Mtu anapaswaje kuichukulia na kuitumia Biblia kwa njia inayokubaliana na mapenzi ya Mungu? Thamani ya asili ya Biblia ni nini?

23/09/2018

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai” (Yohana 5:39-40).

Thamani ya kiasili ya Biblia na jinsi ambavyo mtu huichukulia na kuitumia Biblia kwa njia ambayo inalingana na mapenzi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Leo, Ninaichambua Biblia kwa namna hii na haimaanishi kwamba Naichukia, au kukana thamani yake kwa ajili ya marejeleo. Ninakuelezea na kukufafanulia thamani ya asili na chanzo cha Biblia ili uweze kuondoka katika giza. Maana watu wana mitazamo mingi kuhusu Biblia, na mingi yao ina makosa; kusoma Biblia kwa namna hii sio tu kunawazuia kupata kile wanachopaswa kupata, lakini, muhimu zaidi, kunazuia kazi Niliyokusudia kufanya. Ni kero kubwa kwa kazi ya siku zijazo, na inatoa hasara tu, na wala sio faida. Hivyo, Ninachokufundisha ni hulka tu na kisa cha ndani cha Biblia. Sikwambii kwamba usisome Biblia, au uzunguke ukitangaza kwamba haina thamani kabisa, bali kwamba uweze kuwa na maarifa na mtazamo sahihi juu ya Biblia. Usiegemee upande mmoja sana! Ingawa Biblia ni kitabu cha historia kilichoandikwa na wanadamu, pia kinaandika kanuni nyingi ambazo kwazo watakatifu wa zamani na manabii walimhudumia Mungu, vilevile uzoefu wa hivi karibuni wa mitume katika kumhudumia Mungu—yote haya yalishuhudiwa na kujulikana kwa watu hawa, na inaweza kutumika kama rejeleo kwa ajili ya watu wa enzi hii katika kutafuta njia ya kweli. Hivyo, katika kusoma Biblia watu wanaweza pia kupata njia nyingi za maisha ambazo haziwezi kupatikana katika vitabu vingine. Njia hizi ni njia za maisha ya kazi ya Roho Mtakatifu ambazo manabii na mitume walizipitia katika enzi iliyopita, na maneno mengi ni ya thamani, na yanaweza kutoa kile ambacho watu wanataka. Hivyo, watu wote wanapenda kusoma Biblia. Kwa sababu kuna mambo mengi sana yaliyofichwa katika Biblia, mitazamo ya watu juu ya Biblia ni tofauti na mitazamo yao juu ya maandiko ya viongozi wa kiroho mashuhuri. Biblia ni rekodi na mkusanyiko wa uzoefu na maarifa ya watu ambao walimhudumia Yehova na Yesu katika enzi ya kale na mpya, na pia vizazi vya baadaye vimeweza kupata nuru, mwanga mkubwa na njia za kuweza kutembea kwazo. Sababu ya Biblia kuwa na hadhi ya juu kuliko maandiko ya kiongozi yeyote mkubwa wa kiroho ni kwa sababu maandiko yao yote yanatoka katika Biblia, uzoefu wao wote unatokana na Biblia, na wote wanaelezea Biblia. Na hivyo, ingawa watu wanaweza wakafaidika na vitabu kutoka kwa kiongozi yeyote wa kiroho mashuhuri, bado wanaiabudu Biblia, maana kwao, inaonekana ni ya juu sana na ya kina sana! Ingawa Biblia inaleta pamoja baadhi ya vitabu vya maneno ya uzima, kama vile nyaraka za Paulo na nyaraka za Petro, na ingawa watu wanaweza kusaidiwa na vitabu hivi, vitabu hivi bado vimepitwa na wakati, bado ni vitabu vya enzi ya kale, na haijalishi ni vizuri kiasi gani, vinafaa tu kwa ajili ya kipindi kimoja, na wala sio vya milele. Maana kazi ya Mungu siku zote inaendelea, na haiwezi kusimama tu katika kipindi cha Paulo na Petro, au siku zote ibaki katika Enzi ya Neema, enzi ambayo Yesu alisulubiwa. Na hivyo, vitabu hivi vinafaa tu katika Enzi ya Neema, na wala sio kwa ajili ya Enzi ya Ufalme wa siku za mwisho. Vinaweza tu kuwa na manufaa kwa waumini wa Enzi ya Neema, na sio kwa watakatifu wa Enzi ya Ufalme, na haijalishi ni vizuri kiasi gani, bado havifai kwa kipindi hiki. Ni sawa na kazi ya Yehova ya uumbaji au kazi Yake katika Israeli: Haijalishi kazi hii ilikuwa kubwa kiasi gani, bado imepitwa na wakati, na muda utaendelea kuja wakati umekwishapita. Kazi ya Mungu pia ni ile ile: Ni nzuri, lakini muda utafika ambapo itakoma; siku zote haitaendelea kubaki katikati ya kazi ya uumbaji, wala katikati ya kazi ile ya msalaba. Haijalishi kazi ya msalaba inashawishi kiasi gani, haijalishi ilikuwa ya ufanisi kiasi gani katika kumshinda Shetani, hata hivyo, kazi bado ni kazi, na enzi, hata hivyo bado ni enzi; kazi siku zote haiwezi kubaki katika msingi ule ule, wala nyakati haziwezi kukosa kubadilika, kwa sababu kulikuwa na uumbaji na lazima kuwepo na siku za mwisho. Hii haiepukiki!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (4)

Hili ni kwa sababu Biblia ilifuata miaka elfu kadhaa ya historia ya wanadamu na watu wote wanaichukulia kama Mungu kiasi kwamba watu walio katika siku za mwisho wanambadilisha Mungu na Biblia. Hiki ni kitu ambacho Mungu anachukia sana. Kwa hiyo katika wakati wake wa ziada, Alilazimika kubainisha hadithi ya ndani na asili ya Biblia. La sivyo, Biblia bado ingeweza kuchukua nafasi ya Mungu katika mioyo ya watu na wangeweza kuhukumu na kupima matendo ya Mungu kutegemezwa kwa maneno yaliyo katika Biblia. Maelezo ya Mungu ya asili, uundaji, na hitilafu za Biblia bila shaka sio kukataa kuwepo kwake, wala sio kuishutumu Biblia. Badala yake, ni kutoa ufafanuzi wa busara na wa kufaa, kurejesha sura ya asili ya Biblia, na kurekebisha kuelewa visivyo kwa watu kuhusu Biblia ili watu wote wawe na mtazamo sahihi kuihusu, wasiiabudu tena, na wasipotee tena—wao huchukulia kimakosa imani yao kwa Biblia isiyoweza kutambua kama kumwamini na kumwabudu Mungu, na hata hawathubutu kukabiliana na usuli wake wa kweli na upungufu wake. Baada ya kila mtu kuwa na ufahamu halisi wa Biblia ataweza kuiweka kando bila kusita na kuyakubali maneno mapya ya Mungu kwa ujasiri. Hili ni lengo la Mungu katika sura hizi kadhaa. Ukweli ambao Mungu anataka kuwaambia watu hapa ni kwamba hakuna nadharia au ukweli unaoweza kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu ya sasa au maneno, na hakuna kitu ambacho kinaweza kuchukua nafasi ya Mungu. Ikiwa watu hawawezi kuondoa wavu wa Biblia, hawataweza kuja mbele ya Mungu kamwe. Ikiwa wanataka kuja mbele ya Mungu, lazima kwanza watakase mioyo yao kutokana na chochote ambacho kinaweza kuchukua nafasi Yake—hivi Mungu ataridhika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani, Utangulizi

Ikiwa unatamani kuiona kazi ya Enzi ya Sheria, na kuona jinsi gani Waisraeli waliifuata njia ya Yehova, basi ni lazima usome Agano la Kale; ikiwa unatamani kuelewa kazi ya Enzi ya Neema, basi ni lazima usome Agano Jipya. Lakini unawezaje kuona kazi ya siku za mwisho? Ni lazima ukubali uongozi wa Mungu wa leo, na kuingia katika kazi ya leo, maana hii ni kazi mpya na hakuna ambaye ameirekodi katika Biblia hapo nyuma. Leo, Mungu amefanyika mwili, na Amewachagua wateule wengine katika nchi ya China. Mungu anafanya kazi ndani ya watu hawa, Anaendelea na kazi Yake duniani, Anaendelea kutoka katika kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya leo ni njia ambayo mwanadamu hajawahi kuiendea, na njia ambayo hakuna mtu ambaye amewahi kuiona. Ni kazi ambayo haijawahi kufanywa hapo kabla—ni kazi ya Mungu ya hivi karibuni kabisa duniani. Hivyo, kazi ambayo haijawahi kufanywa kabla sio historia, kwa sababu sasa ni sasa, na bado haijawa muda uliopita. Watu hawajui kwamba Mungu amefanya kazi kubwa, mpya duniani, na nje ya Israeli, yaani imevuka mawanda ya Israeli, na zaidi ya unabii wa manabii, ambayo ni kazi mpya na ya kushangaza nje ya unabii, na kazi mpya kabisa nje ya Israeli, na kazi ambayo watu hawawezi kuielewa au kufikiria. Inawezekanaje Biblia kuwa na rekodi za wazi za kazi kama hiyo? Ni nani ambaye angeweza kurekodi kila hatua ya kazi ya leo, bila kuondoa kitu? Ni nani angeweza kurekodi kazi hii kubwa na yenye hekima ambayo inakataa maagano ya kitabu cha kale? Kazi ya leo sio historia, na kama vile, ikiwa unatamani kutembea katika njia ya leo, basi mnapaswa kutengana na Biblia, unapaswa kwenda mbele zaidi ya vitabu vya unabii au historia ya Biblia. Baada ya hapo tu ndipo utaweza kutembea njia mpya vizuri, na baada ya hapo ndipo utaweza kuingia katika ufalme mpya na kazi mpya. Unapaswa kuelewa ni kwa nini leo unaambiwa usisome Biblia, kwa nini kuna kazi nyingine ambayo inajitenga na Biblia, kwa nini Mungu haonekani mpya na wa kina zaidi katika Biblia, kwa nini badala yake kuna kazi kubwa zaidi nje ya Biblia. Haya ndiyo yote mnayopaswa kuelewa. Unapaswa kuelewa tofauti kati ya kazi ya zamani na kazi mpya, na hata kama hausomi Biblia, unapaswa kuitenganisha; kama hautaweza, bado utakuwa unaiabudu Biblia, na itakuwa ni vigumu sana kwako kuingia katika kazi mpya na kupitia mabadiliko mapya. Kwa kuwa kuna njia ya juu, kwa nini mjifunze hiyo ya chini, njia ya kale? Kwa kuwa kuna matamshi mapya, na kazi mpya, kwa nini uishi katikati ya rekodi za kale za kihistoria? Matamshi mapya yanaweza kukupa, ambayo yanathibitisha kwamba hii ni kazi mpya; rekodi za kale haziwezi kukushibisha, au kutosheleza mahitaji yako ya sasa, kitu ambacho kinathibitisha kwamba ni historia, na sio kazi ya hapa na sasa. Njia ya juu zaidi ni njia mpya zaidi, na kazi mpya, bila kujali njia ya zamani ni ya juu kiasi gani, bado ni historia ya kumbukumbu ya watu, na haijalishi ina thamani kiasi gani kama rejeleo, bado ni njia ya kale. Ingawa imerekodiwa katika “kitabu kitakatifu,” njia ya kale ni historia; ingawa hakuna rekodi yake katika “kitabu kitakatifu,” njia mpya ni ya hapa na sasa. Kwa njia hii inaweza kukuokoa, na kwa njia hii inaweza kukubadilisha, maana hii ni kazi ya Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Biblia (1)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp