Wimbo wa Kusifu | Hatuwezi Kuacha Kuimba Nyimbo za Upendo kwa Mungu (Music Video)

05/01/2020

Hatuwezi kuacha kuimba nyimbo za upendo kwa Mungu.

Tunapoimba zaidi, ndivyo hisia inakuwa nzuri zaidi.

Tunavyomwimbia Mungu zaidi, ndivyo tumpendavyo zaidi!

Tunaimba juu ya kupata mwili kwa Mungu.

Tunainuliwa mbele ya kiti Chake,

na hatutazami mbinguni tena, tukitamani.

Mwenyezi Mungu yuko uso kwa uso nasi.

Atuchunga kwa ukweli, kando yetu, wa kweli na halisi.

Tunafurahia maneno Yake kila siku.

Kuelewa ukweli kuna utamu sana.

Moyo wetu umejaa upendo kwa Mungu,

kwa kuwa tunauona uso Wake wa kupendeza.

Tunaimba na kucheza kwa sifa,

hakuna maneno ya kuelezea kupendeza Kwake.

Hatuwezi kuacha kuimba nyimbo za upendo kwa Mungu.

Tunapoimba zaidi, ndivyo hisia inakuwa nzuri zaidi.

Tunavyomwimbia Mungu zaidi, ndivyo tumpendavyo zaidi!

Twaimba juu ya hukumu ya haki ya Mungu.

Maneno Yake yatutakasa na kutuokoa,

yakifichua asili ya kishetani ya mwanadamu na ukweli wa upotovu wa mwanadamu.

Maneno Yake hutakasa tabia zetu za kishetani,

yakitufanya tuwe watu wapya.

Tumetupa nguvu za Shetani. Tunaona upendo wa Mungu ni wa kweli.

Haki Yake ni ya kupendeza, utakatifu Wake ni mtamu sana.

Hatuwezi kumpenda vya kutosha.

Hivyo tunamsifu Mungu; hatuwezi kuzuia hisia zetu.

Hakuna kinachoweza kuja kati yetu na Mungu.

Hatuwezi kuacha kuimba nyimbo za upendo kwa Mungu.

Tunapoimba zaidi, ndivyo hisia inakuwa nzuri zaidi.

Tunavyomwimbia Mungu zaidi, ndivyo tumpendavyo zaidi!

Neno la Mungu latawala katika maisha ya ufalme.

Tunaishi katika nuru.

Kupata ukweli kumetuweka huru.

Tunamwabudu Mungu kwa moyo, kwa uaminifu.

Tumekuwa wandani Wake, tukimtumikia kwa uaminifu.

Tunambebea mzigo, tukitimiza wajibu wetu kweli,

daima tukiendelea kwenye njia ya kumpenda Mungu.

Sasa tunaweza kumpenda na kumtii Mungu,

kuishi kwa ajili Yake, hii ndiyo furaha kubwa zaidi.

Mwenyezi Mungu, tunakusifu!

Tunakuabudu milele!

Hatuwezi kuacha kuimba nyimbo za upendo kwa Mungu.

Tunapoimba zaidi, ndivyo hisia inakuwa nzuri zaidi.

Tunavyomwimbia Mungu zaidi, ndivyo tumpendavyo zaidi!

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp