Kristo ni Mwana wa Mungu au ni Mungu Mwenyewe?

23/09/2018

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Filipo akamwambia, Bwana, tuonyeshe Baba, na hiyo itatutosha. Yesu akasema kwake, nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba? Huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi? Maneno ninenayo kwenu sineni juu yangu, ila Baba aishiye ndani yangu, anazifanya kazi hizo. Niamini kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi, la sivyo niamini kwa ajili ya kazi hizo” (Yohana 14:8-11).

“Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja” (Yohana 10:30).

Je, Yesu Kristo Ni Mungu au Mwana wa Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili kamwe hangefanya kazi yoyote ambayo inasumbua usimamizi Wake Mwenyewe. Hili ndilo ambalo binadamu wote wanapaswa kuelewa. Kiini cha kazi ya Roho Mtakatifu ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya usimamizi wa Mungu Mwenyewe. Vile vile, kazi ya Kristo ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Kutokana na kwamba Mungu Anapata mwili, Anatambua dutu Yake ndani ya mwili Wake, kama kwamba mwili Wake ni wa kutosha kufanya kazi Yake. Kwa hivyo, kazi zote za Roho wa Mungu zinabadilishwa na kazi ya Kristo wakati wa kupata mwili, na kwenye msingi wa kazi zote wakati wa kupata mwili ni kazi ya Kristo. Haiwezi kuchanganyika na kazi yoyote ile kutoka enzi nyingine yoyote. Na kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, Yeye Anafanya kazi katika utambulisho wa mwili Wake; kwa kuwa Yeye hukuja katika mwili, kisha Yeye humaliza katika mwili kazi hiyo Anayoazimia kufanya. Iwe ni Roho wa Mungu au ni Kristo, wote ni Mungu Mwenyewe, na Anafanya kazi hiyo Anayoazimia kufanya na hufanya huduma hiyo Anayopaswa kufanya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Mungu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hili liliwapa watu fursa ya kukumbana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa binadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukubwa Wake katikati ya unyenyekevu, vilevile na kupata ufahamu wa mwanzo na ufafanuzi wa mwanzo wa uhalali na uhalisi wa Mungu. Hata ingawa kazi iliyokamilishwa na Bwana Yesu, njia Zake za kufanya kazi, na mitazamo ambayo kutoka kwayo Aliongea ilitofautiana na ile ya nafsi halisi ya Mungu katika ulimwengu wa kiroho, kila kitu kumhusu kilimwakilisha kwa kweli Mungu Mwenyewe ambaye binadamu walikuwa hawajawahi kumwona awali—hili haliwezi kukataliwa! Hivi ni kusema, haijalishi ni kwa umbo gani ambalo Mungu huonekana, haijalishi huongea kutoka katika mtazamo upi, au Yeye hukabiliana na binadamu kupitia kwa taswira gani, Mungu hawakilishi chochote isipokuwa Yeye Mwenyewe. Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote—Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote aliyepotoka. Mungu ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kukataliwa.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Yesu alipomwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba alipokuwa akiomba, hili lilifanywa katika mitazamo ya mwanadamu aliyeumbwa, kwa sababu Roho wa Mungu alikuwa amevaa mwili wa kawaida na wa desturi na Alikuwa na umbile la nje la mwanadamu aliyeumbwa. Hata ikiwa ndani yake mlikuwa na Roho wa Mungu, umbo Lake la nje bado lilikuwa lile la mwanadamu wa kawaida; kwa maana nyingine, Alikuwa “Mwana wa Adamu” jambo ambalo watu wote, akiwemo Yesu Mwenyewe, walilizungumzia. Na kwa sababu Anaitwa Mwana wa Adamu, Yeye ni mtu (Mwanamke au mwanamume, kwa vyovyote vile mwenye umbo la nje la mwanadamu) aliyezaliwa katika familia ya kawaida ya watu wa kawaida. Kwa hivyo, Yesu kumwita Mungu wa mbinguni kwa jina la Baba kulikuwa sawa na mlivyomwita mara ya kwanza Baba; Alifanya hivyo kutokana na mtazamo wa Mwanadamu aliyeumbwa. Je, mnakumbuka Sala ya Bwana ambayo Yesu aliwafundisha kukariri? “Baba Yetu Uliye mbinguni….” Aliwaambia wanadamu wote wamwite Mungu wa Mbinguni kwa jina la Baba. Na kwa kuwa Naye pia alimwita Baba, alifanya hivyo kutoka kwa mtazamo wa mtu aliye katika daraja moja nanyi nyote. Kwa kuwa mlimuita Mungu wa mbinguni Baba, hili linaonyesha kuwa Yesu alijichukulia kuwa katika daraja sawa nanyi, kama mwanadamu duniani aliyeteuliwa na Mungu (yaani, Mwana wa Mungu). Kama mnamwita Mungu “Baba,” je, hii si kwa sababu nyinyi ni wanadamu walioumbwa? Haijalishi Yesu alikuwa na mamlaka makubwa kiasi gani duniani, kabla ya kusulubiwa, Alikuwa tu Mwana wa Adamu, akiongozwa na Roho Mtakatifu (yaani, Mungu), Akiwa miongoni mwa viumbe wa duniani, kwani bado Alikuwa hajaikamilisha kazi Yake. Kwa hivyo, kumwita kwake Mungu wa mbinguni Baba kulikuwa tu unyenyekevu na utiifu Wake. Yeye kumwita Mungu (yaani, Roho aliye mbinguni) kwa namna ile, hata hivyo, hakudhibitishi kuwa Yeye ni Mwana wa Roho wa Mungu aliye mbinguni. Badala yake, ni kuwa mtazamo wake ni tofauti, si kwamba ni nafsi tofauti. Uwepo wa nafsi tofauti ni uongo. Kabla ya kusulubiwa kwake, Yesu alikuwa Mwana wa Adamu aliyefungwa katika udhaifu wa kimwili, na Hakuwa na mamlaka kamilifu ya Roho. Hiyo ndiyo maana Angeweza tu kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe. Ni kama tu Alivyoomba mara tatu huko Gethsemane: “Si kama Nitakavyo, bali kama utakavyo.” Kabla Atundikwe msalabani, Hakuwa zaidi ya Mfalme wa Wayahudi; alikuwa Kristo, Mwana wa Adamu, na wala si mwenye utukufu. Hiyo ndiyo maana, kutokana na mtazamo wa mwanadamu, Alimwita Mungu Baba.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Aidha kuna wale wasemao, “je, si Mungu alitaja wazi kuwa Yesu ni Mwanawe mpendwa?” Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, ambaye anapendezwa naye—haya bila shaka yalitamkwa na Mungu Mwenyewe. Huyu alikuwa Mungu akijitolea ushuhuda Mwenyewe, ila kutoka katika mtazamo tofauti, ule wa Roho aliye mbinguni akitolea ushuhuda kupata Mwili Kwake. Yesu ni kupata mwili Kwake, si Mwanake mbinguni. Je, unaelewa? Je, maneno ya Yesu, “Mimi ni ndani ya Baba naye Baba yu ndani Yangu,” hayaonyeshi kuwa Wao ni Roho mmoja? Na si kwa sababu ya kupata mwili kulikosababisha kutenganishwa Kwao kati ya mbinguni na duniani? Uhalisi ni kwamba Wao ni kitu kimoja; hata iweje, ni Mungu anajitolea ushuhuda Mwenyewe. Kutokana na kubadilika kwa enzi, mahitaji ya kazi, na hatua mbalimbali za mpango Wake wa usimamizi, vilevile jina wamwitalo wanadamu hubadilika. Alipokuja kufanya hatua ya kwanza ya kazi, Angeweza kuitwa tu Yehova, mchungaji wa Waisraeli. Katika hatua ya pili, Mungu mwenye mwili Angeweza kuitwa tu Bwana, na Kristo. Lakini wakati huo, Roho aliye mbinguni alikariri tu kwamba Alikuwa Mwana mpendwa wa Mungu, bila kutaja kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu. Hili halikufanyika kabisa. Mungu angewezaje kuwa na Mwana wa pekee? Basi, Mungu asingekuwa mwanadamu? Kwa kuwa Alikuwa Mwili, Aliitwa Mwana mpendwa wa Mungu na kutokana na hili, kukazuka uhusiano wa Baba na Mwana. Ni kwa sababu tu ya utengano kati ya mbingu na dunia. Yesu aliomba kutokana na msimamo wa mwili. Kwa sababu Alikuwa Amepata mwili wa ubinadamu wa kawaida, ni kutokana na msimamo wa mwili ndipo Alisema: “Umbo Langu la nje ni la kiumbe. Kwa sababu Nilijivisha mwili kuja duniani, sasa Niko mbali, mbali sana na mbinguni.” Kwa sababu hii, Angeomba tu kwa Baba kutokana na msimamo wa mwili. Huu ulikuwa wajibu Wake, ambao ni sharti Roho wa Mungu aliyepata mwili anapaswa kupewa. Haiwezekani kusema kwamba Hawezi kuwa Mungu kwa sababu tu Anamwomba Baba kutokana na msimamo wa mwili. Ijapokuwa Anaitwa Mwana mpendwa wa Mungu, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, ni vile tu Yeye ni mwili wa Roho, na kiini chake bado ni Roho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Ikiwa yeyote miongoni mwenu anasema kwamba hakika Utatu upo, basi eleza huyu Mungu mmoja katika nafsi tatu ni nini hasa. Baba Mtakatifu ni nini? Mwana ni nini? Roho Mtakatifu ni nini? Je, Yehova ni Baba Mtakatifu? Je, Yesu ni Mwana? Basi, Roho Mtakatifu je? Je, Baba si Roho? Je, kiini cha Mwana vilevile si Roho? Je, kazi ya Yesu haikuwa ya Roho Mtakatifu? Je, kazi ya Yehova haikufanywa wakati ule na Roho sawa tu na kazi ya Yesu? Mungu Anaweza kuwa na Roho wangapi? Kulingana na maelezo yako hizi nafsi tatu, yaani, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni mmoja; kama ni hivyo, kuna Roho watatu lakini kuwa na Roho watatu kunamaanisha kuwa kuna Mungu Watatu. Hii inamaanisha kuwa hakuna Mungu Mmoja wa kweli; Mungu wa aina hii anawezaje kuwa kiini asili cha Mungu? Kama unakubali kuwa kuna Mungu mmoja tu, basi Anawezaje kuwa na Mwana na awe Baba? Je, hizi si fikra zako mwenyewe? Kuna Mungu Mmoja tu, nafsi moja katika Mungu huyu, na Roho mmoja tu wa Mungu sawa tu na ilivyoandikwa katika Biblia kwamba “Kuna tu Roho Mtakatifu mmoja na Mungu mmoja tu.” Haijalishi kama Baba na Mwana unaowazungumzia wapo, kuna Mungu mmoja tu, na kiini cha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu mnaowaamini ni kiini cha Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, Mungu ni Roho, ila Ana uwezo wa kupata Mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu na vilevile kuwa juu ya vitu vyote. Roho Wake anajumuisha kila kitu na Anapatikana kila mahala. Anaweza kuwa katika mwili na wakati ule ule akawa kote duniani. Kwa kuwa watu wanasema kwamba Mungu ndiye tu Mungu wa kweli, basi kuna Mungu mmoja, ambaye hawezi kugawanywa kwa mapenzi ya awaye yote! Mungu ni Roho mmoja tu, na nafsi moja; na huyo ni Roho wa Mungu. Ikiwa ni kama usemavyo, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, basi Hawa si watatu? Roho Mtakatifu ni kitu kimoja, Mwana ni kingine, na Baba vilevile ni kingine. Ni nafsi tatu tofauti zenye viini tofauti, iweje basi ziwe kila moja sehemu ya Mungu mmoja? Roho Mtakatifu ni Roho; hili ni rahisi kueleweka kwa wanadamu. Ikiwa ni hivyo basi, Baba ni Roho zaidi. Hajawahi kushuka kuja duniani na Hajawahi kupata mwili; Yeye ni Yehova Mungu katika mioyo ya mwanadamu, na kwa hakika Yeye vilevile ni Roho. Basi kuna uhusiano gani kati Yake na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Baba na Mwana? Au ni uhusiano kati ya Roho Mtakatifu na Roho wa Mungu? Je, kiini cha kila Roho ni sawa? Au Roho Mtakatifu ni chombo cha Baba? Hili linaweza kuelezwaje? Aidha kuna uhusiano gani kati ya Mwana na Roho Mtakatifu? Je, ni uhusiano kati ya Roho wawili au ni uhusiano kati ya mwanadamu na Roho? Haya yote ni masuala ambayo hayawezi kuelezewa! Ikiwa Wote ni Roho mmoja, basi hapawezi kuwepo na mjadala kuhusu nafsi tatu, kwani zote zinamilikiwa na Roho mmoja. Kama Zingekuwa nafsi tofauti, basi Roho Zao Zingetofautiana katika nguvu zao na kamwe hawangekuwa Roho mmoja. Hii dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni upuuzi mtupu! Hili linamweka Mungu katika vitengo na kumgawanya kuwa nafsi tatu, kila moja ikiwa na hadhi na Roho; basi Atawezaje kuwa Roho mmoja na Mungu mmoja? Hebu niambie, je, mbingu na dunia na vyote vilivyomo viliumbwa na Baba, Mwana, au na Roho Mtakatifu? Wengine husema Waliviumba kwa pamoja. Basi ni nani alimkomboa mwanadamu? Alikuwa Roho Mtakatifu, Mwana, au Baba? Wengine husema ni Mwana aliyewakomboa wanadamu. Basi Mwana ni nani katika kiini? Siye kupata mwili kwa Roho wa Mungu? Mungu aliyepata mwili anamwita Mungu aliye Mbinguni Baba katika mtazamo wa mwanadamu aliyeumbwa. Je, hufahamu kuwa Yesu alizaliwa kutokana na utungaji mimba kupitia Roho Mtakatifu. Ndani yake mna Roho Mtakatifu; lolote usemalo, Yeye bado ni mmoja na Mungu wa Mbinguni, kwani Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu. Hili wazo la Mwana si kweli Kabisa. Ni Roho mmoja anayefanya Kazi yote; Mungu Mwenyewe pekee, yaani, Roho wa Mungu anafanya kazi Yake. Roho wa Mungu ni nani? Je, si Roho Mtakatifu? Je, si Roho Mtakatifu anayefanya kazi ndani ya Yesu? Ingekuwa kazi haikufanywa na Roho Mtakatifu (yaani Roho wa Mungu), je, kazi Yake ingemwakilisha Mungu Mwenyewe?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Alichokiona mwanadamu mwanzoni kilikuwa ni Roho Mtakatifu Akimshukia Yesu kama njiwa; Hakuwa Roho mwenye upekee kwa Yesu tu, badala yake alikuwa Roho Mtakatifu. Basi roho wa Yesu anaweza kutenganishwa na Roho Mtakatifu? Ikiwa Yesu ni Yesu, Mwana, na Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, basi wangewezaje kuwa kitu kimoja? Ingekuwa hivyo kazi isingefanywa. Roho ndani ya Yesu, Roho aliye mbinguni, na Roho wa Yehova wote ni mmoja. Anaweza kuitwa Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu, Roho aliyezidishwa mara saba, na Roho mwenye vyote. Roho wa Mungu anaweza kufanya kazi nyingi. Ana uwezo wa kuumba na kuiangamiza dunia kwa kuleta mafuriko duniani; Anaweza kuwakomboa wanadamu, aidha, kuwashinda na kuwaangamiza wanadamu wote. Kazi hii yote inafanywa na Mungu Mwenyewe na haiwezi kufanywa na yeyote katika nafsi za Mungu kwa niaba Yake. Roho Wake anaweza kuitwa Yehova na Yesu, na vilevile mwenye Uweza. Yeye ni Bwana na Kristo. Anaweza pia kuwa Mwana wa Adamu. Yuko mbinguni na vilevile duniani; Yuko juu ya dunia na pia miongoni mwa umati. Yeye tu ndiye Bwana wa Mbingu na dunia! Tangu wakati wa uumbaji hadi sasa, kazi hii imekuwa ikifanywa na Roho wa Mungu Mwenyewe. Iwe ni kazi mbinguni au katika mwili, yote hufanywa na Roho Wake Mwenyewe. Viumbe wote, wawe mbinguni au duniani, wamo katika kiganja cha mkono Wake wenye nguvu; yote hii ni kazi ya Mungu na haiwezi kufanywa na yeyote kwa niaba Yake. Mbinguni Yeye ni Roho na vilevile Mungu Mwenyewe; miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwili ila anaendelea kuwa Mungu Mwenyewe. Japo Anaweza kuitwa mamia ya maelfu ya majina, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, na kazi yote[a] ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho Wake. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubiwa Kwake ilikuwa kazi ya moja kwa moja ya Roho Wake, na vilevile tangazo kwa mataifa yote na nchi zote wakati wa siku za mwisho. Wakati wote Mungu anaweza kuitwa mwenye uweza na Mungu mmoja wa kweli, Mungu Mwenyewe mwenye vyote. Nafsi bayana hazipo, aidha dhana ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haipo. Kuna Mungu mmoja mbinguni na duniani!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?

Tanbihi:

a. Matini ya asili haina neno “kazi.”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp