Mtu anawezaje kujua asili ya utukufu wa Kristo?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Yesu akanena kwake, Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu. Kama ninyi mngelinijua, pia mngelimjua Baba yangu: na kuanzia sasa mnamjua, na mmemwona.” (Yohana 14:6-7).
“Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo. Niamini kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi, la sivyo niamini kwa ajili ya kazi hizo” (Yohana 14:10-11).
Maneno Husika ya Mungu:
Kuchunguza kitu cha aina hii sio vigumu, lakini kunahitaji kila mmoja wetu ajue ukweli huu: Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje. Mwanadamu akiona tu sura Yake ya nje, na aipuuze dutu Yake, basi hilo linaonyesha upumbavu na ujinga wa mwanadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji
Kumjua Mungu kunapaswa kufanywa kupitia kwa kusoma na kulielewa neno la Mungu. Wengine husema: “Sijamwona Mungu mwenye mwili, hivyo ningewezaje kumjua Mungu?” Kwa kweli, neno la Mungu ni maonyesho ya tabia ya Mungu. Kutoka kwa neno la Mungu unaweza kuuona upendo na wokovu wa Mungu kwa wanadamu, na mbinu Yake ya kuwaokoa…. Hii ni kwa sababu neno la Mungu linaonyeshwa na Mungu Mwenyewe ikilinganishwa na kumtumia mwanadamu kuliandika. Linaonyeshwa na Mungu binafsi. Anaeleza maneno Yake mwenyewe na sauti Yake ya ndani. Kwa nini inasemekana kwamba ni maneno ya dhati? Kwa sababu hayo hutolewa kutoka ndani kabisa, Akionyesha tabia Yake, mapenzi Yake, mawazo Yake, upendo Wake kwa wanadamu, wokovu Wake wa wanadamu, na matarajio Yake ya wanadamu…. Miongoni mwa maneno ya Mungu kuna maneno makali, maneno ya upole na yenye kuzingatia, na kuna maneno mengine ya ufunuo ambayo hayalingani na matakwa ya binadamu. Ikiwa unayaangalia tu maneno ya ufunuo, utahisi kwamba Mungu ni mkali kabisa. Ikiwa unaangalia maneno ya upole tu, utahisi kuwa Mungu hana mamlaka mengi. Kwa hiyo hupaswi kuelewa hili nje ya muktadha, lakini uliangalie kutoka kila pembe. Wakati mwingine Mungu huzungumza kwa mtazamo mpole na wenye huruma, na watu wanauona upendo wa Mungu kwa wanadamu; wakati mwingine Yeye huzungumza kwa mtazamo mkali, na watu wanaona tabia ya Mungu ambayo haitavumilia kosa lolote. Mwanadamu ni mchafu kwa njia ya kusikitisha na hastahili kuuona uso wa Mungu au kuja mbele za Mungu. Kuwa watu wanaweza sasa kuja mbele za Mungu ni neema ya Mungu tu. Hekima ya Mungu inaweza kuonekana kutokana na jinsi Yeye anavyofanya kazi na maana ya kazi Yake. Watu bado wanaweza kuona mambo haya katika neno la Mungu hata bila kuwasiliana na Yeye moja kwa moja. Mtu ambaye ana ufahamu wa kweli wa Mungu anapowasiliana na Kristo, ataweza kulinganisha hili na ufahamu wake uliopo wa Mungu, lakini wakati mtu ambaye ana ufahamu wa kinadharia tu anakutana na Mungu, hawezi kuona uhusiano. Kipengele hiki cha ukweli ni siri kubwa zaidi; ni ngumu kuelewa. Yafupishe maneno ya Mungu ya siri ya kupata mwili, yaangalie kutoka pande zote, kisha Sali pamoja, tafakari, na kushiriki kuhusu kipengele hiki cha ukweli zaidi. Labda Roho Mtakatifu atakupa nuru na kukupa ufahamu. Kwa kuwa mwanadamu hana nafasi ya kuwasiliana na Mungu, lazima ategemee uzoefu wa aina hii kupata njia yake na kuingia kidogo kidogo, ili kufikia ufahamu wa kweli wa Mungu.
Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Mwenye Mwili” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Mchakato ambamo watu huyapitia maneno ya Mungu ni sawa na mchakato ambamo wanafahamu kujitokeza kwa maneno ya Mungu katika mwili. Kadiri watu wanavyoyapitia maneno ya Mungu, ndivyo wanavyomjua Roho wa Mungu; kwa kuyapitia maneno ya Mungu, watu wanaelewa kanuni za kazi ya Roho na kupata kumjua Mungu wa vitendo Mwenyewe. Kwa hakika, Mungu akiwafanya watu wakamilifu na kuwachukua, Anawafanya wayajue matendo ya Mungu wa vitendo; Anatumia kazi ya Mungu wa vitendo kuwaonyesha watu umuhimu halisi wa kupata mwili, na kuwaonyesha kuwa Roho wa Mungu hakika ameonekana kwa mwanadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe
Ingawa kuonekana kwa Mungu mwenye mwili ni kama mwanadamu, Anajifunza maarifa ya mwanadamu na kuongea lugha ya mwanadamu, na wakati mwingine Anaonyesha hata mawazo Yake kwa jinsi na hisia za mwanadamu, namna Anavyowaona wanadamu, kiini cha vitu, na namna ambavyo watu waliopotoka wanavyomwona mwanadamu na kiini cha vitu kwa hakika si sawa kabisa. Mtazamo Wake na kimo Anachosimamia ni jambo ambalo halifikiwi na mtu aliyepotoka. Hii ni kwa sababu Mungu ni ukweli, mwili Anaouvalia unamiliki pia kiini cha Mungu, na fikira Zake na kile ambacho kinadhihirishwa na ubinadamu Wake pia ni ukweli. Kwa watu waliopotoka, kile Anachoeleza katika mwili ni matoleo ya ukweli na maisha. Matoleo haya si ya mtu mmoja tu lakini kwa wanadamu wote. Kwa mtu yeyote aliyepotoka, katika moyo wake kunao tu wale watu wachache ambao wanahusiana na yeye. Kunao tu hao watu kadhaa ambao anawatunza ambao anajali kuwahusu. Wakati janga linakaribia, anafikiria kwanza kuhusu watoto wake binafsi, mume au mke au wazazi, na mtu mwenye moyo wa kujitoa zaidi kuhusu mwanadamu angefikiria zaidi kuhusu baadhi ya watu wa ukoo au rafiki mzuri; je yeye huwafikiria wengine? La hasha! Kwa sababu binadamu ni, kwa hakika, binadamu, na wanaweza tu kuangalia kila kitu kutoka kwa mtazamo na kutoka katika kimo cha mtu. Hata hivyo, Mungu mwenye mwili ni tofauti kabisa na mtu aliyepotoka. Bila kujali ni vipi ambavyo mwili wa Mungu mwenye mwili ulivyo wa kawaida, ulivyo kama wengine, ulivyo wa chini, au hata namna ambavyo watu wanamdharau Yeye, fikira Zake na mwelekeo Wake kwa wanadamu ni mambo ambayo hakuna binadamu angeweza kufuatisha na wala hakuna binadamu angeweza kuiga. Siku zote Atawaangalia wanadamu kutoka kwa mtazamo wa uungu, kutoka katika kimo cha madaraka Yake kama Muumba. Siku zote Atawaona wanadamu kupitia katika kiini na akili ya Mungu. Hawezi kabisa kuwaona wanadamu kutoka katika kimo cha mtu wa kawaida na kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyepotoka. Watu wanapowaangalia wanadamu, wanawaangalia kwa mtazamo wa binadamu, na wanatumia mambo kama vile maarifa ya binadamu na masharti na nadharia za binadamu kama kipimo. Hali hii imo ndani ya mawanda ya kile ambacho watu wanaweza kuona kwa macho yao; ni ndani ya upana ambao watu waliopotoka wanaweza kutimiza. Mungu anapowatazama wanadamu, Anawatazama kwa macho ya kiungu, na Anatumia kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho kama kipimo. Mawanda haya yanajumuisha mambo ambayo watu hawawezi kuona, na hapo ndipo Mungu mwenye mwili na wanadamu waliopotoka walivyo tofauti kabisa. Tofauti hii inaamuliwa na viini tofauti vya wanadamu na vya Mungu na ndivyo vinavyoamua utambulisho na nafasi zao pamoja na mtazamo na kimo ambacho wanaona mambo.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III
Hamtamwona Mungu akiwa na mitazamo sawa kuhusu vitu ambavyo watu wanavyo, na zaidi hamtamwona Akitumia maoni ya wanadamu, maarifa yao, sayansi yao ama filosofia yao ama fikira za mwanadamu kushughulikia vitu, Badala yake, kila kitu anachofanya Mungu na kila kitu Anachofichua kinahusiana na ukweli. Yaani, kila neno ambalo amesema na kila kitendo amefanya kinahusiana na ukweli. Ukweli huu sio tu ndoto isiyo na msingi; ukweli huu na maneno haya yanaelezwa na Mungu kwa sababu ya kiini cha Mungu na uhai Wake. Kwa sababu maneno haya na kiini cha kila kitu Mungu amefanya ni ukweli, tunaweza kusema kwamba kiini cha Mungu ni kitakatifu. Kwa maneno mengine, kila kitu ambacho Mungu anasema na kufanya kinaleta uzima na mwangaza kwa watu, kinawaruhusu watu kuona vitu vizuri na uhalisi wa vitu hivyo vizuri, na kinaashiria wanadamu njia ili watembelee njia njema. Vitu hivi vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha Mungu na vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha utakatifu Wake.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V
Si kila kitu ambacho kinafunuliwa kiko katika maneno ya sasa ya Mungu kuhusu tabia potovu ya wanadamu? Tabia ya Mungu yenye haki na utakatifu vinaonyesha kupitia mawazo yako na nia zako, na kupitia kwa yale unayoyafunua. Yeye, pia Akiishi katika nchi ya uchafu, hajatiwa waa na uchafu hata kidogo. Anaishi katika dunia ile ile chafu kama wewe, lakini Anamiliki mantiki na umaizi; Anachukia uchafu. Wewe mwenyewe huwezi kuona mambo machafu katika maneno na matendo yako mwenyewe lakini Yeye Anaweza—Anaweza kukuonyesha. Mambo hayo yako ya zamani—ukosefu wako wa kukuza, umaizi, na hisia, maisha yako ya kuelekea nyuma—yote yamefunuliwa kupitia kwa kufichua Kwake kwa mambo hayo sasa. Mungu Amekuja duniani kufanya kazi kwa namna hii, ili watu wauone utakatifu Wake na tabia Yake ya haki. Anakuhukumu na Kukuadibu na Kukufanya ujielewe. Wakati mwingine asili yako yenye pepo mbaya huonekana na Anaweza kukuonyesha. Anakijua kiini cha wanadamu sana. Anaishi kama wewe unavyoishi, Anakula chakula sawa na wewe, Anaishi katika aina ya nyumba kama wewe, ilhali Anajua mengi zaidi kukuliko. Lakini kile Anachochukia hasa ni maisha ya filosofia ya watu na udanganyifu na upotovu wao. Anavichukia vitu hivi na Yeye hana nia ya kuvitilia maanani. Yeye hasa anachukia maathiriano ya kimwili ya watu. Ingawa Haelewi kabisa baadhi ya maarifa ya jumla ya maathiriano wa binadamu, Anafahamu kikamilifu wakati ambapo watu wanafichua baadhi ya tabia zao potovu. Katika kazi Yake, Ananena na kuwafundisha watu kupitia mambo haya ndani yao, na kupitia haya Yeye huwahukumu watu na kufichua tabia yake yenye haki na takatifu. Hivi ndivyo watu wanakuwa foili kwa ajili ya kazi Yake. Ni Mungu mwenye mwili tu ambaye Anaweza kufichua kila aina ya tabia potovu za mwanadamu na nyuso zote mbaya za Shetani. Yeye hakuadhibu, Angeweza tu kukufanya wewe uwe foili kwa utakatifu wa Mungu na kisha huwezi kusimama imara mwenyewe kwa sababu wewe ni mchafu sana. Anaongea kupitia mambo yale ambayo watu wanadhihirisha na Yeye huyafunua ili watu waweze wajue jinsi Mungu ni mtakatifu. Hataacha uchafu hata kidogo ndani ya binadamu, sio hata wazo dogo zaidi chafu katika mioyo yao au maneno na matendo ambayo si sambamba na mapenzi Yake. Kupitia kwa maneno Yake, hakuna uchafu na hakuna kitu ndani ya mtu kitabaki—vyote vitawekwa wazi. Ni hapo tu ndipo utakapoona ya kwamba Yeye kweli yuko tofauti na watu. Anachukizwa kabisa na uchafu hata kidogo zaidi katika wanadamu. Wakati mwingine watu hata hawaelewi, na wanasema: “Mungu, kwa nini Wewe una hasira kila mara? Kwa nini Huujali udhaifu wa wanadamu? Kwa nini Huna msamaha kidogo kwa wanadamu? Kwa nini Hujali hisia za mwanadamu? Unajua jinsi watu walivyo wapotovu, hivyo kwa nini bado Unawatendea watu kwa njia hii?” Anachukizwa na dhambi; Anachukia dhambi. Yeye anachukizwa hasa na uasi wowote unaoweza kuwa ndani yako. Wakati ambapo unafichua tabia ya uasi Anachukizwa kupita kadiri. Ni kwa kupitia mambo haya ambapo tabia Yake na asili vinaweza kuonyeshwa. Unapoilinganisha na wewe mwenyewe, utaona kwamba ingawa Anakula chakula sawa, Anavaa mavazi sawa, na Ana starehe sawa na watu, ingawa Anaishi kandokando na pamoja na watu, Yeye si sawa. Je, hii si maana halisi ya kuwa foili? Ni kupitia mambo haya kwa watu ndiyo maana nguvu kuu ya Mungu inaonekana kwa urahisi sana; ni giza ambalo huchochea kuwepo kwa mwanga wa thamani.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi Athari za Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Zinavyotimizwa
Anatambua vizuri asili ya mwanadamu, Anaweza kufunua aina za matendo yote yanayohusiana na kila aina ya watu. Ni mzuri hata katika kufunua tabia ya dhambi ya mwanadamu na tabia yake ya uasi. Haishi miongoni mwa watu wa kidunia, lakini Anatambua asili ya watu wenye mwili wa kufa na upotovu wote wa watu wa duniani. Hicho ndicho Alicho. Ingawa Hashughuliki na dunia, Anajua kanuni za kushughulika na dunia, kwa sababu Anaielewa vizuri asili ya mwanadamu. Anajua kuhusu kazi ya Roho ambayo jicho la mwanadamu haliwezi kuiona na kwamba masikio ya mwanadamu hayawezi kusikia, wanadamu wa leo na wanadamu wa enzi zote. Hii inajumuisha hekima ambayo sio falsafa ya maisha na makuu ambayo watu hupata ugumu kuelewa. Hiki ndicho Alicho, kuwekwa wazi kwa watu na pia kufichika kwa watu. Kile Anachoonyesha sio kile ambacho mwanadamu asiye wa kawaida alicho, bali ni tabia za asili na uungu wa Roho. Hasafiri ulimwenguni mzima lakini anajua kila kitu kuhusu ulimwengu. Anawasiliana na “sokwe” ambao hawana maarifa au akili, lakini Anaonyesha maneno ambayo ni ya kiwango cha juu kuliko maarifa na juu ya watu wakubwa duniani. Anaishi miongoni mwa kundi la wanadamu wapumbavu na wasiojali ambao hawana ubinadamu na ambao hawaelewi mila na desturi za ubinadamu na maisha, lakini Anaweza kumwambia mwanadamu kuishi maisha ya kawaida, na kwa wakati uo huo kufichua ubinadamu duni na wa chini wa binadamu. Haya yote ndiyo kile Alicho, mkuu kuliko vile ambacho mwanadamu yeyote wa damu na nyama alicho. Kwake Yeye, si lazima kupitia maisha ya kijamii magumu na changamani, ili Aweze kufanya kazi Anayotaka kufanya na kwa kina kufichua asili ya mwanadamu aliyepotoka. Maisha duni ya kijamii ambayo hayauadilishi mwili Wake. Kazi Yake na maneno Yake hufichua tu kutotii kwa mwanadamu na hayampi mwanadamu uzoefu na masomo kwa ajili ya kushughulika na ulimwengu. Hahitaji kuipeleleza jamii au familia ya mwanadamu wakati Anapompa mwanadamu uzima. Kumweka wazi na kumhukumu wanadamu sio maonyesho wa uzoefu wa mwili Wake; ni kufichua vile mwanadamu asivyokuwa na haki baada ya kufahamu kutotii kwa mwanadamu na kuchukia upotovu wa mwanadamu. Kazi yote Anayoifanya ni kufichua tabia Yake kwa mwanadamu na kuonyesha asili Yake. Ni Yeye tu ndiye anayeweza kuifanya kazi hii, sio kitu ambacho mtu mwenye mwili na damu anaweza kukipata. Kwa kuangalia kazi Yake, mwanadamu hawezi kuelezea Yeye ni mtu wa aina gani. Mwanadamu hawezi kumwainisha kama mtu aliyeumbwa kwa misingi ya kazi Yake. Kile Alicho pia kinamfanya Asiweze kuainishwa kama mtu aliyeumbwa. Mwanadamu anaweza kumwona tu kama Asiye mwanadamu, lakini hajui amwainishe katika kundi gani, kwa hivyo mwanadamu analazimika kumwainisha katika kundi la Mungu. Si busara kwa mwanadamu kufanya hivi, kwa sababu Amefanya kazi kubwa miongoni mwa watu, ambayo mwanadamu hawezi kufanya.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu
Mungu Mwenyewe hana mambo ya kuasi; dutu Yake ni nzuri. Yeye ni udhihirisho wa uzuri wote na wema, vile vile upendo wote. Hata katika mwili, Mungu hafanyi lolote linalomuasi Mungu Baba. Hata kwa gharama ya kutoa sadaka maisha Yake, Angekuwa kwa ukamilifu tayari na kutofanya uchaguzi mwingine. Mungu hana mambo ya ukamilifu wa kibinafsi na umuhimu wa kibinafsi, au yale wa kujiona na kiburi; Hana mambo yasiyo aminifu. Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na ile ya Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelaghaiwa na kufinyangwa Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani. Haijalishi ugumu wa kazi, au udhaifu wa mwili, Mungu, wakati Anapoishi katika mwili, kamwe hatafanya kitu chochote kitakachopinga kazi ya Mungu Mwenyewe, wala kuacha mapenzi ya Mungu Baba kwa njia ya uasi. Ni afadhali Ateseke maumivu ya mwili kuliko kwenda kinyume na matakwa ya Mungu Baba; ni kama vile Yesu Alisema katika sala, “Baba, kama inawezekana, kikombe hiki kiniondokee: hata hivyo si kama Mimi Nipendavyo, bali kama Wewe upendavyo.” Wanadamu watachagua, bali Kristo hawezi. Ingawa Anao utambulisho wa Mungu Mwenyewe, bado Yeye Anatafuta mapenzi ya Mungu Baba, na Anatimiza kile Alichokabidhiwa na Mungu Baba, kutoka kwa mtazamo wa mwili. Hili ni jambo ambalo haliwezi kupatikana kwa binadamu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni
Pasipo sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua moja baada ya nyingine ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, kuvumilia kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunapata kujua kuhusu tabia ya Mungu ya haki na uadhama, kufurahia, pia, upendo na huruma Zake, tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake, tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua tabia na kiini cha Mungu, kufahamu mapenzi ya Mungu, kujua asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya wokovu na ukamilifu. Maneno Yake hutufanya sisi “tufe,” na tena hutufanya “kuzaliwa upya”; maneno Yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno Yake hutuletea furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa sana. Wakati mwingine sisi ni kama wanakondoo wa kuchinjwa mikononi Mwake; wakati mwingine sisi ni kama kipenzi cha roho Yake na kufurahia upendo Wake wenye upole; wakati mwingine sisi ni kama adui Yake, na chini ya macho Yake tunageuzwa majivu na ghadhabu Yake. Sisi ni jamii ya wanadamu waliookolewa Naye, sisi ni funza machoni Pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao, usiku na mchana, Yeye hunuia kuwapata. Yeye ni mwenye huruma kwetu, hutudharau, Yeye hutuinua, Yeye hutufariji na kutuhimiza, Yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Usiku na mchana, Yeye hakomi kamwe kuwa na wasiwasi nasi na hutulinda na kututunza usiku na mchana, Asiwache upande wetu kamwe, bali humwaga damu ya moyo Wake kwa ajili yetu na hulipia gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa matamshi ya mwili huu mdogo na wa kawaida wa nyama, tumefurahia ukamilifu wa Mungu na kuona hatima ambayo Mungu ametupa. Licha ya haya, majivuno bado yanazua rabsha mioyoni mwetu, na sisi bado hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu. Ingawa Yeye ametupa mana nyingi sana, nyingi sana ya kufurahia, hamna kati ya haya ambalo linaweza kuchukua nafasi ya Bwana katika mioyo yetu. Tunaheshimu utambulisho maalum na hadhi ya huyu mwanadamu kwa kusita sana. Bora hafungui mdomo Wake kututaka tukiri kwamba Yeye ni Mungu, sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni Mungu ambaye yuko karibu kuja na ilhali amekuwa akifanya kazi kati yetu kwa muda mrefu sana.
Mungu huendelea na matamshi Yake, akitumia mbinu mbalimbali na mitazamo kutuonya kuhusu kile tunachofaa kufanya na wakati uo huo akipea moyo Wake sauti. Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, hutuonyesha njia tunayopasa kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi Anavyoongea, na bila hiari tunaanza kuvutiwa na hisia za ndani kabisa za mwanadamu huyu asiye wa ajabu. Yeye hutema damu ya moyo Wake kwa niaba yetu, hupoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa akigumia kwa ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na uasi wetu na kufa ganzi kwetu kunatoa machozi na damu kutoka kwa moyo Wake. Njia hii ya kuwa na kumiliki si ya mtu wa kawaida, wala haiwezi kumilikiwa au kufikiwa na mtu yeyote aliyepotoka. Anaonyesha uvumilivu na subira isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake si kitu ambacho kiumbe chochote kimepewa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana na utumwa wa Shetani na tabia yetu potovu. Yeye humwakilisha Mungu. Yeye huonyesha moyo wa ndani zaidi wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya Mungu kwa wanadamu wote. Ameanzisha enzi mpya, nyakati mpya, na kuleta mbingu na nchi mpya na kazi mpya, na ametuletea matumaini, akimaliza maisha ambayo tuliishi katika hali isiyo dhahiri, na kuwezesha nafsi yetu nzima kuona njia ya wokovu kwa udhahiri kamili. Ameshinda ubinadamu wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili zetu zimepata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na ambaye amekataliwa na sisi zamani—Je, huyu si ni Bwana Yesu, ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, tukiwa tumeamka au kuota, na ambaye tunamtamani usiku na mchana? Ni Yeye! Ni Yeye kweli! Yeye ni Mungu wetu! Yeye ndiye ukweli, njia, na uzima! Yeye ametuwezesha kuishi tena na kuona nuru, na amekomesha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu, tumerejea mbele ya kiti Chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na Yeye, tumeshuhudia uso Wake, na tumeona njia iliyo mbele. Wakati huu, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye ni nani tena, hatupingi tena kazi Yake na neno Lake, na tunasujudu, mbele Yake. Hakuna tunachotaka zaidi yakufuata nyayo za Mungu maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila Yake, na kulipa upendo Wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio Yake, na kushirikiana na kazi Yake, na kufanya kila kitu tunachoweza ili kukamilisha kile Anachotuaminia.
Kushindwa na Mungu ni kama mashindano ya kareti.
Kila neno la Mungu hugonga eneo letu moja la kufisha, likituwacha na uchungu na kujawa na hofu Yeye hufichua dhana zetu, mawazo yetu, na tabia zetu potovu. Kutoka kwa yale yote sisi husema na kutenda, hadi kwa kila wazo na fikra zetu, asili na kiini chetu kinafichuliwa katika maneno Yake, yakituweka katika hali ya hofu na kutetemeka na bila mahali pa kuficha aibu yetu. Mmoja baada ya mwingine, Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua sisi wenyewe, na kutufanya tuhisi kwamba tumewekwa wazi katika dosari zetu mbaya na hata zaidi kushindwa kikamilifu. Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba, machoni Pake, hatuna sifa hata moja inayoweza kutuokoa, kwamba sisi ndio Shetani anayeishi. Matumaini yetu yanavunjika, na hatuthubutu tena kumpa madai yoyote yasiyo na busara au kuendeleza matumaini yoyote ya Yeye, na hata ndoto zetu hupotelea mara moja. Huu ni ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na ambao hakuna yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Katika muda mfupi, tunapoteza usawa wetu wa ndani, na hatujui jinsi ya kuendelea kwa njia iliyo mbele wala jinsi ya kuendelea katika imani zetu. Inaonekana kana kwamba imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na tena ya kana kwamba hatujawahi kukutana na Bwana Yesu au kupata kumjua. Kila kitu machoni petu hutujaza na mkanganyo, na kutufanya kuyumba kwa shaka. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu kuna ghadhabu isiyozuilika na aibu. Tunajaribu kujieleza, kupata suluhisho, na, aidha, sisi huendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, ili tuweze kujieleza kwa dhati Kwake. Ingawa kuna nyakati zingine ambazo sisi huonekana hatuyumbiyumbi kwa kutazamwa nje, tusio wenye kiburi wala wanyenyekevu, mioyoni mwetu tunateseka na hisia ya hasara kuliko ile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaweza kuonekana ni kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, akili zetu zinasokoteka kwa mateso kama bahari yenye dhoruba. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimechukua matumaini na ndoto zetu zote, kukomesha tamaa zetu kuu na kutuacha tusitake kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu na anayeweza kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kati yetu na Yeye, ghuba kubwa kiasi kwamba hakuna aliye tayari hata kujaribu kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni mara ya kwanza ambapo sisi tumepitia pingamizi kubwa hivi, udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo maishani mwetu. Hukumu na kuadibu Kwake kwa kweli zimetusababisha kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia Kwake kosa la binadamu, ambazo tukilinganishwa nazo, sisi ni waovu sana, wachafu sana. Hukumu Yake na kuadibu zimetufanya sisi kutambua kwa mara ya kwanza jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hataweza kulingana na Mungu, ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya tutumaini kutoishi tena katika tabia potovu hivi, kujiondoa asili na kiini hiki haraka iwezekanavyo, na kuwacha kuwa waovu na wa kuchukiwa na Yeye. Hukumu na kuadibu Kwake zimetufanya tufurahie kutii maneno Yake, na tusiasi matayarisho na mipangilio Yake tena. Hukumu na kuadibu Kwake kwa mara nyingine zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa ya kutafuta uzima, na zilituwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi wetu…. Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, nje yaa kuzimu, tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti…. Mwenyezi Mungu ametupata, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na kuwashinda adui Zake wengi!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 4: Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake
Tanbihi:
a. Maandiko ya awali yanasema “na kwa.”
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?