Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Maana ya Kuwa Mtu Halisi | Dondoo 349

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Maana ya Kuwa Mtu Halisi | Dondoo 349

80 |13/08/2020

Mwanadamu ameendelea kwa maelfu ya miaka ya historia mpaka kufikia walipo leo. Hata hivyo, wanadamu wa uumbaji Wangu wa awali kwa muda mrefu uliopita wameshazama katika upotovu. Tayari wao wamecha kuwa kile Nilichotaka, kwa hivyo wanadamu, Ninavyowaona, tayari ni wasiostahili jina la uanadamu. Badala yake wao ni uchafu wa wanadamu, walioporwa na Shetani, na ni maiti mbovu zinazotembea ambamo Shetani anaishi na Shetani kuvalia. Watu hawaamini hata kidogo kuwepo Kwangu, wala hawakaribishi kuwasili Kwangu. Mwanadamu kwa shingo upande tu huyajibu maombi Yangu, na kwa muda anakubaliana nayo, na hashiriki katika furaha ya maisha na huzuni kwa kweli pamoja na Mimi. Kama vile binadamu wanavyoniona Mimi kama Asiyeeleweka, bila ya kutaka wao hujifanya wanatabasamu Kwangu, na kusaliti namna yao ya kujidekeza kwa madaraka. Hii ni kwa sababu watu hawana ufahamu wa kazi Yangu, wala ule wa nia Yangu leo. Nitakuwa wazi na nyinyi nyote—siku itakapofika, mateso ya mwanadamu yeyote anayeniabudu yatakuwa rahisi kubeba kuliko yenu. Kiwango cha imani yako Kwangu hakiwezi, kwa hakika, kuzidi kile cha Ayubu—na hata imani ya Mafarisayo Wayahudi inaishinda yenu—hivyo katika siku zinazokaribia za moto, utapata mateso zaidi kuliko ya Mafarisayo walipokemewa na Yesu, kali zaidi kuliko ya wale viongozi 250 waliompinga Musa, na mateso zaidi kuliko Sodoma chini ya moto mkali wakati wa uharibifu wake. Musa alipougonga mwamba, na maji aliyokuwa Ameyatoa Yehova yakaruka, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Daudi alipocheza muziki wa sifa Kwangu, Yehova—moyo wake ukiwa umejaa furaha—ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Ayubu alipowapoteza wanyama wake wote kote milimani, akapoteza mali yenye thamani kwa familia yake, na mwili wake kujawa na majipu, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Alipoweza kusikia sauti Yangu, Yehova, na kuuona utukufu Wangu, Yehova, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Kwamba Petro aliweza kumfuata Yesu Kristo, ilikuwa ni kwa imani yake. Kwamba Alitundikwa misumari msalabani kwa ajili Yangu na kutoa ushahidi mtukufu, pia ilikuwa kwa imani yake. Yohana alipoona mfano wa utukufu wa Mwana wa Adamu, ilikuwa kwa imani yake. Alipoona maono ya siku za mwisho, yote yalikuwa zaidi kwa sababu ya imani yake. Watu wanaojulikana kama wa taifa la Mataifa walipopokea ufunuo Wangu, walipojua kwamba Nimerudi katika mwili kufanya kazi Yangu miongoni mwa wanadamu, pia ni kwa sababu ya imani yao. Je si wote ambao wamepigwa na neno Langu kali na hivyo kufarijiwa na kuokolewa wamefanya hivyo kwa sababu ya imani yao? Wale wanaoamini Kwangu na kupitia mateso, je si pia wanakabiliwa na kukataliwa na dunia? Wale wanaoishi nje ya neno Langu, waliokimbia mateso ya majaribu, si wao wanazurura tu ulimwengu? Wao ni sawa na majani ya msimu wa kupukutika kwa majani yanayopeperuka hapa na pale na pasipo na pahali pa kupumzika, wala pasiwe na neno Langu la kufutia machozi. Ingawa kuadibu Kwangu na usafishaji hauwafuati wao, je, wao si waombaji, wanaoelea kila mahali, ambao wanatangatanga katika mitaa iliyo nje ya Ufalme wa mbinguni? Je, dunia ni mahali pako pa mapumziko kweli? Je, unaweza kupata tabasamu dhaifu ya kutosheleza kutoka kwa dunia kwa kuepuka kuadibu Kwangu? Je, unaweza kweli kutumia starehe zako za kidunia kama maficho ya utupu ulio katika moyo wako usioweza kufichika? Unaweza kumdanganya mtu yeyote katika familia yako, ilhali huwezi kunidanganya Mimi kamwe. Kwa kuwa imani yako ni ndogo, mpaka wa leo huna uwezo wa kupata raha inayoletwa na maisha. Nawashauri: ni heri kutumia nusu ya maisha yako Kwangu kwa dhati kuliko kuishi maisha yako yote katika hali hafifu na kujishughulisha kwa ajili ya mwili, kuvumilia mateso yote ambayo ni vigumu binadamu kuvumilia. Kutakuwa na faida gani ya wewe kujipenda sana mpaka kiwango cha kuikimbia kuadibu Kwangu? Utafaidi nini ukijificha kutoka kwa kuadibu Kwangu kwa muda mfupi tu, na mwishowe upate aibu ya milele, na kuadibu kwa milele? Mimi, kwa hakika, Sitamlazimisha yeyote kufanya mapenzi Yangu. Iwapo mtu kweli anayo nia ya kujiwasilisha kwa mipango Yangu yote, Sitamtendea vibaya. Lakini Nahitaji kwamba watu wote waamini ndani Yangu, kama vile Ayubu alivyoamini ndani Yangu, Yehova. Iwapo imani yako inazidi ile ya Tomaso, basi imani yako itapata pongezi Zangu, katika uaminifu wako utapata furaha Yangu, na wewe hakika utapata utukufu Wangu katika siku zako. Hata hivyo watu, wanaoamini katika dunia na wanaomwamini shetani, wamefanya mioyo yao kuwa migumu, kama vile halaiki za mji wa Sodoma, chembe za mchanga zikivuma katika macho yao na sadaka za Shetani zikiwa zimeshikiliwa vinywani mwao. Nyoyo zao zilizodanganywa kwa muda mrefu uliopita zimemilikiwa na yule mwovu aliyekuwa ameipora dunia, na karibu mawazo yao yote yameporwa na pepo za kale. Kwa hivyo imani ya mwanadamu imekwenda na upepo, na wao hawawezi hata kuitambua Kazi Yangu. Wanachoweza kufanya ni kuvumilia tu au kuchambua kwa kukisia sana, kwa sababu wao tayari wamejawa na sumu ya Shetani.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi