Tenzi ya Rohoni | Upendo Safi Bila Dosari

28/06/2019

I

Upendo ni hisia safi, safi bila dosari.

Tumia moyo, tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza.

Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga.

Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza.

Ukipenda hudanganyi, hulalamiki, hugeuki,

hutazamii kupata kitu, cha malipo.

Ukipenda utajitolea, ukubali taabu, kuwa kimoja, Mungu katika mapatano.

II

Upendo hauna shauku, ujanja wala uongo.

Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza.

Upendo haujitengi, upendo hauna dosari.

Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza.

Ukipenda hudanganyi, hulalamiki, hugeuki,

hutazamii kupata kitu cha malipo.

Ukipenda utajitolea, ukubali taabu, kuwa kimoja, Mungu katika mapatano.

III

Utatoa familia, ujana wako na siku za usoni.

Utoe ndoa yako kwa Mungu, toa vyote kwake.

Utatoa familia, ujana na siku za usoni.

Utoe ndoa yako kwa Mungu, toa vyote kwake.

Ama upendo wako si upendo kabisa, bali uongo, usaliti kwa Mungu.

IV

Upendo ni hisia safi, safi bila dosari.

Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza.

Upendo hauna masharti, vizuizi au kujitenga.

Tumia moyo, Tumia moyo, kupenda, kuhisi, kutunza.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp