Dance of Praise | Tunamsifu Mungu Kwa Mioyo Yetu Yote (Swahili Subtitles)

29/08/2020

Ni bahati yetu nzuri zaidi kusikia sauti ya Mungu

na kurudi mbele Yake.

Tunapokula na kunywa maneno Yake kila siku,

tunazidi kuhisi wachangamfu.

Zamani tulipokuwa waraibu wa mtandao, tulizidi kupotoka na kukengeuka.

Lakini sasa tuna maneno ya Mungu ya kutuongoza

na tunatembea kwenye njia ng’avu ya maisha.

Maneno ya Mungu yanatunyunyizia na kutustawisha

yakitufanya tuelewe ukweli

na kukua kwa furaha katika nyumba ya Mungu.

Kwa kuwa hatufuati tena mitindo ya ulimwengu,

tunaishi mbele za Mungu na tunafurahia maisha yenye baraka.

Kwa sauti zivumazo, tuimbe tukimsifu Mungu pamoja,

kwa kuwa Ananena ili kutuletea wokovu.

Tucheze pamoja tukimsifu Mungu, hadi mioyo yetu iridhike,

kwa maana tunajifunza kutokana na maneno Yake jinsi ya kuwa mwanadamu halisi.

Kwa sauti zivumazo, tuimbe tukimsifu Mungu pamoja,

na tuonyeshe upendo wetu wa dhati Kwake.

Tucheze pamoja tukimsifu Mungu, hadi mioyo yetu iridhike,

tukimshukuru na kumsifu Mwenyezi Mungu milele.

Tunakusanyika makanisani,

tukisikiliza matamshi ya Mungu na kujaribu kuwa watu waaminifu.

Tunapokula na kunywa maneno Yake na kushiriki juu ya ukweli,

tunaelewa ukweli na tunahisi wachangamfu sana.

Tunaposoma maneno ya Mungu na kuja kujijua,

hatusemi uongo wala kudanganya tena.

Kwa kuyatenda na kuyapitia maneno ya Mungu,

sisi si wakaidi wala wenye kiburi tena.

Tunasaidiana na kuungana mikono na hatutengani au kubaguana tena.

Ni upendo wa Mungu ambao umetuunganisha pamoja kwa karibu sana.

Tunapofunguliana mioyo yetu katika ushirika

na kuacha ulaghai na udanganyifu,

tunaishi mbele za Mungu tukiwa na mioyo ya uaminifu.

Kwa sauti zivumazo, tuimbe tukimsifu Mungu pamoja,

kwa kuwa Ananena ili kutuletea wokovu.

Tucheze pamoja tukimsifu Mungu, hadi mioyo yetu iridhike,

kwa maana tunajifunza kutokana na maneno Yake jinsi ya kuwa mwanadamu halisi.

Kwa sauti zivumazo, tuimbe tukimsifu Mungu pamoja,

na tuonyeshe upendo wetu wa dhati Kwake.

Tucheze pamoja tukimsifu Mungu, hadi mioyo yetu iridhike,

tukimshukuru na kumsifu Mwenyezi Mungu milele.

Hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu

hutulinda dhidi ya majaribu ya Shetani.

Tunapotimiza wajibu wetu katika nyumba ya Mungu,

tunafanya wajibu wetu ili kulipa upendo Wake.

Kwa sauti zivumazo, tuimbe tukimsifu Mungu pamoja,

kwa kuwa Ananena ili kutuletea wokovu.

Tucheze pamoja tukimsifu Mungu, hadi mioyo yetu iridhike,

kwa maana tunajifunza kutokana na maneno Yake jinsi ya kuwa mwanadamu halisi.

Kwa sauti zivumazo, tuimbe tukimsifu Mungu pamoja,

na tuonyeshe upendo wetu wa dhati Kwake.

Tucheze pamoja tukimsifu Mungu, hadi mioyo yetu iridhike,

tukimshukuru na kumsifu Mwenyezi Mungu milele.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp