Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Mawazo ya Kidini | Dondoo 283

20/07/2020

Kwa sababu kazi ya Mungu mara zote huwa na masuala mapya, hivyo pana kazi mpya, na hivyo basi kuwepo na kazi iliyopitwa na wakati. Hapana ukinzani kati ya kazi mpya na ya zamani, ila zinatoshelezana, kila hatua ikifuata iliyotangulia. Kwa kuwa kuna kazi mpya, mambo ya zamani, kwa hakika, ni sharti yaondolewe. Kwa mfano, baadhi ya vitendo vilivyokita mizizi na misemo ya mwanadamu iliyozoeleka, kuongeza juu miaka mingi ya mazoea na mafundisho ya mwanadamu, ilimuumbia mwanadamu kila aina ya dhana. Maelezo ya mwanadamu kuhusu dhana kama hizi ni kwamba bado Mungu hajafichua uso Wake halisi na tabia Yake asili kwa mwanadamu, pamoja na kuenea kwa nadharia za kale kwa miaka mingi. Ni haki kusema kuwa katika kipindi cha imani ya mwanadamu kwa Mungu, ushawishi wa dhana mbalimbali umesababisha kutengenezwa na kubadilika kwa ufahamu kwa mwanadamu ambapo mwanadamu ana kila aina ya dhana kumhusu Mungu—na matokeo yake ni kuwa wengi wa watu wa kidini wanaomhudumia Mungu wamegeuka kuwa adui Zake. Kwa hivyo, kadiri dhana za watu ya kidini zinavyokuwa thabiti, ndivyo wanavyozidi kumpinga Mungu, na ndivyo wanavyozidi kuwa maadui wa Mungu. Kazi ya Mungu daima huwa mpya, si kongwe na huwa haitengenezi mafundisho ya kidini na badala yake inabadilika kila mara na kuwa mpya kwa kiwango fulani. Kazi hii ni onyesho la tabia ya asili ya Mungu Mwenyewe. Vilevile ni kanuni ya asili ya kazi ya Mungu na mojawapo ya njia ambazo Mungu hutimiza usimamizi Wake. Iwapo Mungu asingefanya kazi kwa njia hii, mwanadamu asingebadilika au kuweza kumfahamu Mungu, na Shetani asingeshindwa. Hivyo basi, kila mara katika Kazi Yake, kunatokea mabadiliko ambayo yanaonekana hayatabiriki, ila ambayo, kwa hakika, yana kipindi chake. Njia mwanadamu anavyomwamini Mungu hata hivyo ni tofauti: anashikilia mifumo ya zamani ya kidini na kadiri yalivyo ya zamani, ndivyo yanavyokuwa ya kupendeza kwake. Akili ya kipumbavu ya mwanadamu, akili isiyobadilika kama mawe inawezaje kukubali kazi nyingi isiyoeleweka mpya na maneno ya Mungu? Mwanadamu anamchukia Mungu ambaye ni mpya kila siku na si wa zamani; anampenda Mungu wa zamani ambaye Amejaa mvi na Asiyepiga hatua. Hivyo, kwa sababu Mungu na mwanadamu kila mmoja analo alipendalo, mwanadamu amekuwa adui wa Mungu. Kwa kiwango kikubwa, huu utata upo hata leo, wakati ambao Mungu amekuwa akifanya kazi mpya kwa takribani miaka 6000. Hawawezi kusaidika. Labda ni kwa sababu ya usumbufu wa mwanadamu, au kutokiukwa kwa kazi ya Mungu—ila hawa wahubiri bado wanashikilia vitabu vizee na karatasi ilhali Mungu anaendelea na kazi Yake ambayo haijakamilika ya usimamizi kana kwamba hana msaidizi. Japo huu utata unaleta uadui kati ya mwanadamu na Mungu, kiasi kwamba hawapatanishiki, Mungu haujali ukinzani huu. Hata hivyo mwanadamu bado anashikilia imani na dhana zake. Na kamwe haiachilii. Ila kitu kimoja kiko wazi: japo mwanadamu haachi misimamo yake, Mungu mara zote anapiga hatua na kubadilisha misimamo Yake kulingana na muktadha na hatimaye ni mwanadamu atakayeshindwa bila mapambano. Mungu ndiye adui mkubwa zaidi wa maadui wake walioshindwa na vilevile ni bingwa wa wale miongoni mwa wanadamu ambao wameshindwa na wale ambao bado hawajashindwa. Ni nani anaweza kushindana na Mungu na ashinde? Dhana za mwanadamu zinaonekana kutoka kwa Mungu kwani wengi wao walizaliwa kipindi cha kazi ya Mungu. Na bado Mungu hamsamehi mwanadamu kwa sababu ya hili na hata zaidi Hammiminii sifa mwanadamu kwa “kumzalishia Mungu” mazao baada ya mazoa ambayo yamo nje ya kazi ya Mungu. Badala yake Mungu hughadhabishwa sana na dhana, imani za zamani za mwanadamu na hata kuzipuuza tarehe ambayo hizi dhana zilitokea. Hakubali kamwe kwamba hizi dhana zinaletwa na kazi Yake kwani dhana za mwanadamu husambazwa na mwanadamu; chanzo chao ni fikira na akili za mwanadamu, na si Mungu, ila ni Shetani. Madhumuni ya Mungu mara zote ni kuona kazi Yake ikiwa mpya na hai, si kongwe na iliyokufa, na kile Anachotaka mwanadamu ashikilie kwa nguvu kinabadilika kulingana na enzi na kipindi, na si cha kudumu milele na kisichobadilika. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu ambaye husababisha mwanadamu kuishi na kuwa mpya, tofauti na ibilisi anayemsababishia mwanadamu kufa na kuwa mzee. Je, bado hulielewi hili? Una dhana kuhusu Mungu na umeshindwa kuziacha kwa kuwa hutafakari. Si kwamba kuna maana kidogo katika kazi ya Mungu, au kwa sababu kazi ya Mungu haina ubinadamu—wala kwamba Mungu mara zote ni “mzembe katika wajibu Wake.” Huwezi kuacha dhana zako kwa kuwa umepungukiwa na utiifu, na huna sifa hata kidogo za kiumbe wa Mungu, na si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu. Yote haya umejisababishia na hayana uhusiano na Mungu; mateso na misukosuko yote husababishwa na mwanadamu. Dhamira za Mungu mara zote huwa nzuri: hakusudii kukufanya uzitoe dhana, ila angependa ubadilike na uwe mpya kadiri enzi zinavyopita. Ila bado huwezi kutofautisha chokaa na jibini na kila mara ama unachunguza au unachanganua. Si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu, ila ni kuwa humheshimu Mungu na uasi wako umezidi. Kiumbe mdogo anathubutu kuchukua sehemu ndogo ya kile alichopewa mwanzo na Mungu na kukitumia ili kumvamia Mungu—je, huu si uasi wa mwanadamu? Ni haki kusema kuwa mwanadamu hana sifa kabisa za kutoa maoni yake mbele za Mungu, sembuse kubuni apendavyo kanuni zozote zile zisizo na thamani, za kuchukiza na zilizooza—bila kutaja chochote kuhusu hizo dhana zilizooza. Haina maana?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp