sana kwamba kinatoka kwa Mungu, na kwamba ni kazi ya Mungu. Kwa hivyo, wakati wa kuchunguza kama kitu ni kazi ya Mungu au la, mtu hawezi kufanya uamuzi huu kwa msingi wa iwapo dunia ya dini na wale walio mamlakani wanakikiri au kukikubali au la. Tunaweza kuona kutoka kazi zote zilizofanywa katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema kwamba, ili kuamua iwapo kitu ni kazi ya Mungu au la, inategemea hasa iwapo kile ambacho njia hii kinaonyesha ni ukweli au la, iwapo ni kitu kinachohitajika kwa haraka na wanadamu wakati uliopo au la, na iwapo ni kazi ya Roho Mtakatifu au la. Ni kwa njia hii tu ndio kinaweza kutambulika kiasili kama ni kazi ya Mungu au la—hii ni muhimu sana.

Katika siku za mwisho, wanadamu wanakuwa wenye kupotoshwa kwa kina zaidi na zaidi. Wanadamu wako chini ya udhibiti wa asili zao potovu na za kishetani, mara nyingi wakitenda dhambi bila kutaka, wote wakiishi maisha ambapo wanatenda dhambi mchana na kisha kukiri jioni, na kuishi katika maumivu yasiyovumilika. Wanadamu wanakuwa mbali zaidi na zaidi na Mungu, na tumaini lao la kupata wokovu linakuwa la mashaka zaidi na zaidi. Ili kuwaokoa wanadamu kutokana na hali hii ya kutenda dhambi na kukiri, kukiri na kutenda dhambi, na ili waweze kutupa kabisa tabia zao potovu za kishetani na vizuizi na vipingamizi vyao vya dhambi na kutakaswa na kupata wokovu wa Mungu, Mungu amepata mwili tena ili kuonyesha ukweli na kuwahukumu wanadamu wapotovu, na Anatenda kazi mpya ambayo inawatakasa na kuwaokoa wanadamu kabisa. Wakati huu, Mungu alipata mwili Mashariki mwa dunia—huko Uchina—akionekana na kufanya kazi Yake. Amehitimisha Enzi ya Neema na kuanzisha Enzi ya Ufalme, Ameleta ukweli mkuu zaidi, tele zaidi kuliko awali, Amefunua siri za kazi zote za Mungu tangu uumbaji wa ulimwengu na amewapa wanadamu ukweli wote ambao utawatakasa na kuwaokoa. Wale wanaokubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho wanaelewa ukweli mwingi kutoka kwa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, wanaona wazi kwamba Mwenyezi Mungu ambaye anaonyesha ukweli katika siku za mwisho kwa kweli ni Bwana Yesu aliyerudi, wamepata kuwa na maarifa dhahiri ya asili zao potovu na chanzo cha msingi cha dhambi zao, wamepata njia ya kutatua tabia zao potovu na za kishetani, na mioyo yao ni changamfu na dhahiri. Kwa kupitia hukumu, kuadibu, majaribu na usafishaji wa maneno ya Mungu, tabia zao za maisha zinabadilika siku zote, wanaona tumaini la wokovu, na wana maarifa ya kweli ya asili nzuri na takatifu ya Mungu na tabia Yake ya haki na isiyokiukwa. Wana ufahamu na maarifa zaidi ya utendaji ya kile Mungu anacho na alicho, kama vile uweza, hekima na mamlaka ya Mungu, na wote wanaweza kuona kwamba imani yao katika Mungu si tupu au ya mashaka tena, lakini badala yake inakuwa halisi zaidi na zaidi. Kwa kweli wanakuwa na uzoefu wa Mungu kama mwenye kupendeza na mwenye upendo sana, hivyo kuibua mioyo inayomcha Mungu, wanakuja kuwa na utii na kumfikiria Mungu kwa kweli, na wote wanafahamu kwa dhahiri kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho kweli inaweza kumtakasa na kumwokoa mwanadamu. Katika siku za mwisho, wakati wa kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu na utakaso ni mfupi, kasi ni ya haraka, kama radi. Katika zaidi ya miongo miwili mifupi, injili ya ufalme ya Mungu imeenea kwa bara lote la Uchina na imeunda kikundi cha washindi, na sasa injili inapanuka kwa kasi katika kila upande kwa mataifa yote ya dunia. Hili hasa linatimiza unabii wa Bwana Yesu: “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27). Hata hivyo, wachungaji na wazee wa dunia ya dini wanashikilia dhana za dini kwa ukaidi na, wakiwa wamekabiliwa na kazi mpya ya Mungu ambayo inatofautiana na dhana za mwanadamu, hawakosi tu kuitafuta na kuichunguza, wanaitia Biblia tahabibu na kutafuta makosa ambayo wanaweza kutumia dhidi ya Mungu, wakihukumu na kushutumu kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho kwa uzembe, na kusingizia Kanisa la Mwenyezi Mungu kama “kikundi kibaya cha Umeme wa Mashariki” na kama uzushi. Matendo na vitendo vyao ni sawa kabisa na vile vya makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo walipomshutumu Bwana Yesu. Kwamba wanaweza kuasi na kushambulia kazi ya Mungu katika siku za mwisho hivyo, na kuwazuia watu dhidi ya kuchunguza na kufuata nyayo za Mungu na kutii kazi ya Mungu, hilo kweli haliwafanyi kuwa Mafarisayo wa kisasa waliomwasi na kumshutumu Kristo? Je, asili ya matendo yao siyo ile ambayo inachukia ukweli na kumkufuru Roho Mtakatifu? Shutuma katili ya viongozi wa dunia ya dini kwa kuonekana na kazi ya Mungu pia inatimiza kikamilifu maneno ya Bwana Yesu alipotabiri kiurudi Kwake: “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki(Luka 17:24-25).

Kama Mwenyezi Mungu hangezungumza maneno Yake na kufunua siri, basi hatungewahi kuelewa kweli maana ya unabii: “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi.” Mwenyezi Mungu anasema: “Watu wote wanapotilia maanani, wakati vitu vyote vinafanywa upya na kuhuishwa, wakati kila mtu anamtii Mungu bila shaka, na yuko tayari kubeba jukumu zito la mzigo wa Mungu—hapa ndipo wakati umeme wa mashariki unatoka, ukiangaza yote kutoka Mashariki hadi Magharibi, ukiyatisha yote ya ulimwengu na ujaji wa mwanga huu; na wakati huu, Mungu tena huanza maisha Yake mapya. … Ambayo ni kusema, katika Mashariki ya dunia, kutoka wakati ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe huanza, hadi wakati Yeye huanza kufanya kazi, mpaka wakati uungu huanza kushika madaraka makuu pande zote duniani—huu ni mwale unaong’aa wa umeme wa mashariki, ambao daima umemulika kwa ulimwengu mzima. Wakati ambapo nchi duniani zinakuwa ulimwengu wa Kristo ndio wakati ambapo ulimwengu mzima unatiwa nuru. Sasa ndio wakati ambapo umeme wa mashariki unatoka: Mungu mwenye mwili Anaanza kufanya kazi, na, zaidi ya hayo, Anaongea moja kwa moja katika uungu. Inaweza kusemwa kwamba Mungu anapoanza kuongea duniani ni wakati ambapo umeme wa mashariki unatoka. Kwa usahihi zaidi, wakati ambapo maji ya uhai yanatiririka kutoka katika kiti cha enzi—wakati ambapo matamshi kutoka katika kiti cha enzi huanza—bila shaka ni wakati ambapo matamshi ya Roho saba huanza kirasmi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 12). “Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Kama mtoto mchanga aliyezaliwa hivi karibuni, wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki…. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni ‘mtoto mchanga’ Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni). Kutokana na maneno ya Mwenyezi Mungu tunaona kuwa kazi ya Mungu na neno la siku za mwisho ni umeme ambao huangaza kutoka Mashariki. “Umeme” ni mwanga mkubwa, kumaanisha neno la Mungu, njia ya Mungu ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho. Kifungu “unavyotokea mashariki” kinamaanisha hutoka China, na “kumulika pia magharibi” kikimaanisha kuwasili katika nchi za Magharibi. Mwisho, “ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia” kinahusu Mungu kupata mwili na kwanza akijifichua Mwenyewe na kuanza kazi Yake nchini China katika Mashariki. Huko Analifanya kundi la watu ambao kwa kweli wanamjua Mungu, na wao ni washindi kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo. Kisha kupitia watu hawa, injili ya siku za mwisho itaenea Magharibi, ili kila mmoja atapokea wokovu wa Mungu wa siku ya mwisho. Hili limefanikishwa sasa na ni ukweli ambao unaweza kuonekana na kila mtu! Umeme wa Mashariki (yaani, kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho nchini China) unaweza kuturuhusu tupokee upendo wote na wokovu ambao Mungu humfadhilia mwanadamu, unaweza kuturuhusu tuujue uso wa kweli wa Mungu, na husababisha ndani yetu uchaji na ibada ya kweli ya Mungu. Kama tu pigo la umeme, neno la Mungu humpa mwanadamu mwanga na matumaini. Wale wote ambao huukubali Umeme wa Mashariki—kazi ya Mungu ya siku za mwisho—wote wanaweza kulishuhudia jambo hili.

Sasa, mnaposoma hili, naamini nyinyi nyote mna jibu dhahiri kwa swali la ni nini asili ya Umeme wa Mashariki. Mungu ni Muumba wa mbingu na nchi na vitu vyote. Kwa sababu mtu alipotoshwa na Shetani, Mungu alianza kazi Yake ya kumwokoa mwanadamu. Mungu anataka kuwafanya watu wote katika ulimwengu kuyaona matendo Yake, kwamba dini zote zitakuwa moja, zikimwabudu Muumba. Kisha Atawaruhusu wale wote watafutao kuonekana kwa Mungu na kufuata nyayo Zake kufanikisha usafi na kufikia wokovu. Atawachukua watu hawa ambao wanaupendeza moyo wa Mungu katika ufalme kupumzika na Yeye. Kwa hiyo, kila mmoja wa ndugu zetu wa kiume na wa kike ambao kweli wanaamini katika Mungu na kwa shauku hungoja kurudi kwa Bwana Yesu lazima waweke dhana zetu za kidini kando na kuchunguza njia ya kweli. Usitilie maanani uvumi, kupinga njia ya kweli kwa upofu, kwa kuwa itaishia katika kuupoteza wokovu wa Mungu katika siku za mwisho. Ni lazima tufanye hima kufuata hatua za kazi ya Mungu, kufuata nyayo za Mungu kwa karibu. Hii ndiyo njia ya pekee ambayo kwayo tunaweza kupata wokovu Wake hatimaye na kuletwa na Mungu katika ufalme Wake.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp