Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 165

18/07/2020

Ningependa kuwazungumzia kuhusu kitu mlichofanya kilichonishangaza mwanzoni mwa mkusanyiko wetu leo. Wengine wenu pengine mlikuwa na hisia za shukrani hivi karibuni, ama kuhisi shukrani, na hivyo mlitaka kuonyesha kimwili kile mlichokuwa nacho akilini mwenu. Hili si la kushutumiwa, na si sahihi wala makosa. Lakini ningependa muelewe kitu. Ni nini hiki? Kwanza Ningetaka kuwauliza kuhusu mlichokifanya hivi sasa. Je, kulikuwa ni kusujudu ama kupiga magoti kuabudu? Kuna yeyote anayeweza kuniambia? (Tunaamini ilikuwa kusujudu.) Mnaamini kulikuwa kusujudu, kwa hivyo ni nini maana ya kusujudu? (Kuabudu.) Kwa hivyo ni nini kupiga magoti kuabudu basi? Sijashiriki hili na ninyi awali, lakini leo nahisi ni muhimu kushiriki mada hii na ninyi. Je, mnasujudu katika mikusanyiko yenu ya kawaida? (La.) Je, mnasujudu mnaposema sala zenu? (Ndiyo.) Je, mnasujudu kila wakati mnaposema sala zenu, hali zinaporuhusu? (Ndiyo.) Hivyo ni vizuri sana. Lakini ni nini Ningependa nyinyi muelewe leo? Ni aina mbili za watu ambao kupiga magoti kwao kunakubaliwa na Mungu. Hatuhitaji kutafuta maoni katika Biblia ama tabia za watu wa kiroho, na Nitawaambia kitu kweli hapa na sasa. Kwanza, kusujudu na kupiga magoti kuabudu si kitu sawa. Mbona Mungu anakubali kupiga magoti kwa wale wanaosujudu wenyewe? Ni kwa sababu Mungu humwita mtu Kwake na humwita mtu huyu kukubali agizo la Mungu, kwa hivyo anasujudu mwenyewe mbele ya Mungu. Huyu ni mtu wa aina ya kwanza. Aina ya pili ni kupiga magoti kuabudu kwa mtu anayemcha Mungu na kuepukana na maovu. Kuna watu hawa wa aina mbili tu. Kwa hivyo mko katika aina gani? Mnaweza kusema? Huu ni ukweli kabisa, ingawa unaweza kuumiza hisia zenu kidogo. Hakuna kitu cha kusema kuhusu kupiga magoti kwa watu wakati wa sala—hii ni sahihi na ndivyo inavyopaswa kuwa, kwa sababu wakati watu wanasali wakati mwingi ni kuombea kitu, kufungua mioyo yao kwa Mungu na kukutana Naye uso kwa uso. Ni mawasiliano na mazungumzo, moyo kwa moyo na Mungu. Mkiifanya kama urasmi tu, basi haipaswi kufanya hivyo. Simaanishi kuwashutumu kwa yale ambayo mmefanya leo. Mnajua kwamba nataka tu kuweka wazi kwenu ili muelewe kanuni hii, mnajua? (Tunajua.) Ili msiendelee kufanya hili. Je, watu basi wana fursa yoyote ya kusujudu na kupiga magoti mbele ya uso wa Mungu? Daima kutakuwa na fursa. Hatimaye siku itakuja lakini wakati sio sasa. Mnaona? (Ndiyo.) Je, hili linawafanya kuhisi vibaya? (La.) Hivyo ni vizuri. Labda maneno haya yatawatia moyo ama kuwashawishi ili muweze kujua katika mioyo yenu taabu ya sasa kati ya Mungu na mwanadamu na aina ya uhusiano uliopo sasa kati yao. Ingawa tumeongea na kuzungumza sana hivi karibuni, uelewa wa mwanadamu kuhusu Mungu bado uko mbali na kutosha. Mwanadamu bado ana umbali mrefu wa kwenda katika njia hii ya kutafuta kumwelewa Mungu. Si nia yangu kuwafanya mfanye hivi kwa dharura, ama kuwaharakisha kuonyesha matamanio na hisia za aina hizi. Yale mliyofanya leo yanaweza kufichua na kuonyesha hisia zenu za kweli, na Niliyafahamu. Kwa hivyo wakati mlipokuwa mkiyafanya, nilitaka tu kusimama na kuwatakia mema, kwa sababu Nataka nyote muwe wazima. Kwa hivyo katika maneno na vitendo vyangu vyote ninafanya yote ninayoweza kuwasaidia, kuwaongoza, ili muwe na uelewa sahihi na mtazamo sahihi wa mambo yote. Mnaweza kuelewa haya, sivyo? (Ndiyo.) Hivyo ni vizuri sana. Ingawa watu wana baadhi ya uelewa wa tabia mbalimbali za Mungu, kipengele cha kile anacho Mungu na alicho na kazi Mungu anafanya, wingi wa uelewa huu hauendi mbali na kusoma maneno kwenye ukurasa, ama kuyaelewa katika kanuni, ama tu kuyafikiria. Yale wanayoyakosa sana watu ni uelewa na mtazamo wa kweli unaotoka kwa uzoefu halisi. Ingawa Mungu hutumia njia mbalimbali kuamsha mioyo ya wanadamu, bado kuna njia ndefu ya kutembea kabla mioyo ya wanadamu iamshwe kikamilifu. Sitaki kumwona yeyote akihisi kana kwamba Mungu amemwacha nje kwa baridi, kwamba Mungu amemwacha ama amempuuza. Ningetaka tu kuona kila mtu katika njia ya kufuatilia ukweli na kutafuta kumwelewa Mungu, akiendelea mbele kwa ujasiri na utashi usiosita, bila wasiwasi, bila kubeba mizigo. Haijalishi umefanya makosa gani, haijalishi umepotoka aje ama vile ulivyotenda dhambi, usiwache haya yawe mizigo ama vikorokoro ziada kubeba katika ufuataji wako wa kumwelewa Mungu: Endelea kutembea mbele. Haijalishi itafanyika lini, moyo wa Mungu ambao ni wokovu wa mwanadamu haubadiliki: Hii ni sehemu ya thamani sana ya kiini cha Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp