Wimbo wa Injili | Jinsi ya Kutafuta Nyayo za Mungu (Music Video)

26/05/2020

Mkitafuta nyayo za Mungu, mlipuuza maneno kuwa,

“Mungu ni ukweli, njia, na uzima.”

Hivyo watu wengi wapokeapo ukweli,

hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu

na hata kukosa kutambua kuonekana kwa Mungu.

Ni kosa kubwa sana!

Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulingana na dhana za mwanadamu,

sembuse Mungu kuonekana kwa ombi la mwanadamu.

Anapofanya kazi Yake, Anafanya chaguo Lake, anayo mipango Yake.

Zaidi ya hayo, ana malengo Yake mwenyewe.

Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu,

lazima tutafute mapenzi ya Mungu, tutafute maneno ya Mungu.

Kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, pana sauti ya Mungu;

palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu.

Palipo na maonyesho ya Mungu, pana sura, sura ya Mungu,

na palipo na sura ya Mungu, pana ukweli, njia, na uzima.

Anapofanya kazi Yake, hahitaji kujadili kazi Yake na mtu,

sembuse kumuarifu kila mtu.

Hii ni tabia ya Mungu, inafaa kujulikana na wote.

Ukiwa na hamu kushuhudia kuonekana kwa Mungu,

ukiwa tayari kutafuta nyayo za Mungu,

basi kwanza lazima uvuke dhana zako mwenyewe.

Usifanye masharti kwa kile Mungu anapaswa kufanya

wala kumwekea mipaka na dhana zako.

Badala yake, wafaa kuuliza jinsi ya kutafuta nyayo za Mungu,

kukubali kuonekana kwa Mungu,

na jinsi unavyopaswa kutii kazi mpya ya Mungu.

Kwa kuwa hakuna, mwingine aliye ukweli,

na hakuna aliye na, aliye na ukweli,

mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii.

Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu,

lazima tutafute mapenzi ya Mungu, tutafute maneno ya Mungu.

Kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, pana sauti ya Mungu;

palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu.

Palipo na maonyesho ya Mungu, pana sura, sura ya Mungu,

na palipo na sura ya Mungu, pana ukweli, njia, na uzima.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp