Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 108

09/07/2020

Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri

Kutoweza kuvumilia kosa kwa Mungu ndicho kiini Chake cha kipekee; hasira ya Mungu ndiyo tabia Yake ya kipekee; adhama ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya kipekee. Kanuni inayoelezea ghadhabu ya Mungu inaonyesha utambulisho na hadhi ambayo Yeye tu ndiye anayemiliki. Mtu hana haja kutaja kwamba ni ishara pia ya hali halisi ya Mungu Mwenyewe wa kipekee. Tabia ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya asili. Haibadiliki kamwe na kupita kwa muda, wala haibadiliki kila wakati mahali panapobadilika. Tabia Yake ya asili ndiyo kiini Chake halisi cha kweli. Haijalishi ni nani anayetekelezea kazi Yake, hali Yake halisi haibadiliki, na wala tabia ya haki Yake pia. Wakati mtu anapomghadhibisha Mungu, kile Anachomshushia ni tabia Yake ya asili; wakati huu kanuni inayoelezea ghadhabu Yake haibadiliki, wala utambulisho na hadhi Yake ya kipekee. Haghadhibishwi kwa sababu ya mabadiliko katika hali Yake halisi au kwa sababu ya tabia Yake kusababisha dalili tofauti, lakini kwa sababu upinzani wa binadamu dhidi Yake hukosea tabia Yake. Uchochezi waziwazi wa binadamu kwa Mungu ni changamoto kubwa katika utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu. Kwa mtazamo wa Mungu, wakati binadamu anapompinga Yeye, binadamu huyo anashindana na Yeye na anampima ghadhabu Yake. Wakati binadamu anapompinga Mungu, wakati binadamu anaposhindana na Mungu, wakati binadamu anapojaribu kila mara ghadhabu ya Mungu—na ndio maana pia dhambi huongezeka—hasira ya Mungu itaweza kufichuka kwa kawaida na kujitokeza yenyewe. Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitasita kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote katili zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu. Wakati heshima na utakatifu wa Mungu vinapopata changamoto, wakati nguvu za haki zinapata kuzuiliwa na kutoonekana na binadamu, Mungu atashusha hasira Yake. Kwa sababu ya hali halisi ya Mungu, nguvu hizo zote ulimwenguni zinazoshindana na Mungu, zinazompinga Yeye na kushindana na Yeye ni za maovu, kupotoka na kutokuwa na dhalimu; zinatoka Kwake na zinamilikiwa na Shetani. Kwa sababu Mungu ni wa haki, wa nuru na mtakatifu bila dosari, vitu vyote viovu, vilivyopotoka na vinavyomilikiwa na Shetani vitatoweka baada ya kuachiliwa kwa hasira ya Mungu.

Ingawaje kumwagwa kwa hasira ya Mungu ni dhana ya maonyesho ya tabia ya haki Yake, hasira ya Mungu kwa vyovyote vile haibagui walengwa wake au haina kanuni. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu si mwepesi wa ghadhabu, wala Hakimbilii kufichua hasira Yake na adhama Yake. Aidha, hasira ya Mungu inadhibitiwa na kupimwa kwa kiwango fulani; hailinganishwi kamwe na namna ambavyo binadamu atakavyowaka kwa hasira kali au kutoa ghadhabu zake. Mazungumzo mengi kati ya binadamu na Mungu yamerekodiwa kwenye Biblia. Maneno ya baadhi ya watu hawa binafsi yalikuwa ya juujuu, yasiyo na ujuzi na yasiyofaa, lakini Mungu hakuwaangusha chini, wala Hakuwashutumu. Hususan, wakati wa majaribio ya Ayubu, je, Yehova Mungu aliwachukuliaje marafiki watatu wa Ayubu na wale wengine baada ya kusikia maneno waliyomzungumzia Ayubu? Je, Aliwashutumu? Je, Aligeuka na kushikwa na hasira kali kwao? Hakufanya kitu kama hicho! Badala yake Alimwambia Ayubu kuwasihi, kuwaombea; Mungu, kwa mkono mwingine, hakuchukua lawama zao na kutia moyoni. Matukio haya yote yanawakilisha mtazamo mkuu ambao Mungu anashughulikia binadamu waliopotoka, na wasiojua. Kwa hivyo, kushushwa kwa hasira ya Mungu si kwa vyovyote vile maonyesho au hali ya kutoa nje hali Yake ya moyo. Hasira ya Mungu si mlipuko mkubwa wa hasira kali kama vile binadamu anavyoielewa. Mungu hawachilii hasira Yake kwa sababu hawezi kuidhibiti hali ya moyo Wake binafsi au kwa sababu ghadhabu Yake imefikia kilele na lazima itolewe. Kinyume cha mambo ni kwamba, hasira Yake ni maonyesho ya tabia ya haki Yake na maonyesho halisi ya tabia ya haki Yake; ni ufunuo wa ishara ya hali Yake halisi takatifu. Mungu ni hasira, asiyevumilia kosa—hivi si kusema kwamba ghadhabu ya Mungu haitofautishi sababu za kufanya hivyo au haifuati kanuni; ni binadamu waliopotoka ambao unafuata mkondo wa kipekee wa kutokuwa na kanuni, mlipuko wa hasira kali bila mpango usiotofautisha hali hii miongoni mwa sababu mbalimbali. Mara tu binadamu anapokuwa na hadhi, mara nyingi atapata ugumu wa kudhibiti hali ya moyo wake, na kwa hivyo atafurahia kutumia nafasi mbalimbali kueleza kutotosheka kwake na kutoa nje hisia zake; mara nyingi atawaka kwa hasira kali bila sababu yoyote, ili kuonyesha uwezo wake na kuwafanya wengine kujua kwamba hadhi yake na utambulisho wake ni tofauti na ule wa watu wa kawaida. Bila shaka, watu waliopotoka wasiokuwa na hadhi yoyote mara kwa mara pia watapoteza udhibiti wao. Ghadhabu yao mara nyingi husababishwa na uharibifu wa manufaa yao ya kibinafsi. Ili kulinda hadhi yake binafsi na heshima, mwanadamu aliyepotoka mara kwa mara atatoa nje hisia zake na kufichua asili yake yenye kiburi. Binadamu atalipuka kwa ghadhabu na kutoa nje hisia zake ili kutetea uwepo wa dhambi, na matendo haya ndiyo njia ambayo binadamu anaonyesha kutotosheka kwake. Matendo haya yamejaa hadi pomoni kwa kuchafuliwa; yamejaa kwa mifumo na mbinu mbalimbali; yamejaa kupotoka na maovu ya binadamu; zaidi ya hayo, yanajaa kwa malengo na matamanio ya binadamu. Wakati haki inaposhindana na maovu, binadamu hataruka juu kwa ghadhabu ili kutetea uwepo wa haki; kinyume ni kwamba, wakati nguvu za haki zinatishwa, zinateswa na kushambuliwa, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutotilia maanani, kukwepa, au kushtuka. Hata hivyo, wakati anapokabiliwa na nguvu za maovu, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutunza, na kunyenyekea mno. Hivyo basi, kutoa nje ghadhabu kwa binadamu ni kimbilio la nguvu za maovu, maonyesho ya mwenendo wa maovu uliokithiri na usiositishwa wa binadamu wa kimwili. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, hata hivyo, nguvu zote za maovu zitasitishwa; dhambi zote za kudhuru binadamu zitasitishwa; nguvu zote katili zinazozuia kazi ya Mungu zitawekwa wazi, zitatenganishwa na kulaaniwa; washirika wote wa Shetani ambao wanampinga Mungu wataadhibiwa, na kuondolewa. Badala yake, kazi ya Mungu itaendelea huru bila vizuizi vyovyote; mpango wa usimamizi wa Mungu utaendelea kuimarika hatua kwa hatua kulingana na utaratibu uliopo; watu walioteuliwa na Mungu watakuwa huru dhidi ya kusumbuliwa na Shetani na kudanganywa; wale wanaomfuata Mungu watafurahia uongozi na ujazo wa Mungu miongoni mwa mazingira yenye utulivu na amani. Hasira ya Mungu ni usalama unaozuia nguvu zote za maovu dhidi ya kuzidishwa na kutapakaa kwa nguvu, na pia ni usalama unaolinda kuwepo na kuenea kwa mambo yote ya haki na mazuri na daima dawamu unayalinda mambo haya dhidi ya kukandamizwa na kuangamizwa.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp