Kanisa la Mungu ni nini? Shirika la kidini ni nini?

24/09/2018

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Kanisa … ni mwili Wake, ukamilifu wa Yeye anayekamilisha yote katika yote” (Waefeso 1:22-23).

“Na Yesu akaingia katika hekalu la Mungu, naye akawaondoa wote waliokuwa wakiuza na kununua katika hekalu, naye akaziangusha meza za wabadilishaji wa fedha, na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa, Na akawaambia, imeandikwa, nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi; lakini mmeifanya pango la wezi” (Mathayo 21:12-13).

“Naye akalia sana kwa sauti kubwa, akisema, Babeli mkuu umeanguka, umeanguka, na umekuwa makazi ya pepo, ngome ya kila pepo mwovu, na tundu la kila ndege mchafu na mwenye kuchukiza. Kwani mataifa yote yamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa ulimwengu wamefanya uasherati naye, na wafanya biashara wa ulimwengu wametajirika kupitia kwa utele wa uzuri wake” (Ufunuo 18:2-3).

Kanisa la Mungu na mashirika ya kidini ni nini

Maneno Husika ya Mungu:

Wale wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikiwa na uwepo na nidhamu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo katika mkondo wa Roho Mtakatifu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na hali ikiwa mbaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao wanakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wataishi katika mkondo wa Roho Mtakatifu, wapokee utunzaji na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wako tayari kuweka ukweli katika vitendo wanapewa nuru na Roho Mtakatifu na wale wasiotaka kuweka ukweli katika vitendo wanafundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu na huenda hata wakaadhibiwa. Bila kujali wao ni aina gani ya watu, ilimradi tu wamo katika mkondo wa Roho Mtakatifu, Mungu atawawajibikia wote wanaoikubali kazi Yake mpya kwa minajili ya jina Lake. Wale wanaolitukuza jina Lake na wako radhi kuweka maneno Yake katika vitendo watapokea baraka Zake; wale wasiomtii na wasioyaweka maneno Yake katika vitendo watapokea adhabu Yake. Watu walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya, na kwa sababu wameikubali kazi mpya, wanafaa kuwa na ushirika wa kufaa na Mungu na hawafai kuwa kama waasi wasiofanya wajibu wao. Hili ndilo sharti la pekee la Mungu kwa mwanadamu. Sio hivyo kwa watu wasioikubali kazi mpya: Wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na nidhamu na lawama ya Roho Mtakatifu hayatumiki kwao. Kila siku hawa watu wanaishi ndani ya mwili, wanaishi ndani ya akili zao, na yote wayafanyayo ni kulingana na mafundisho ya kidini yaliyozalishwa na uchanganuzi pamoja na utafiti wa bongo zao. Si matakwa ya kazi mpya ya Roho Mtakatifu sembuse ushirika na Mungu. Wale wasioikubali kazi mpya ya Mungu hawana uwepo wa Mungu na, zaidi, wanakosa baraka na ulinzi wa Mungu. Maneno na matendo yao mengi yanashikilia matakwa ya zamani ya kazi ya Roho Mtakatifu; ni mafundisho ya kidini, si ukweli. Mafundisho na taratibu kama hizo ni thibitisho la kutosha kuwa kitu cha pekee kinachowaleta pamoja ni dini; si watu walioteuliwa au vyombo vya kazi ya Mungu. Mkutano wa wale wote walio miongoni mwao unaweza tu kuitwa mkutano mkubwa wa watu wa dini, na bali hauwezi kuitwa kanisa. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa. Hawana kazi mpya ya Roho Mtakatifu; wakifanyacho kinaonekana chenye kunuka dini, wanachoishi kwa kudhihirisha katika maisha yao kinaonekana kimejaa dini; hawana uwepo na kazi ya Roho Mtakatifu, sembuse kustahiki kupokea nidhamu au nuru ya Roho Mtakatifu. Watu hawa wote ni miili isiyo na uhai, na funza wasio na mambo ya kiroho. Hawana ufahamu wa uasi na pingamizi wa mwanadamu, hawana ufahamu wa uovu wote wa mwanadamu, sembuse kujua kazi yote ya Mungu na mapenzi ya sasa ya Mungu. Wote ni watu wapumbavu, waovu, ni watu duni wasiostahili kuitwa waumini! Hakuna wafanyacho kinachohusiana na usimamizi wa Mungu, sembuse kuweza kuidhoofisha mipango ya Mungu. Maneno na matendo yao yanaudhi sana, yanasikitisha mno, na hayafai kutajwa kabisa. Hakuna chochote wakifanyacho walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu kinahusiana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu hata kidogo. Kwa sababu hii, haijalishi wanafanya nini, hawana nidhamu ya Roho Mtakatifu na zaidi, hawana nuru ya Roho Mtakatifu. Kwani wao ni watu wasiopenda ukweli, na wamechukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Wanaitwa watenda maovu kwani wanatembea katika mwili, na kufanya chochote kiwafurahishacho kwa kisingizio cha bango la Mungu. Mungu anapofanya kazi, wao wanakuwa maadui Kwake kwa makusudi, na kumkimbia Yeye. Kutoweza kushirikiana kwa mwanadamu na Mungu ni uasi wa hali ya juu, kwa hivyo wale watu wanaokimbia kinyume na Mungu makusudi si watapokea hakika malipo yao ya haki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Je, Mungu huwaita nini wale waliomwamini Yehova? Uyahudi. Waligeuka kuwa aina ya kundi la dini. Na Mungu huwafafanuaje wale wanaomwamini Yesu? (Ukristo.) Machoni pa Mungu, Uyahudi na Ukristo ni vikundi vya dini. Kwa nini Mungu anawafafanua hivyo? Miongoni mwa wale wote ambao ni washiriki wa mashirika haya ya dini yaliyofafanuliwa na Mungu, je, kuna wowote wanaomcha Mungu na kuepukana na uovu, kufanya mapenzi ya Mungu, na kufuata njia ya Mungu? (La.) Hili limekuwa dhahiri. Machoni pa Mungu, wale wote wanaomfuata Mungu kwa maneno tu wanaweza kuwa wale ambao Mungu amewatambua kuwa waumini? Je, wote wana uhusiano na Mungu? Je, wote wanaweza kuwa walengwa wa wokovu wa Mungu? (La.) Hivyo siku itakuja ambapo mtashushwa na kuwa kile ambacho Mungu anaona kama kundi la dini? (Inawezekana.) Kushushwa hadi kiwango cha kundi la kidini, hiyo inaonekana isiyowazika. Watu wakiwa sehemu ya kikundi cha dini machoni pa Mungu, je, wataokolewa na Yeye? Je wao ni wa nyumba ya Mungu? (La, sio.) Kwa hivyo jaribu kufupisha: Watu hawa ambao wanamwamini Mungu wa kweli kwa maneno tu lakini ambao Mungu anawaamini wao kuwa sehemu ya kikundi cha dini—wanaitembea njia gani? Je, inaweza kusemekana kwamba watu hawa wanaitembea njia ya kupeperusha bendera ya imani bila kamwe kufuata njia Yake, ya kumwamini Mungu lakini kutomwabudu, na badala yake kumtelekeza? Yaani, wanaitembea njia ya kumwamini Mungu lakini kutofuata njia ya Mungu na kumwacha Mungu; njia yao ni ile ambayo wanamwamini Mungi lakini wamwabudu Shetani, wanamwabudu ibilisi, wanajaribu kutekeleza usimamizi wao wenyewe, na kujaribu kuanzisha ufalme wao wenyewe. Je, hiki ni kiini cha hilo? Je, watu kama hawa wana uhusiano wowote na mpango wa Mungu wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu? (La.) Bila kujali ni watu wangapi wanamwamini Mungu, mara tu imani zao zinapofafanuliwa na Mungu kama dini au kikundi, basi Mungu ameamua kuwa hawawezi kuokolewa. Kwa nini nasema hivi? Katika kundi au umati wa watu ambao hawana kazi na mwongozo wa Mungu na ambao hawamwabudu hata kidogo, wanamwabudu nani? Wanamfuata nani? Katika umbo na jina wanamfuata mtu, lakini ni nani wanayemfuata hasa? Katika mioyo yao wanamtambua Mungu, lakini kwa kweli, wao huathiriwa na utawala wa hila, mipangilio na udhibiti wa binadamu. Wanamfuata Shetani, ibilisi; wanafuata nguvu ambazo zina uhasama kwa Mungu, ambazo ni maadui wa Mungu. Je, Mungu anaweza kuokoa kundi kama hili la watu? (La.) Kwa nini? Je, wana uwezo wa kutubu? (La.) Wao hupeperusha bendera ya imani, wakitekeleza shughuli za binadamu, wakitekeleza usimamizi wao wenyewe, na wanakwenda kinyume na mpango wa Mungu wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Matokeo yao ya mwisho ni kuchukiwa na kukataliwa na Mungu; Mungu hawezi kamwe kuwaokoa watu hawa, hawawezi kamwe kutubu, tayari wamekamatwa na Shetani—wamo mikononi mwa Shetani kabisa. … Ikiwa hawawezi kufuata njia ya Mungu na hawawezi kuitembea njia ya wokovu, matokeo yao ya mwisho yatakuwa yapi? Matokeo yao ya mwisho yatakuwa sawa na wale wanaoamini Ukristo na Uyahudi; hakutakuwa na tofauti. Hii ni tabia ya Mungu ya haki! Bila kujali umeyasikia mahubiri mangapi, na umeelewa ukweli kiasi gani, ikiwa hatimaye bado unawafuata watu na kumfuata Shetani, na hatimaye, bado huwezi kufuata njia ya Mungu na huwezi kumcha Mungu na kuepukana na uovu, basi watu kama hawa watachukiwa na kukataliwa na Mungu. Kadiri ionekanavyo, watu hawa ambao wanachukiwa na kukataliwa na Mungu wanaweza kuzungumza mengi kuhusu maandiko na mafundisho, wamekuja kuelewa ukweli mwingi, na ilhali bado hawawezi kumwabudu Mungu; hawawezi kumcha Mungu na kuepukana na uovu, na hawawezi kuwa na utiifu mkamilifu kwa Mungu. Machoni pa Mungu, Mungu anawafafanua kama dini, kama kikundi tu cha wanadamu, genge la wanadamu, na kama makao ya Shetani. Wanajulikana kwa jumla kama kikundi cha Shetani, na wanadharauliwa kabisa na Mungu.

kutoka katika “Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Kwanza, hebu tuseme ni imani gani “imani” katika “watu wenye imani” inarejelea nini: Inamaanisha Uyahudi, Ukristo, Ukatoliki, Uisilamu, na Ubudha, dini hizi kuu tano. …

…………

Miongoni mwa dini tano tulizozungumzia, Ukristo ni maalum kiasi fulani. Ni nini maalum kuhusu Ukristo? Hawa ni watu wanaomwamini Mungu wa kweli. Je, inawezekanaje wale wanaomwamini Mungu wa kweli waorodheshwe hapa? Kwa sababu Ukristo ni aina ya imani, basi, bila shaka, unahusiana tu na imani—ni aina ya sherehe, aina ya dini, na kitu tofauti na imani ya wale wanaomfuata Mungu kweli. Kilichonifanya kuuorodhesha miongoni mwa hizi dini tano ni kwa sababu Ukristo umeshushwa hadi kiwango sawa na Uyahudi, Ubudha, Uislamu. Wakristo wengi hawaamini kuna Mungu, au kwamba Anatawala juu ya vitu vyote, seuze kuamini katika uwepo Wake. Badala yake, wanatumia tu Maandiko Matakatifu kuzungumza kuhusu elimu ya dini, wakitumia elimu ya dini kuwafundisha watu kuwa wema, kuvumilia mateso, na kufanya vitu vizuri. Ukristo ni wa aina hiyo ya dini: Unazingatia tu nadharia za mafundisho ya kidini, hauna kabisa uhusiano wowote na kazi ya Mungu ya kusimamia na kuokoa wanadamu, ni dini ya wale wanaomfuata Mungu ambayo haitambuliwi na Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

“Lakini nasema kwenu, Kwamba mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu. Lakini iwapo mngejua maana ya hili, Naitaka rehema, na siyo sadaka, msingewashutumu wale wasio na hatia. Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya sabato” (Mat 12:6-8). “Hekalu” hapa linamaanisha nini? Kwa ufupi, “hekalu” linaashiria jengo refu la kupendeza, na katika Enzi ya Sheria, hekalu lilikuwa ni pahali pa makuhani kumwabudu Mungu. Bwana Yesu aliposema “mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu,” “mmoja” ilikuwa ikirejelea nani? Ni wazi, “mmoja” ni Bwana Yesu katika mwili kwa sababu Yeye tu ndiye aliyekuwa mkuu kuliko hekalu. Na maneno hayo yaliwaambia watu nini? Yaliwaambia watu watoke hekaluni—Mungu alikuwa tayari ameshatoka nje na hakuwa tena akifanyia kazi ndani yake, hivyo basi watu wanafaa kutafuta nyayo za Mungu nje ya hekalu na kufuata nyayo Zake katika kazi Yake mpya. Usuli wa Bwana Yesu kusema haya ilikuwa kwamba chini ya sheria, watu walikuwa wameiona hekalu kama kitu kilichokuwa kikuu zaidi kuliko Mungu Mwenyewe. Yaani, watu waliliabudu hekalu badala ya kumwabudu Mungu, hivyo basi Bwana Yesu akawaonya kutoabudu sanamu, lakini kumwabudu Mungu kwa sababu Yeye ndiye mwenye mamlaka ya juu zaidi. Hivyo basi, alisema: “Naitaka rehema, na siyo sadaka.” Ni wazi kwamba katika macho ya Bwana Yesu, watu wengi sana katika sheria hawakumwabudu tena Yehova Mungu, lakini walikuwa tu wakipitia mchakato wa kutoa sadaka na Bwana Yesu aliamua kwamba mchakato huu ulikuwa ibada ya sanamu. Waabudu sanamu hawa waliliona hekalu kama kitu kikuu, cha juu zaidi kuliko Mungu. Ndani ya mioyo yao kulikuwa tu na hekalu, wala si Mungu, na kama wangelipoteza hekalu, wangepoteza mahali pao pa kukaa. Bila ya hekalu hawakuwa na mahali popote pa kuabudu na wasingeweza kutoa sadaka zao. Mahali pao pa kukaa kama palivyojulikana ndipo walipofanyia shughuli zao kwa jina la kumwabudu Yehova Mungu, na hivyo basi wakaruhusiwa kuishi katika hekalu na kutekeleza shughuli zao binafsi. Ule utoaji sadaka wao kama ulivyojulikana ulikuwa tu kutekeleza shughuli zao za kibinafsi za aibu wakisingizia kwamba walikuwa wanaendesha ibada yao katika hekalu. Hii ndiyo iliyokuwa sababu iliyowafanya watu wakati huo kuliona hekalu kuwa kuu kuliko Mungu. Kwa sababu walilitumia hekalu kama maficho, na sadaka kama kisingizio cha kuwadanganya watu na kumdanganya Mungu, Bwana Yesu alisema haya ili kuwaonya watu. Mkitumia maneno haya kwa wakati wa sasa, yangali bado halali na yenye umuhimu sawa. Ingawa watu wa leo wameweza kupitia kazi tofauti za Mungu kuliko watu wa Enzi ya Sheria walivyowahi kupitia, kiini cha asili yao ni kile kile.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp