Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi? | Dondoo 466

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi? | Dondoo 466

154 |26/08/2020

Ijapokuwa imani yako ni ya kweli, hakuna kati yenu anayeweza kueleza kunihusu kabisa, na hakuna kati yenu anayeweza kushuhudia uhalisi mnaouona. Tafakari kuhusu jambo hili. Sasa hivi wengi wenu hamyatimizi wajibu wenu, mkifuata vitu vya mwili, mkishibisha mwili na kuburudika kwa mwili. Mnamiliki ukweli mdogo. Unawezaje basi kushuhudia yote ambayo umeyaona? Una uhakika kuwa utakuwa shahidi Wangu? Iwapo siku moja utashindwa kushuhudia yote ambayo umeyaona leo, basi utakuwa umepoteza jukumu la kiumbe aliyeumbwa. Hakutakuwa na maana kabisa ya kuwepo kwako. Utakuwa hustahili kuwa binadamu. Mtu anaweza hata kusema kuwa wewe si binadamu! Nimefanya kazi isiyo na kifani kwako. Lakini kwa sababu kwa sasa hujifunzi chochote, hujui chochote, na kufanya kazi bure, Nikitaka kuipanua kazi Yangu utatazama bila kuelewa, bila kusema chochote na kuwa asiye na umuhimu wowote. Hiyo haitakufanya mtenda dhambi mkubwa zaidi? Wakati huo utakapofika, je, hutakuwa na majuto makuu? Hutazama katika huzuni kubwa? Sifanyi kazi hii yote sasa kwa sababu ya uchoshi, bali kuweka msingi kwa kazi Yangu ya baadaye. Sio eti Niko katika njia isiyopitika na Nahitajika kubuni kitu kipya. Unafaa kuelewa kuwa kazi ambayo Nafanya si mchezo wa kitoto bali ni kwa uwakilishi wa Baba Yangu. Unafaa kujua kuwa si Mimi tu Ninayefanya haya yote pekee Yangu bali Namwakilisha Baba Yangu. Wakati uo huo, jukumu lako ni kufuata, kuheshimu, kubadilika, na kushuhudia kwa makini. Unachofaa kuelewa ni kwa nini unafaa kuniamini. Hili ndilo swali muhimu kwa kila mmoja wenu kuelewa. Baba Yangu, kwa ajili ya utukufu Wake, ndiye Aliyewachagua ninyi kwa ajili Yangu kutoka wakati Alipoumba dunia. Haikuwa kwa ajili ya kitu kinginge ila kwa ajili ya kazi Yangu na kwa ajili ya utukufu Wake, ndio maana Aliweka hatima yenu awali. Ni kwa sababu ya Baba Yangu ndio unaniamini; ni kwa sababu ya Baba Yangu kukuamua kabla ndio maana unanifuata Mimi. Hakuna kati ya haya ambayo ulichagua kwa hiari yako mwenyewe. La muhimu zaidi ni kwamba muelewe kuwa ninyi ni wale ambao Baba Yangu alinitawazia kwa ajili ya kushuhudia kwa niaba Yangu. Kwa sababu Aliwatawaza Kwangu, mnafaa kuzifuata njia ambazo Natawaza kwenu na njia na maneno ambayo Ninawafunza, kwani ni jukumu lenu kuzifuata njia Zangu. Hili ndilo kusudi la asili la imani yenu Kwangu. Kwa hivyo Nawaambieni, ninyi ni watu tu ambao Baba Yangu Alitawaza Kwangu ili mfuate njia Zangu. Hata hivyo, mnaamini tu Kwangu; ninyi si wa Kwangu kwa sababu ninyi si wa familia ya Wayahudi bali ni wa joka la zama. Kile Ninachowauliza ni muwe washahidi Wangu, lakini leo lazima mtembee kwa njia Zangu. Haya yote ni kwa ajili ya ushuhuda wa baadaye. Mkihudumu tu kama watu ambao wanasikiliza njia Zangu pekee, basi hamtakuwa na thamani yoyote na umuhimu wa Baba Yangu kuwatawaza Kwangu utapotea. Ninachosisitiza kuwaambia ni hiki: “Mnapaswa kutembea katika njia Zangu.”

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi