Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 190

06/08/2020

Wale ambao hawana imani huamini kuwa kila kitu ambacho kinaweza kuonekana kipo, ilhali kila kitu kisichoonekana, au ambacho kiko mbali sana na watu, hakipo. Wanapenda kuamini kuwa hakuna “mzunguko wa uhai na mauti,” na hakuna “adhabu,” na kwa hiyo wanatenda dhambi na kufanya maovu bila majuto—ambayo baadaye wataadhibiwa kwayo, au watapata miili kama mnyama. Wengi wa watu mbalimbali miongoni mwa Wasioamini wanapatikana katika mzunguko huu. Ni kwa sababu hawajui kuwa ulimwengu wa kiroho ni mkali katika kuviendesha viumbe hai wote. Ikiwa unaamini au la, huu ukweli upo, na hakuna mtu hata mmoja au chombo chochote kinaweza kuepuka mawanda ya ambacho kinaonwa na macho ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja au chombo kinachoweza kuepuka sheria na mipaka ya sheria za peponi na amri za Mungu. Na hivyo basi mfano huu rahisi unamwambia kila mtu kwamba haijalishi kama unamwamini au humwamini Mungu, haikubaliwi kutenda dhambi na kufanya maovu, na kuna matokeo. Wakati mtu aliyemlaghai mwingine pesa anaadhibiwa hivyo, hiyo adhabu ni ya haki. Mienendo inayoonekana ya kawaida kama hii inaadhibiwa na ulimwengu wa kiroho, inaadhibiwa na amri na sheria za mbinguni za Mungu, na vivyo hivyo uhalifu mkubwa na matendo maovu—ubakaji na unyang’anyi, ulaghai na udanganyifu, wizi na ujambazi, mauaji na uchomaji, na kadhalika—yanapitia adhabu za aina zenye ukali wa viwango mbalimbali. Na hizi adhabu zenye ukali wa viwango mbalimbali zinajumuisha nini? Baadhi yake zinatumia muda kufikisha kiwango cha ukali, na nyingine hufikiwa kwa mbinu mbalimbali, na nyingi hufikiwa kupitia mahali mtu aendapo akipata mwili. Kwa mfano, watu wengine wana maneno machafu. Kuwa na “maneno machafu” kunamaanisha nini? Kunamaanisha kuwaapiza wengine mara kwa mara, na kutumia lugha chafu, lugha inayowalaani watu wengine. Lugha yenye nia mbaya inaashiria nini? Inaashiria kuwa mtu ana roho mbaya. Lugha yenye nia mbaya inayowalaani watu wengine mara nyingi inatoka vinywani mwa watu kama hao, na lugha yenye nia mbaya kama hiyo mara nyingi inaandamana na matokeo makali. Baada ya hawa watu kufa na kupokea adhabu stahili, wanaweza kuzaliwa kama mabubu. Watu wengine ni wajanja sana wakiwa hai, mara kwa mara wanawatumia watu wengine kwa manufaa yao, njama zao huwa zimepangwa barabara, na wanafanya mengi yanayowadhuru wengine. Wakizaliwa upya, wanaweza kuwa wazimu au punguani. Watu wengine mara nyingi huwachungulia watu wengine wakiwa faraghani; macho yao huona mengi ambayo hawakutakiwa kuona, na hujua mengi ambayo hawakupaswa kujua, hivyo basi wazaliwapo upya, wanaweza kuwa vipofu. Watu wengine ni hodari sana wakiwa hai, wanapigana mara kwa mara, na kufanya mengi ambayo ni maovu, na kwa hiyo wanapozaliwa upya, wanaweza kuwa vilema au wakakosa mkono, vinginevyo wanaweza kuwa vibyongo, au wenye shingo iliyopinda, huenda wakatembea wakichechemea, au wakawa na mguu mmoja mfupi kuliko mwingine, na kadhalika. Katika hali hii, wanapewa adhabu mbalimbali kutegemea kiwango cha maovu waliyotenda walipokuwa hai. Mwasemaje, kuhusu ni kwa nini watu huwa na makengeza? Je, kuna watu wengi wa hivyo? Kuna wengi wao siku hizi. Watu wengine wana makengeza kwa sababu waliyatumia macho yao sana katika maisha yao yaliyopita, walifanya mambo mengi mabaya, na kwa hiyo wazaliwapo katika haya maisha macho yao hupata makengeza, na katika hali mbaya, hata huwa vipofu. Haya ni malipo! Watu wengine wanaelewana vizuri na wengine kabla hawajafa, wanafanya mambo mengi mazuri kwa wapendwa wao, marafiki, wenza, au watu wanaohusiana nao. Wanatoa hisani na matunzo kwa wengine, au kuwasaidia kifedha, wengine wanawaheshimu sana, na watu kama hao warudipo katika ulimwengu wa kiroho hawaadhibiwi. Kwa asiyeamini kukosa kuadhibiwa kwa njia yoyote inamaanisha alikuwa mtu mzuri sana. Badala ya kuamini katika uwepo wa Mungu, wanaamini tu katika Mzee aliye Angani. Wanaamini tu kuwa kuna roho juu yao akitazama yote wafanyayo—hayo tu ndiyo wanaamini. Na matokeo ni yapi? Wanakuwa na mwenendo mzuri. Hawa watu ni wenye huruma na wakarimu, na mwishowe wakirudi katika ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa kiroho utawapokea vizuri sana na watapata mwili na kuzaliwa upya mapema. Na watafikia katika familia za aina gani? Japo familia yake haitakuwa ya kitajiri, itakuwa tulivu, kutakuwa na maelewano miongoni mwa wanafamilia, watakuwa na siku mwanana, za kupendeza, kila mmoja atafurahia, na watakuwa na maisha mazuri. Naye atakapokuwa mtu mzima, atapata wana na mabinti wengi, na kuwa na familia kubwa na jamaa wengi, watoto wake watakuwa na vipawa na kufanikiwa, yeye pamoja na familia yake watakuwa na bahati nzuri—na matokeo kama hayo yanahusiana kwa kiasi kikubwa na maisha ya zamani ya mtu. Yaani, mahali mtu huenda baada ya kufa na kupata mwili, wawe wanaume au wanawake, wito wao ni upi, watapitia nini maishani, vikwazo vyao, watapata baraka gani, watakutana na nani, ni nini kitawatokea—hakuna awezaye kulitabiri hili, kuliepuka, au kujificha kutokana nalo. Yaani, baada ya maisha yako kupangwa, kitakachokutokea, hata ujaribu namna gani kukikwepa, hata ukitumia mbinu gani kukiepuka, huna njia ya kuvuruga mkondo wa maisha uliopangiwa na Mungu katika ulimwengu wa kiroho. Kwani upatapo mwili, majaaliwa yako tayari huwa yameishapangwa, ikiwa yatakuwa mazuri au mabaya, kila mtu anapaswa kuyakubali yalivyo, na anapaswa kusonga mbele; hili ni jambo ambalo hakuna mtu aishiye katika maisha haya anaweza kuliepuka, na huu ndio uhalisia.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp