Wimbo wa Kusifu | Nimeuona Upendo wa Mungu (Music Video)

10/01/2020

Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda.

Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi!

Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,

nikiishi maisha ya kanisa, nikifurahia maneno Yako kila siku.

Kuwa na baraka kama hizo ni Wewe kuniinua leo!

Mwenyezi Mungu, nimeuona upendo Wako,

na ninachotaka kufanya ni kulipa upendo Wako.

Ninachotaka kufanya ni kutimiza wajibu wangu Kwako.

Nimeuona upendo Wako na nitalipa upendo Wako!

Ni yote ninayotaka kufanya.

Mwenyezi Mungu, Unatembea kati ya makanisa.

Umeonyesha ukweli juu ya tabia zetu potovu.

Unatupogoa na kutushughulikia,

naam, Unatupogoa na kutushughulikia: uasi na upinzani wetu wote.

Unahukumu mawazo yetu yote na fikira zetu zote ili kututakasa.

Mwenyezi Mungu, nimeuona upendo Wako,

na ninachotaka kufanya ni kulipa upendo Wako.

Ninachotaka kufanya ni kutimiza wajibu wangu Kwako.

Nimeuona upendo Wako na nitalipa upendo Wako!

Ni yote ninayotaka kufanya.

Mwenyezi Mungu, Umetuokoa.

Unanena maneno kila siku ili kuturuzuku na kutunyunyizia.

Kupitia shida na mateso yangu,

shida na mateso yangu yote,

Maneno Yako yamekuwa ubavuni mwangu kila wakati.

Kwa kuishi ndani ya maneno Yako, Nimekua maishani mwangu.

Mwenyezi Mungu, nimeuona upendo Wako,

na ninachotaka kufanya ni kulipa upendo Wako.

Ninachotaka kufanya ni kutimiza wajibu wangu Kwako.

Nimeuona upendo Wako na nitalipa upendo Wako!

Ni yote ninayotaka kufanya.

Umetoholewa kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp