Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 312

16/10/2020

Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanazunguka kila pembe, wakihadaa na kudanganya, wakitoa shutuma zisizokuwa na msingi, wakiwa wakatili na waovu, wakiukandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo imeijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa visivyo kawaida. Nani awezaye kuuona ulimwengu zaidi ya anga? Shetani anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kukifunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa mashetani amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la mapepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yenye hasira, wakiogopa sana kwamba Mungu atawapata kwa ghafula na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha bila mahali pa amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamewahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa mapenzi ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili bado Amefichwa kabisa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo mashetani hawana huruma nao ni katili, inawezekanaje mfalme wa mashetani anayeua watu kwa kufumba na kufumbua, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na pia mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, na hawana hata chembe ya wema, na wanawajaribu watu wasio na hatia na kuwa watu wasio na uwezo wa kuhisi. Wahenga wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umewaacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote ni njama za kufunika dhambi! Nani ambaye ameikumbatia kazi ya Mungu? Nani ametoa maisha yake au kumwaga damu kwa ajili ya kazi ya Mungu? Kwa kizazi baada ya kizazi, kutoka kwa wazazi hadi watoto, mwanadamu aliye katika utumwa amemfanya Mungu mtumwa bila heshima—hii inawezaje kutoamsha hasira? Maelfu ya miaka ya chuki imejaa moyoni, milenia ya utendaji dhambi zimeandikwa katika moyo—inawezekanaje hii isichochee ghadhabu? Mlipize Mungu, mwondoe kabisa adui Yake, usimruhusu kutangatanga tena, na usimruhusu kufanya fujo zaidi kama anavyotaka! Sasa ni wakati: Mwanadamu amepata nguvu kwa muda mrefu, ametumia nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa ajili ya hili, kuuchana uso uliojificha wa pepo huyu na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kumwacha Shetani huyu wa zamani. Kwa nini kuweka kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini kutumia hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali viko wapi? Haki iko wapi? Faraja iko wapi? Wema uko wapi? Kwa nini kutumia mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini kutumia nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini asimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini kumubana Mungu hadi Anakosa mahali pa kupumzisha kichwa Chake? Wema uko wapi miongoni mwa wanadamu? Ukarimu uko wapi miongoni mwa wanadamu? Kwa nini kusababisha matamanio makubwa kiasi hicho katika Mungu? Kwa nini kumfanya Mungu kuita tena na tena? Kwa nini kumlazimisha Mungu kumhofia Mwana Wake mpendwa? Kwa nini jamii hii ya giza na mbwa walinzi wake wasimruhusu Mungu kuja bila kizuizi na kuzunguka dunia ambayo Aliiumba? Kwa nini mwanadamu haelewi, mwanadamu anayeishi katika maumivu na mateso? Mungu amevumilia mateso makubwa kwa ajili yenu, kwa maumivu makubwa Amemtoa Mwanawe wa pekee, mwili na damu Yake, kwenu—hivyo kwa nini bado hamuoni? Katika mtazamo mzima wa kila mtu, mnakataa ujio wa Mungu, na kukataa urafiki wa Mungu. Kwa nini mnakosa busara kiasi hicho? Mko tayari kuvumilia uonevu katika jamii ya giza kama hii? Kwa nini, badala ya kujaza tumbo zenu kwa milenia ya uadui, mnajishindilia “kinyesi” cha mfalme wa mashetani?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp