Tenzi ya Rohoni | Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

02/05/2020

I

Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia,

unaanza kutenda wajibu wako.

Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako,

na unaanza safari ya maisha.

Vyovyote vilivyo msingi wako ama safari iliyo mbele yako,

hakuna anayeweza kuepuka utaratibu na mpango ambao Mbingu imeweka,

na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake,

kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote

ndiye ana uwezo wa kazi kama hii.

II

Tangu siku ambayo mwanadamu alikuja kuwepo

Mungu amekuwa imara katika kazi Yake,

Akisimamia ulimwengu huu

na kuelekeza mabadiliko na kusonga kwa vitu vyote.

Kama vitu vyote, mwanadamu kwa kimya na bila kujua anapokea

uboreshaji wa utamu, mvua na umande kutoka kwa Mungu.

Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini

ya utaratibu wa mkono wa Mungu.

III

Moyo na roho ya mwanadamu viko mkononi mwa Mungu,

na maisha yote ya mwanadamu yanatazamwa machoni mwa Mungu.

Bila kujali kama unaamini katika hili ua la,

chochote na vitu vyote, viishivyo au vilivyokufa,

vitageuka, vibadilike, vifanywe upya, na kupotea

kulingana na fikira za Mungu.

Hivi ndivyo Mungu hutawala juu ya vitu vyote.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp