Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 322

29/08/2020

Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamumwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno. Kile Ninachomwomba binadamu, si tu yeye kuniita Mimi kwa shauku kwa njia hii au kuniamini Mimi kwa mtindo huu wa kukosa mwelekeo. Kwani kazi Ninayoifanya ni yake binadamu kunijia Mimi na kunijia Mimi, wala si kwa binadamu kuvutiwa na kuniangalia Mimi kwa njia mpya kwa sababu ya kazi Yangu. Awali Nilijionyesha katika ishara na maajabu mengi na kufanya miujiza mingi. Waisraeli wakati huo waliniangalia Mimi kwa tamanio kuu na walistahi pakubwa uwezo Wangu wa kipekee wa kuponya wagonjwa na kupunga mapepo. Wakati huo, Wayahudi walifikiri nguvu Zangu za uponyaji zilikuwa za kistadi na zisizo za kawaida. Kwa matendo Yangu mengi kama hayo, wote walinichukulia Mimi kwa heshima; waliweza kuhisi tamanio kuu katika nguvu Zangu zote. Kwa hiyo yeyote aliyeniona Mimi nikifanya miujiza alinifuatilia Mimi kwa karibu kiasi kwamba maelfu ya watu walinizunguka ili kunitazama nikiwaponya wagonjwa. Nilionyesha ishara na maajabu mengi, ilhali binadamu alinichukulia Mimi kama daktari stadi; Niliongea maneno mengi ya mafunzo kwa watu hao wakati huo, ilhali wote walinichukulia Mimi tu kama mwalimu aliyekuwa na mamlaka zaidi kwa wanafunzi wake! Hadi siku ya leo, baada ya binadamu kuona rekodi za kihistoria za kazi Yangu, ufasiri wao unaendelea kuwa kwamba Mimi ni daktari mkuu anayeponya wagonjwa na mwalimu kwa wasiojua. Na wameniita Mimi Bwana Yesu Kristo Mwenye huruma. Wale wanaofasiri maandiko huenda walizidi mbinu Zangu katika uponyaji, au huenda pengine wakawa wanafunzi ambao tayari wamempita mwalimu wao, ilhali binadamu kama hao wanaofahamika sana ambao majina yao yanajulikana kote ulimwenguni wananichukulia Mimi kwa kiwango cha chini sana cha kuwa daktari tu! Matendo Yangu ni mengi zaidi kwa kuhesabiwa kuliko chembechembe za changarawe kwenye ufuo na hekima Yangu kubwa zaidi kuliko ile ya watoto wote wa kiume wa Suleimani, ilhali binadamu wanafikiria kwamba Mimi ni daktari tu asiye na mengi kumhusu na mwalimu wa binadamu asiyejulikana! Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze tu kupata uponyaji? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu niweze kutumia nguvu Zangu kupunga roho chafu kutoka kwenye miili yao? Na ni wangapi wanaoniamini Mimi hili tu waweze kupokea amani na furaha kutoka Kwangu? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili kuhitaji kutoka Kwangu utajiri mwingi zaidi wa dunia, na ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuishi maisha hayo kwa usalama na kuwa salama salimini katika maisha yajayo? Ni wangapi wanaoniamini Mimi ili waweze kuepuka tu mateso ya kuzimu na kupokea baraka za mbinguni? Ni wangapi wanaoniamini Mimi hili wapate tulizo lakini hawatafuti kupata chochote kutoka kwa ulimwengu ujao? Niliposhushia hasira Zangu binadamu na kuchukua furaha na amani yote aliyokuwa nayo mwanzo, binadamu akaanza kuwa na shaka. Nilipomkabidhi binadamu mateso ya kuzimu na kuchukua tena baraka za mbinguni, aibu ya binadamu iligeuka na kuwa hasira. Wakati binadamu aliponiomba Mimi kumponya, bado Sikumtambua na vilevile nilimchukia pakubwa, binadamu alienda mbali sana na Mimi na akatafuta njia za waganga na wachawi. Nilipochukua kila kitu ambacho binadamu alitaka kutoka Kwangu, kisha kila kitu kilitoweka bila kuonekana tena. Kwa hivyo, Ninasema kwamba binadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata. Wayahudi waliniamini Mimi kwa neema Yangu, na wakanifuata Mimi popote Nilipoenda. Binadamu hawa wasiojua wenye maarifa na uzoefu finyu walitafuta tu kuona ishara na maajabu ambayo nilionyesha. Walinichukulia Mimi kuwa mkuu wa nyumba ya Wayahudi ambaye angeweza kutekeleza miujiza mikubwa zaidi. Kwa hivyo, Nilipopunga mapepo kutoka kwa binadamu walijizungumzia miongoni mwao kwa mkanganyo mkubwa wakisema Mimi ni Eliya, kwamba Mimi ni Musa, kwamba Mimi ndimi nabii wa kale zaidi kati ya wote, kwamba Mimi ndimi daktari mkuu zaidi kuliko wote. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Mimi ndimi maisha, njia na ukweli, hakuna yeyote angejua uwepo Wangu au utambulisho Wangu. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba mbingu ndipo ambapo Baba Yangu anapoishi, hakuna aliyejua kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu, na tena Mungu Mwenyewe. Mbali na Mimi Mwenyewe kusema kwamba Nitaleta ukombozi kwa wanadamu wote na kulipia mwanadamu fidia, hakuna aliyejua Mimi ni Mkombozi wa mwanadamu; binadamu alinijua tu Mimi kama mtu mkarimu na mwenye huruma. Na mbali na Mimi Mwenyewe kuweza kufafanua kila kitu kuhusu Mimi, hakuna aliyeweza kunitambua Mimi, hakuna aliyeamini kwamba Mimi ni Mwana wa Mungu aliye hai. Binadamu pia anayo imani kama hii Kwangu Mimi, na ananidanganya Mimi kwa njia hii. Binadamu anawezaje kunitolea Mimi ushuhuda wakati anayo mitazamo kama hii kunihusu Mimi?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp