Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 522

17/09/2020

Sasa unafaa uweze kuona waziwazi njia iliyochukuliwa na Petro. Kama umeiona waziwazi, basi huenda umejua kazi inayofanywa leo, kwa hiyo usingelalamika au kuwa mtulivu tu, au kutamani chochote. Unafaa kupitia hali halisi aliyopitia Petro wakati huo: Alikumbwa na huzuni; hakuomba tena kuwa na mustakabali wowote au baraka zozote. Hakutafuta faida, furaha, umaarufu, au utajiri wa ulimwengu na alitafuta tu kuishi maisha yenye maana zaidi, ambayo yalikuwa ya kulipiza upendo wa Mungu na kujitolea kile alichokuwa nacho cha thamani zaidi kwa Mungu. Kisha angetosheka katika moyo wake. Mara nyingi aliomba kwa Yesu akitumia maneno haya: “Bwana Yesu Kristo, niliwahi kukupenda Wewe, lakini sikukupenda Wewe kwa kweli. Ingawa nilisema nina imani kwako Wewe, sikuwahi kukupenda kwa moyo wa kweli. Nilikuwa nakutazamia tu, nikikuabudu Wewe, na kukupeza Wewe, lakini sikuwahi kukupenda Wewe au kuwa na imani ya kweli kwako Wewe.” Siku zote aliomba ili kutoa azimio lake, alihimizwa kila wakati na maneno yake Yesu na kuyageuza kuwa motisha. Baadaye, baada ya kipindi cha kile alichopitia, Yesu alimjaribu yeye, akimchochea kumtaka Yeye zaidi. Alisema: “Bwana Yesu Kristo! Ninakupeza kweli, na kutamani kukutazamia. Ninakosa mengi mno, na siwezi kufidia upendo Wako. Ninakusihi kunichukua hivi karibuni. Utanihitaji mimi lini? Utanichukua lini? Ni lini nitakapoutazama uso Wako tena? Sitamani tena kuishi katika mwili huu, kuendelea kupotoka, na vilevile sipendi kuasi zaidi ya nilivyoasi. Niko tayari kujitolea kile nilichonacho Kwako wewe haraka iwezekanavyo, na singependa kukuhuzunisha Wewe zaidi ya hivi nilivyofanya.” Hivi ndivyo alivyoomba, lakini hakujua wakati huo kwamba Yesu angemfanya kuwa timilifu. Kwenye kipindi hicho cha makali ya majaribio yake, Yesu alijitokeza kwake tena na kusema: “Petro, Ningependa kukufanya kuwa timilifu, ili uwe kipande cha tunda ambacho kitaonyesha kugandishwa kwa wewe kufanywa kuwa timilifu na Mimi, ambacho Nitafurahia. Unaweza kweli kunishuhudia Mimi? Umefanya kile Nilichokuomba kufanya? Umeishi kwa kudhihirisha yale maneno Niliyoyaongea? Uliwahi kunipenda Mimi, lakini Ingawa ulinipenda Mimi, umezidi kwa kunipenda? Ni nini ulichonifanyia Mimi? Unatambua kwamba wewe hufai upendo Wangu, lakini wewe umenifanyia nini?” Petro aliona kwamba alikuwa hajamfanyia chochote Yesu na akakumbuka kiapo cha awali cha kumpa Mungu maisha yake. Na kwa hiyo, hakulalamika tena, na maombi yake baadaye yakazidi kuwa bora zaidi. Akaomba, akisema: “Bwana Yesu Kristo! Niliwahi kukuacha Wewe, na Wewe pia uliwahi kuniacha mimi. Tumekuwa mbalimbali kwa kipindi cha muda, na muda kiasi tukiwa pia pamoja. Ilhali unanipenda mimi zaidi ya kila kitu kingine. Nimekuasi Wewe mara nyingi na nikakuhuzunisha mara nyingi. Ninawezaje kusahau mambo kama haya? Kazi uliyofanya ndani yangu mimi na kile kwenye akili yangu, huwa ulichoniaminia kwa imani ndicho ninachofikiria siku zote sisahau. Pamoja na kazi uliyonifanyia mimi nimejaribu kadri ya uwezo wangu. Unajua kile ninachoweza kufanya, na unajua zaidi wajibu ninaoweza kutekeleza. Ombi lako ndilo amri yangu na nitajitolea kila kitu nilichonacho Kwako. Wewe tu ndiwe unayejua kile ninachoweza kukufanyia Wewe. Ingawa Shetani alinidanganya sana na nikakuasi Wewe, ninaamini kwamba hunikumbuki mimi kwa dhambi hizo, kwamba hunichukulii mimi kutokana na hizo dhambi. Ningependa kuyatoa maisha yangu yote kwa ajili Yako wewe. Siombi chochote, na wala sina matumaini au mipango mingine; ningependa tu kuchukua hatua kulingana na nia Zako na kutimiza mapenzi Yako. Nitakunywa kutoka kwenye kikombe Chako kichungu, na mimi ni Wako wa kuamuru.”

Lazima muwe wazi kuhusu njia mnayotembelea; lazima muwe wazi kuhusu njia mtakayotumia kwenye siku za usoni, ni nini haswa ambacho Mungu atafanya kuwa timilifu na ni nini mlichoaminishiwa. Siku moja, pengine, utajaribiwa, na kama wakati huo mtaweza kupata mhemko kutoka kwa yale aliyopitia Petro, utawaonyesha kwamba kwa kweli unatembea njia ya Petro. Petro alipongezwa na Mungu kwa imani na upendo wake wa kweli, na kwa utiifu wake kwa Mungu. Na ilikuwa kutokana na uaminifu wake na kutamani kwake kwa Mungu katika moyo wake ndiposa Mungu akamfanya kuwa timilifu. Kama kweli unao upendo na imani kama hiyo ya Petro, basi Yesu kwa kweli atakufanya kuwa timilifu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp