Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 367

21/08/2020

Mwanadamu ni kiumbe asiyejifahamu. Hata ingawa hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja cha mkono wake, kana kwamba watu wengine wote wamepitia ukaguzi wake na kupokea kibali chake kabla waseme au kufanya chochote, na hivyo ionekane kama yeye amewapima kikamilifu wengine wote mpaka katika hali yao ya kisaikolojia. Binadamu wote wako namna hii. Mwanadamu ameingia katika Enzi ya Ufalme leo hii, lakini asili yake bado haijabadilika. Yeye bado anafanya kama Ninavyofanya akiwa mbele Yangu, lakini nyuma Yangu anaanza kufanya “shughuli” zake mwenyewe za kipekee. Hata hivyo, mara hiyo inapokamilika na anarudi mbele Yangu tena, yeye huwa kama mwanadamu tofauti, akiwa na hali ya utulivu safihi, hali yake ni shwari, na mpigo wa moyo wake ni mtulivu. Je, si hili ndilo hasa hufanya mwanadamu kudharauliwa? Ni watu wangapi huvaa sura mbili tofauti kabisa, moja mbele Yangu na nyingine nyuma Yangu? Wangapi kati yao ni kama wanakondoo wachanga mbele Yangu lakini nyuma Yangu hugeuka na kuwa chui wabaya wenye milia wakali kinyama, na kisha kugeuka ndege wadogo wanaorukarukakwa furaha milimani? Ni wangapi huonyesha lengo na uamuzi mbele Yangu? Ni wangapi huja mbele Zangu, kutafuta maneno Yangu kwa kiu na hamu lakini, nyuma Yangu, kukerwa nayo na kuyaacha, kana kwamba maneno Yangu ni mzigo unaosumbua? Mara nyingi, Nikiona jamii ya binadamu ikipotoshwa na adui Yangu, mimi Nimeacha kuweka matumaini Yangu katika mwanadamu. Mara nyingi, Nikiona mwanadamu akija mbele Zangu kwa machozi akiomba msamaha, lakini kwa sababu ya kutojiheshimu kwake, utundu wake usiorekebika, Nimefunga macho Yangu kwa vitendo vyake kwa hasira, hata wakati moyo wake ni wa kweli na nia yake ni ya dhati. Mara nyingi, Naona mwanadamu akiwa na uwezo wa kuwa na imani ya kushirikiana na Mimi, na jinsi, mbele Yangu, anaonekana kuwa amekaa katika kumbatio Langu, akionja joto la kumbatio Langu. Mara nyingi, kwa kuona upole, uchangamfu, na uzuri wa watu Wangu Niliowachagua, katika Moyo wangu Mimi daima Nimekuwa na furaha kwa sababu ya mambo haya. Binadamu hawajui jinsi ya kufurahia baraka Nilizowaamulia kabla katika mikono Yangu, kwa sababu wao hawajui ni nini hasa maana ya baraka au mateso. Kwa sababu hii, wanadamu wako mbali na kweli katika jitihada zao za kunitafuta. Kama hakungekuwa na kesho, nani kati yenu, mlio mbele Yangu, angekuwa mweupe kama theluji inayoendeshwa, bila doa kama jiwe safi la thamani? Hakika upendo wako Kwangu si kitu ambacho kinaweza kubadilishwa kwa mlo wenye ladha, au suti yenye ufahari, au ofisi ya juu na mishahara mikubwa? Au inaweza kubadilishwa na upendo ambao wengine wako nao kwako? Hakika, kupitia majaribu hakutawafukuza wanadamu waache upendo wao Kwangu? Hakika, mateso na dhiki hayatasababisha mwanadamu alalamike dhidi ya kile Nimepanga? Hakuna mwanadamu aliyewahi kweli kufahamu upanga ulio katika kinywa Changu: Yeye anajua maana yake ya juu bila kufahamu undani wake. Kama binadamu wangeweza kufahamu kwa kweli ukali wa upanga wangu, wangetoroka kwa uoga kama vile panya wanavyokimbilia mashimo yao. Kwa sababu ya kutokuwa kwao na hisia, wanadamu hawaelewi kitu chochote cha maana halisi ya maneno Yangu, na hivyo wao hawana kidokezo kuhusu jinsi maneno Yangu ni yenye kuogofya, au kiasi gani asili yao imefichuliwa, na ni kiasi gani cha upotovu wao umepokea hukumu, ndani ya maneno hayo. Kwa sababu hii, kulingana na mawazo yao yasiyo kamili kuhusu maneno Yangu, watu wengi wamechukua msimamo vuguvugu na usio wa kuwajibika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 15

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp